Hazina Haina Mpunga. Imefulia. Inapumulia Mashine

Pesa zipo tena nyingi

Wanajaribu kutupotezea na hiyo issue ukizingatia sasa hv Kwenye akili zetu kumejaa hili neno DOWANS.

Toka lini serikali ikaishiwa??
 
Naomba niamini hii kama taarifa na sio tetesi kwa sababu moja hii hapa Chini.
Hivi majuzi nimesikia serikali itawalipa watumishi wake dirishani ili kubaini watumishi hewa!

MY TAKE:
Hazina itakua haina hela za kutosha so wameamua kupunguza zigo la kulipa na watumishi hewa, Kumbe walikua wanajua kuna watumishi hewa wanakujla mshahara?
Mkiona hivyo jueni kweli fungu la mshahara hautoshi. Nawashauri mtakaolipwa dirishani muwahi foleni kwasababu unaweza kuwa kwenye foleni ukasikia mapesa yameisha.

SWALI:
Hivi hzi foleni zitakua ndefu kama zile za NMB mwisho wa Mwezi?

Taarifa mbaya sana kwa benki ya makabwela NMB maana biashara yao kubwa ni kulipa mishahara ya watumishi wa serikali
 
kwenye council ndo mbaya zaidi makandarasi wanandai acha mchezo. umeshamsikia tena magufuli siku izi? atampigia nani kelele wakati serikali inadaiwa?
 
Ni kweli bajeti zimekatwa kwa aslimia 40. Lakini hakuna cha kushangaza kama rcs na dcs wanapewa handshake ya 40 million kila mmoja nje ya sheria ya mafao ya wastaafu unatarajia nini. Mwanzo cag alipinga hili lakini kanywea. Dhuluma kila mahali. Binafsi nimeanza ku question uthabiti wa utto.

Hayo ni mapungufu ya Katiba yetu ndugu yangu huyu Utto unamwonea bure tu. Hawezi kuzuia malipo kama yameamriwa na Rais wa Jamhuri ambaye kimsingi ndiye mwajiri "appointing authority" wake.
 
WAna JF , kuna uvumi kuwa HAZINA IMEKAUKA, na BUDGET ZILIZOPITISHWA ZINATAKIWA KUKATWA KWA ASILIMIA NYINGI. Hizi taarifa zimezagaa kila kona nchini......Je, watoto wetu watasoma tena wakati tunalipa ada kwa installments? Je, familia zetu zitaendelea kuwepo?

tafadhali mwana jamii yeyote mwenye news atujuze.

Haitaji kusoma sana Uchumi kuelewa hili, kama kuna mgao wa umeme maana yake less production, shughuli za biashara kupungua, kodi kupungua, TRA watakusanya chini ya target na BOT kukusa mapato.

Tulishasema tunahitaji serikali Mpya, yenye watu abunifu lakini .... tumechagua walewale na mambo yaleyale tunategemea nini?
 
Inawezekana hakuna peza kwa sababu zilitumika sana wakati wa kampeni au ni danganya toto ili waweze hata kuarisha kikao cha bunge february 8 kukwepa mjadala wa DOWANs, au kuhamisha mawazo ya walalahoi kutoka Dowans mpaka serikali haina hela tufanye kazi kwa bidii
 
Pesa zipo tena nyingi

Wanajaribu kutupotezea na hiyo issue ukizingatia sasa hv Kwenye akili zetu kumejaa hili neno DOWANS.

Toka lini serikali ikaishiwa??

Ya IDI Amin DADA ilifisika akamwelekeza MALYAMUNGU (GOVERNOR) atengeza fedha zikawa kama toilet paper.
 
Machungu nimeshaanza kuyaona...., nimeagiza mzigo from abroad ushuru 40,000/= Customs wamekadilia eti inabidi nilipe 400,000/= ; palikuwa hapatoshi... nimewapelekea evidence zote na gharama za mzigo....., Hawa watu watatukamua hata kile ambacho hatuna...
 
Election campain 2010. Ndiyo maana wanataka hizo za Dowans zilipwe haraka ili wapate mishahara. nahisi walikopa hela nyingi sana kwa lostam na ER. Sasa anawadai kwa kasi ya ajabu sana
 
inawezekana fedha zimeisha kwqeli, na zitakuwa zimeisha wakati wa kampeni, maana hali ilivyokuwa ngumu fedha nyingi za wilayani na mikoani ziliitwa kwenda kufanya kampeni, na kuna miradi mingi sana imesimama kwa kukosa fedha ambazo zilishapelekwa huko
 
Hakuna uthibiti na nidhamu ya matumizi ya Fedha serikalini..,serikali imekuwa kama ufalme wa Kambare kila mtu sharubu,kila mwenye upenyo anakomba,matumaini yanabaki kwa wabunge je wataweza kuibana serikali kuelezea wapi fedha zinakwenda ? na kuwawajibisha watendaji wabadhirifu??? wacha tusubiri tuone ila hali ya kifedha ni mbaya..

Mkuu hapo kwenye RED!

Naomba nitofautiane na wewe; hawa wabunge wetu wote hawana tofauti na wengine walioko serikalini. Wao upiga kelele lakini ikifika kwenye kujadili mafao yao utaona maajabu, si Cuf, Ccm, Chadema, Tlp, Udp wala Updp wote uungana pamoja na kujinoneshea malipo yao bila kuangalia sie wenye nchi tuna hali gani.

Nitakuwa si muungwana kama nitashindwa kumtoa mmoja tu ambaye ni Dr. Slaa na peke yake ndiye aliwahi kusima kupinga pesa lukuki wanazojilipa wawakilishi wetu! Labda tutapata mrithi wake bungeni.

Kwahiyo ndugu yangu, usiweke imani kubwa kwa hawa wabunge wetu. Ufujaji wa mali za nchi si kwenye wizara tu, hata uko kwao bungeni ni yale yale.

Hii ya malipo ya wabunge nayo tutaianzishia thread yake!
 
Hakika hali ni mbaya
Mpaka tarehe ya leo mishahara ya watumishi haijalipwa
miradi mingi ya maendeleo ktk Halmashauri imesimama hakuna fedha
mafungu ya kuendeshea serikali kwa matumizi ya kawaida OC hazijatolewa
toka Novemba

Hakika tutakula majani mwaka huu!!!!
 
mimi mwenyewekuna jamaa yangu anafanya kazi,ni katibu wa wilaya amekwenda mkoani kuchukua check kakuta watu wanalia ile mbaya bajet imepunguzwa sana,ila mishahara iko pale pale na italipwa kwa taabu kwelikweli ndugu zanguni
 
Wala sitashangaa kwani si mnajua hii nji ilivyoshamba la bibi? Kila mtu anachuma tu!
 
Haya mnaolipwa na serikali mbona mko kimya? si ndio tarehe zenyewe hizi? tujuzeni tujue jinsi ya kujibana ili tugawane tulichonacho

Mishahara bado haijalipwa.Katika miezi ya hivi karibuni serikali ili jitahidi kuwa makini,ila mwezi huu naona kama kuna matatizo kidogo,tusubiri tuone.
 
kwenye council ndo mbaya zaidi makandarasi wanandai acha mchezo. umeshamsikia tena magufuli siku izi? atampigia nani kelele wakati serikali inadaiwa?

Sheria ya manunuzi ya umma hairuhusu taasisi yoyote kuingia mkataba wa manunizi kama haina bajeti ya kufanya hivyo; maana yake kama Halmashauri zinadaiwa kuna mahali pesa zimetumika vibaya tofauti na zilivyopangwa kwenye bajeti
 
Back
Top Bottom