Kwa vijana walioajiriwa na kwenye vibanda vya Tigo Pesa, MPesa, Zpesa, Airtel Money au kwa wenye ndugu walioajiriwa huko, kaeni chonjo, sasa hivi kuna mambo yanaendelea, hamko salama hata kidogo.
Ndugu yangu yuko polisi sasa hivi, issue ilikua hivi (kulingana na maelezo yake),
ametuma pesa kwa mtu, mtandao ukamjibu kuwa hiyo transaction haijafanikiwa, akarudia rudia badae akafanikiwa, lakini kumbe pale alipokua anajaribu afu inashindikana pesa ilikua inakwenda, sasa huyu mwenye kibanda, (aliyemuajiri dogo) amekwenda polisi na sasa wamemuweka ndani (kituo cha polisi kawe)
Sasa nilipofika polisi kawe hali ilikua hivi
Uswe: Habari Afande
Afande: Unataka nini? (huku kakunja ndita tayari)
Uswe: Nakusalimia Afande, habari!
Afande: Nzuri
Uswe:Nimepata taarifa kwamba mdogo wangu kashikiliwa hapa, nimekuja kum-check.
Afande: Unataka kumwona kwani hapa hospitali? hospitali ndio wanaenda kuona watu, hapa kama unakuja unaleta chakula basi, hakuna kuona watu polisi
Uswe:nimepata habari kwamba huyu mtu yuko hapa, nafikiri cha kwanza ni kuthibitisha afande, naweza kweli kuleta chakula wakati hata sina uhakika kama huyu mtu yupo au lah?
Afande: nanii (akataja jina la afande mwezake) lete register (lakini yeye hakusema register alisema kitu kingine sijui PD au OD sikumbuki, ila aliletewa kitabu chenye orodha ya watu)
Afande: Anaitwa nani ndugu yako
Uswe:Nikataja jina
baada ya kuangalia
Afande: Yupo, unaona jina, yupo ndani
Uswe: Nashukuru, ninaweza kumuwekea dhamana.
Afande: Hapana
Uswe: Kwanini?
Afande: Mi sio mpelelezi wa kesi yake, mtafute mpelelezi wa kesi yake
Uswe: Nawezaje kumpata huyo mpelelezi, Unaweza kunisaidia afande?
Afande: Hapana
Uswe: Sasa nifanyaje
Afande:Hayupo, nenda njoo jumatatu.
Uswe: Dah afande, jumatatu mbali sana, leo ni jumamosi, na huyu dogo hana kosa.
Afande: Sasa mi nifanyaje? kwani mi ndio nimemuweka? nimekwambia njoo jumatatu.
uswe: Basi ngoja nikamtafutie chakula, si inawezekana?
Afande: We kalete.
Muendelezo huu hapa
Dogo alikua amelala Polisi Jumamosi, Jumapili tumeweza kumuwekea dhamana lakini ilikua shughuli pevu, Kuna dalili zote za rushwa! Mazingira yanaonesha kuna mtu kapewa pesa ili amfundishe adabu dogo.
Toka asubuhi tuko polisi, waliokuwepo wanasema hiyo issue anaishughulikia afande Nuru (ni mwanamke) afande nuru kapigiwa simu asubuhi saa mbili kasema yuko njiani anakuja, hadi saa nne hajafika, saa nne akapigiwa akasema nyie endeleeni na shughuli njooni saa saba, ilipofika saa saba akapigiwa simu akasema yupo njiani anakuja, hadi saa tisa alikua hajafika!
Alipofika kitu cha kwanza anasema tumsubiri Richard (huyo bwana aliyeshtaki), baada ya kueleweshana na kujiridhisha kwamba dhamana kwa mtu anayetuhumiwa sio lazima anayetuhumu awepo (sio requirement ya kisheria) Afande Nuru akasema anataka huyo Richard aje ili kuepusha majungu!
Tuliendelea kumsubiri huyo Richard hadi karibu saa kumi na moja jioni! Afande anasita kutoa dhamana kwa sababu anaogopa majungu.
Kitu kingine cha ajabu, dogo alipokamatwa jumamosi, hakuchukuliwa hata maelezo ya awali, Kwa maelezo niliyoyapata polisi ni kwamba Richard alimpigia simu afande kwamba kuna mtu kamdhulu, afande bila ushahidi wowote wa awali, bila hata kuchukua maelezo kutoka upande wa pili akafanya maamuzi ya kumkata dogo na kumtupa rumande, Jana (baada ya kuwa dogo kuwa amelala rumande tayari) Afande Nuru ndio kachukua kamwandikisha maelezo (hiyo ilikua saa tisa mchana)
Nitaendelea kuwajuza mambo yanayoendelea katika hili sakata la bwana mdogo.