Taasisi za dini zinazomiliki shule hapa nchini ziache kutumia shule kama chanzo cha mapato, zianze kuitazama elimu kama huduma

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,523
5,574
Habari za wakati,

Mimi ni mdau na muumini wa utoaji wa elimu bora kwa gharama nafuu au BURE kabisa.

Leo nimejulishwa kwamba shule ya Mtakatifu JUDE iliyoko jijini Arusha inafanya usaili wa wanafunzi ambao kama wakifanikiwa kupita katika usaili huo watapata ufadhili wa elimu bure shuleni hapo. Elimu inayotolewa shuleni hapo ni mfumo wa English medium na inatolewa bure kupitia michango ya wafadhili kwa watoto wanaotoka katika kaya maskini na wenye vipaji/uwezo mzuri katika masomo

Shule ya mtakatifu JUDE ni moja kati ya initiative bora kabisa kuweza kufanyika hapa nchini katika sekta ya elimu.Nashangaa ni kwa nini shule za makanisa kama vile kanisa katoliki kwa kushirikiana na serikali hazijaiga mfumo huu au hata kwenda Pale ST JUDE kujifunza wanawezaje kutoa elimu BURE na BORA.

Binafsi nafahamu kwamba shule yoyote inahitaji uwekezaji mkubwa lakini pia naffahamu kwamba jamii yote inafahamu umuhimu wa elimu na faida za kuhakikisha kwamba kila mtu ana uwezo wa kupata elimu bora na bure. Kwa kuangalia mfumo wa ST JUDE naonakabisa inawezekana kutoa elimu BORA na BURE kwa watoto wetu kwa kuzingatia kwamba elimu ni haki ya msingi. Sisemei hii elimu bora ambayo wanafunzi wanasongamana madarasani na uhaba wa walimu huku walimu wakiwa wamejaa vijiweni hawana najira ya kufanya.

Niseme tu kwamba ni wakati sasa kwa taasisi za kidini hasa KANISA KATOLIKI ambalo linamiliki shule sana hapa nchini kuacha kutumia shule kama chanzo cha mapato.Waanze kuitazama elimu kama huduma na badala ya kutumia mfumo wa sasa wa ada watumie mfumo wa CHARITY ambapo jamii wakiwamo wazazi wenye watoto na wasio na watoto wanapewa FURSA ya kudhamini mtoto kwa kiwango chochote cha PESA kwa kutegemea kipato chao.

Naamini serikali tukufu ya JPM itaweka mazingira wezeshi ya kuwapa wafanyakazi TAX credits ambazo zinaweza kuwapunguzia mzigo wa kodi kwa kuchangia elimu (SPONSORING STUDENTS)

Ninapozungumzia student sponsorship namnaanisha kwamba unaweza kumsponsor mtoto wako na mwingine zaidi mradi mfumo mzuri wa kuratibu michango na matumizi yote uwepo ili kuepuka elimu kuwa ni chanzo cha mapato.

Nimechokoza mjadala ili tuweze kutoa maoni. KAMA ST JUDE WAMEWEZA KWA NINI wengine washindwe?

Tujadili
 
Bure haipo hapo, kuna wanaocover hizo cost tayari kama ulivyosema.
 
Bure haipo hapo,kuna wanaocover hizo cost tayari kama ulivyosema
Mkuu, unajisikia kubishana au unajisikia kusema kwamba haiwezekani? Hakuna Cha bure ila ELimu lazima iwe kipaumbele.
 
Back
Top Bottom