Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Wabarbaig watangaza vita
Na Novatus Makunga
20th December 2009
Atakayesogelea eneo lao kuligawa kukiona
Wasema JK alishawapa mashamba hayo
Makundi ya jamii ya wafugaji wa kibarbaig yakiibuka kutoka msituni tayari kupambana na atakayevamia eneo lao.
Wafugaji wa kabila la Wabarbaig katika kijiji cha Mogitu na vijiji vya jirani, wametangaza vita kupambana na yeyote atakayeingia katika eneo hilo kwa lengo la kuligawa upya.
Kama njia ya kujilinda na kujihami, wafugaji hao wamejipanga kwenye makundi na kujificha katika moja ya mlima kijijini hapo kupambana na atakayethubutu kuingia kwa ajili ya zoezi la kuligawa upya eneo wanalodai lilishatengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo.
Sakata hilo linatokana na mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na Shirika la Chakula na Kilimo (Nafco), yaliyopo eneo la Basotu ambayo mwaka 2006 serikali iliyaachia kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi.
Wananchi hao ambao pia wanatoka katika vijiji vya Mingenyi na Gidagamu wanapinga kile kinachoonekana kutaka kumegwa kwa eneo lililotengwa kwa ajili ya ufugaji ili kuwapatia maeneo wananchi walioondolewa katika mlima Hanang.
Nipashe imeshuhudia maelfu kwa maelfu ya Wabarbaig wazee kwa vijana waliogawanyika katika makundi ya watu wasiozidi 200 kila moja likiwa na kiongozi wake, wakiwa na silaha za jadi yaani mikuki, pinde na sime wakiibuka katika mlima Kujo.
Taarifa zilizopatikana katika eneo hilo lililopo umbali wa kilomita takribani 50 kutoka katika mji wa Katesh ambao ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Hanang, zilisema kuwa Jumatatu iliyopita wafugaji hao waliwakurupusha maofisa waliokwenda katika eneo hilo kwa ajili ya zoezi la upimaji.
Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Parmena Sumario, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema walilazimika siku ya pili yake kumkamata Mwenyekiti wa kijiji cha Mogitu, Israel Dawi na watu wengine 16 ambao inawashikilia.
Kiongozi wa kimila kwa upande wa vijana, Mangi Gidagurenda, alisema kuwa hadi kufikia juzi ni siku ya nne wanalala nje ya nyumba zao kwa lengo la kulinda ardhi yao isichukuliwe na wapo tayari kwa mapambano na polisi.
Mimi hapa nilipo ni miongoni mwa wanaotafutwa na polisi kukamatwa lakini tumejizatiti kupambana nao mpaka mtu wa mwisho kamwe hatutakubali kuonewa na kunyanganywa ardhi yetu, alisema.
Alishangazwa na hatua ya polisi kuwakamata wenzao wanaotetea haki akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Mogitu na kueleza kuwa wanajiandaa kuandamana hadi polisi wilayani Hanang kujua kulikoni.
Kijana wa Kibarbaig, Herje Giter, alisema anashangazwa na uongozi wa Wilaya ya Hanang kuingilia upya suala la ugawaji wa eneo hilo ambao ulishakamilika na maeneo kutengwa kwa shughuli za ukulima na ufugaji.
Mheshimiwa Jakaya Kikwete alishatoa mashamba hayo kwa nia nzuri kwa wananchi sasa hawa viongozi wanataka kuharibu nia nzuri ya mheshimiwa Rais, alisema Giter.
Gidambusa Mwarja, alisema kuwa wananchi wa maeneo hayo walishazoea kuwekwa mahabusu katika magereza tangu mwanzo mwa miaka 80 wakati serikali ilipowapokonya mashamba hayo na kuanzisha mradi wa Nafco kwa hiyo hawatashindwa kutumia nguvu ili kuhakikisha ardhi yao haimegwi.
"Tumejiandaa kwa lolote litakalojitokeza na wote tayari tumeshaandika urithi wa mali zetu kwani mwanaume lazima afe na mali yake na sisi ardhi ni mali yetu lazima tuipiganie," alisema.
Alidai kuwa kuwepo kwa watu kutoka mlima Hanang kunatumiwa tu kuwahalalisha wafanyabiashara na watu kutoka maeneo mbalimbali kwani wanadai wengi walishagawiwa na kuyauza maeneo hayo.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Hanang alipopigiwa simu ili kutoa ufafanuzi alikuwa mbogo.
Watafuteni hao hao waliowaleta huku na kuwapa taarifa za huo mgogoro mimi siko tayari kuzungumzia ujinga huo nina kazi nyingi, alisema Ligubi na kukata simu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hanang alivyofuatwa ofisini kwake alikataa kutoa ufafanuzi kwa madai hatakuwa tayari kuzungumza mpaka atakapokuwa na Mkuu wa Wilaya Lugubi.
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, alisema kuwa yupo katika mkutano Mwanza hata hivyo katika vikao vilivyopita vilivyowashirikisha pia viongozi wa vijiji hivyo walikubaliana kuwa sehemu ya eneo lililotengwa kwa mifugo limegwe kwa ajili ya wananchi.
Kwa kweli hali ni mbaya mimi nitapita kwenda kuzungumza na hao wananchi lakini nashangaa kama hata wenyeviti wa vijiji wanaongoza hali hiyo wakati nao tulikubaliana katika vikao, alisema Shekifu.
Katika mpango wa awali chini ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo kapteni mstaafu John Ngatuni, halmashauri ilipitisha mgawo wa kutenga ekari 500 kwa ajili ya kuhifadhi kwa matumizi mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji na kugawa ekari 6000 kwa wakulima na kiasi kingine kama hicho kwa wafugaji.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
http://www.ippmedia.com/
0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni