Ni nani atusaidie Tanzania Kama Taifa katika Matamasha?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Nimekuwa Nikufuatilia Matamasha Mbali Mbali Ya Muziki Tanzania, Muziki wa Injili hata Ule wa Kizazi Kipya. Ni kiri wazi Kuwa Wapenzi wa haya Matamasha Wamekuwa Hawatendewi Haki kabisa Kabisa Kutokana na Gharama wanazo tumia Kuhudhuria haya Matamasha na Burudani wanayo pewa.

Hakuna Tamasha Tanzania Ambalo limewahi kuwapa watazamaji burudani ile Wanayo itegemea, kuanzia Sound, Mpangilio wa matukio, muda na vitu vingine.

Mfano Mkubwa Ni Tamasha LA MTOKO WA PASAKA lililo Andaliwa na WASAFI MEDIA. Hili ni Tamasha La Nyimbo za Injili Lililo wakutanisha Nguri wa Mziki wa Injili Nchi Tanzania, Malkia Rose Muhando na Christina Shusho. Ni Kiri Kwa Kusema Kuwa Limekuwa Tamasha BOVU, BAYA na La Kufedhehesha Kuliko Matamasha Mengi yaliyo wahi kufanyika Nchini.

Ukiangalia Ukubwa Wa Viingilio, Ukubwa wa Hawa wasanii na Ukubwa waandaji kulinganisha na walichotupatia Basi Niseme Tanzania Hadi sasa Hatuna Waandaaji wa Matamasha Tanzania Wanaoweza Kuandaa Tamasha Usijutie Gharama Ulizo Zitumia. Rose Muhando Alikuwa ni Main Artist na ndio Ana Beba Ukubwa Wa Tamasha La Leo kwa Wingi na Uzuri wa Nyimbo zake, Si Ajabu Kaaingia Na Kaimbia Nyimbo 3 tuuu kati ya Zote Alizo nazo, Baada ya Kutangaza hili Tamasha Kwa Miezi 2 anakuja Anaimba Nyimbo 3 na Masimango juu. Dada Rose Ulikuwa Umelewa? Dada Rose Unataka watu wakusaidiaje Kimaisha? Kama Unapewa Nafasi huwezi kuzitumia? Ina Fedhehesha Sana Na Kuhuzunisha Wengi hasa Ukubwa Wa Kiingilio watu walicho Kitumia.

Tangu Lini Tamasha likawa na Mgeni rasmi? Lengo huwa ni Nini? Tena Mgeni rasmi wa Kisiasa, Waandaji wa Matamasha Lengo Huwa Ni Nini kama Sio Kuharibu Tamasha? Uliwahi kuona wapi mwananchi wa Kawaida analipa Hela (Kiingilio) kwenda Kumuona Mwanasiasa? Tanzania Nchi Yangu ni Lini Wasanii Mtabadirika na Kuanza kufanya Vitu Vizuri?

Binafsi Sijawahi pata shida kwenda Kununua Ticket ili niingie kwenye Tamasha Lolote lile Tanzania kwasababu, Najua nitakuwa Disappointed Na Mambo Ya Kisiasa, Uandaji na Vitu vingine.

Wasafi Media Mmejiabisha Kama ambavyo Huwa Mnajiabisha Siku Zote. Dada Rose Muhando na Christina Shusho Mmeshusha Hadhi zenu kwa kiwango cha Juu kwa Kufanya Tamasha Bovu kuwahi Kutokea Nchini. Ma Mc’s wa Leo ni Wabovu wa hovyo kuliko wote, Nani Alisema Ukiwa Mtangazaji Lazima Uwe Mc? Kutangaza na kuwa Mc ni Vipaji Viwili Tofauti lakini miaka ya Hivi Karibuni Kila Mtangazaji anataka kuwa Mc mwishowe Wanaharibu Shughuli inakuwa Hovyo Kabisa.

Tamasha kama Linafanyika kwa zaidi ya Masaa 10 na Katika Hayo masaa 10 hakuna kinachofanyika zaidi ya Kuongea na Kurekebisha Mic basi Tanzania Hatuna Waandaaji Wa Matamasha. Hili Tamasha Limenikumbusha Ubovu wa Matamasha Mengine yote kuwahi kufanyika Tanzania. Si Wasafi Media, Si Clouds Media, Si EFM hakuna Mbabe wa Kuandaa Tamasha Tanzania. Imagine Katika Masaa 10 Main Artist Anaimba Nyimbo 3 anashushwa Na Mc
 
Tunashukuru umetusemea sie wengine tusioweza kuandika, mimi ni Muislam ila jana nilikua very excited kumuona Rose Muhando hasa ukizingatia alikua anatimiza miaka 20 kwenye game, pia nilikua very excited kumuona mwanamama mrembo mwenye sauti nzuri Christina Shusho ila walichotufanyia nikawahurumia waliolipa viingilio vyao,

Picha linaanza channel ya Wasafi inakata kata hakuna hata raha,

Mcs walikua wamepooza utasema wapo kwenye mfungo, hawakua na mvuto hata robo wa ushereheshaji (hii hujirudia rudia sana kwenye shughuli za Wasafi)

Camera setup ilikua mbovu, mbovu, mbovu tena,

Mpangilio wa Ratiba ulikua wa hovyo sana mambo yalienda shaghala baghala,

Mgeni rasmi akaharibu na siasa zake, katumia muda mwingi kuinadi serikali utadhani ni tamasha la serikali, mara mia mgeni rasmi wangewaweka viongozi wao wakubwa wa Dini kama Mwamposa au Nabii Mkuu ingevutia kuliko huyo Waziri na siasa zake,

Rose hakuonekana Meza kuu muda mrefu sijui alichelewa kuingia ukumbini au alikua anapiga kwanza masanga hadi alipofika jukwaani kila mtu alikua anamuona kama mende tu maneno kibaoooooo wakati ilikua siku yake alipaswa kuitumia kuonesha kweli title ya Queen ni sahihi kwake

Alinikera yule Mtumishi aliyeomba sadaka usiku wa saa 7 eti aziombee

Christina na yule shoga ake wa Rwanda nilipenda perfomance yao, mmama anaimba yule sikumtegemea,

Hongera zao kwa kufanikisha jambo lao.
 
Nime Cheka hapo kwenye sadaka
 
Huwa nawaambia watu kuliko utoe pesa yako ukaingie kwenye tamasha la muzik Tanzania ni heri uende night pub ukanywe bia zako na mziki wa dj ulewe urudi home... Bongo hawajui kuset vyombo vya mziki, hawajui kuset mic, hawajui kuset jukwaa, hawajui kupanga ratiba na events, hawajui kutumbuiza... Bongo hakuna Event Planners...
 
Bora ata sikwenda maana sijui ningefanyaje kupunguza machungu bora ata club unaeza kusepa na mrembo 🤣🤣🤣🤣
 
Mbele unakuta msanii anapumzi balaa. Anapiga nyimbo kumi+ kupumzika ni kunywa maji. Sasa huku Yo Yo na piga kelele zinakuwa nyingi sana.
 
Mbele unakuta msanii anapumzi balaa. Anapiga nyimbo kumi+ kupumzika ni kunywa maji. Sasa huku Yo Yo na piga kelele zinakuwa nyingi sana.
Tena hpo analazimisha mashabiki kuimba, mara mikono juu, mara twende kulia mara kushoto yn tafrani 😂😂
 
Nime Cheka hapo kwenye sadaka
Acha tu, saa 7 usiku bila haya anawaomba watu sadaka tena kajikausha hata hana tabasamu la aibu,
Pia nilisahau watu walianza kuondoka kabla hata tukio halijaisha, walichoka mno imagine mtu kuanzia saa 10 jioni hadi saa 7 bado tamasha halijaisha na anaombwa sadaka
 
Andaa la kwako kaka,,achana na matasha yaliyo andaliwa na wengine!!!
 
Back
Top Bottom