Hazina Haina Mpunga. Imefulia. Inapumulia Mashine

Halafu utaambiwa tumepiga hatua kiuchumi, eti uchumi wetu umepanda. Hazina kuishiwa ni sawa maana walikuwa wanachota kama wehu kununua na kulisha watu wali ili wachaguliwe. Sikilizia vat na kodi zingine coming june kwenye bajeti, ful maumivu.
 
Habari za chini ya kapeti zinaelezwa kuwa Ofisi ya Bwana Mkulo haina fedha. Imefulia na hali ya nchi kifedha ni tete.

Wakati huo wahisani hawana habari na wala hawataki kusikia nchi iliyotumia mamilioni ya pesa kutundika mabango ya kampeni ya JK, kuchakachua matokeo na upuuzi mwingine uliogharimu mabilioni ya pesa za kodi za wananchi eti leo inalia njaa.

Habari ndiyo hiyo.

Source please hatutaki umbea humu
 
Habari za chini ya kapeti zinaelezwa kuwa Ofisi ya Bwana Mkulo haina fedha. Imefulia na hali ya nchi kifedha ni tete.

Wakati huo wahisani hawana habari na wala hawataki kusikia nchi iliyotumia mamilioni ya pesa kutundika mabango ya kampeni ya JK, kuchakachua matokeo na upuuzi mwingine uliogharimu mabilioni ya pesa za kodi za wananchi eti leo inalia njaa.

Habari ndiyo hiyo.

Maajabu hayatakoma! Halafu bajeti ya 2011/2012 itaongezeka ukilinganisha na 2010/2011, ba bado wabunge wataiunga mkono kwa 100% bila maelezo ya kutosheleza kwa nini mapato ya bajeti ya 2010/2011 hayakufikiwa kama ilivyotarajiwa (tena kwa asilimia kubwa)
 
Naomba niamini hii kama taarifa na sio tetesi kwa sababu moja hii hapa Chini.
Hivi majuzi nimesikia serikali itawalipa watumishi wake dirishani ili kubaini watumishi hewa!

MY TAKE:
Hazina itakua haina hela za kutosha so wameamua kupunguza zigo la kulipa na watumishi hewa, Kumbe walikua wanajua kuna watumishi hewa wanakujla mshahara?
Mkiona hivyo jueni kweli fungu la mshahara hautoshi. Nawashauri mtakaolipwa dirishani muwahi foleni kwasababu unaweza kuwa kwenye foleni ukasikia mapesa yameisha.

SWALI:
Hivi hzi foleni zitakua ndefu kama zile za NMB mwisho wa Mwezi?

Hili la kulipia dirishani ni janja nyingine ya watu kuweza kudraw pesa nyingi in cash in excess ya mishahara yenyewe. Lengo ni kupata fedha za kulipia madeni ya kampeni na ahadi kibao za First Lady na Riziwani wakati ule wakijifanya kutuliza migogoro ya wana CCM. maana silaha yao kubwa ilikuwa ni cash, sasa watapata wapi zaidi ya kuja na mbinu hii ya hovyo?
Tafakari
 
Mungu anaipenda tanznaia na sasa anataka kuikomboa.kama Mungu amepanga kuifuta serikali ya jk basi kila mti utateleza hawataweza kukimbilia popote. Hatakama watu watavumilia shida zote ngumu Mungu bado atashuka na mapigo ambayo hamtaweza kuvumilia zaidi bali mtatii kuingia barabarani kuiong'oa serikali. Tuombeni Mungu ili mapenzi yake yatimie.

Umenena.....hakuna kitu kitakachowaamsha wa TZ zaidi ya hali ngumu ya maisha. Kwa speed hii ya uporaji, ukombozi uko karibu....
 
Nasikia JWTZ huwa wakihitaji hela wanaenda TRA moja kwa moja kuzichukua, hawasubiri hazina wala wizarani!
Kwani wao ni kina nani mpk wawe wanakiuka taratibu za kibajeti??
C'mon lets not complicate them their service is mere like other services for this nation like Hospitals,Police,Mamlaka ya Maji,Tanesco etc
 
Na bado more to come. Hasira mpaka mtu unabaki kutazama tu
 
Haya mnaolipwa na serikali mbona mko kimya? si ndio tarehe zenyewe hizi? tujuzeni tujue jinsi ya kujibana ili tugawane tulichonacho
Wfanyakazi wa serikali si huwa wanalipwe tarehe 40, sasa hivi hawawezi kujua kama mshahara utakuwepo au? mpaka ikifika tarehe 40 Februery ndipo wataweza kujua kama mwezi huu wamejitolea.
 
Habari za chini ya kapeti zinaelezwa kuwa Ofisi ya Bwana Mkulo haina fedha. Imefulia na hali ya nchi kifedha ni tete.

Wakati huo wahisani hawana habari na wala hawataki kusikia nchi iliyotumia mamilioni ya pesa kutundika mabango ya kampeni ya JK, kuchakachua matokeo na upuuzi mwingine uliogharimu mabilioni ya pesa za kodi za wananchi eti leo inalia njaa.

Habari ndiyo hiyo.

Huna tofauti na Gazeti la udaku la Tanzania Daima, hela zipo na mipango ya serikali inaendelea kama kawa. Na ukitaka kujua kuwa pesa ziko mpaka sasa bunge limeisha pewa pesa zake za kikao kijacho, wakandarasi wa barabara wanalipwa, mahakama inatayarishiwa pesa za kuendesha shughuli zao nk
 
Naam, nimepata taarifa kwamba wizara zimeagizwa kurevise bajeti zao ili kupunguza between 40% hadi 70%. ruzuku za halimashauri kwa idara kadhaa za quaerter ya pili hazijatumwa.

Nimepata taarifa, za uhakika, kwamba wafadhili vihoro juu. Imani yao kutoa pesa kwa serikali kupitia GBS imewatokea puani. Hofu yao ni kwamba, kama pesa zimefujwa, ajira zao zitaingia matatani. Kwa maneno ya mmojawao "Paris Declaration has exploded at a time when our gov at home are challenged to cut foreign aid"

kwamba ile donor cut ya mwaka jana ilitokanana baadhi yao kuwa tayari walishasikia harufu mbaya. Donors wachache walijitoa kwenye GBS 2010/11 na wengine tayari wanajiandaa kujiondoa 2011/12. Kutokana na mdororo wa uchumi, wananchi wa nchiwahisani wanashinikiza serikali zao kupunguza misaada kwa nchi masikini fisadi.

Kama kweli serikali ya tz imefuja pesa na habari hizi zikawa hadharani, basi uwezekano wa misaadakupungua mwaka wa fedha ujao ni mkubwa. Kama misaada ikipungua, ajira za baadhi yawazungu Hapa tz zitakoma. Can they, then, become partners in crime?
 
Back
Top Bottom