Hatma ya Ndoa ya Dr Slaa na Josephine leo: Ni Rose kamili au Josephine??

Mwacheni dokta achukue jiko lake jumla jumla! Rose kamili huna wivu lakini roho inakuuma! Josephine atakuwa first lady! Rose una nafasi yako cos mtalaka hatongozwi! Rose tutakuachia EOTF ya mama mkapa,Josephine ataendelea na WAMA.

first lady ya wapi?.
 
this is nice....enjoy!
602305_235645973229750_144230431_n.jpg


mambo ya matanuzi toto la kihaya
 
hivi hiyo nayo ni dini au kikundi cha kufanyia uhalifu bila kutafakari unalolifanya? Hivi leo nikizusha tu kwamba kuna mtu kaingia na viatu kwenye vijengo vyenu mtaanza kuandamana bila hata kutafuta ushahidi.! Ptuuuuuuu!!

heri hao kuliko nyie mnaojifanya maaskofu kumbe mnafi.r.a.na na kuwageuza masista chakula cha maaskofu na kuzaa na wake za watu kisiri huku mkiwajengea majumba makubwa makubwa na kuwavunjia ndoa zao.
 
hivi maisha ya mtu kama huyu anaweza kutufaa kweli wa tz?

Ameshindwa upadri, akao, mke akamshinda kaenda kupora mwingine na kazaa nae na sasa anataka kufunga ndoa.

Kama padri msaafu kashindwa kuheshimu amri za bibilia inayokataza kuzini na inayokataza kumtamani mke wa mtu, atawezaje kuiheshimu katiba?

Unapotaka ushauri kwa mtu, angalia kwanza maisha yake kabla ya kusikiliza mawazo yake.

Mtu ambae kashindwa kujiongoza kwenye maisha yake hawezi kuwa kiongozi mzuri.
 
Mwacheni dokta achukue jiko lake jumla jumla! Rose kamili huna wivu lakini roho inakuuma! Josephine atakuwa first lady! Rose una nafasi yako cos mtalaka hatongozwi! Rose tutakuachia EOTF ya mama mkapa,Josephine ataendelea na WAMA.

Kivipi Mkuu,mbona naona usingizi kutokana na hii coment???!!!
 
Naona tangu vurugu za kidini kuanza wiki hii, thread kuhusu Chadema, Dr. Slaa na Zitto zimekua adimu sana.
Hii sio dalili nzuri ukizingatia ukosefu mkubwa wa 'ajira' kwa vijana hapa Tanzania.

Angalau sasa tumeanza tena kuona thread kama hizi zinazozalisha 'ajira' kwa vijana wa Nape !!
Lakini bado zile zinazomhusu Zitto na Chadema kwa ujumla hatujaziona kwa takribani wiki nzima sasa.

Hii inadhhirisha wazi kuwa vurugu za kidini ni noma sana, maana zinakosesha 'ajira' kwa watu wengi sana !!
 
heri hao kuliko nyie mnaojifanya maaskofu kumbe mnafi.r.a.na na kuwageuza masista chakula cha maaskofu na kuzaa na wake za watu kisiri huku mkiwajengea majumba makubwa makubwa na kuwavunjia ndoa zao.

Mkuu taratibu,kwa sababu nasikia harufu ya mabomu,hivi unajua ukweli unauma????!!
 
Yes Candid inanishangaza sana

Kwetu wakatoliki kuna sakramenti saba. Sakramenti ya sita ni Upadre na ya saba ni ndoa. katika hizo, huwa hairuhusiwi kushiriki sakramenti zote mbili hizo kwa sababu utumishi katika kanisa unaisha kwa kifo kama ndoa inavyofikia tamati kwa kifo tu. (I stand to be corrected here as naamini Fr Mapunda ni member humu anaweza kusaidia ufafanuzi wa kina).

Mfano mzuri ni Askofu Mkuu Milingo yule Mzambia ambaye alikataliwa katakata na Papa kufunga ndoa licha ya kujitoa upadri kama Dr Slaa, na mwisho Askofu uyo aliamua kuanzisha kanisa lake na kufunga ndoa kupitia kanisa lake.

Leo nilipoona Dr Slaa kuwa anataka kufunga ndoa ya kikatoliki, kwakweli imenishangaza na nitapenda nipate maelezo ya kina ili nielewe vema

Ni kweli unalosema, lakini Dr. Slaa hakukimbia upadre bali alifuata procedure za kuuacha akaruhusiwa. Yuko huru na maisha mengine kama walivyo waumini wengine.
Cha muhimu wazee wa sheria za kanisa wanaweza kufunguka zaidi.
 
Mwacheni dokta achukue jiko lake jumla jumla! Rose kamili huna wivu lakini roho inakuuma! Josephine atakuwa first lady! Rose una nafasi yako cos mtalaka hatongozwi! Rose tutakuachia EOTF ya mama mkapa,Josephine ataendelea na WAMA.
Jamani tuhurumieni wenzenu,manaka JF ni mtambo wa vichekesho unacheka hata kama ulikuwa na simanzi
 
Yes Candid inanishangaza sana

Kwetu wakatoliki kuna sakramenti saba. Sakramenti ya sita ni Upadre na ya saba ni ndoa. katika hizo, huwa hairuhusiwi kushiriki sakramenti zote mbili hizo kwa sababu utumishi katika kanisa unaisha kwa kifo kama ndoa inavyofikia tamati kwa kifo tu. (I stand to be corrected here as naamini Fr Mapunda ni member humu anaweza kusaidia ufafanuzi wa kina).

Mfano mzuri ni Askofu Mkuu Milingo yule Mzambia ambaye alikataliwa katakata na Papa kufunga ndoa licha ya kujitoa upadri kama Dr Slaa, na mwisho Askofu uyo aliamua kuanzisha kanisa lake na kufunga ndoa kupitia kanisa lake.

Leo nilipoona Dr Slaa kuwa anataka kufunga ndoa ya kikatoliki, kwakweli imenishangaza na nitapenda nipate maelezo ya kina ili nielewe vema

Una hakika Askofu huyo wa Zambia aliachishwa kazi ya Uaskofu au alipumzishwa majukumu ya Kiaskofu?

Kuna askofu mmoja Tanzania ambaye alikuwa askofu wa jimbo la Arusha kabla ya Josephat Lebulu. Askofu huyo alipumzishwa shughuli za kiaskofu si kuvuliwa uaskofu. Hali kadhalika kuna askofu mmoja kanda hiyo hiyo ya kaskazini yalisemwa mengi kwamba huenda alikuwa kwenye ile kitu dini (freemanson)..... ambako alikuwa anapata mapesa ya kujengea majengo ya maendeleo jimboni, naye alipumzishwa shughuli za utumishi wa kiaskofu. Hao hawakuvuliwa uaskofu bali kupumzishwa shughuli za kiaskofu.

Kanisa haliwezi kumwondolea mtu ahadi ya useja kama mwenyewe hajaomba hivyo, kwa sababu yaliyotokea kwa hao maaskofu ni kutokana na huduma ya utumishi wao kuwaelemea na hivyo kanisa kuona bora kuwapunguzia mzigo huo wa utumishi kwa kuwapumzisha, lakini kanisa halikuwaondolea kile walichoahidi kwa vile ni ahadi ya mtu na Mungu wake na kanisa ni mashuhuda. Kama wanataka kanisa liwaondelee hilo ilitakiwa waombe.

Kwa ufahamu wangu ni kwamba, Dr. Slaa katika barua yake ya kuomba kuacha shughuli za kanisa katika barua hiyo ni lazima alianisha mazingira na hoja ambazo Holly see ilipima na kukubali ombi lake. Moja ya mambo muhimu ya kuomba ni kuacha huduma za uchungaji katika kanisa na pia kurejeshewa haki za kuwa regular laity, maana yake kuondolewa ahadi ya useja kwa sababu ya upadre ili arejeshewe haki za walei wa kawaida, hii ni kwa sababu zifuatazo:

  • Sharti la huduma za kipadre kanisani pamoja na kuwa na sakrament haziainishi kwamba sakrament ya upadre inamzuia padre aliyeacha huduma hiyo kisheria kutooa kama ataonyesha hivyo katika ombi lake la kuacha huduma ya upadre.
  • Sharti la useja kwa mapadre katika kanisa katoliki ni kwa ajili ya huduma zao za utume kufanyika kwa ufanisi zaidi kwani mtu akiwa na familia anaelekeza nguvu kwenye familia yake kwanza badala ya utume wa kiroho kwa kondoo zake.
  • Dr. Slaa ni mwanasheria, alijua namna ya kuandika ombi lake kwa Holly See na kumshawishi amkubalie ikiwa ni pamoja na kurejeshea haki ya ulei wa kawaida katika kanisa ambao unampa nafasi ya kufunga Ndoa.
  • Bila hivyo Dr Slaa asingethubutu kufunga ndoa kanisani bali serikalini jambo ambalo kwa mwumini mzuri wa dini yake ni kama kujidhalilisha.
  • Naamini kabisa kama ombi lake kwa kwa holly see lilikuwa la utaratibu niliosema juu kwa vyo vyote holisee ilimwondolea ahadi ya useja ambayo alifungwa nayo kwa sababu ya huduma za kipadre.
  • Hoja dhaifu ya kisiasa inapoonekana kujengeka hewani bila mizizi kuhusu kuvimbisha mishipa kichwani na kuweka mambo ya kufikirika kuhusu Dr. Slaa kuliko ukweli wenyewe, lao ameonyesha kufunga ndoa kanisani na kanisa limekubali, sasa wanatafuta kisingizio kingine.

Tofauti ya ahadi na Nadhiri

Mtawa hufunga nadhiri ya usafi wa moyo (useja), utii na ufukara mambo ambayo anatakiwa kuyaishi katika maisha yake na ndiyo dhana ya utumimishi wake kwa Muumba wake.
Padre hafungi nadhiri ya useja ila anaweka ahadi ya useja kwa sababu ya majukumu ya huduma za utumishi wa kipadre

Wakati hata anayefunga nadhiri ya useja/ubikira bado ana nafasi mambo akiona hayawezi kuomba kanisa limfungulie na aishi kama laity wa kawaida na kufunga ndoa kanisani, sembuse ahadi ya useja inayomfunga padre?

JF hapaharibiki neno tunao wengi hapa wanajua hilo na sidhani kama watakuwa mbali sana na maoni yangu kutokana na kulifahamu kanisa hilo kwa muda mrefu. Jambo hili tunalijadili ni geni sana nchi za kiafrika, lakini mataifa ya Ulaya na Marekani ni jambo linalofanyika mara kwa mara na hakuna anayeshangaa kwa sababu ni uamuzi wa mtu mwenyewe, na kanisa halikumlazimisha mtu huyo kujifunga bali alihiari mwenyewe na sasa mwenyewe anaamua kuomba kanisa limrejeshee hayo. Ndio maana anapopewa huulizwa mbele ya hadhara ya wamuni waliojazana ajibu kwa sauti ya juu kila mmoja asikie kama ameamua kwa hiari yake au ameshinikizwa. Ikitokea ajibu kwamba ameshinikizwa zoezi hilo litasitiswa papo hapo kwa sababu shughuli hizi ni ridhaa ya mtu anayejisikia kuwa na wito, na kuna wakati mtu hajisikii wito tean.

Biblia kwa wenye kuifahamu kuna sememu inasema, ni vema kuamua kuoa kama wajisikia hivyo kuliko kuendelea kuishi ukiwaka tamaa.
 
Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kumfanya mtu aliyewahi kuwa padre kurejeshwa kwenye hali ya ulei (yaani kuondolewa kabisa kazi na haki ya kufanya kazi za upadre na kuwa muumini wa kawaida kabisa).

Mtu ambaye ameondolewa upadre kwa utaratibu wa Kanisa (laicization –kufanywa mlei) na kibali cha Vatikani anaondolewa haki na majukumu yote ya mapadre wengine isipokuwa mambo mawili tu yaani useja (celibacy) na kusikiliza maungamo ya mtu aliyekaribu na kifo.

Hilo la useja linahitaji kibali kingine ili aruhusiwe kuoa. Kama Dr. Slaa aliomba na kupata hicho kibali kingine ili aweze kuoa, hapo sioni tatizo. Pia sidhani kama yeye ni mjinga kiasi cha kutaka kuoa bila kibali.

Huyo wa Zambia aliomba hivyo vibali viwili au alijifanyia mwenyewe tuu?
Hee?kumbe ukatoliki unasheria ngumu namna hii??duh yaan ni mgumu kupindukia,mtu kufanya maisha yake mpaka apate vibali??kweli dini si mchezo wa kuigiza,full controll.
 
Re: Hatma ya Ndoa ya Dr Slaa na Josephine leo: Ni Rose kamili au Josephine??
Siku zote ndoa hailazimishwi,Swali kwa Rose Kamili alikuwa wapi mpaka uchumba wa Mhe na Josephine ukakolea?
 
Waziri wa nishati na vito altangazia umma wa Tanzania kuwa mgaowa umeme utakuwa Historia nchi hii"
Sasa hivi mji wetu wa Mo town kuna mgao wa umeme bila taarifa.
 
Back
Top Bottom