Hatimaye Babaj Yawa Zimamoto

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua Bajaj ambayo imetengenezwa ili kumudu kazi ya kuzima moto hasa kwenye maeneo yenye barabara nyembamba katika maonesho yaliyoandaliwa na Kampuni ya Spray and Fumigation Services Limited, bungeni Dodoma Alhamisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

04_11_bcuf58.jpg
 
Karne ya 21 tunatumia bajaj kuzima moto! Jameni usanii mwingine haufai, hizi zimamoto zinazobeba zaidi ya lita 30,000 za maji zina shindwa kuzima nyumba moja itakuwaje bajaji ya lita 500 au 1000! Huu si utani jameni?
 
Mungu wangu nisaidie Nchi hii ina viongozi au Wendawimu? Tunaelekea wapi sasa? huu siutani
 
Huu ni mbadala wa gari la zimamoto hasa uswazi ambako hakuna njia. Swali ni je hii bajaji inabeba maji kiasi gani?

Serikali ya Kikwete kiboko, haya sio masihara kweli??.

208308_1918882580898_1507034707_32048858_6018225_n.jpg
 
nchi ya abrakadabra,mtoto wa mkulima nae kafunga safari koote huko kwenda kuangalia huu upuuzi,kweli viongozi tunao:rip:
 
Mungu wangu nisaidie Nchi hii ina viongozi au Wendawimu? Tunaelekea wapi sasa? huu siutani
Nchi hii ni kama haina viongozi mkuu, maana kila siku hatukosi kushangaa, bado bajaji za kubebea kina mama wajawazito. Si mchezo tunaelekea kwenye ujima kwa kasi. Kwa nini barabara ziwe nyembamba kama nyumba zimejengwa kwa kufuata utaratibu. Hii inaonyesha serikali haina mpango wa kuzuia ujenzi wa makazi bila mpangilio.
 
Mkubwa mzima Pinda anashangaa kitu cha kitoto sijui ninini hicho!...Tangu lini bajaji ikawa zima moto jamani?
Hivi vidudud ni kama vile vya kubebea wajawazito, nadhani aliyewasupply vile ndo huyohuyo kaleta na hivi tena!
Amewashika masikio hawafurukuti!..Ashagundua kuwa ni mazezeta wote!...my hairs!
 
Huu ni mbadala wa gari la zimamoto hasa uswazi ambako hakuna njia. Swali ni je hii bajaji inabeba maji kiasi gani?

Serikali ya Kikwete kiboko, haya sio masihara kweli??.

208308_1918882580898_1507034707_32048858_6018225_n.jpg

haya ndio maisha mapya kwa kila mtanzania! Ari mpya zaidi, nguvu mpya zaidi na kasi mpya zaidi. CCM oyeee
 
Wajawazito bajaj, moto bajaj, bado nini sijui... yeye mbona hapandi bajaj, hivi hiyo bajaj ikijaza hicho kitenki chake itatembea kweli, I think these people are trying our patience. kwa hiyo ndio ubunifu huo, kweli kiboko!!! hicho labda wakitumie kuzimia sigara. I wont buy this crap.
 
hii ndo creativity ya mtoto wa mkulima na Mr.handsome? Haya ndo marejesho ya pesa ya kagoda,EPA kwa watanzania
 
Nina wasiwasi na Elimu ya huyu Waziri Mkuu, jamani!!! huu ni utani, Jokes
 
Madai yao eti ni wabunifu, hebu cheki matairi ya hiyo bajaji kama yanahimili walau lita 1000?

Ngoja tusubiri bajaji ijayo itakuwa maalum kwa ajili ya nini?? mi nahisi watabuni bajaji mfano wa trekta...
 
Naona aibu kujiiita Mtanzania hawa viongozi wetu sijui akili zao zipo nyumba ndogo tuuuu, upuuzi gani huu jamni :rip::rip::rip::rip::rip:
 
Mmepata bei yake ni kiasi gani? serikali imetoa order ya ngapi? inaweza enda kasi kiasi gani? ilikuwa ilishatumika nchi gani? n.k,n.k,n.k. Watu wamepata baraka za mkuu na wamesha tengeneza ulaji, Tanzania bana, naipenda.
 
Nasikia ili kukabiliana na hali ya jotomabasi ya bajaj nayo yatatua bongo hivi karibuni

1tuktuktuk1.jpg
 
Ukweli sina uwezo kuiwezesha Tanzania kiuchumi ila bajaji kuzimia moto jamani hata huo ufisadi huu ni noma ::help:
 
Back
Top Bottom