Elections 2010 Hebu ona huu upuuzi

Akifika Mza kwa kampeni, Dr Slaa atangaze wanafunzi hakuna ruhusa kwenye mikutano yake ya kampeni kote nchi nzima -- na alizungumzie sana hili -- akiunganisha na jinsi shule zetu zilivyoharibika na wanafunzi kukosa maadili mema kwa kutaja sababu kama hizo.

Mimi polepole naanza kuamini kwamba ni kweli CCM imeanza kupoteza umaarufu nchini, kwani inalazimisha hata wanafunzi kujaza wahiudhuriaji wa mikutano yake? Na wakubwa kulipwa mapesa na kupatiwa usafiri? Sioni sababu nyingine kwa CCM kufanya kitu kama hiki!
 
Sijaona upuuzi wa aina yoyote hapo! Zaidi ni kampeni murua zaidi!
Hawa watoto wa watu mnawakosesha masomo ili wafeli muendeleze kilinge chenu cha mafioso kwa kutawala taifa la wajinga..ama, kweli mipango yenu inafanikiwa!
 
Wanaosema upuuzi basi wao ndio wapuuzi,kwani kuna sheria gani inayomkataza mwanafunzi kushabikia Chadema?Na je hao wanafunzi wa sekondari hawapigi kura iwapo wametimiza miaka 18?Acheni ujinga kuweni wakubwa na si kushabikia upuuuuuuzi tuuuu.Sema ndio palipo ndio na Sio pasipo sio!
 
Hakika huu ni upuuzi tena wa kijinga hawa ni wanafunzi wa sekondari Nganza sijui wametumwa na nani Wasamehewe maana hawajui walitendalo wamesema wanafunzi wa vyuo vikuu wasogee jukwaani wakajitokeza wao na hao ndio wasomi wa form 5 na 6 lakini hawajitambui ni elimu gani wanayopewa hawa viumbe natamani kuhamia Rwanda kuliko kukaa kondoo kama hizi za watanzania Aghhhhhhhhh!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Wanaosema upuuzi basi wao ndio wapuuzi,kwani kuna sheria gani inayomkataza mwanafunzi kushabikia Chadema?Na je hao wanafunzi wa sekondari hawapigi kura iwapo wametimiza miaka 18?Acheni ujinga kuweni wakubwa na si kushabikia upuuuuuuzi tuuuu.Sema ndio palipo ndio na Sio pasipo sio!

shida si wanafunzi kuhudhuria kampeni za sisiem bali ni lile tatizo la sirikali ya sisiem kuwawekea vikwazo wanafunzi kuwa wafuasi wa vyama vingine. Kwa mfano ikiwa wanafunzi wataenda kwenye mkutano wa CHADEMA basi huenda mwalimu mkuu wa shule hiyo akapoteza ajira yake. Huo ni upuuzi kwa kuwa hakuna uhuru wa kuchagua vyama.....

CCM imejiwekea mazingira ya kuwafungia nira wananchi wa tanzania kuwa wafuasi wake bila hata ya ridhaa yao.
Si wanafunzi tu, bali hata wafanyabiashara wa nji hii wanaonewa sana na siri-kali ya CCM pale wanapoonyesha kuunga mkono chama fulani cha siasa ambacho si CCM.
 
Hata Zanzibar ilikuwa hivi hivi. Ukiangalia zile Video, ni vitoto vya shule vimejaa.

Dr. Slaa akataze wanafunzi kuja na Uniform. Kama wakitaka basi waje kama Raia.

Hebu ona hivi vitoto......

supporters.jpg
 
Hao walikuwa wanacheza nini sasa...mdundiko?
 
Hata Zanzibar ilikuwa hivi hivi. Ukiangalia zile Video, ni vitoto vya shule vimejaa.

Dr. Slaa akataze wanafunzi kuja na Uniform. Kama wakitaka basi waje kama Raia.

Hebu ona hivi vitoto......

supporters.jpg

Inasikitisha sana, tuna kazi kubwa sana mbele yetu - hiki ndicho kizazi kipya, hiki ni kizazi tunachotegemea kitetee mageuzi ili kuwepo na demokrasia ya kweli, ni hiki hiki kizazi kinachoambiwa kina kiherehere - leo hii kipo juu kuwakilisha wenzao kwamba CCM numberi One. Wakubwa hayaniingii akilini kabisa. - huu ni uonevu mamboleo.

Nafika mbali zaidi kuna wanafunzi (watoto) waliokuwa under 16, tunafanya nini kama taifa? tunawajengea nini vichwani mwao? uwezo wa kufikiria na kutatua matatizo yanayowazunguka kwa style hii? hii ndiyo bulding capacity tunayofanya? Shame!
 
Kibaya zaidi ni kuwa walishaambiwa ila naona hawakumbuki. Sintashangaa akishinda tena atarudia kuwaambia haya maneno.....

Na vyenyewe ukiviangalia hadi unakubali kuwa kiherehere hicho, hizo mimba ni kesho tu.

Masikini vitoto vya watu havifahamu kuwa anayesababisha hayo ni hiyo CCM wanayoshangilia.

Ila kweli nimesikia jamaa akisema CCM OYEEE........ watu kimyaaaaa....
supporters.jpg

attachment.php

Inasikitisha sana, tuna kazi kubwa sana mbele yetu - hiki ndicho kizazi kipya, hiki ni kizazi tunachotegemea kitetee mageuzi ili kuwepo na demokrasia ya kweli, ni hiki hiki kizazi kinachoambiwa kina kiherehere - leo hii kipo juu kuwakilisha wenzao kwamba CCM numberi One. Wakubwa hayaniingii akilini kabisa. - huu ni uonevu mamboleo.
 
Huyu mwimbaji wa nyimbo zadini sijui amefunuliwa kwamba JK na crew yake wanafaa, au ndo kalipwa!
We are suddenly doomed!

Huu sidhani kama ni ufunuo, ufunuo wa kweli ungemwelekeza akawaimbie masikini na wagonjwa waliokata tamaa na maisha, lakini kuimbia mafisadi kunafanya tufikiri otherwise! Sidhani kama roho yake inamwambia kama anafanya jambo jema huku mamilioni ya wananchi wakiugua bila dawa mita chache toka hapo Nyamagana alipokuwa. Ufalme wa Mungu ni kazi kuufikia kwa namna hii.
 
NL, mnaweza kuwa na hili tatizo la kutumia IE. Mkiweza basi tumieni Firefox kama ni computer zenu. Na kama mnatumia hiyo Firefox basi mnaweza kuwa kwenye options kuna kitu mnazuia. Kama ni Laptop, nafikiri Max Mello na vijana wake huwa wanasaidia sana kama uko Dar.
......nilifikiri pekee yangu naona maluweluwe.......!
 
NL, mnaweza kuwa na hili tatizo la kutumia IE. Mkiweza basi tumieni Firefox kama ni computer zenu. Na kama mnatumia hiyo Firefox basi mnaweza kuwa kwenye options kuna kitu mnazuia. Kama ni Laptop, nafikiri Max Mello na vijana wake huwa wanasaidia sana kama uko Dar.

Nafikiri ni sababu ya kuzuia.......!
 
Kama kuna mtu ana email ya F.Mbasha atuwekee hapa, tumtumie ujumbe Mahususi maana hajui alitendalo; ameniboa sana na Music Pack zake sinunui tena!!
 
Niko Bongo, Mbeya in particular for a vacation kwa hali ya mambo jinsi ilivyo huku huyu mtu hawezi kuja kufanya mambo kama haya huku kwanza anajiuliza hata kuja kwenyewe
 
hivi, mnachukizwa na nini haswa? vijana kusherekea na kuonyesha furaha yao? kwa vile bado wanafunzi wasiwe na any preferences whatsoeva? mimi ninachokiona kwenye hii clip ni nyuso za furaha! kila mtu yuko entitled to his/her opinion hata kama bado mwanafuzi kuita upuuzi huu tena ni kusimanga watu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom