Hawataki kuhama: Wamang'ati wajiandaa kupambana na Polisi

Madhara ya kutosoma na kutambua wajibu wao kama raia wa nchi. Sheria inasema ardhi ni mali ya serikali na rais ni mdhamini mkuu,hivyo matumizi yake yanaweza kubadilishwa wakati wowote,after all wanaogaiwa ardhi hiyo ni watanzania wenzao kama huo si upumbavu ni nini? wanawaza ng'ombe tu badala ya kuuza wakawa matajiri na kubaki na mifugo michache wamekalia ujinga wacha wanyang'anywe.

Na hiyo mikuki yao sidhani kama wataweza mudu AK47 zikiingia. Hawa jamaa wana utani mmbaya hekari 6000 warande tu na n'gombe.

Wana haki ya kuendendekeza mila zao za ajabu lakini not to the tune of 6000 acres. Hila sio ardhi tena akapewe muarabu kama ni hivyo bora waichezee tu hawa wazawa.
nafuu ya hao ni weengi wanalinda ardhi yao !! na sumaye je ekari 6000 morogoro na mkapa ekari 600 morogoro na huko Tanga wananchi wanalia hawana pamkulima mbona wao wasiligawe hilo eneo???
acheni uoneze bwna
 
Mbona JK na baraza lake lote la mawaziri wamesoma na hakuna maendeleo yoyote Tanzania? Usomi wenu ni upi huo? Nyie mliosoma mbona hatuoni maendeleo yenu badala yake ni kutafuna pesa ya walipa kodi!

Au wale waarabu mliowaweka Loliondo ndio maendeleo? Au kukatika kwa umeme au Kuwapigia magoti kina RA na Sin bin clair ndio maendeleo? Au kuwafukia raia wa Buzwagi ndio mnaita maendeleo?

Hii ndio paranoia yenyewe huta accuse kila mtu kwa mtaji huo. Its not about playing your tunes all the time ebu angalia na long term solutions.

wapo wanao husiana na wa usika uliowataja unfortunately mimi ni nobody humu ndani. Africa yenyewe longtime sasa sijui hasira zako unataka kunitupia mimi za nini.
 
Unatumia kigezo au takwimu gani kusema hawajasoma? Chuki binafsi mbaya sana! Inazaa dhambi ya ubaguzi!

Mtu mwenye elimi huwa anaangalia maendeleo yake na anakuwa mkweli kwake mwenyewe; mwishowe huu adapt necessary changes come on yaani ina maana toka miaka ya sabini mpaka leo bado walikua wanasubiri hiyo sehemu kwa ajili ya kuranda.

hapa hata kama kuna elimu basi bado kuna high ignorance as well. Since ignorance is much associated with luck of education. huitaji takwimu kukwambia community inayo lilia to cling with the past; isiyokua na manufaa ni watu wa aina gani let me help you there ni wasio na elimu.
 
nafuu ya hao ni weengi wanalinda ardhi yao !! na sumaye je ekari 6000 morogoro na mkapa ekari 600 morogoro na huko Tanga wananchi wanalia hawana pamkulima mbona wao wasiligawe hilo eneo???
acheni uoneze bwna

Kwangu mimi si issue hawa vigogo kuwa na ardhi wala wewe kuwa na hekari kazaa. Hapa labda tatizo ni jinsi walivyozipata hizo hekari ndio unaweza sema kuna tatizo.

Pili wanafanyia nini hizo ardhi kwa manufaa ya Taifa; nao wao kama hawaitumii productively yes warudishe.

This is not about baraigh's au anybody else personal attack its about us learning to maximise the potential of land. The less we have the more we will learn to value it. Hivyo ni muhimu watu wanaodhani wataichezea milele waelewe kuna mwisho kama hao watu wenu.

Its about time waji fence as individuals na waweke strong arguments kwamba ardhi imeshakua ya kwao through evidence like communities living on it; mifugo rely on it and a strong evidence of farming on it. Hii itakua ni argument ambayo serikali hata aitofikiria kufika huko kama vile ilivyokua sehemu zingine. lakini kitendo cha kuwaachia tu wazurure maporini alafu wa claim ni mali yao hell no. There are better ways to look after cattle na kuzurura is not one of them.
 
Madhara ya kutosoma na kutambua wajibu wao kama raia wa nchi. Sheria inasema ardhi ni mali ya serikali na rais ni mdhamini mkuu,hivyo matumizi yake yanaweza kubadilishwa wakati wowote,after all wanaogaiwa ardhi hiyo ni watanzania wenzao kama huo si upumbavu ni nini? wanawaza ng'ombe tu badala ya kuuza wakawa matajiri na kubaki na mifugo michache wamekalia ujinga wacha wanyang'anywe.

Get serious!!!

With all due respect,take back what you have just posted!Now I believe why Tanzanians are acting this way despite the fact kila kitu kinajieleza.Are you among the 70% JK aliowasema nini?I am behind Wamang'ati kwa sababu haya mambo tutachekelea tu(kama wewe unavyo-entertain)then mwisho wake ndio unasikia Waarabu wengine wameshapewa eneo la 'kupumzikia'.WAKE UP UACHE KUWA BENDERA FUATA UPEPO.Elimu uliyopewa ipo wapi?Ebi usitutie hasira hapa!
 
Madhara ya kutosoma na kutambua wajibu wao kama raia wa nchi. Sheria inasema ardhi ni mali ya serikali na rais ni mdhamini mkuu,hivyo matumizi yake yanaweza kubadilishwa wakati wowote,after all wanaogaiwa ardhi hiyo ni watanzania wenzao kama huo si upumbavu ni nini? wanawaza ng'ombe tu badala ya kuuza wakawa matajiri na kubaki na mifugo michache wamekalia ujinga wacha wanyang'anywe.

Hii imenifanya nitoke nilikojificha kwa sababu iko too low ni hatari kwa kila mtu.
Hiyo ni sheria ya nchi kweli, lakini haijakaa vizuri.
Ni sheria itumiwayo kuwanyang'nya wanyonge kile kidogo walicho nacho.
Ni sheria itumiwayo pale tu wao washika mpini wakiona inalipa kwao.

Mangi wa Moshi ana Maelfu ya ekari za kahawa kule moshi ikiwa ni pamoja na ardhi isiyolimwa. Sijawahi kumsikia mtu yeyote akijadiri kuigawa ardhi yake ambayo kwa sheria ni mali ya umma. Kama huyo umma yupo kweli.

Wanyalu wa Mufindi walihamishwa kama mbuzi mwitu kutoka kwenye malungulu yao, bila kufidiwa hata shilingi. Uwazi ulipopatikana miti ikapandwa. Leo hii wamiliki wa ardhi ile ni masikini wa kutupwa kazi yao ni umanamba.

Kule Madibila wanyalu na wasangu waliporwa ardhi yao ikaundwa NAFCO. ilipobuma wakaungana kuta wauziwe wao waendeleze kilimo cha mpunga Mbunge wa Mufindi MH Mungai akasimama kidete kuhakikisha wanyalu hao hawauziwi ardhi hiyo ambayo kimsingi ilitakiwa wapewe bure, na kuhakikisha Choli wa Kihindi anauziwa ili alime Nyonyo za kupeleka kwao India kwaajili ya Biodiesel.

Sijui matumizi ya Bonde la mpunga kubadirishwa kuwa Bonde la nyonyo yanamsaidia nani?

Eti tu kwamba unapokonywa ardhi na Mtanzania mwenzako anapewa ukisimama kidete unaitwa mpumbavu??

Mimi si mtaalamu wa lugha lakini nadhani maana ya Upumbavu katika jamvi hili tukalialo imeongezewa maji kwa mlima na kuchujuka kabisa. Ardhi ya Wahaya,Wachagga, Wanyakyusa wa kule TKY na hata ile ya familia ya Nyerere pale Butiama haimo kwenye list ya ardhi zozote za kuongelewa katika Mgao sembuse kumpa Mtanzania mwingine??

Kwa lugha nyepesi ni kwamba upumbavu wa kutetea ardhi yako kwa nguvu zako zote ni pale tu mtu aliyealiyewekwa kwenye kundi la Majuha wasio soma akikwapuliwa ardhi yake na kujifanya kudinda.

Ukisha mfukuza mtu aliyeishi miaka elfu katika ardhi yake na kumleta mtu ambaye tayari kwao ana ardhi ila tu choyo pupa na UFISADI vimemzidi, untaka huyu mnyonge aende wapi, afanye nini, au akufanye nini??

Kama kusoma ni kutambua herufi za maandishi fulani basi Wasomi ni wengi. Lakini kama kusoma kujiongezea maarifa ya kumudu mazingira yako.Basi nadhani Wamang'atii hawa wamesoma ipasavyo. Watu hawa wanajua wazi kwamba ardhi waliyonayo ndiyo kila kitu walichonacho. Zaidi wanatambua kwamba hii ndo nafasi yao ya mwisho ya kupigana ili waendelee kuwa wao.
Wanatambua wazi unyonge wao ndiyo asili ya walio na madaraka serikali kuwaonea, ndiyo maana wanakuja pamoja katika hali waliyo nayo.

Kwako wewe mwenye mazoea ya kufungua vitabu na kuvikodolea mijicho kwa sana, ukionacho ni Lubega na mikuki na sura zifananazo na ng'ombe." What you see is not all that can be seen".

Vitani watu hupigana kwa silaha na ni dhahiri kwamba silaha ni muhimu katika vita yeyote. Hatahivyo jua kwamba silaha si bunduki tu, silaha ni kila kitu chochote tangible au nontangible kiwezacho kufanikisha vita.
Ndiyo maana Goliath, mwenye umbile la kuparama na suti ya delaya, ngao, jambia na mkuki mzito, alipigwa kizembe na David mwenye kombeo na vijiwe kadhaa vya manati tu.

Huko Afghanstan Marekani inabuma kishenzi mbele ya wenye nchi pamoja na silaha zao kali zote.

Vitani, kikubwa si silaha uliyonayo mkononi ila ni Nia uliyo nayo moyoni.


Mwenye nguvu na silaha kali aweza pata ushindi wa haraka na wa jumla lakini katika masafa marefu akabuma na kuachia mchuma kama levi wa gongo.

Mapambano ya Uhuru wa kusema katika Tanzania yalianza miaka michache mara tu baada ya Uhuru na bado yanaendelea mpaka leo hii.
Mshindi wa awali katika mapambano hayo alikuwa ni serikali ya CCM. Baaada ya miaka karibu 40 ni wazi kwamba meza inageuka na serikali ya CCM iko kwenye MCHECHE Mode, na tayari inaziona ngazi ni za moto kishenzi na imeanza kuuachia mchuma na hivi punde itajibwaga chini yenyewe kwa uzito wa umbile lake tofi.

Wao( Wamang'ati) na sisi wengine tuonao visivyo onwa na kila jicho tunaona nguvu ya kweli ianziayo mahali pasipo na kitu,heshima wala matumaini na kushikamana kwa pamoja kwa nia ya kulinda umoja wao na kuamsha msukumo uanziao chini kwenda juu na kuondolea mbali vikwazo vyote mithili ya Volkano.

Wanawaza ng'ombe tu! Sijui wewe unwaza nini?
VX,GX au makalio mazuri na laini ya wanawali?
Kitita cha noti za kijani?
Safari ya kwenda PIKADILI Uk?
Kumpiga mtu roba?
Kumwibia Mshua Fisadi?
Kuzibua mademu wawili kwa pamoja?

Wamekalia ujinga!

Ni kweli ujinga ni kitu cha kukalia.
Ukimkalia mtu kooni maana yake umemshinda nguvu.
Wengi wetu hapa badala ya kuweka matacko yetu juu ya ujinga na kuusahau, tunayaweka juu ya maarifa na kuuacha ujinga utumalize.

Ndiyo maana kwa kukalia akili na kuabudu ujinga Oysterbay nzima inanuka mavi ya ng'ombe. Kila nyumba ina ng'ombe wachache kwani ni dalili ya akili.
Naona ng'ombe wanazidi kukaribia vyumbani mwenu. Miaka michache ijayo mtalala chumba kimoja na ng'ombe wenu kwani mtakuwa mmeuza mabanda yote ya uani kwa wawekezaji na kubakia na mifugo michache. Du!


Pengine wewe na mimi tusichoelewa au tunaelewa hatutaki kujadili ni ukweli kwamba nchi yote imeuzwa, au imewekwa rehani kwa mahasimu kwa faida iliyo sawa shanga za kiunoni. Hapa akichekwa Mtemi aliye muuzia Karl Peters kwa hila, tutamcheka vipi Rais wa nchi, Waziri mkuu,Mbunge,Jaji mkuu, Mkurugenzi wa Idara serikalini na wasomi wote ndani ya serikali kwa kuuza nchi bila hila yeyote??
 
Mkuu sijapendezwa kabisa na hapo nilipoweka red....kwa nini unawaona wapuuzi?..je tukianza lingalisha kati yako na wao nani atakua mpuuzi wa kweli unazani?....wanalinda ardhi yao waliyogawiwa na serikali hiyo hiyo inayotaka kuwanyang'anya tena,wanaishi maisha yao mazuri tu ya kimila,kwao mkoloni mweusi na mweupe haingii kamwe.


Angalia wewe unavyodanganya wenzako. Jaribu kutumia kirungu na mkuki kukupatia chakula chako kila siku na uone kama ndio maisha ya kimila ni mazuri.
 
Uhasama dhidi ya mfumo wa ufugaji
Ufugaji umekuwa ukilaumiwa sana kwa kuchangia migogoro ya ardhi lakini katika hali halisi, sekta ya ufugaji ni mojawapo ya sekta majeruhi wa mfumo mbovu wa usimamizi wa rasilimali za ardhi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa wafugaji wamekuwa wakielekezewa lawama nyingi bila kuwekewa huduma zinazowawezesha kutulia na
kuacha kuzurura na mifugo yao kutafuta malisho na mahitaji mengine. Takwimu za Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo zinaonyesha kwamba kati ya hekta milioni 88.62 za raslimali ardhi hekta milioni 60 ni uwanda ufaao kwa malisho ya mifugo yenye
uwezo wa kubeba jumla ya ng’ombe milioni 20, kwasasa takwimu zinaonyesha kwamba tuna jumla ya ng’ombe 18, 398,327 ( National sample Census of Agriculture 2002/03- National report). Takwimu za Wizara ya Kilimo na Chakula zinaonyesha kwamba kuna jumla ya hekta 44 milioni za ardhi yenye rutuba ifaayo kwa kilimo na kati ya hizo jumla ya hekta milioni 10.1 ndio zinazotumika kwa sasa. Kwa takwinu hizo, yapo maeneo ambayo yakigawiwa kwa wafugaji bila kuingiliwa na watumiaji wengine, migogoro mingi ya ardhi inaweza kuepukwa. Lakini tofauti na hilo, maeneo mengi yanatengwa
kuwa hifadhi za wanyamapori (takribani 30% ya ardhi ya Tanzania) na kwa shughuli nyingine za kiutalii.

Chanzo: http://www.hakiardhi.org/HA-Docs/conflicts.pdf
 
Angalia wewe unavyodanganya wenzako. Jaribu kutumia kirungu na mkuki kukupatia chakula chako kila siku na uone kama ndio maisha ya kimila ni mazuri.

Acha kuuongopea umma, nani kakuambia Wabarabaig wanatumia virungu na mikuki kujipatia chakula chao? Get to know them instead of relying on your persistence prejudices on pastoralists!
 
Acha kuuongopea umma, nani kakuambia Wabarabaig wanatumia virungu na mikuki kujipatia chakula chao? Get to know them instead of relying on your persistence prejudices on pastoralists!

Watachungaje ng'ombe bila kuwa na virungu au fimbo? Na utawalindaje ngo'mbe bila kuwa na mikuki? Tools zao ni virungu na mikuki na huo ni ukweli wa mambo.
 
Watachungaje ng'ombe bila kuwa na virungu au fimbo? Na utawalindaje ngo'mbe bila kuwa na mikuki? Tools zao ni virungu na mikuki na huo ni ukweli wa mambo.

Tools za kujipatia chakula chao kama ulivyodai hapo awali anti-pastoralist?
 
"We hold these truths to be self evident that all men are created equal"....

You hold these truths na nani wewe Mnyantuzu? Mizungu? Hebu rudi upiganie ardhi na wafugaji wenzako ili m-hold these truths huku? Au umeshji-naturalize/jilipua mbele ya maneno haya ya 'Statue of Liberty':

Give me your tired, your poor,
Your huddled masses yearning to breathe free,
The wretched refuse of your teeming shore.
Send these — the homeless, tempest-tossed — to me;
I lift my lamp beside the Golden Door.


P.S. Mbona umeicha Golden Door yenu Unyantuzuni ihodhiwe na Barrick Gold?
 
Madhara ya kutosoma na kutambua wajibu wao kama raia wa nchi. Sheria inasema ardhi ni mali ya serikali na rais ni mdhamini mkuu,hivyo matumizi yake yanaweza kubadilishwa wakati wowote,after all wanaogaiwa ardhi hiyo ni watanzania wenzao kama huo si upumbavu ni nini? wanawaza ng'ombe tu badala ya kuuza wakawa matajiri na kubaki na mifugo michache wamekalia ujinga wacha wanyang'anywe.

Pamoja na kutosoma wameelimika kuliko wewe ndio maana wameweza kutambua kuwa jamii haiwatendei haki na njia pekee ya kujikomboa ni silaha sio kulialia na watu wasiosikia. Ardhi wanayopigania ni mali yao ndio inayowapatia mahitaji yao ya kila siku sasa unapotaka kuwagawia wageni wao waende wapi? Au ndio yaleyale ya kuwachomea nyumba zao.

Ardhi ni mali ya serikali na inaweza kubadili matumizi yake kwa maslahi ya umma sio kiujanja ujanja kama wanavyotaka kufanya, unamnyang,anya mtanzania unampa mgeni kwa kisingizio cha mwekezaji.

Nusu karne baada ya uhuru serikali ilitakiwa iwe imeshawaelimisha hao wababaig - kwa kuwapatia miundombinu ya kuwawezesha kufanya ufugaji wa kisasa na sio kuwalaumu ati wapunguze mifugo!! halafu wafanye nini?
 
Mkuu Madela wa Madilu, umesema vizuri, thank you. Watu wanakariri vitabu vilivyotungwa na wenzao halafu wanajidanganya wamesoma. Wenzetu waarabu mafuta yakigundulika kwenye ardhi yako unapewa share kwenye hiyo kampuni ya mwekezaji, sisi unatuliwa kwa fidia ya magugu yanayoonekana lakini thamani ya mafuta wanagawana wanasiasa kwa kisingizio cha sheria. Upuuzi mtupu
 
http://www.roughguides.com/website/...t.aspx?titleid=93&xid=idbox_head60207824_0274


The unremittingly dry expanse of savannah that stretches south of Mount Hanang, the Mang'ati Plains, is at first sight a deeply inhospitable place. Yet the plains are home to some 200,000 Barbaig (or Barabaig), a semi-nomadic, cattle-herding tribe distantly related to the Maasai. The key to their existence in such a barren land lies on the other side of Mount Hanang in the shape of Lake Balangida, a large freshwater expanse at the foot of the Malbadow Escarpment. The lake is fed by the mountain, which ensures that even when the lake is dry (an increasingly common occurrence), the deep wells that have been dug around its periphery still contain enough water for the Barbaig's herds.


Tall, handsome and proud, the Barbaig are at first glance very similar to the Maasai. They dress alike, and are also herders, in whose culture cattle occupy a pivotal place. Like the Maasai, their society is organized into age-sets and a clan system (doshinga) which governs rights over pasture and water sources. But for all their similarities, there's no love lost between the two peoples. The Maasai have two names for the Barbaig. One is Mbulu, by which many other tribes south of the Maasai are also known, and which means "unintelligent people". The other, reserved for the Barbaig alone, is Il-Mang'ati, meaning "the enemy", a simple tag which, coming from East Africa's most feared and warlike people, is almost akin to a compliment. The name Barbaig itself comes from bar (to beat) and baig (sticks), alluding to a unique dance that is still held today, in which fights are mimicked using sticks for weapons.


The Barbaig are one of nineteen tribes that originally made up a broader cluster of people called Datooga (or Tatoga). Like the Maasai and Kalenjin of Kenya, the Datooga are linguistically classed as Nilotic, meaning that they share a common origin, presumed to be in Sudan's Nile Valley. A fascinating relic from this time, which could also explain the extreme ritual importance of cattle in all Nilotic societies, is the Barbaig word for God, Aseeta, which is related to the Kalenjin word Asiis, which also means sun. Both words have their root in the name of the ancient Egyptian goddess Isis, who wore a solar disc and the horns of a cow and was the focus of a cattle and fertility cult throughout much of antiquity. According to Roman mythology – which adopted many Egyptian cults – the beautiful Isis, whom the Romans called Io, was kidnapped by an amorous Jupiter, but her mother, Juno, gave chase. Rather than give her back, Jupiter rather unfairly turned his love into a cow. Not content with this punishment, he called down a bumble bee from the heavens and commanded it to sting the cow. Not terribly enchanted with this treatment, the miserable Io fled to Egypt, where she cried so much that her tears formed the Nile.


The Datooga's southward migration is believed to have started around 3000 years ago, possibly prompted by the massive climate changes that coincided with the expansion of the Sahara Desert. Around 1500, the Datooga arrived at Mount Elgon on the Kenya-Uganda border, where they stayed until the eighteenth century, when they migrated south once more into Tanzania. The Datooga first settled at Ngorongoro before being pushed further south by the Maasai, after which they separated into various tribes, many of which have now been assimilated by others. Lamentably, the Barbaig's southward migration continues even today. Loss of their ranges to commercial ranches, flower farms and seed-bean plantations, and encroachment by Maasai (who have themselves been pushed south in recent decades by the creation of the Serengeti and Tarangire national parks) mean that the Barbaig are among Tanzania's poorest people. Child mortality rates are high, as is the incidence of cattle disease. The fact that none of this used to be the case supports the Barbaig claim that nothing other than the loss of their traditional land has caused these problems, but unfortunately the scattered nature of Barbaig society means that they have largely been absent from politics, and have consequently been marginalized. Their latest efforts to regain access to their land via a series of legal actions in the courts have stalled on the absurd grounds that they lack legally recognized title to the land.


For more information on the problems Barbaig culture faces, see Passions Lost by Charles Lane (Initiatives Publishers, Nairobi, 1996).

Thats why I consider Pan Africanists as most reasonable. Ukiangalia historia ya kila kabila utakuta wote tunatoka sehemu fulani katika Afrika tofauti na tulipo sasa.
 
Back
Top Bottom