FT: TZ Prisons FC 1-2 Yanga SC | NBC Premier League | Sokoine Stadium | 11.02.2024

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
17,655
14,817
Match Day
1000036439.jpg

#NBCPremierLeague
️ TZ PrisonsYoung Africans SC
11.02.2024
Sokoine
10:00 Jioni

Yanga wanaingia kwenye mchezo wao wa kukamilisha mzunguko wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons wakiwa na alama 37. Kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara.

Wameshinda Michezo 12, wamepoteza 1 na kwenda sare 1.

Wenyeji wao Tz Prisons wako nafasi ya 9 kwenye msimamo wakiwa na alama 17. Wameshinda Michezo 4. Sare 5 na Wamepoteza michezo 5.

Historia inaonyesha Kwenye michezo 29 iliyowakutanisha.
Prisons wameshinda mchezo 1. Wameenda sare mara 10.
Yanga wameshinda mara 18.

Inaweza kuwa game yenye ushindani kwa hali ilivyo katika ligi yetu.

HAPPY BIRTHDAY YOUNG AFRICANS SC
1000036438.jpg


Kikosi cha Tz Prisons Kinachoanza.
1000036470.jpg


Kikosi cha Yanga kinachoanza.
1000036473.jpg


#DaimaMbeleNyumaMwiko#.

Mpira umeanza kwa kasi ndogo!
Unachezwa zaidi kati.

Dakika ya 03'
Mpira unaendelea.
0-0

Dakika 06'
Yanga wanapata kona, inapigwa haileti madhara. Inaondolewa na Prisons.

Dakika 07'
Gooooooooal...
Yanga wanapata goli zuri sana likifungwa na Mzize, kupitia assist safi sana kutoka kwa Pacome!!
0-1

Dakika 10'
Prisons wanapata kona, inapigwa inaondolewa.

Dakika 13'
Kuna mchezaji wa Prisons anapata injury kubwa kidogo.
Ambulance imesogezwa uwanjani.
Inawazekana ameumia sana.
Aligongana na Lomalisa.
Akajigonga kichwa.
Lomalisa anapewa kadi ya Njano!!

Dakika 16'
Linatokea shambulizi langoni mwa Prisons.
Mzize anakosa goli hapa.

Dakika 25'
Free kick inapigwa na Prisons inakuwa haina faida.

Dakika 27'
Free Kick nyingine kwa Prisons inapigwa inakuwa goli kick.

Dakika 33'
Chona wa Prisons anapata kadi ya njano.
Yanga wanapata free Kick haileti shida kwa Prisons.

Dakika 37'
Yanga wanapata kona haileti faida kwao.

Dakika 44'
Prisons wanapata kona, haileti faida kwao.
Yanga wanajaribu kufanya kaunta attack inazimwa.

Gooooli wamekosaa goli la wazi kabisa hapa Yanga.
Max Nzengeli anakosa goli la wazi kabisa kabisaa.

Dakika 45'
Nyongeza ni 4' kukamilisha kipindi cha pili.

Pacomeeeeee....Goliiiiiiii.
45+3'
Goli la pili kwa Yanga.

MAPUMZIKO....

0-2.
=========================
Kipindi cha Pili.

Dakika 47'
Mpira unaendelea timu zote zinacheza kwa mashambulizi ya kujihami hapa.
Kuna mabadiliko wamefanya Prisons. Kipindi hiki cha pili.

Dakika 56'
Metacha anacheza faulo hapa, inakuwa mkanganyiko kama faulo ama vipi.
Metacha anapewa Red

Dakika 63'
Farid Anatoka anaingia Msheri.
Free kick kwa Prisons nje kidogo ya 18.
Gooooli!!!
Mgunda anaipatia Prisons goli la kwanza.
1-2

Dakika 65'
Mayombya wa Prisons anapewa kadi ya njano.

Dakika 75'
Prisons wanapata free kick nje kidogo ya 18. Inapigwa haileti faida

Wakati huo wanafanya
Sub.
Mzize Out
Guede Inn

Dakika 79'
Yanga wanapata kona, inapigwa haiwapi faida yoyote.

Dakika 84'
Yanga wanapata free kick nje kidogo ya 18.
Haiwapi faida yoyote.

Dakika 86'
Kadi nyekundu kwa Mchezaji wa Prisons ameshika mpira kwa maksudi.

Azizi anapiga Free kick haileti faida.

Dakika 90'
Prisons wanapata kona hapa.
Anapiga wanakosa kosa hapa Prisons.

Dakika zilizoongezwa ni 7'

Full Time.
Prisons 1 -2 Yanga.

1000036506.jpg


HAPPY ANNIVERSARY YANGA.
 
Kesho saa tisa na nusu lazima nifike dimbani hapo Sokoine kuona miujiza ya kina Yao Yao, Pacome, Muda, Aziz Ki wakisumbuana na askari magereza wanaopenda kucheza mpira wa nguvu

Kuna raha ya kucheki mechi live na kesho game itakua nzuri sana kama kutakuwa hakuna mvua.

Ni dakika ya 43 Yanga inapata faulo, Aziz Ki anapiga shuti kali linanesa kipa anapangua lakini mpira unamzidi nguvu , Goaaaal !!
 
Guede aanze ili kupata uzoefu.

Tahadhari kwa Refa.
Kama Prison watafunga goli halali wana kila haki ya kupewa goli lao.
Guede naona anachezeshwa ili Gamondi akwepe lawama za kukalisha wachezaji benchi wanaosajiliwa kwa gharama na kulipwa mishahara mikubwa,

Apewe mechi tatu tu, kama hakuna kitu ni heri ya Kibabage afosi kupanda, nikikumbuka goli la kibabage kule Ghana lililokataliwa naumia sana.
 
Kesho saa tisa na nusu lazima nifike dimbani hapo Sokoine kuona miujiza ya kina Yao Yao, Pacome, Muda, Aziz Ki wakisumbuana na askari magereza wanaopenda kucheza mpira wa nguvu

Kuna raha ya kucheki mechi live na kesho game itakua nzuri sana kama kutakuwa hakuna mvua.

Ni dakika ya 43 Yanga inapata faulo, Aziz Ki anapiga shuti kali linanesa kipa anapangua lakini mpira unamzidi nguvu , Goaaaal !!
Hii imekaa vizuri sana.
Utatuwakilisha
 
Guede naona anachezeshwa ili Gamondi akwepe lawama za kukalisha wachezaji benchi wanaosajiliwa kwa gharama na kulipwa mishahara mikubwa,

Apewe mechi tatu tu, kama hakuna kitu ni heri ya Kibabage afosi kupanda, nikikumbuka goli la kibabage kule Ghana lililokataliwa naumia sana.
Kibabage ni bonge la mchezaji.
Binafsi namkubali sana.
Hata ukimweka namba 9 anafunga magoli bila shida.
Kumbuka hata Mayele hakuanza kama mfungaji.
 
Posta ya mechi yenyewe inajieleza, kazi kazi.

Prisons ni wagumu ila muhimu ushindi, wakicheza vizuri kama DRC na sisi tukiondoka na ushindi kama SA ndilo jambo la msingi.
 
Back
Top Bottom