Hatma ya Ndoa ya Dr Slaa na Josephine leo: Ni Rose kamili au Josephine??

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Hatimaye jibu linapatikana leo hii mahakamani

Uamuzi ndoa ya Dk Slaa leo Send to a friend
Thursday, 18 October 2012 22:50

James Magai

HATIMA ya ndoa ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa na mpenzi wake, Josephine Mushumbusi sasa itajulikana leo.

Mahakama Kuu leo inatarajia kutoa uamuzi juu ya pingamizi la awali lililotolewa na Dk Slaa akisema mlalamikaji, Rose Kamili hana haki ya kupinga asifunge ndoa.

Dk Slaa na Josephine walitarajia kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki Julai 21, mwaka huu, lakini Rose anayedai kuwa alikuwa mkewe, alifungua kesi hiyo kupinga ndoa hiyo na kudai fidia ya Sh550 milioni.

Hata hivyo, Dk Slaa pia kupitia kwa wakili wake, Phillemon Mutakyamirwa aliweka pingamizi la awali (PO), dhidi ya Rose akidai kuwa hana haki ya kufungua kesi kupinga yeye kufunga ndoa na Josephine, huku akiomba mahakama ifutilie mbali kesi hiyo.

Jaji Laurence Kaduri anayesikiliza kesi hiyo, atatoa uamuzi wa pingamizi hilo la awali la Dk Slaa, baada ya kusikiliza hoja katika pingamizi hilo pamoja na hoja za utetezi dhidi kupitia majibu ya Rose, zilizowasilishwa mahakamani hapo kwa njia ya maandishi.

Umuzi huo ndio utakaotoa hatima ya ndoa hiyo, kwani iwapo mahakama hiyo itakubaliana na pingamizi hilo la awali la Dk Slaa, basi kesi hiyo itatupilia iliyofunguliwa mahakamani na Rose itatupwa na badala yake Katibu huyo Mkuu wa Chadema atakuwa huru kufunga ndoa.

Ikiwa mahakama itatupilia mbali pingamizi hilo la awali la Dk Slaa, basi ndoa hiyo itakuwa mashakani kufungwa kwa kuwa iatasubiri uamuzi wa kesi iliyofunguliwa na Rose.

Katika pingamizi hilo, Dk Slaa anadai kuwa hawakuwa na ndoa halali kisheria na Rose na kwamba ndoa hiyo ni dhana tu ambayo haiwezi kumfanya awe na nguvu ya kumpinga kufunga pingu za maisha na Josephine.

Akitoa ufafanuzi wa pingamizi hilo, Wakili wa Dk Slaa Phillemon Mutakyamirwa alisema kuwa kutokana na sababu hiyo, Rose hakupaswa kufungua kesi mahakani kupinga Dk Slaa kufunga pingu za maisha na Josephine kisheria.

SIKUJUA KAMA KUMBE WANATAKA KUFUNGA NDOA YA KIKATOLIKI KANISANI

Nini kinakuchangaza Dr. Slaa kufunga ndoa ya Kanisani? Ana haki hiyo kwa vile hana ngoa nyingine. Ukitaka kujua zifahamu kwanza Canon Law. Padre hajazuiliwa kufunga ndoa, ila ameahidi maisha ya useja sababu ya utumishi, lakini utumishi wake unapokoma kwa kutaka mwenye au kwa njia nyingine yuko huru kufunga ndoa kisheria mradi utenguzi wa jukumu la utumishi wa kiroho aliamu kusitisha na kukubaliwa na Holly See.
 
Yes Candid inanishangaza sana

Kwetu wakatoliki kuna sakramenti saba. Sakramenti ya sita ni Upadre na ya saba ni ndoa. katika hizo, huwa hairuhusiwi kushiriki sakramenti zote mbili hizo kwa sababu utumishi katika kanisa unaisha kwa kifo kama ndoa inavyofikia tamati kwa kifo tu. (I stand to be corrected here as naamini Fr Mapunda ni member humu anaweza kusaidia ufafanuzi wa kina).

Mfano mzuri ni Askofu Mkuu Milingo yule Mzambia ambaye alikataliwa katakata na Papa kufunga ndoa licha ya kujitoa upadri kama Dr Slaa, na mwisho Askofu uyo aliamua kuanzisha kanisa lake na kufunga ndoa kupitia kanisa lake.

Leo nilipoona Dr Slaa kuwa anataka kufunga ndoa ya kikatoliki, kwakweli imenishangaza na nitapenda nipate maelezo ya kina ili nielewe vema
 
Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kumfanya mtu aliyewahi kuwa padre kurejeshwa kwenye hali ya ulei (yaani kuondolewa kabisa kazi na haki ya kufanya kazi za upadre na kuwa muumini wa kawaida kabisa).

Mtu ambaye ameondolewa upadre kwa utaratibu wa Kanisa (laicization –kufanywa mlei) na kibali cha Vatikani anaondolewa haki na majukumu yote ya mapadre wengine isipokuwa mambo mawili tu yaani useja (celibacy) na kusikiliza maungamo ya mtu aliyekaribu na kifo.

Hilo la useja linahitaji kibali kingine ili aruhusiwe kuoa. Kama Dr. Slaa aliomba na kupata hicho kibali kingine ili aweze kuoa, hapo sioni tatizo. Pia sidhani kama yeye ni mjinga kiasi cha kutaka kuoa bila kibali.

Huyo wa Zambia aliomba hivyo vibali viwili au alijifanyia mwenyewe tuu?
 
Mwacheni dokta achukue jiko lake jumla jumla! Rose kamili huna wivu lakini roho inakuuma! Josephine atakuwa first lady! Rose una nafasi yako cos mtalaka hatongozwi! Rose tutakuachia EOTF ya mama mkapa,Josephine ataendelea na WAMA.
 
Suala la ndoa kwa Dr Slaa halina utata wowote. Tatizo ni siasa uchwara za ccm na rushwa aliyopewa Rose kamili ili kulumbana na Dr Slaa bila sababu ya msingi!!
 
Yes Candid inanishangaza sana

Kwetu wakatoliki kuna sakramenti saba. Sakramenti ya sita ni Upadre na ya saba ni ndoa. katika hizo, huwa hairuhusiwi kushiriki sakramenti zote mbili hizo kwa sababu utumishi katika kanisa unaisha kwa kifo kama ndoa inavyofikia tamati kwa kifo tu. (I stand to be corrected here as naamini Fr Mapunda ni member humu anaweza kusaidia ufafanuzi wa kina).

Mfano mzuri ni Askofu Mkuu Milingo yule Mzambia ambaye alikataliwa katakata na Papa kufunga ndoa licha ya kujitoa upadri kama Dr Slaa, na mwisho Askofu uyo aliamua kuanzisha kanisa lake na kufunga ndoa kupitia kanisa lake.

Leo nilipoona Dr Slaa kuwa anataka kufunga ndoa ya kikatoliki, kwakweli imenishangaza na nitapenda nipate maelezo ya kina ili nielewe vema
Hii theology yako ni ya Utinta! Wewe ni mkatoliki wa jina na mafundisho ya kanisa katoliki yalikupita kushoto. Ni canon law namba ngapi inayokuambia utumishi wa kanisa unaisha kwa kifo??? No research, no right to speak!!!!
 
Simpo. Abadilishe dini awe muislam aoe wote

hivi hiyo nayo ni dini au kikundi cha kufanyia uhalifu bila kutafakari unalolifanya? Hivi leo nikizusha tu kwamba kuna mtu kaingia na viatu kwenye vijengo vyenu mtaanza kuandamana bila hata kutafuta ushahidi.! Ptuuuuuuu!!
 
Haki?? Josephine ana ndoa ya kanisani. Na yeye pia anaruhusiwa kufunga tena ndoa ya kanisani??? Double standard
 
Mie nadhani hata Dr slaa akiwa mkatoliki safi anajua huo utaratibu wa ufungaji wa ndoa ya kikristu, lakini hilo sio zuio kwani yaweza pia kufungwa kiserikali kwani issue ni kuwa na official marriage,
 
This is nice....enjoy!
602305_235645973229750_144230431_n.jpg

Attachments

  • BILA BILA.jpg
    BILA BILA.jpg
    61 KB · Views: 106
Back
Top Bottom