Haya si matumizi ya mali za serikali kwa manufaa ya chama?

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Nimefuatilia kwa karibu sana Tangazo linalorushwa na REDIO CLOUDS linalowahamasisha wapenzi wa CHADEMA kukichangia chama hicho nami nikiwa miongoni mwa wakereketwa wa kuchangia chama hiki ambacho kinaonekana kuja juu sana katika medani ya kisiasa. Lakini kilichonishangaza Kipande cha wimbo wa Taifa ndani ya tangazo hili.

Je ni sahihi chama cha siasa kutumia wimbo wa Taifa kujitangaza wakati wimbo wa Taifa ni chombo cha mali serikali na kwa maana hiyo ni mali ya vyama vyote vya siasa? Haya si matumizi ya mali za serikali kwa ajili chama kujipatia umaarufu?

Watanzania tunajua na tumezoea kuusikia wimbo wa Taifa Wkati Kiongozi mkuu wa Nchi akihutubia, wakati kuna sherehe za kitaifa, wakati kuna taarifa mbaya inatolewa na Mkuu wa nchi kama ilivyokuwa wakati tunaarifiwa kifo cha baba wa Taifa na vile vile wakati nchi inatangaziwa hali ya hatari kama vita n.k

Iweje leo wimbo wa Taifa uchezewe na vyama vya siasa kujitafutia umaarufu tena kwa kuwahadaa wananchi kuwa wananchangisha pesa za kuendeleza chama wakati pesa hizo zinapotelea kwenye matumbo ya wachache.
 
Matumizi mabaya ya mali za Serikali kwanza anza na chama kilichoko madarakani otherwise akili yako inaonekana tu kama nazi za pale magogoni
 
Nimefuatilia kwa karibu sana Tangazo linalorushwa na REDIO CLOUDS linalowahamasisha wapenzi wa CHADEMA kukichangia chama hicho nami nikiwa miongoni mwa wakereketwa wa kuchangia chama hiki ambacho kinaonekana kuja juu sana katika medani ya kisiasa. Lakini kilichonishangaza Kipande cha wimbo wa Taifa ndani ya tangazo hili.
Je ni sahihi chama cha siasa kutumia wimbo wa Taifa kujitangaza wakati wimbo wa Taifa ni chombo cha mali serikali na kwa maana hiyo ni mali ya vyama vyote vya siasa? Haya si matumizi ya mali za serikali kwa ajili chama kujipatia umaarufu?
Watanzania tunajua na tumezoea kuusikia wimbo wa Taifa Wkati Kiongozi mkuu wa Nchi akihutubia, wakati kuna sherehe za kitaifa, wakati kuna taarifa mbaya inatolewa na Mkuu wa nchi kama ilivyokuwa wakati tunaarifiwa kifo cha baba wa Taifa na vile vile wakati nchi inatangaziwa hali ya hatari kama vita n.k. Iweje leo wimbo wa Taifa uchezewe na vyama vya siasa kujitafutia umaarufu tena kwa kuwahadaa wananchi kuwa wananchangisha pesa za kuendeleza chama wakati pesa hizo zinapotelea kwenye matumbo ya wachache.
Hujui usemalo, wimbo wa taifa hutumiwa na yeyote
 
Kwa tafsiri yako hii, wimbo wa taifa ni mali ya matukio makubwa ya taifa, kama kifo tena cha viongozi wakuu, sherehe za uhuuru, hotuba ya raisi. Naamini tafsiri hii umeipata kutokana na mazoea tu. Huu umekuwa ni utamaduni. Nikupe mfano: Kuna mama mmoja, kila mwaka wakati wa sikukuu ya Krismasi alikuwa hupika nyama ya kuku kwenye sufuria mbili.

Mtoto wake wa kike alizaliwa na akakua akimwona mama yake akifanya hivyo. Na yeye alioolewa alitafuta sufuria za ukubwa ule ule kwa ajili ya kupikia nyama wakati wa Krismas. Siku moja mama yake alimtembelea wakati wa sikukuu ya Krismas. Baada ya kumwona mtoto wake akihangaika kuwasha majiko mawili kwa ajili ya kupika nyama ya kuku, alimuuliza kwa nini unapika nyama kwenye sufuria mbili?

Yule mtoto alijibu, nilikuona wewe ukifanya hivyo katika maisha yangu yote nikiwa nyumbani. Mama yake akamwambia, "Mwanangu, mimi nilifanya hivyo kwa kuwa sikuwa na sufuria kubwa na uweza wa kununua sufuria kubwa sikuwa nao. Sasa wewe unasufuria kubwa nyingi usihangaike."

Stori hii inafanana sana na tafsiri yako ya wimbo wa taifa. Wimbo wa taifa si wa raisi,si ishara ya kifo cha kiongozi wa ngazi ya juu. Wimbo wa taifa ni sala ya taifa, ni wa kila mwanataifa la Tanzania. Ndiyo hasa, kitambulisho chetu, ndiyo unaoweza kuonesha umoja wetu, ndiyo unaoshuhudia utu wetu wa kitaifa, na mshikamano wetu.
 
Nimefuatilia kwa karibu sana Tangazo linalorushwa na REDIO CLOUDS linalowahamasisha wapenzi wa CHADEMA kukichangia chama hicho nami nikiwa miongoni mwa wakereketwa wa kuchangia chama hiki ambacho kinaonekana kuja juu sana katika medani ya kisiasa. Lakini kilichonishangaza Kipande cha wimbo wa Taifa ndani ya tangazo hili.
Je ni sahihi chama cha siasa kutumia wimbo wa Taifa kujitangaza wakati wimbo wa Taifa ni chombo cha mali serikali na kwa maana hiyo ni mali ya vyama vyote vya siasa? Haya si matumizi ya mali za serikali kwa ajili chama kujipatia umaarufu?
Watanzania tunajua na tumezoea kuusikia wimbo wa Taifa Wkati Kiongozi mkuu wa Nchi akihutubia, wakati kuna sherehe za kitaifa, wakati kuna taarifa mbaya inatolewa na Mkuu wa nchi kama ilivyokuwa wakati tunaarifiwa kifo cha baba wa Taifa na vile vile wakati nchi inatangaziwa hali ya hatari kama vita n.k. Iweje leo wimbo wa Taifa uchezewe na vyama vya siasa kujitafutia umaarufu tena kwa kuwahadaa wananchi kuwa wananchangisha pesa za kuendeleza chama wakati pesa hizo zinapotelea kwenye matumbo ya wachache.

Serikali ni nani? Au hiyo Tz ni ya nani? Tumia akili
 
Wimbo wa taifa si wa raisi,si ishara ya kifo cha kiongozi wa ngazi ya juu. Wimbo wa taifa ni sala ya taifa, ni wa kila mwanataifa la Tanzania. Ndiyo hasa, kitambulisho chetu, ndiyo unaoweza kuonesha umoja wetu, ndiyo unaoshuhudia utu wetu wa kitaifa, na mshikamano wetu.

Ni kweli kwamba wimbo wa Taifa ni mali ya watanzania lakini mbona hujasema kwa upande wa vyama vya siasa, je vinaruhusiwa kutumia? Kwa upande wangu ninatambua kuwa wimbo wa taifa ni moja ya alama za kitafa (National symbols) zingine zikiwa ni Nembo (Court of arms) na Bendera (National flag). Kama ambavyo huwezi kuona bendera ya taifa ikipepea katika ofisi za vyama vya siasa hasa ambavyo havijaunda serikali ndiyo inavyotakiwa kuwa hata kwa wimbo wa taifa.
 
Kumbe wimbo amabao unahimiza umuhimu wa umoja na amani kwa africa na nchi yetu? wewe hushangai mali za serikali kama magari, ofisi,nk zinavotumiwa na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi kufanyia kampeni za CCM???mawaziri ambao kisheria ni watumishi wa umma na wanalipwa na serikali kutokana na kodi zetu wameacha ofisi za umma na kwenda kufanya kampeni za CCM Arumeru muda ambao wanatakiwa wawe ofisini wanafanya kazi za umma??Hizi ndizo rasilimali za serikali zinazotumika vibaya!!
 
Kwa tafsiri yako hii, wimbo wa taifa ni mali ya matukio makubwa ya taifa, kama kifo tena cha viongozi wakuu, sherehe za uhuuru, hotuba ya raisi. Naamini tafsiri hii umeipata kutokana na mazoea tu. Huu umekuwa ni utamaduni. Nikupe mfano: Kuna mama mmoja, kila mwaka wakati wa sikukuu ya Krismasi alikuwa hupika nyama ya kuku kwenye sufuria mbili. Mtoto wake wa kike alizaliwa na akakua akimwona mama yake akifanya hivyo. Na yeye alioolewa alitafuta sufuria za ukubwa ule ule kwa ajili ya kupikia nyama wakati wa Krismas. Siku moja mama yake alimtembelea wakati wa sikukuu ya Krismas. Baada ya kumwona mtoto wake akihangaika kuwasha majiko mawili kwa ajili ya kupika nyama ya kuku, alimuuliza kwa nini unapika nyama kwenye sufuria mbili? Yule mtoto alijibu, nilikuona wewe ukifanya hivyo katika maisha yangu yote nikiwa nyumbani. Mama yake akamwambia, "Mwanangu, mimi nilifanya hivyo kwa kuwa sikuwa na sufuria kubwa na uweza wa kununua sufuria kubwa sikuwa nao. Sasa wewe unasufuria kubwa nyingi usihangaike."
Stori hii inafanana sana na tafsiri yako ya wimbo wa taifa. Wimbo wa taifa si wa raisi,si ishara ya kifo cha kiongozi wa ngazi ya juu. Wimbo wa taifa ni sala ya taifa, ni wa kila mwanataifa la Tanzania. Ndiyo hasa, kitambulisho chetu, ndiyo unaoweza kuonesha umoja wetu, ndiyo unaoshuhudia utu wetu wa kitaifa, na mshikamano wetu.
ongera sana kwakutoa elimu ya bure,atakua amekuelewa yule mweu.
 
Ni kweli kwamba wimbo wa Taifa ni mali ya watanzania lakini mbona hujasema kwa upande wa vyama vya siasa, je vinaruhusiwa kutumia? Kwa upande wangu ninatambua kuwa wimbo wa taifa ni moja ya alama za kitafa (National symbols) zingine zikiwa ni Nembo (Court of arms) na Bendera (National flag). Kama ambavyo huwezi kuona bendera ya taifa ikipepea katika ofisi za vyama vya siasa hasa ambavyo havijaunda serikali ndiyo inavyotakiwa kuwa hata kwa wimbo wa taifa.

Bendera ya taifa mbona matrja wanavaa kichwani, afterall wimbo wa taifa xaxa vyama vya siasa si sehemu ya Taifa?. Well ni mali ya serikali, serikali ni nani sasa kama sio wananchi na Rais ni kiongozi mkuu
 
Ni kweli kwamba wimbo wa Taifa ni mali ya watanzania lakini mbona hujasema kwa upande wa vyama vya siasa, je vinaruhusiwa kutumia? Kwa upande wangu ninatambua kuwa wimbo wa taifa ni moja ya alama za kitafa (National symbols) zingine zikiwa ni Nembo (Court of arms) na Bendera (National flag). Kama ambavyo huwezi kuona bendera ya taifa ikipepea katika ofisi za vyama vya siasa hasa ambavyo havijaunda serikali ndiyo inavyotakiwa kuwa hata kwa wimbo wa taifa.
Je vyama vya siasa ni vya nani? Je ni vya wamarekani? Kama vyama vya siasa ni vya Watanzania, je havimilikiwi na serikali ya Tanzania? Kwa nini basi vinapewa ruzuku na serikali ya Tanzania? Acha kujichanganya. Kama dhumuni lako ni kutaka kujua kwa nini chadema wanatumia wimbo wa taifa nimeshakupa jibu. Ukiendelea wenyewe wapo, utaona.
 
Mtoa mada umepotelea wapi..? Jibu hoja hizo au kama umekubaliana nao pia useme, halafu swala la matumizi ya fedha za michango kwa matumbo ya viongozi hilo unapaswa kulitolea ufafanuzi ni lini na wapi na kiasi gani kilitumika kwenye matumbo na si kazi za chama kama inavyokusudiwa.
 
Mtoa mada naomba ukajipange upyaaaaaaaaaaaaaaaaaaa....huna dira wala mwelekeo wa mada yako hiiiiiii ya KIJIMA...

KWAHERI
 
mimi kila nikiaamka lazma niimbe mwimbo wa taifa langu kama wewe unauogopa inaonekana wewe sio mtz
 
Hili la kutumia wimbo wa Taifa kwenye vyama vya siasa naona kuna haja ya kuliangalia..
 
Tuacheni ushabiki wa kisiasa; kwa kuzingatia elimu tulonazo matumizi ya wimbo wa Taifa sina shaka kila mmoja anayafaham; sidan kama chama binafsi kinaruhusiwa kutumia wimbo wa Taifa kwa sababu zao tofauti si CCM wala CDM labda uwe ni utaratibu mpya na kama ndivyo basi tunakoelekea tutaanza kuutumia hadi kwenye kumbi za starehe na kama haitoshi ataibuka mtu atataka aufanyie remix na kuachia single yake; na mwingine (Njeree) ataibuka na bendera ya taifa ajifunge rubega akate kitaa la hasha tunapotoka"
 
Back
Top Bottom