Haya matamasha ya dini yanatupeleka wapi...???

kumbuka huuo uwanja wanalipia siyo bure, kuna spika na vipaza sauti wanalipia, kama uwanjani hakuwa umeme kuna mafuta ya jenereta, kuna mapambo ya uwanja yananunuliwa.
halafu kwa soko gani Tanzania la kuza kanda hadi aweze kurudisha gharama zote,

zamani ni zamani, zamani zipi unazoziongelea wewe za pontio pilato au?mbona kina makoma wanakuja huku mnalipa viingilio na wenyewe si wanaimba gospel? kwa ninin wasitumbuize bure.

binadamu anabadilika kutokana na mazingira yake. ndo maana sasa hivi wanapiga modern gospel ili hata wale waliokuwa hawapendi kusikiliza wasikilize.
Jocelyne. Hao Makoma unawatolea mfano hawajapona kwenye tuhuma za mtoa mada.Kama nao wanatumia huo mfumo unaolalamikiwa pia wana la kujibu..si ndiyo?kwa hiyo tusitumie mapungufu ya watu wengine kuhalalisha uchafu wetu.
 
Look. Wapo wanaotumia vipaji vyao vya kimuziki kuimba nyimbo za gospel. Hawa ni wanamuziki kama vile alivyo Lady Jay Dee. Banana Zoro etc. Ni muziki wake alivyoona kwa njia hii atapata mashabiki na itamlipa. Hata mzee mzima Remmy Ongala , na yule mwingine waliamua kubadili genre za muiziki wao. Kwa hiyo kusema bwana asifiwe ni utambulisho tu na salam kama zilivyo nyingine za Regge na Bongo Flavor . Airee , Yo yo yo etc. Hawa ni wafanya biashara wa muziki wa dini na hata wasambazaji wao hawajui
hata Bwana asifiwe ni nini. Ni wahindi na wana madhehebu yao.

Upande wa pili wa shilingi ni kuwa viko vikundi vya kwaya za makanisani ambao wao wanarekodi na kuimba purely kwa kumtukuza mungu. Wanaweza kuuza kanda zao au cd kwa ajili ya kuendesha kwaya lakini hata wasipouza bado kwaya zipo na zinaendelea kufanya kazi. Mfano mzuri ndio kwaya ulizozitaja ambazo zote ni za RC . Roman Catholic.

Hata mifumo yao ya uimbaji unafuata maelekezo ya kiturjia ya kikatoliki. Utaona mara nyingi wao hutumia kinanda zaidi kuliko magitaa kama zilivyo bendi au kwaya zinazojitemea. Labda uchezaji sasa ambao mwanzo haukuwepo , sasa upo ila nao sio wa Kiwanzenza kama wengine.

My take. Matamasha yaendelee kuwepo ili na hao waliotumia nguvu za mikono yao waweze kupata riziki ya kidunia. Angalia nguvu wanazotumia jukwaani na muda wanaotumia , pamoja na hela. Hii ni biashara halali na ndio maana akialikwa VIP hamna tatizo. Hawa wanafanya kueneza injili kwa kutumia muziki wao kama vile Bongo flavor wanavyopeleka ujimbe wao kwa jamii through that flavour.

Mtoa mada swala la injili kupatikana bure sijui kama lipo. Hao wanatangaza hiyo injili watakula , kunywa , kuvaa nini kama waumini hawakuchanga kwa mifumo mbali mbali. Sadaka, zaka, etc ndio kuchangia injili. Usione akina Kakobe , GeoDavy na mingurumo ya upako tele ukadhani wanpiga makelele hadi mapovu yanatoka bure. PESA, PESA PESA tuuu ndugu yangu.
 
Pamoja na kwamba wanaimba injili, lakini unatakiwa ujue ndio njia yao ya kuendesha maisha yao kwa hiyo lazima kuwe na kipato, kwa sababu kuna gharama ametumia mpaka kufika huko, nauli , vyombo kurekodi, kulipa waimbaji wanaomsaidia,
Kwenye biblia sikumbuki kitabu nikikumbuka nitakuambia , inasema kila mtu atakula mahali pake pa kazi, yani kutokana na kazi yake anatakiwa ale, ikiwa ni pamoja na hayo mapato.
ndo maaa hata kwa watumishi wa Mungu ni lazima tutoe sadaka, zaka ili na wenyewe waendeshe maisha yao.

Kweli kabisa, hata kama ni mambo ya kidini yote yanahitaji pesa. Kumbuka hata Biblia yenyewe haitolewi bure nayo pia si inauzwa?
 
Jamani sasa wasipo kusanya huo mshiko huo uwanja wa ccm kirumba wataukodi na nini?

Na hivyo vifaa vya muzic watavitoa wapi?

Na wao watakula muzic tu bila ugali?

any way ni mawazo yako endeleeni kujadili na kuchangia mada,
Badala tujiulize Kagoda atafungwa lini?,
mnaleta mambo ya watu Huyo mdada anatoza pesa kama yeye na wewe pia ukianzisha bureeeee its ok kuna watakao kuja na wapo ambao hawatakuja.
 
Jamani sasa wasipo kusanya huo mshiko huo uwanja wa ccm kirumba wataukodi na nini?

Na hivyo vifaa vya muzic watavitoa wapi?

Na wao watakula muzic tu bila ugali?

any way ni mawazo yako endeleeni kujadili na kuchangia mada,
Badala tujiulize Kagoda atafungwa lini?,
mnaleta mambo ya watu Huyo mdada anatoza pesa kama yeye na wewe pia ukianzisha bureeeee its ok kuna watakao kuja na wapo ambao hawatakuja.

Ni kwanini waende CCM kirumba..?? kuna viwanja vingapi vya wazi mitaani hata pale karibu na huo uwanja wa CCM kirumba kuna kiwanja cha furahisha cha wazi na wahubiri wengi huwa ndio wanatumia.
Kwani wanakwaya wengine kama wa makanisa ya wasabato na wale niliowaandika katika mada wao wanato/ama walitoa wapi vifaa...??
Suala ni kutumia dini kwa maana isiyo.. sasa itakuwaje mtu aachwe huku anaonekana kabisa anaelekea sehemu isiyo..??
 
Mkuu mwendapole,out of all huyu (post # 17) katoa majibu mujarab. Lakini hilo la kuwa na VIP kwenye tamasha la dini mimi sijaridhika nalo.dini inatambua uwepo wa VIP?..mbona wanalikwepa?
Mkuu tupo ukuraha mmoja, jamaa ameezea vizuri kabisa kuwa watu watumia mgongo wa injili kujinufaisha, hii hakuna tofauti na kuwapumbaza watu.
Pia hilo suala la kugawa viingilio na kuwepo na ma VIP wanalikwepa na hapo
ndio hasa panapokubaliana na maelezo ya mchangiaji wa hapo juu.
 
kumbuka huuo uwanja wanalipia siyo bure, kuna spika na vipaza sauti wanalipia, kama uwanjani hakuwa umeme kuna mafuta ya jenereta, kuna mapambo ya uwanja yananunuliwa.
halafu kwa soko gani Tanzania la kuza kanda hadi aweze kurudisha gharama zote,

zamani ni zamani, zamani zipi unazoziongelea wewe za pontio pilato au?mbona kina makoma wanakuja huku mnalipa viingilio na wenyewe si wanaimba gospel? kwa ninin wasitumbuize bure.

binadamu anabadilika kutokana na mazingira yake. ndo maana sasa hivi wanapiga modern gospel ili hata wale waliokuwa hawapendi kusikiliza wasikilize.
Kwanini wachague ama waende kwenye uwanja huo wa kulipia?? kuna viwanja vingapi vya wazi mitaani ambavyo ndio huwa vinatumiwa kila siku kwa mambo haya ya dini?? Wahubiri wanavitumia kila siku na hapo karibu huo uwanja wa CCM kirumba kuna kiwanja kikubwa sana tu cha wazi. Kwani wanakwaya wengine hivyo vifaa wao wanavitoa wapi..?? na hayo ya umeme na vitu vingine kwani kwa wanakwaya/wahubiri wao hawavitumii hivyo..?? kama hakuna soko la kanda zao kwanini wasifanye shughuli nyingine na dini ikawa ni sehemu ya huduma tu kama inavyotakiwa iwe..?? inamaana unakubaliana na wazo la kuifanya dini kuwa biashara..??
Ni wazi utakubaliana na mimi kuwa huu utamaduni wa kuwa na viingilio katika shughuli za kidini hasa haya mambo ya Nyimbo yameanza siku za hivi karibuni tu na ni vyema watu wakaamka bado mapema na kupinga hii kitu.
Kama wanataka namna ya kujiendesha waweke sadaka tu mwenye nacho atatoa na asiyenacho mungu atasaidia tu lakini wote wapate neno la mungu. Na sio kuweka mabaunsa milangoni na kuwagawa watu katika makundi wengine eti ni ma VIP na wengine ni mwenzangu na mimi..!!!
 
Nimekuwa nikisilikiza radio maria na kwa siku kadhaa kumekuwa na tangazo la tamasha ambalo limepangwa kufanyika mkoani mwanza na huyu Msanii wa nyimbo za injili Flora Mbasha akishikilikiana na wengine. Ni tamasha linalohusu uzinduzi wa album yake pamoja na video CD. Tamasha litafanyika katika uwanja wa CCM kirumba na kitu kinachonishangaza ni kuwa kutakuwa na kiingilio katika tamasha hili la nyimbo za injili...!! kana kwamba hiyo haitoshi viingilio vimegawanywa katika makundi mawili, kawaida ni sh 2000 na VIP ni sh 5000.
Wakuu kadri siku zinavyokwenda hii inaonekana kama ni kitu ya kawaida kabisa kwa hawa wasanii wa nyimbo za injili kufanya matamasha na kuweka viingilio.
swali ni kwamba je? Inamaana kuna VIP kwenye dini...????? na inamaana watu inabidi sasa watambue kuwa injili sasa haipatikani bure..?? Je hayo ndio maagizo ya maandiko matakatifu..?? mbona dini sasa imevamiwa..?? na hawa wasanii wenyewe wanavyofanya hizo performance zao siku hizi hakuna tofauti kabisa na hawa wanamuziki wa lingara/boringo kutoka congo ama FM academia, je hii ni sawa kwa nyimbo za injili?? naomba mnisaidie kwani nina maswali mengi kuliko majibu manake hawa wanajiita wasanii wa nyimbo za injili wa siku hizi ni balaa, especially huyu Lady amekuwa so deep in business kabisa katika dini, you can tell it quite easily.
I miss those moments enzi za Mwanza town kwaya, Ulyankulu Tabora, Upendo Kwaya na pia kulikuwa na wenzetu kule Arusha walikuwa wanaimba vizuri sana .
Nisaidieni maoni yenu, Rev Kishoka, Exaud, Mchungaji na wengine woote nawasubiria....

hapo umenena. ule mchiriku anaocheza na wachezashoo wake na mumewe unanipa shaka kama kuna Mungu pale. Sio Flora mbasha yule niliyemfahamu alipoanza na wimbo wake "vumulia"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom