Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Chakula cha Usiku na Timu ya Yanga kwa ajili ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Magogoni jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Juni, 2023.


6e3d3d10-4c8c-4042-b209-2313adf78995.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Medali kama ishara ya shukrani kutoka kwa Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said wakati wa hafla ya kuipongeza timu ya Yanga iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.

381e9f82-ebd5-44ad-9c4d-cedb2e3c0620.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi, wachezaji wa timu ya Yanga pamoja na wadau mbalimbali wa michezo wakati wa hafla aliyowaandalia kuwapongeza Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.


Rais wa TFF Wallace Karia akitoa salamu za Shirikisho hilo amemshukuru Rais kwa mwaliko wa leo.

IMG_7471.jpeg

Wallace Karia, Rais wa TFF
Ameipongeza timu ya Yanga kwa nafasi waliyofikia kwa kucheza fainali na kushinda mchezo wa mwisho hivyo kuiletea heshima Nchi.

Ushindi wa Yanga umeleta deni kubwa kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ambayo itacheza huko Algeria ili kufuzu michuano ya AFCON.

Shirikisho la Mpira litahakikisha mwakani timu zote 4 zinazoshiriki kimataifa zitafanya vizuri zaidi ikiwezekana kuchukua kombe.

Rais wa Yanga Eng. Hersi amemshukuru Rais kwa motisha aliyotoa, ilisababisha wavuke hatua ya mtoano, na kuongoza kwenye hatua ya makundi.

Hamasa ya Rais iliwapa hamasa vijana hao na kwa mara ya kwanza klabu kutoka Tanzania imevaa medali ya CAFCC.
Mzee mpili.jpg

Mzee Mpili

IMG_7470.jpeg

Eng. Hersi Said, Rais wa Yanga
Eng. Hersi amesema Medali waliyovaa Rais Samia anastahili kuliko mtu mwingine yeyote. Vijana wa Yanga walipigana vita kubwa nchini Algeria, mchezo uligubikwa na kila aina ya vioja. Pamoja na hayo, vijana wa Yanga waliweza kushinda.

Amemuahidi Rais Samia kuendelea kuongeza idadi ya Makombe kwenye utawala wake na kwamba timu ya Yanga itakuwa ya kwanza kuleta kombe la Afrika Tanzania.

Ili kujenga uwanja wake, Hersi amemuomba Rais Samia kuwaongezea sehemu ya ardhi ya mtaa wa jangwani ili uwanja uwe mkubwa.

Naye Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma amesema Rais Samia amesaidia sana kuleta hamasa. Jumla ya magoli 26 yamefungwa na Tsh. 190 Milioni imetolewa kama motisha.
83228b9b-038b-429c-8ab4-78d8e8d325f6.jpg

IMG_7472.jpeg

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma
Amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege, ni motisha na hamasa iliyotoa maana kuwa Serikali ilikuwa pamoja na timu ya Yanga.

Amewashukuru pia viongozi wa Yanga kwa kuendeleza maono ya waasisi wa klabu hiyo hivyo wanastahili heshima.

Utani wa jadi ni suala lenye manufaa makubwa sana katika kukuza michezo. Simba wanakataa mafanikio ya Yanga sababu ya utani wa jadi lakini moyoni wanayatambua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapongeza timu nzima na upngozi wa Yanga wa kuitoa kimasomaso Tanzania.

Amemtambulisha Rubani Neema kwa kuileta ndege kubwa ya mizigo na kuifikisha salama kwenye ardhi ya Tanzania.

Mwanzoni mwa mashindano lilikuwa ni suala la timu binafsi lakini baada ya kufika hatua ya juu zaidi, Timu ya Yanga ililiwa inasimama kwa niaba ya Taifa.

Kufika fainali kwa Yanga kumerejesha heshima ya Tanzania, sasa nchi imerudi kwenye ramani ya michezo. Haikuwa rahisi kwa kuwa nchi nyingi zilitoa timu zao, sio jambo jepesi.

Amewaomba Viongozi na wadhamini wa Yanga kuendelea kutoa ari, motisha na hamasa kwa vijana kwa kuongeza maslahi yao.

Amesema mwaka 1993 timu ya simba ilifika pia hatua hii ya juu zaidi, sasa kinachotakiwa ni matayarisho na hamasa.

Timu yoyote itakayokuwa inawakilisha taifa kimataifa itakuwa timu ya kitaifa. Mambo ya utani wa jadi yaishie humu ndani maana mafanikio yanapotokea yatakuja Tanzania. Utaifa uwe mbele kuliko mengine.
b30b874b-0b40-41a6-a5bd-e30343926951.jpg

IMG_7473.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Tanzania inadhamiria kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027 pamoja na Uganda na Kenya hivyo ujenzi wa viwanja na kurekebisha vilivyopo uendelee.

Amewataka wafanyabiashara wa Sekta binafsi kuwekeza zaidi kwenye michezo kwani ni ajira, pia kwa kuwa Serikali imewaachia wafanye biashara kwa uhuru wanapaswa kurudisha kwa jamii.

Rais amesema huwa anafuatilia sana mashindano ya ndondo, mashindano yanayoibua vipaji vya timu ya taifa. Waandaaji wa mashindano hayo atawashika mkono ili waendelee kuibua vipaji hivyo kwa kuwa samaki hukunjwa akiwa bado mbichi.

Amevitaka vilabu kujipanga zaidi mwakani ili kombe hilo lije Afrika.

Pia, ameeleza kuwa hafurahii ugomvi ulipo kati ya Yanga na Feitoto na amewataka viongozi wa klabu hiyo kuumaliza mzozo huo.

71e27fda-1c83-417a-b9e3-24e59047b97a.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji na Makocha wa timu ya Yanga wakati wa hafla ya kuwapongeza kwa kufanikiwa kufika na kucheza mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Shirikisho Afrika (CAF) nchini Algeria. Hafla hiyo ya kuwapongeza Yanga imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.

ce0b43ff-602c-479b-97d7-0163ecc9f37f.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji, Makocha na viongozi wa timu ya Yanga wakati wa hafla ya kuwapongeza kwa kufanikiwa kufika na kucheza mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Shirikisho Afrika (CAF) nchini Algeria. Hafla hiyo ya kuwapongeza Yanga imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.
 
Nchi isiyo na mafanikio yoyote yale yaliyo ya maana, kwenye nyanja yoyote ile, inaona timu kufikia fainali ya kakombe kaliko obscure duniani kuwa ni mafanikio.

Pity the fools.
Fool ni wewe mwenyewe kutokana na akili yako iliyo ndogo kuliko ya mende. Wenye akili wanajuwa nini kinaendelea.

Michezo ndiyo inaunganisha watu wenye itikadi tofauti hata kama hupendi bali huo ndiyo ukweli. Siasa za Tanzania ziko kwenye hizi timu 2
 
Nchi isiyo na mafanikio yoyote yale yaliyo ya maana, kwenye nyanja yoyote ile, inaona timu kufikia fainali ya kakombe kaliko obscure duniani kuwa ni mafanikio?

Pity the fools.

Hawajali chochote kuhusu nchi its is all about power, hapo mbinu ni kuwateka washabiki wote wa Yanga ili wampiganie na kumtetea, anajaribu kila awezalo abakie, kama mnakumbuka alipoingia na kuona mambo magumu alikuja na machief akataka kuleta mambo waliotumia Wakoloni akitaka kufufua uchief ili wampiganie kikabila ikabumu sasa kaingia kwenye mpira mwisho wa siku its all about power na haina uhusiano wowote na football wakishindwa kila kitu watahamia kwenye Uislamu ni swala la muda tu, na huo ndio utakuwa mwisho wa Tanzania, wanaingiza hii nchi shimoni kwa uroho wa madaraka, …
 
Naangalia live dinner Ikulu. Naona wachezaji wa Yanga wameandaliwa kwenye protocol, hasa positioning ya mikono kiheshima. Hili nililiona kwa Mandonga akiwa Kenya kama mtu anayefahamu protocol za nchi hasa kuvua kofia wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa. Sasa shida nimeiona kwa Naibu Waziri akiwa anapiga picha na Mh Rais ameachia mikono, hii kiprotokali inaruhusiwa kwa mh Rais peke yake. Ile semina kule Ngurdoto nadhani ilikuwa fupi sana.
 
Back
Top Bottom