Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
Nimefuatilia kwa karibu sana Tangazo linalorushwa na REDIO CLOUDS linalowahamasisha wapenzi wa CHADEMA kukichangia chama hicho nami nikiwa miongoni mwa wakereketwa wa kuchangia chama hiki ambacho kinaonekana kuja juu sana katika medani ya kisiasa. Lakini kilichonishangaza Kipande cha wimbo wa Taifa ndani ya tangazo hili.
Je ni sahihi chama cha siasa kutumia wimbo wa Taifa kujitangaza wakati wimbo wa Taifa ni chombo cha mali serikali na kwa maana hiyo ni mali ya vyama vyote vya siasa? Haya si matumizi ya mali za serikali kwa ajili chama kujipatia umaarufu?
Watanzania tunajua na tumezoea kuusikia wimbo wa Taifa Wkati Kiongozi mkuu wa Nchi akihutubia, wakati kuna sherehe za kitaifa, wakati kuna taarifa mbaya inatolewa na Mkuu wa nchi kama ilivyokuwa wakati tunaarifiwa kifo cha baba wa Taifa na vile vile wakati nchi inatangaziwa hali ya hatari kama vita n.k
Iweje leo wimbo wa Taifa uchezewe na vyama vya siasa kujitafutia umaarufu tena kwa kuwahadaa wananchi kuwa wananchangisha pesa za kuendeleza chama wakati pesa hizo zinapotelea kwenye matumbo ya wachache.