Falsafa ya 4R inavyombeba Rais Samia

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,675
59,775
1705490652434.png

MIAKA mitatu tangu Rais Samia Suluhu Hassan akabidhiwe kijiti cha kuiongoza Tanzania wadau wa demokrasia wanaielewa falsafa yake ya 4R yaani maridhiano, ustahamilivu, mageuzi na kujenga upya.

Wakati akikabidhiwa kijiti Machi 2021, Rais Samia alisitiza dhamira yake ya kuijenga Tanzania moja yenye ustawi kwa wananchi wote na mara zote wito wake umekuwa kutaka kujenga jamii yenye maelewano, umoja na mshikamano, uzalendo, maridhiano, ustahamilivu na yenye uchumi unaokua kwa wote.

Rais Samia anasema ataj i tahidi kuf anya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria za uchaguzi ili Tanzania iende na wakati na kutoa fursa zaidi kwa watu wengi kunufaika kiuchumi.

“Tutajitahidi kuijenga Tanzania yenye haki, demokrasia na usawa na mafanikio na ndiyo maana katika kipindi hiki tulikuja na ‘idea’ nne (akimaanisha maridhiano, ustahamilivu, mabadiliko na kujenga upya)…vyama vya siasa tunazungumza, tunaelewana,” anasema Rais Samia.

Katika mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam 4R ilikuwa moja moja ya mada iliyojadiliwa ambapo wadau mbalimbali wa demokrasia wameeleza namna walivyozielewa.

Taifa Tanzania Page 10_page-0001.jpg
 
Unaweza ukasoma hapa kwa undani zaidi
 
Attachments

  • Taifa Tanzania Page 10.pdf
    289.3 KB · Views: 4
..Ni ulaghai mtupu.

..Kama kuna 4R kwanini anataka kutumia Jwtz dhidi ya Chadema?

..Samia angekuwa anaamini ktk 4R asiwateua watu waliohusika na makandokando ya utawala wa Jpm.
 
..katika ufafanuzi wote huu sijaona neno HAKI!!

Tindo, Pascal Mayalla
NAMNA GANI HAKI INAWEZA KUPATIKA KUTOKANA NA FALSAFA YA 4R

1. Reconciliation (Maridhiano):
- Kupitia maridhiano, jamii inaweza kusonga mbele kutoka kwenye migogoro ya zamani na kujenga mazingira ya amani. Kukuza maridhiano kunaweza kuleta upatanishi kati ya makundi yanayokumbana na migogoro ya kisiasa, kijamii, au kitamaduni.

2. Resilience (Ustahimilivu):
- Ustahimilivu wa kijamii unaweza kujenga mazingira ambayo jamii inaweza kukabiliana na changamoto bila kuvunja misingi ya haki. Kusaidia jamii kuwa na uwezo wa kurejea na kujikwamua kutokana na mizozo na matatizo inaweza kusaidia kudumisha haki.

3. Reform (Marekebisho):
- Marekebisho ya miundo ya kisheria na kisiasa yanaweza kuleta haki na usawa. Kupitia marekebisho, serikali inaweza kuboresha utawala wa sheria, kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote, na kusimamia haki za binadamu.

4. Rebuild (Ujenzi Upya):
- Ujenzi upya wa jamii unaweza kutoa fursa ya kuhakikisha kuwa haki inazingatiwa katika kila hatua. Kupitia ujenzi upya, jamii inaweza kuimarisha mifumo ya elimu, huduma za afya, na miundombinu, na hivyo kuhakikisha upatikanaji sawa wa rasilimali na fursa.

Kwa kuzingatia hayo, hapa ni jinsi falsafa ya 4R inaweza kuchochea mchakato wa kujenga haki nchini Tanzania:

1. Kusaidia Kupatikana kwa Haki:
- Mchakato wa maridhiano unaweza kusaidia katika kutatua migogoro na kutafuta suluhisho linalozingatia haki na usawa kwa pande zote.

2. Kuimarisha Mifumo ya Haki:
- Marekebisho ya miundo ya kisheria yanaweza kusaidia kuimarisha mifumo ya haki na kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa kila mwananchi.

3. Kutetea Haki za Wanyonge:
- Marekebisho na ujenzi upya wa jamii unaweza kutoa fursa za kuboresha haki za wanyonge, kama vile wanawake na vijana, na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo.

4. Kupinga Ubaguzi na Unyanyasaji:
- Marekebisho na ujenzi upya wa jamii vinaweza kuwa na lengo la kupinga ubaguzi na unyanyasaji, kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa kila mwananchi bila kujali hali yao.

5. Kukuza Usawa wa Kijinsia:
- Kupitia marekebisho ya kijamii na kiuchumi, falsafa ya 4R inaweza kusaidia kujenga mazingira yanayoshughulikia tofauti za kijinsia na kusaidia kufikia usawa wa kijinsia.
 
..hayo yote ni zao au tunda la HAKI.

..sasa Samia hataki haki, hata kuitamka tu hataki.
 
Labda nikuulize Bwana JokaKuu
Unaposema haki kwa upande wako una maana gani?
Je, unajua kuwa palipo na HAKI lazima kuwe na WAJIBU?
Je, kipi kinatngulia kati ya WAJIBU na HAKI?
 
..wewe uko katika biashara ya kupumbaza Watanzania.

..huu ujinga unaofanya munchie Abduli. At least yeye tunasema anatetea utawala wa Mama yake.

..kuwa Mzalendo. Tetea nchi yako.
 
Bado hujanijibu maswali langu. Naomba please unijibu kwa uelewa wako

Labda nikuulize Bwana @JokaKuu
Unaposema haki kwa upande wako una maana gani?
Je, unajua kuwa palipo na HAKI lazima kuwe na WAJIBU?
Je, kipi kinatngulia kati ya WAJIBU na HAKI?
 
Labda nikuulize Bwana JokaKuu
Unaposema haki kwa upande wako una maana gani?
Je, unajua kuwa palipo na HAKI lazima kuwe na WAJIBU?
Je, kipi kinatngulia kati ya WAJIBU na HAKI?

..HAKI ndio inatangulia yote.

..Ssh amelazimika kuja na 4R kwasababu watangulizi wake walivunja haki za wananchi.

..Nakushangaa sana jinsi neno HAKI linavyokusumbua.
 
1. Reconciliation (Maridhiano):
- Kupitia maridhiano, jamii inaweza kusonga mbele kutoka kwenye migogoro ya zamani na kujenga mazingira ya amani. Kukuza maridhiano kunaweza kuleta upatanishi kati ya makundi yanayokumbana na migogoro ya kisiasa, kijamii, au kitamaduni.

2. Resilience (Ustahimilivu):
- Ustahimilivu wa kijamii unaweza kujenga mazingira ambayo jamii inaweza kukabiliana na changamoto bila kuvunja misingi ya haki. Kusaidia jamii kuwa na uwezo wa kurejea na kujikwamua kutokana na mizozo na matatizo inaweza kusaidia kudumisha haki.

3. Reform (Marekebisho):
- Marekebisho ya miundo ya kisheria na kisiasa yanaweza kuleta haki na usawa. Kupitia marekebisho, serikali inaweza kuboresha utawala wa sheria, kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote, na kusimamia haki za binadamu.

4. Rebuild (Ujenzi Upya):
- Ujenzi upya wa jamii unaweza kutoa fursa ya kuhakikisha kuwa haki inazingatiwa katika kila hatua. Kupitia ujenzi upya, jamii inaweza kuimarisha mifumo ya elimu, huduma za afya, na miundombinu, na hivyo kuhakikisha upatikanaji sawa wa rasilimali na furs
Ujio wa Nchimbi ndio kifo cha 4R za mama.
4R au MUMU(Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko, Ujenzi Upya) ni sumu kwa wanamtandao.
 
..HAKI ndio inatangulia yote.

..Ssh amelazimika kuja na 4R kwasababu watangulizi wake walivunja haki za wananchi.

..Nakushangaa sana jinsi neno HAKI linavyokusumbua.
Hakuna sehemu nimesema neno haki linanisumbua. Hebu niambie haki ipi unaona wewe hapo umenyimwa?
 
Falsafa gani Kichefuchefu tu hata Ngonjera zina maana kuliko hizo R4.
 
..kwanini kwenye 4R haki haizungumziwi?
Haki ni matokeo baada ya utekelezaji wa 4R. 4R ni msingi na matokeo yake ni Taifa linalofuata Haki na Wajibu.

Kwa hiyo pale 4R philosophy itakapotekelezwa matokeo yake ni kujenga taifa linalosimamia Haki na Wajibu.
Kila haki inapotolewa mbele yake hutangulia wajibu.

Mfano: Mungu kakuumba upo na haki ya kula lakini upo na wajibu wa kufanya kazi. Ndio hata katika maandiko matakatifu yanasema

10 Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.” 2 WATHESALONIKE 3

Wewe hapo unataka upatiwe HAKI je, umetimiza wajibu gani?
 
Back
Top Bottom