Hawataki kuhama: Wamang'ati wajiandaa kupambana na Polisi

Ni vipi tunaposema waende na wakati, tunaweza kuwaelimisha wakaondokana na mila na jadi zao na kuwafanya waendane na mkao wetu tunaodai ni wa kisasa na kimaendeleo?

Mkao gani huo - wa kukaa kwenye nyumba za kifisadi na kuendesha magari ya kifisadi pamoja na kula chakula cha kifisadi kwenye mahoteli ya kifisadi?
 
Juma Contena na Zakumi tunawajua kuwa ninyi mna chuki binafsi na jamii za wafugaji. Hizi ndio chuki zinazosababisha haya matatizo yote. Mnaona sawa wawekezaji wa jatrofa kupewa ekari zetu laki 6 ila taabu kwa Wabarbaig kubaki na ekari zao elfu 6! Alafu Zakumi unadai waandaliwe eneo la kuwahifadhi wa na jadi zao, sasa hiyo ina tofauti gani na kuwaacha waishi maisha yao ya transhumansi huko Hanang? Ninyi kama mmeshindwa kuishi kwa kufuga na kulima huku endeleeni tu kubeba maboksi huko! Ardhi ni mali ya Umma!

Katika nchi zote zilizoendelea kuna watu kama hawa. Na solution ni kuwatafutia maeneo hili waendeleze upuuzi wao.

Ukija Marekani kuna reservations kwa ajili ya wahindi wekundu na Maghetto kwa ajili ya watu weusi.

Hivyo proposition yangu ya kuanzisha tribal areas kwa makabila yalioshindwa ku-couple na mabadiliko ni ombi zuri tu kwani sioni hao jamaa wakaweza ku-survive kwa kutumia mikuki na virugu.
 
Sawa, waachieni/warudishieni basi hayo mashamba ya ngano Hanang yawe their 'commons'!
 
Wabarbaig watangaza vita

Na Novatus Makunga

20th December 2009

headline_bullet.jpg
Atakayesogelea eneo lao kuligawa kukiona
headline_bullet.jpg
Wasema JK alishawapa mashamba hayo

Barbaig.jpg

Katika mpango wa awali chini ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo kapteni mstaafu John Ngatuni, halmashauri ilipitisha mgawo wa kutenga ekari 500 kwa ajili ya kuhifadhi kwa matumizi mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji na kugawa ekari 6000 kwa wakulima na kiasi kingine kama hicho kwa wafugaji.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

http://www.ippmedia.com/

0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni

Ukisoma hapo kwenye red, utaona kabisa hawa Wafugaji wa haki ya kupigania arthi yao...kumbe mgao ulishafanyika kama wanavyodai JK aliwapa..!!
 
Wafugaji hawa wana haki ya kupewa (in fact kurudishiwa) maana walinyang'anywa na serikali enzi zile za nafco

Kama serikali lazima ifahamu kuwa wafuagaji wanahaitaji ardhi kubwa kwakuwa mifugo yao ni makundi makubwa na yanayotambaa na kutembea (ufugaji wa kienyeji)

Bado mahitaji ya nyama ni makubwa na soko lake ni ndani na nje kuwabughuzi hawa wafuagaji ni kuonyesha kuwa hatuthamini mchango wao mkubwa kabisa katika pato la Taifa.
Serikali iwasadie kuwafundisha ufugaji wa kisasa ili waweze kutumia eneo kidogo bila ya kuathiri kiasi cha mapato tokana na mifugo waliyonayo.
Mabadiliko ndio kitu cha kawaida kwa binadamu hivyo hata siku moja wasitegemee maisha yao ya kimila kua hayatobadilika hasa ukijua kua idadi ya watu nayo yazidi kuongezeka.
 
Serikali ndio inawahitaji wafugaji hao waifundishe transhumansi, mfumo maridhawa wa kutunza mazingira na kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa mliyokuwa mnayajadili kizembe huko Kopinihageni - waachieni eneo lao muone jinsi wanavyofuga kwa usasa wa kitransihumansi ambao wasomi bugizi mliobugiana kudesa elimu bugizi ya kimagharibi hamuujui na wala hamtaki kuujua maana mna kasumba inayowafanya mdhani miafrika ni mijinga!
 
Ukisoma hapo kwenye red, utaona kabisa hawa Wafugaji wa haki ya kupigania arthi yao...kumbe mgao ulishafanyika kama wanavyodai JK aliwapa..!!

Ndugu 'precision/preciseness' ni jambo muhimu hapo, JK 'hakuwapa' - "aliwarudishia"!
 
Kuwarudishia ni kukiuka The survival of the fittest.

Nafco ndio fittest - mbona imekufa? Au hao wawekezaji ambao hata kulima nusu ya mashamba ya nafco hawawezi ndio fittest? Hivi unajua wanayakodisha kwa wananchi hao hao? Who is made to 'survive'?
 
wana haki ya kupigania ardhi yao!walau kidogo wenzetu hawataki/hawako tayari/wamechoka KUBURUZWA
 
Silencer tafadhali naomba usihariri hicho kichwa cha habari. Kwanza kwa taarifa yako hao watu hawaitwi Wamangati. Hilo ni miongoni mwa majina ya dharau ambayo watu wenye chuki binafsi na jamii hii waliwapa. Inaashiria mtazamo hasi kwa jamii hii unaopelekea kunyanganywa kwa ardhi yao. Mitazamo hii inapaswa kupigwa vita! Silencer tafadhali acha ku-silence 'uhuru maoni'! Kilichoanza hapo ni vita na ndicho tunachopaswa kuzuia!
 
Silencer tafadhali naomba usihariri hicho kichwa cha habari. Kwanza kwa taarifa yako hao watu hawaitwi Wamangati. Hilo ni miongoni mwa majina ya dharau ambayo watu wenye chuki binafsi na jamii hii waliwapa. Inaashiria mtazamo hasi kwa jamii hii unaopelekea kunyanganywa kwa ardhi yao. Mitazamo hii inapaswa kupigwa vita! Silencer tafadhali acha ku-silence 'uhuru maoni'!
hivi huyu ni moderator kumbe?
 
Na hiyo mikuki yao sidhani kama wataweza mudu AK47 zikiingia. Hawa jamaa wana utani mmbaya hekari 6000 warande tu na n'gombe.

Wana haki ya kuendendekeza mila zao za ajabu lakini not to the tune of 6000 acres. Hila sio ardhi tena akapewe muarabu kama ni hivyo bora waichezee tu hawa wazawa.

Acre 6000 sio nyingi kwa wafugaji 300. Jiulize kwanza wana ngombe wangapi hao watu, halafu uliza wataalamu wa mifugo kila ngombe ili afugwe vizuri anahitaji acre ngapi halafu zidisha na hao ng'ombe utapata jibu. Usisahau pi kuwa kuna ongezeko la watu duniani ukiongeza hiyo factor utaona wana haki ya kufanya hivyo.

Hawajasoma lakini wanaakili na ni jasiri, big up kwao, sie acha tulale na kukoroma wakati ardhi inakwenda
 
JC:

Mi naona ipitishwe sheria ya kuanzisha tribal areas or reservations hili watu wanaopenda kubakia kwenye jadi zao wabakie huko.

Zakumi, hapa tatizo sio mila tatizo ni ardhi basi, jamani ugomvi wa ardhi ni mbaya kuliko ugomvi wowote tuangalie jinsi ardhi inavyogawanywa na kuchukuliwa
 
Wafugaji hawa wana haki ya kupewa (in fact kurudishiwa) maana walinyang'anywa na serikali enzi zile za nafco

Kama serikali lazima ifahamu kuwa wafuagaji wanahaitaji ardhi kubwa kwakuwa mifugo yao ni makundi makubwa na yanayotambaa na kutembea (ufugaji wa kienyeji)

Bado mahitaji ya nyama ni makubwa na soko lake ni ndani na nje kuwabughuzi hawa wafuagaji ni kuonyesha kuwa hatuthamini mchango wao mkubwa kabisa katika pato la Taifa.

Umepatia kabisa. Kwa makosa hayo ya kuthamini zaidi kilimo na kudharau mifugo ndio maana mapigano kilosa hayaishi na ihefu watu manahamishwa bila kujali kuwa mifungo ndio njia yao ya survival toka enzi na enzi. Tumewasahau sana wafugaji.
 
Siku zote huwa najiuliza Tanzania ina ardhi kubwa sana ambayo haitumiki na haijaguswa kabisa, kwanini hawa wawekezaji wasipewe ardhi ambayo haitumiki badala ya kwenda kuondoa wanamchi kwenye ardhi ambayo walishughulika kuisafisha/kuindaa misitu na kuwa ardhi ya matumizi ya kilimo
 
Umepatia kabisa. Kwa makosa hayo ya kuthamini zaidi kilimo na kudharau mifugo ndio maana mapigano kilosa hayaishi na ihefu watu manahamishwa bila kujali kuwa mifungo ndio njia yao ya survival toka enzi na enzi. Tumewasahau sana wafugaji.

Mkuu umesahau kuwa sirikali imeshasema "Kilimo kwanza?" haya ni marejeo yanayoanza kuingia taaaaaratibu, bado wa-Kenya nao wanataka, Uganda, Burundi, Rwanda, S/A etc etc..... hapo ndio patakuwa patamu kwani jamaa wanakuja na mihela kibao, viongozi wetu wengi wao wakiwa mafisadi hawataruka mtego wa fedha kwa kujibanza na mwavuli wa kilimo kwanza
 
Hii ni effect ya kugawa ardhi kwa wawekezaji bila kuangalia wananchi waliopo sehemu hiyo, sisi ni wagumu kuelewa natamani wote tungekuwa na akili kama hao ndugu zetu nadhani tungekuwa mbali sana.
 
Back
Top Bottom