Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,753
- 218,340
Kwa kweli tunawashukuru sana wale wote waliojitolea kwa hali na mali kusaidia wahanga wa Hanang , na tunachukua nafasi hii kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu ili awajazie pale palipopungua, Amina.
Hata hivyo ni vizuri tukafahamu huko ilikotokea misaada hii , wala haijawahi kuwa dhambi kufahamu chanzo cha msaada wowote ule , lengo la kujua hili ni kuepuka magenge ya utakatishaji wa fedha ama kupokea misaada ya wauza unga.
Hawa wanaojiita Wenza wa Viongozi ni akina nani , ni wake zao au ni nyumba ndogo zao? hii Taasisi ya wenza wa viongozi imesajiliwa lini na wapi , namba ya usajili wao ni ipi na malengo yao ni yapi? wanapata wapi hela za kutoa misaada hii na ni nani anayewapa hela hizo na kwanini?
Tukiacha mambo haya bila kuhoji iko siku watakuja Watoto wa viongozi , binamu wa viongozi au Hata umoja wa wazazi wa viongozi
Ni vema utaratibu unaoeleweka ukatumika kwa yeyote anayetaka kuchangia chochote kwenye maafa , badala ya kuleta makundi yasiyo na tija yoyote .
Naomba kuwasilisha .