Kleptomaniacs
Member
- Apr 23, 2008
- 86
- 2
Hawa wengineo wabishia kitu hata wasichokielewa, Wana wa Hanang' wameamua kuonyesha ujasiri wapo tayari kuifia ardhi yao, ni upuuzi eti kusema hawapo tayari kushirikiana na wenzao, kama serikali kweli ina nia ya dhati kutatua mgogoro huu, Rais atumie mamlaka yake ya uhawilishaji ahawilishe shamba jingine awapatie jamii ya wakazi waliohamishwa kutoka katika hifadhi ya mlima Hanang' mashamba yapo saba, mawili ndio hayo yamerudishwa kwa wananchi na mizengwe bado yaendelea, sasa kama yapo mengine matano kwanini moja lisihawilishwe wakapewa wakazi wa milimani na la hayo mawili wapambanaji wetu wakaachiwa! au maslahi ya taifa siku hizi ni kodi na uwekezaji tu!