Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Mpira ni biashara kubwa yenye kuhitaji mtaji mkubwa,kwa mfumo wetu klabu inaendeshwa na mwanachama anayelipa sh 12 Elfu kwa mwaka kamwe hatutaenda popotr ndio maana miaka 70 imepita sifa ni kuifunga Simba!ni bora kabisa tujaribu namna nyingine.
 
Of course wameona fursa. Hivi vilabu ni tajiri sana. Tatizo ni ujinga na njaa za wanachama na wapenzi wake. Wao wameona fursa wacha waikamue. Kama matajiri "weusi" hawakuona fursa wakaridhika na hela ndogondogo walizojinufaisha kupitia vilabu hivi basi wacha hawa kanjibai wavune lakini angalau na mafanikio yatakuwepo ukilinganisha na hao "wahisani weusi."
 
Ndo wameanza ndugu yangu. Kma mradi hii hi pilot . yanga are so scared of manji. Ni mbabe sana kwao....

Wakuu,hebu nisaidieni mfano wa timu moja ya mpira iliyowahi kukodishwa ili tuseme yanga wameitumia kama kiolezo katika kufanya maamuzi yao..
 
Manji baba tunashukuru, nasi tukodi tu washabiki ututumie miaka 10 . sasa simba ndo wasahau kuifunga yanga. Na yanfa tutapanda sana ndege. Tutapanda mpka ma air hostess watufaham...
 
Unafki utawaua nyie mikia fc wa matopeni. Timu lenu linakufa kwa ukame wa vikombe mmekalia kushupalia ya Yanga. Hata huo mkataba wa kukodishwa hamjauona tayari mavi yanawagonga vyupi vyenu. Tuacheni wa kimataifa kama tulivyo hatuwahusu nyie. Nyambaaaaffff
 
watanzania wanajifanya wajuaji, wakati hawajui hata gharama za uendeshaji timu. Hata wasipompa timu Manji utakuta bado analipa gharama zote kuendesha timu hiyo. Ni sawa na kuoa kimada ulichokuwa unakihudumia kwa kila kitu.
 
Mpira ni biashara kubwa yenye kuhitaji mtaji mkubwa,kwa mfumo wetu klabu inaendeshwa na mwanachama anayelipa sh 12 Elfu kwa mwaka kamwe hatutaenda popotr ndio maana miaka 70 imepita sifa ni kuifunga Simba!ni bora kabisa tujaribu namna nyingine.

Mkuu, mimi naunga mkono mkono Ila hapo kwenye % ya klabu angefanya atleast 35!
 
Wanachama Yanga wamkabidhi Yusuf Manji aiendeshe Yanga kama klabu binafsi, mikataba ya kumkabidhi nembo kusimamiwa na Baraza la Wadhamini.

Katika mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kipindi hiki, Manji amesema amepeleka ombi la kuikodisha Yanga kwa miaka 10.

“Nitaikodisha kwa asilimia 75 na 25 inabaki kwa wanachama. Nataka kuikodisha timu na nembo, majengo ya klabu yanabaki kuwa mali ya wanachama.

“Katika miaka 10, ikipatikana faida 25 inakwenda kwa wanachama na klabu na 75 kwangu. Kama itakuwa ni hasara basi inakuwa hasara yangu, hakuna hasara upande wa wanachama au klabu,” alisema.

Manji amesema masuala ya timu kuhusu usajili, mishahara, uendeshaji kama safari na gharama nyingine zitakuwa chini yake

Wakati huo huo, Wajumbe watatu wa Kamati Utendaji ya Yanga Ayoub Nyenzi, Hashim Abdallah na Salum Mkemi wavuliwa uanachama wa klabu hiyo.
 
Nimefurahishwa na wanachama wa Yanga kumkubalia Manji kujikopesha Klabu ya Yanga kwa asilimia 75% huku wanachama wakibaki kuhudhuria mechi tu ambazo klabu yao itakuwa inacheza na kushangilia ikishinda au kuzomea ila hawatakuwa na sauti hata kidogo ya mwenendo wa klabu yao. Manji akiamua Yanga ipate matokeo mabaya hakuna wa kumpinga, kwani wanachama hawatakuwa na sauti.

Nilitegemea wanachama wa Yanga wangekubaliana kuwa Manji auziwe hisa tena asilimia 50% na zilizobaki ziwe za wanachama ili pande zote mbili zishiriki kwenye maamuzi ya Klabu, lakini kwa utaratibu wa kumkopesha Manji kwa asilimia 75% wanayanga make mkao wa kulia tu hamtakuwa na maamuzi kwa miaka 10 bora mngempa hata miaka 5 kwanza ya majaribio.
 
Back
Top Bottom