Halima Nabalang'anya: Serikali Isimamishe Mchakato wa Kuuzwa Kiwanda Saruji Tanga

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
HOTUBA YA WAZIRI KIVULI WA VIWANDA NA BIASHARA -ACT WAZALENDO NDG. HALIMA YUSUF NABALANG’ANYA KUHUSU MPANGO WA BAJETI WA WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24.

Utangulizi.
Tunafahamu kuwa tupo katika kipindi cha mijadala ya bajeti mbalimbali, wadau na wananchi wanaofuatilia kwa karibu ili kujiridhisha na mgawanyo wa rasilimali na mipango ya Serikali kuhusu kutatua changamoto nchi macho, masikio yapo Bungeni. Jana Alhamisi tarehe 04 Mei 2023, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb.), aliwasilisha Bungeni mpango wa Wizara na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Sisi, ACT Wazalendo kupitia Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara tumefanya uchambuzi wa mpango na bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, taarifa ya utekelezaji kwa miaka miwili iliyopita na kutumia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/22.

Kwaniaba ya Waziri wa Biashara na Viwanda (Mimi Ndugu Edgar Mkosamali, Waziri Kivuli wa Madini) nitawasilisha uchambuzi wa hotuba hiyo. Katika kutekeleza wajibu huu, hotuba hii ya Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara wa ACT Wazalendo imeangazia maeneo makuu saba (7) kuhusu hotuba ya bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2023/234.

1. Mchango mdogo wa Sekta ya viwanda katika pato la taifa na ajira.
Mchango wa sekta ya viwanda katika pato la taifa letu bado hauridhishi, tofauti na matarajio ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (5). Mpango ulibainisha kwamba, ili nchi yetu ifanikiwe kufika uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025, ni sharti sekta ya uzalishaji (manufacturing) ichangie wastani walau wa 40% katika pato la taifa ifikapo 2025.

Katika kufuatilia utekelezaji wa bajeti na mwenendo wa mchango wa sekta ya viwanda kwa miaka mitatu; (3) yaani 2019, 2020 na 2021 taarifa za wizara zinaonyesha kuwa mchango viwanda katika uchumi ni wakusuasua. Kwa mwaka 2019 mchango wa sekta ya viwanda kwenye pato la taifa ulikuwa 8.5%, 2020 ulikuwa 8.3% na mwaka 2021 ulikuwa ni 7.8% na 2022 ni 7.8%

Pamoja na hayo, taarifa ya ofisi ya taifa ya takwimu (NBS, 2021) inaonyesha mchango wa sekta ya viwanda kwenye ajira ni 8.0% pekee. Kwa mujibu wa Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara katika hotuba ya bajeti ameeleza ajira zinazotokana na viwanda ni takribani 345,615 kwa mwaka 2021 ukilinganisha ajira 370,485 zilizozalishwa mwaka 2020. Ndani ya mwaka mmoja, ajira 24,870 zimepotea.

Kwa kutazama mwelekeo huu wa sekta ya viwanda ni wazi mpango wa taifa unapotea, dira ya viwanda kuwa injini ya kusukuma maendeleo na ustawi wa wananchi inafifia. Suala la maendeleo ya viwanda linabaki katika hotuba na maneno matupu ya viongozi, hata sehemu ya ajira anazotaja waziri ni ajira za muda mfupi, ni chache ndio ajira za moja kwa moja.

Hivyobasi, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali iweke mikakati madhubuti ya kuhakikisha Sekta hii ya Viwanda inapewa kipaumbele ili malengo ya “Kujenga Uchumi Shindani wa Viwanda kwa Maendeleo ya watu” yaweze kufikiwa, vinginevyo Viwanda vilivyopo havitakua na maana yoyote kama havisaidii kuleta maendeleo ya watu.

2. Sekta ya viwanda haifungamani vya kutosha na uzalishaji wa malighafi - kilimo, uvuvi na madini:
Katika historia ya nchi yetu na nchi nyingine nyingi Afrika hususani katika dunia ya tatu ajenda ya viwanda kwa muda mrefu imekuwa ikijadiliwa kwa namna tofauti tofauti. Katika kufuatilia hotuba ya bajeti na mipango ya wizara kwa mwaka huu, ina ukosefu wa mahusiano na uwiano mdogo sana wa malengo ya ujenzi/ uwekezaji wa viwanda na sekta ya uzalishaji wa malighafi hususani kilimo.

Hakuna viwanda vya kutosha kujikita katika usindikaji wa mazao ya kilimo (hususani mazao mkakati) na uzalishaji wa bidhaa muhimu kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini. Shabaha ya sasa ya uwekezaji na uendelezaji wa viwanda sio katika kujenga uwezo wetu wa nchi kujinasua katika hali ya utegemezi.

Takwimu za viwanda kwa mujibu wa wizara ni kuwa tuna viwanda vidogo sana 62,400 sawa na 77.07%, viwanda vidogo ni 17,274 navyo vinachukua 21.33% na viwanda vya kati vipo 684 sawa na 0.84% na viwanda vikubwa vipo 618 sawa na 0.76%. Licha ya takwimu hizi bado mazao mengi yanapotea shambani haizidi hata asilimia 20 ya viwanda hivyo vyenye mafungamano ya moja kwa moja na kilimo, uhakika wa masoko ya wakulima wetu bado ni mdogo sana.

Mazao kama ya kahawa, pamba, chai, ufuta, korosho na chikichi ndio mazao yanayoongozwa kuuzwa nje na kwenda kuwa malighafi katika viwanda vya nchi zingine huku nchi yetu ikibaki na uhitaji wa Bidhaa zinazotokana na mazao hayo, wakulima wa mazao mengine kama machungwa, nanasi, embe, tikiti na parachichi nao hawaoni mwanga wowote wa kuwakwamua kutupa Mazao yao kila msimu kwa kukosa soko.

Upande mwingine, hakuna viwanda vya kutosha vya kuzalisha bidhaa za kutosha kuhudumia Sekta ya kilimo, bado mbolea kwa sehemu kubwa inaagizwa kutoka nje hadi Februari, 2023 mahitaji ya mbolea ilikuwa ni tani 698,260. Huku uzalishaji wa ndani ni tani 28,672 sawa na asilimia 4.1.

Aidha, viuatilifu na viuwadudu (petsides and insectside) kwa sehemu kubwa vinaingizwa kutoka nje. Aidha, vifaa na zana za kilimo kwa sehemu kubwa zinatoka nje, viwanda vyetu havijibu mahitaji na soko la kilimo. Kwa maneno mengine, Sekta ya Viwanda na Sekta za Kilimo na Uvuvi zinatembea njia tofauti, jambo hili halina Afya katika maendeleo ya Taifa.

Waziri Dkt. Ashatu Kijaji hakuliambia Bunge mkakati wao kama Wizara wa Kuhakikisha Zana za Kilimo na Pembejeo nyengine zaidi ya Mbolea zinazalishwa nchini, hiyo inamaanisha kuwa Wakulima wataendelea kuumia kwa kuzalisha kwa gharama kubwa zaidi zinazotokana na Pembejeo na kidogo watakachovuna hawatakua na Uhakika wa Viwanda vya kununua hapa nchini.

Katika bajeti ya Serikali mwaka huu, fedha zilizotengwa kuendeleza viwanda vinavyoweza kuleta uhusiano na uwiano na sekta za uzalishaji bado ni kidogo, hivyo haiwezi kukidhi shabaha ya kufungamanisha uzalishaji na maendeleo ya viwanda.
Kilimo na viwanda ni pande mbili za sarafu moja, ni lazima vifungamanishwe. Katika Ilani ya ACT Wazalendo 2020 tulisema “Tutafungamanisha sekta ya kilimo na sekta ya viwanda, kwa kuhakikisha kwamba viwanda vya ndani vinapata zaidi ya asilimia 80 ya mahitaji yao kutoka kwa wakulima, na kwamba wakulima wanafaidi bei nzuri ya mazao yao na soko la uhakika,”

ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuhakikisha inasimamia uwekezaji na ujenzi wa viwanda unaotegemea zaidi malighafi kutoka ndani. Pia, Serikali ifungamanishe uendelezaji wa viwanda na sekta ya madini hususani makaa ya mawe na chuma kwa kuharakisha utekelezaji wa Mradi Linganga na Mchuchuma.

3. Mazingira ya biashara kwa Wafanyabiashara wadogo (Machinga) sio mazuri.
Kwa kutazama uelekeo wa hotuba ya bajeti ya wizara, mikakati iliyowekwa katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara imewagusa zaidi Wafanyabiashara wa kati na Wafanyabiashara wakubwa. Mazingira ya Wafanyabiashara madogo (wamachinga, mamalishe, na wajasiriamali wengine) bado hayajawekewa mkakati wa kuondoa changamoto zao. Sekta ya biashara ndogo ina mchango mkubwa sana nchini kwenye pato la taifa wastani wa asilimia 22 na mchango wake kwenye sekta ya ajira ni wastani wa asilimia 14 ya nguvu kazi nchini zinapatikana kwenye biashara ndogo.

Hali ya sasa ya wafanyabiashara hawaonekani wakilindwa kisheria au shughuli zao kutambulika kama halali kwenye mchango wa uchumi wetu. Kwa, kifupi Wafanyabiashara wadogo hawachukuliwi kama injini ya maendeleo ya miji na majiji. Uamuzi wa kuwapanga Wafanyabiashara wadogo umetikisa uaminifu wao kwa taasisi za kifedha. Matukio kuungua moto kwa Wafanyabiashara wadogo yamesababisha hasara kubwa sana kwa Wafanyabiashara.

Tafiti nyingi, zinaonyesha kuna uhusiano mkubwa shughuli za wafanyabiashara wadogo na ukuaji na uendelezaji wa viwanda vidogo nchini. 47% ya biashara ndogo zinahusisha bidhaa za kilimo ambazo zinaongezwa thamani.

Katika Miji na Majiji Wamachinga, wamekua kama wahalifu, migambo wa Jiji katika Jiji la Arusha, Tanga, Mwanza, Dar es salaam na Mbeya wanawageuza kitega uchumi kwa kuwavunjia Biashara zao na kupora Mitaji Yao, Serikali hii inayosemwa kua ni Serikali ya Huruma haioni njia Bora ya kuwawekea mazingira na Sera Rafiki wafanyabiashara wadogo Bali kuwapora mitaji Yao.

Tunataka “Taifa la Wote kwa Maslahi ya Wote” Wizara hii si ya Wawekezaji pekee, Serikali iache ubaguzi na upendeleo, iweke mbele aslahi ya Watanzania inapoweka mipango yake isiishue tu mipango kwa ajili ya Wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa bali pia ijumuishe na kuweka wazi mipango kama hiyo kwa wafanyabiashara wadogo;

Hivyo, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kusitisha maramoja Operesheni za Mara kwa mara za kuwaondosha Machinga katika miji, mitaa na majiji badala yake iweke mipango miji itakayozingatia mahitaji ya makundi yote nchini.

Vilevile, tunapendekeza kuwa Serikali kwa kushirikiana wizara ya viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na wizara ya TAMISEMI kusikiliza na kuondoa vikwazo kwa wafanya biashara wadogo.

4. Kufufua viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazoweza kukidhi mahitaji ya ndani
Mkakati wa ujenzi wa viwanda nchini bado hauleweki. Wakati Serikali ikisema inaweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kwa ajili ya kuhakikisha sekta ya viwanda inazalisha bidhaa zinazohitajika kwa wingi nchini ili kukidhi mahitaji na kuondoa utegemezi kutoka nje, mwenendo wa uwezo na uzalishaji wa viwanda vinavyojibu mahitaji ya watu wengi kama vile sukari, mafuta ya kula, nguo na mavazi, viwanda vya mbolea, saruji, na sabuni haujibu wito huo.

Viwanda vingi vya nguo, mafuta ya kula, sukari na hata saruji, vilibinafsishwa na baadaye vikageuzwa kua maghala ya kuhifadhi bidhaa kutoka nje. Viwanda kama Urafiki, Karibu Textile (KTM), mfano ni viwanda vya madawa ya binadamu kama kile cha Keko, viwanda vya tumbaku, korosho n.k. Kuuliwa kwa viwanda hivi kumeongeza utegemezi wa bidhaa muhimu kutoka nje kiasi cha kuondoa uhuru wetu wa kujiamulia juu ya mahitaji ya ndani.

Tunategemea mbolea ya kuagiza kwa zaidi ya asilimia 95, nguo na mavazi kwa zaidi ya asilimi 90, sukari kwa asilimia zaidi ya 50, dawa asilimia 95 na bidhaa zingine.
Kama tulivyoonyesha huko nyuma kuwa bado uzalishaji wa viwanda vyetu nchini hauendani na mahitaji ya ndani. Hii ni kusema kuwa viwanda vyetu vinazalisha bidhaa nyingi za anasa au bidhaa kwa ajili ya kusafirisha nje. Ni muhimu kwa Serikali kusimamia sekta ya viwanda kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya walio wengi (goods for mass consumption).

Ni rai yetu kuwa Serikali ianze sasa na ionyeshe kwenye bajeti yake katika kufufua viwanda vya nguo, viatu na vifaa vya kilimo. ACT Wazalendo kwenye Ilani yetu ya Uchaguzi 2020 tulisema kuwa “Serikali ya ACT Wazalendo itawezesha ufufuaji wa viwanda vya kuchakata pamba na kuzalisha nguo (textile industries) ili kuzalisha bidhaa kama vile vitenge, vijora, madera na batiki zenye ubora wa hali ya juu”

5. Kupanda kwa bei za bidhaa muhimu nchini:
Kumekuwa na mwenendo wa kupanda kwa bei ya bidhaa nchini kuliko kawaida. Suala hili tulilizungumzia katika hotuba yetu ya mwaka jana lakini inaonyesha bado mwenendo wa bei za bidhaa unazidi kupaa. Miongoni mwa bidhaa zinazoonyesha kupanda kwa kasi ni pamoja na vifaa vya ujenzi [saruji, nondo na bati] na bidhaa za vyakula [mchele, maharage na mahindi].

Ingawa katika hotuba ya bajeti 2023/24 Waziri wa uwekezaji viwanda na biashara ameonyesha kushuka kwa bei ya vifaa vya ujenzi. Kwa mfano, nondo moja ya mm 12 imeshuka kutoka shilingi 26,865 kwa mwaka 2022 hadi kufikia 24,417 kwa Februari 2023 sawa na 9%, nondo moja ya mm16 imeshuka kutoka 46,097 kwa mwaka 2022 mpaka 45,887 sawa na asilimia 1. Kushuka kwa asilimia 1 bado hakujaweza kumrahisishia mwanachi wa kawaida kuweza kumudu gharama hizo. Kwa upande wa saruji mfuko wa kg 50 haujashuka bei. Kwa upande wa mabati ndiyo yameongezeka bei.

Katika bidhaa za vyakula Waziri amekiri kupanda kwa bei ya vyakula nchini kama mchele mahindi na maharage. Maharage yamepanda kutoka shilingi 215,193 kwa gunia la kilo 100 kwa mwaka 2022 na kufikia 301,297 mwaka 2023 ongezeko la asilimia 40, Mahindi gunia la kilo 100 limeongezeka kutoka 90,330 kwa mwaka 2022 mpaka kufikia 115,141 kwa mwaka 2023 ni sawa na ongezeko la asilimia 27.5, mchele gunia la kilo 100 limeongezeka kutoka shilingi 216,738 kwa mwaka 2022 mpaka kufikia 291,819 mwaka 2023.

Hali ya ongezeko hili kubwa la bidhaa limepandisha gharama za maisha kwa wananchi. Ingawa Serikali imekiri kupaa kwa bei hizo, lakini Waziri hajaonyesha mpango na hatua za kukabiliana na mwenendo huu.

ACT Wazalendo inaendelea kusisitiza Serikali kufufua viwanda vya ndani vitakavyoweza kuzalisha bidhaa za kukidhi mahitaji ya ndani. Aidha, katika suala la bei ya bidhaa za vyakula tunaitaka Serikali kudhibiti mfumuko huo holela wa bei kwa kuipa uwezo NFRA kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha angalau kwa muda wa miezi mitatu.

6. Mfumo mbovu wa Stakabadhi za Ghalani:
Wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara kupitia Bodi ya Leseni ya Maghala (Tanzania Warehouse Licensing Board - TWLB) inasimamia mfumo wa Stakabadhi za mazao ghalani ulioanzishwa kisheria kwa Sheria Na. 10 ya mwaka 2005 na kutekelezwa kwa kanuni za mfumo za mwaka 2006. Mfumo huu sasa unatumika katika maeneo mbalimbali nchini kwa mazao ya Korosho, Kahawa, Pamba, Ufuta, tumbaku, Mpunga na Mahindi.

Uzoefu wa utekelezaji wa mfumo huu umekuwa ukiacha maumivu makubwa sana kwa wakulima wetu badala ya kuwa msaada. Serikali na vyama vya ushirika wamekuwa madalali wa mazao badala ya kuwa watafuta wateja wa bei yenye tija kwa wakulima. Mfumo huu wa masoko unawanufaiaha zaidi watumishi wa vyama vya ushirika, watumishi wa Serikali na Wafanyabiashara wanaonunua mazao kwa mtindo wa kangomba. Mazao yaliyoathirika zaidi na sheria hii ni korosho, ufuta, mbaazi na tumbaku.

Katika kutazama mpango wa bajeti na vipaumbele vya Serikali kwa mwaka 2023/24 Serikali imewekeza kwenye kutangaza na kutaoa elimu kwa kupanua zaidi matumizi ya Stakabadhi ghalani lakini hatujaona mkakati wa kuboresha mfumo huo ili kuwezesha na kunufaisha wakulima na kuboresha sekta ya viwanda kupitia kuimarisha kilimo chetu.
ACT Wazalendo tunapendekeza mfumo wa malipo wa stakabadhi ghalani uimarishwe uwe wa kieletroniki na uwe wa papo kwa papo.
Pia, utumike mfumo wa soko la bidhaa (commodities exchange) kwa kuwashirikisha moja kwa moja wakulima wenyewe.

7. Mgogoro wa utwaaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga.
Pamekuwepo na mivutano, mijadala na mabishano miongoni mwa wadau kuhusu uamuzi wa Tume ya ushindani wa Haki (FCC) kuidhinisha muungano wa Kampuni za Saruji za Twiga na Tanga. Uamuzi huo ulitokana na makubaliano yaliyofanyika mapema mwezi Oktoba 2021, kati ya Kampuni ya Scancem International DA (Scancem) – kampuni tanzu ya Heidelberg Cement AG, inayomiliki kampuni ya Tanzania Portland Cement Limited Plc (Twiga Cement) – na AfriSam Mauritius Investment Holdings Limited, mmiliki wa Tanga Cement, kwa kukubali kuuza asilimia 68.33. hisa za Tanga Cement.

Msingi wa mgogoro ulitokana na uamuzi huo (FCC kukubali Muungano) ulifanywa kinyume na sheria na taratibu za soko la ushindani za nchi. Sheria ya FCC inahitaji ubia wowote usizidi kiwango cha juu cha asilimia 35 ya hisa ya soko ili kuhakikisha ushindani wa haki.
Kutokana na uamuzi huo wa awali wa FCC, wadau walijitokeza kuuupinga kwa kukata rufaa katika Mahakama ya haki ya ushindani (FCT). Hatimaye, mnamo Septemba 23, 2022 uamuzi wa kuruhusu muungano huo ulibatilishwa na Mahakama hiyo.

Mgogoro mpya umezaliwa na unaoendelea sasa ulitokana na FCC kufanya ukiukwaji wa sheria na kuonyesha dharau za wazi kwa Mahakama ya Ushindani (FCT). Kwa kuanzishwa upya kwa zabuni ya uuzaji wa hisa za kiwanda hicho (utwaaji) mwishoni mwa Desemba 2022 na Mnamo Februari 11, 2023 FCC iliweka tangazo kwa umma kupata maoni ya wadau juu ya kuendelea na uamuzi wa kuuza hisa hizo. Kuendelea kwa mchakato huo licha ya uamuzi wa mahakama ni kiashiria kuwa kuna mgongano wa kimaslahi ulioonyeshwa na FCC hata kukubali kuvunja sheria za nchi.

Sekta ndogo ya viwanda vya saruji ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Uzalishaji na soko lake linapaswa kuendeshwa kwa mujibu wa taratibu na sheria ili kuhakikisha hakutokei majanga ya uhaba, uhodhi wa soko na hatima ya upatikanaji wa saruji kuwekwa kwenye mikono ya mtu mmoja. Uamuzi wa FCC kuidhinisha utwaaji wa kiwanda cha saruji cha Tanga kwa Kampuni ya Twiga sio tu unakiuka sheria. Bali unaonyesha wazi athari za kuacha hatima ya soko la saruji kwenye uamuzi wa kampuni moja jambo ambalo sio afya kwa maendeleo ya watu.

Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika mpango wake wa bajeti 2023/24 licha kelele zilizopigwa na wabunge, wananchi na wadau wengine haijatoa uamuzi wowote katika kuhakikisha mazingira ya uwekezaji na uratibu wa biashara ya ushindani yanakuwepo. Wizara ndio inaratibu na kuisimamia FCC. Kukaa kimya ni kama inabariki kuvunjwa kwa taratibu na sheria za nchi. Hii ni kuandaa mazingira ya kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi siku za usoni.

ACT Walendo tunaitaka Serikali isimamishe mchakato kwa lengo la kuanzisha upya kwa uwazi na kwa kuzingatia sheria za nchi yetu.
Aidha, tunaitaka Tume ya Ushindani ijiuzulu kwa kufanya kosa kubwa la kukaidi amri ya Mahakama ya Ushindani (FCT).
Mwisho, Serikali ihakikishe kuwa inalinda viwanda vya Mji wa Tanga kwa kushawishi Makampuni kuanzisha viwanda vingine ili kuongeza washindani katika soko la saruji nchini.

Hitimisho.
Mpango na mwelekeo wa bajeti ya wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara unapaswa kutumika kujibu na kutimiza shabaha ya nchi yetu katika kujikwamua kiuchumi. Mwelekeo wa ukuaji wa sekta ya viwanda kwa sasa bado hauridhishi katika kubeba dhamiri hiyo.

Mchango wa sekta ya viwanda kwenye ajira, pato la taifa, uendelezaji wa sekta za kilimo, uvuvi na madini ni mdogo mno. Aidha, tunaona licha ya mazingira ya biashara kuanza kuboreshwa wafanyabiashara wadogo wana mazingira magumu. ACT Wazalendo inatoa wito wa jumla kwa wizara kufuata sheria, kutimiza lengo la kuwainua watanzania na kuliendeleza taifa letu.

Imetolewa na;
Ndg. Halima Yusuf Nabalang’anya
Twitter: @HalimaYusuf_N
Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara

Imesomwa na Edgar Mkosamali
Waziri Kivuli wa Madini
ACT Wazalendo.
05 Mei, 2023
View attachment D33A9306.JPG
 
Hongera kwa kutoa hoja hiyo Mhe. Waziri Kivuli.

Ila usichojua ni kuwa Serikali haiwezi kufanya biashara. Yaani badala ya Serikali kujikita kwenye kutoa huduma kwa Wananchi wake, wewe ungependa iendelee kufanya biashara ya Viwanda wakati imeonesha maeneo mengi tu jinsi ilivyo feli.

Nadhani mambo ya biashara tuwaachie Sekta binafsi, na Serikali ijikite kutoa huduma na kukusanya kodi.
 
Msingi wa mgogoro ulitokana na uamuzi huo (FCC kukubali Muungano) ulifanywa kinyume na sheria na taratibu za soko la ushindani za nchi. Sheria ya FCC inahitaji ubia wowote usizidi kiwango cha juu cha asilimia 35 ya hisa ya soko ili kuhakikisha ushindani wa haki.
Kutokana na uamuzi huo wa awali wa FCC, wadau walijitokeza kuuupinga kwa kukata rufaa katika Mahakama ya haki ya ushindani (FCT). Hatimaye, mnamo Septemba 23, 2022 uamuzi wa kuruhusu muungano huo ulibatilishwa na Mahakama hiyo.

Mgogoro mpya umezaliwa na unaoendelea sasa ulitokana na FCC kufanya ukiukwaji wa sheria na kuonyesha dharau za wazi kwa Mahakama ya Ushindani (FCT). Kwa kuanzishwa upya kwa zabuni ya uuzaji wa hisa za kiwanda hicho (utwaaji) mwishoni mwa Desemba 2022 na Mnamo Februari 11, 2023 FCC iliweka tangazo kwa umma kupata maoni ya wadau juu ya kuendelea na uamuzi wa kuuza hisa hizo. Kuendelea kwa mchakato huo licha ya uamuzi wa mahakama ni kiashiria kuwa kuna mgongano wa kimaslahi ulioonyeshwa na FCC hata kukubali kuvunja sheria za nchi.
Aisee..
Hiyo mahakama ya haki ya ushindani (FCT) haina meno?!!
Yaani FCT haina namna ya ku enforce utekelezaji wa maamuzi yake na kuwadhibiti hao watukutu wa FCC ?!!!

Matokeo yake ukiritimba utatamalaki halafu bei ya saruji itakuwa haina ushindani tena
 
View attachment 2610977
Huwezi kuwa waziri kivuli kama sio Mbunge na Act wazalendo sio chama kikuu cha upinzani Acheni wenge

USSR
 
Back
Top Bottom