HATARI: Tigo Pesa, MPesa, Zpesa, Airtel Money Zinaweza kukupeleka Jela dakika yeyote!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Kwa vijana walioajiriwa na kwenye vibanda vya Tigo Pesa, MPesa, Zpesa, Airtel Money au kwa wenye ndugu walioajiriwa huko, kaeni chonjo, sasa hivi kuna mambo yanaendelea, hamko salama hata kidogo.

Ndugu yangu yuko polisi sasa hivi, issue ilikua hivi (kulingana na maelezo yake),

ametuma pesa kwa mtu, mtandao ukamjibu kuwa hiyo transaction haijafanikiwa, akarudia rudia badae akafanikiwa, lakini kumbe pale alipokua anajaribu afu inashindikana pesa ilikua inakwenda, sasa huyu mwenye kibanda, (aliyemuajiri dogo) amekwenda polisi na sasa wamemuweka ndani (kituo cha polisi kawe)

Sasa nilipofika polisi kawe hali ilikua hivi

Uswe: Habari Afande
Afande: Unataka nini? (huku kakunja ndita tayari)

Uswe: Nakusalimia Afande, habari!
Afande: Nzuri

Uswe:Nimepata taarifa kwamba mdogo wangu kashikiliwa hapa, nimekuja kum-check.
Afande: Unataka kumwona kwani hapa hospitali? hospitali ndio wanaenda kuona watu, hapa kama unakuja unaleta chakula basi, hakuna kuona watu polisi

Uswe:nimepata habari kwamba huyu mtu yuko hapa, nafikiri cha kwanza ni kuthibitisha afande, naweza kweli kuleta chakula wakati hata sina uhakika kama huyu mtu yupo au lah?
Afande: nanii (akataja jina la afande mwezake) lete register (lakini yeye hakusema register alisema kitu kingine sijui PD au OD sikumbuki, ila aliletewa kitabu chenye orodha ya watu)

Afande: Anaitwa nani ndugu yako
Uswe:Nikataja jina

baada ya kuangalia
Afande: Yupo, unaona jina, yupo ndani
Uswe: Nashukuru, ninaweza kumuwekea dhamana.

Afande: Hapana
Uswe: Kwanini?

Afande: Mi sio mpelelezi wa kesi yake, mtafute mpelelezi wa kesi yake
Uswe: Nawezaje kumpata huyo mpelelezi, Unaweza kunisaidia afande?
Afande: Hapana
Uswe: Sasa nifanyaje
Afande:Hayupo, nenda njoo jumatatu.

Uswe: Dah afande, jumatatu mbali sana, leo ni jumamosi, na huyu dogo hana kosa.
Afande: Sasa mi nifanyaje? kwani mi ndio nimemuweka? nimekwambia njoo jumatatu.

uswe: Basi ngoja nikamtafutie chakula, si inawezekana?
Afande: We kalete.

Muendelezo huu hapa
Dogo alikua amelala Polisi Jumamosi, Jumapili tumeweza kumuwekea dhamana lakini ilikua shughuli pevu, Kuna dalili zote za rushwa! Mazingira yanaonesha kuna mtu kapewa pesa ili amfundishe adabu dogo.

Toka asubuhi tuko polisi, waliokuwepo wanasema hiyo issue anaishughulikia afande Nuru (ni mwanamke) afande nuru kapigiwa simu asubuhi saa mbili kasema yuko njiani anakuja, hadi saa nne hajafika, saa nne akapigiwa akasema nyie endeleeni na shughuli njooni saa saba, ilipofika saa saba akapigiwa simu akasema yupo njiani anakuja, hadi saa tisa alikua hajafika!

Alipofika kitu cha kwanza anasema tumsubiri Richard (huyo bwana aliyeshtaki), baada ya kueleweshana na kujiridhisha kwamba dhamana kwa mtu anayetuhumiwa sio lazima anayetuhumu awepo (sio requirement ya kisheria) Afande Nuru akasema anataka huyo Richard aje ili kuepusha majungu!

Tuliendelea kumsubiri huyo Richard hadi karibu saa kumi na moja jioni! Afande anasita kutoa dhamana kwa sababu anaogopa majungu.

Kitu kingine cha ajabu, dogo alipokamatwa jumamosi, hakuchukuliwa hata maelezo ya awali, Kwa maelezo niliyoyapata polisi ni kwamba Richard alimpigia simu afande kwamba kuna mtu kamdhulu, afande bila ushahidi wowote wa awali, bila hata kuchukua maelezo kutoka upande wa pili akafanya maamuzi ya kumkata dogo na kumtupa rumande, Jana (baada ya kuwa dogo kuwa amelala rumande tayari) Afande Nuru ndio kachukua kamwandikisha maelezo (hiyo ilikua saa tisa mchana)

Nitaendelea kuwajuza mambo yanayoendelea katika hili sakata la bwana mdogo.

Sijatumwa na benki, nimetoka Polisi na nimeshindwa kujaribu kumuwekea dhamana ndugu yangu!

Pole mkuu Uswe! Ndio hivyo, nadhani watu wa mitandao tunao humu,ujumbe umeshafika!
 
Basi huyo kahusika. Km mteja hajapata pesa system si zipo kuona pesa imeenda wapi? Au iko wapi? Na wala haihitaji masuala ya Polisi unless ndugu yko kuna kamchezo. Labda pengne utueleze swala lilivyokuwa.
 
Lakini transactions zote si zinarekodiwa huko Voda, tigo etc!
Kwanini wasifuate ushahidi huko?
 
mbona akina lowasa,chenge,kalamagi,ngeleja,riziwan,na orodha yote ya wez walituibia mabilioni ya nchi yetu bado tunanawaona mitaani?...
 
Pole mkuu Uswe! Ndio hivyo, nadhani watu wa mitandao tunao humu,ujumbe umeshafika!

Nashukuru Mshuza, baada ya kuongea na dogo nimeedit kidogo thread yangu ili kuweka kitu kilichotokea

Sasa nilipofika polisi kawe hali ilikua hivi

Uswe: Habari Afande
Afande: Unataka nini? (huku kakunja ndita tayari)

Uswe: Nakusalimia Afande, habari!
Afande: Nzuri

Uswe:Nimepata taarifa kwamba mdogo wangu kashikiliwa hapa, nimekuja kum-check.
Afande: Unataka kumwona kwani hapa hospitali? hospitali ndio wanaenda kuona watu, hapa kama unakuja unaleta chakula basi, hakuna kuona watu polisi

Uswe:nimepata habari kwamba huyu mtu yuko hapa, nafikiri cha kwanza ni kuthibitisha afande, naweza kweli kuleta chakula wakati hata sina uhakika kama huyu mtu yupo au lah?
Afande: nanii (akataja jina la afande mwezake) lete register (lakini yeye hakusema register alisema kitu kingine sijui PD au OD sikumbuki, ila aliletewa kitabu chenye orodha ya watu)

Afande: Anaitwa nani ndugu yako
Uswe:Nikataja jina

baada ya kuangalia
Afande: Yupo, unaona jina, yupo ndani
Uswe: Nashukuru, ninaweza kumuwekea dhamana.

Afande: Hapana
Uswe: Kwanini?

Afande: Mi sio mpelelezi wa kesi yake, mtafute mpelelezi wa kesi yake
Uswe: Nawezaje kumpata huyo mpelelezi, Unaweza kunisaidia afande?
Afande: Hapana
Uswe: Sasa nifanyaje
Afande:Hayupo, nenda njoo jumatatu.

Uswe: Dah afande, jumatatu mbali sana, leo ni jumamosi, na huyu dogo hana kosa.
Afande: Sasa mi nifanyaje? kwani mi ndio nimemuweka? nimekwambia njoo jumatatu.

uswe: Basi ngoja nikamtafutie chakula, si inawezekana?
Afande: We kalete.
 
Basi huyo kahusika. Km mteja hajapata pesa system si zipo kuona pesa imeenda wapi? Au iko wapi? Na wala haihitaji masuala ya Polisi unless ndugu yko kuna kamchezo. Labda pengne utueleze swala lilivyokuwa.

Rogi, najaribu kumpata huyo ndugu aliyemuajiri ndugu yangu simpati, Anaitwa Richard kibanda chake kilikua kinzudi, salasala.

Hata mi najua system ya mitandao ya simu inaweza kuonyesha pesa iko kwa nani, na hata kama ilitumwa kwa mteja (kwa sababu wateja waliandikishwa) wana uwezo wa kumpata, shida hapa ni huyu bwana alimwajiri dogo hapatikani, na Tigo wanasema hawawezi kutoa statement kwa mtu mwingine, hadi huyo wakala wao, huyu wakala baada ya kum-tupa dogo celo, kazima simu yake, na sijui namna ingine ya kumpata ili tusaidiane namna ya ku-trace hiyo pesa

Pole sana Mkuu..sasa itabidi usubiri mpk jumatatu..lkn usitie shaka dogo atapewa dhamana tu. Polisi wenyewe pia wanaweza kuandika barua kuomba print out ya hyo agent store/till na kufanya uchunguzi wao. Mwsho wa siku km unavyosema kijana hausiki bc ataachiwa tu. Mungu awaongoze masuala ya Polisi kwakweli yanasumbua na kupoteza muda.

Nimerudia kusoma post yako..hii ishu ni ndogo sana..km alikuwa anarudiarudia maana yake pesa imeenda kwenye namba ile ile ambayo alikuwa anaiwekea pesa..ni kiasi tu cha kuingiza kwenye system na kurudisha pesa iliyozidi.. Km hiyo pesa mteja ameshaitoa itabidi mteja atafutwe na Polisi(kwa watu wenye system hii ishu ndogo sana).
 
Pole sana Mkuu..sasa itabidi usubiri mpk jumatatu..lkn usitie shaka dogo atapewa dhamana tu. Polisi wenyewe pia wanaweza kuandika barua kuomba print out ya hyo agent store/till na kufanya uchunguzi wao. Mwsho wa siku km unavyosema kijana hausiki bc ataachiwa tu. Mungu awaongoze masuala ya Polisi kwakweli yanasumbua na kupoteza muda.

Wacha tu Rogi, again Nashukuru Sana.

Wakati Napigiwa Simu nilikua tight sana bse niko na dealinea kibao, niaamua niende kawe, nimetoka saa kumi, barabarani hakupitiki na hata nilipofika polisi hakueleweki, kwa kifupi siku imepotea!

Na hapa nawaza kesho inabidi kwenda tena huko kupeleka angalau msosi.

Mi nilikua sijui kama kuna shida, nimeshtukizwa tu dogo yuko polisi, kama huyu bwana aliyemuajiri angetaka ushirikiano tungeweza kusaidiana ku-trace.

Sasa naona ameamua apite njia ingine, to me it was wrong taking this boy to police, pesa inayodaiwa ni laki 5.

kama lengo ni kuitafuta hiyo laki tano sijui kama polisi ni njia rahisi, tungesaidiana tungeweza kuwatafuta hao watu, lakini sasa labda tunaongea habari ya kwenda mahakamani au yaani sijui hata anawaza nini. ila hizi kesi zinapoteza muda.

Kesi hii ikiisha DOGO inabidi apate shughuli ingine, hizo tigoPesa anaweza kwenda Jela, hii ni laki 5 je ingekua milions ingekuwaje?

Pole..huyo mwenye kibanda nae anaonekana sio mstaarabu huwez mpeleka mtu Polisi wkt suala linatakiwa uwasiliane na Kampuni ya Simu kwa msaada. Tatizo pia Polisi wetu,wangeweza kumuuliza mwenye kibanda km ameshafanya mawasiliano na kampuni ya simu na wamefikia hatua gani.
Vumilia mpk jumatatu kwa maana kwa vyovyote vile lazima atakuwa ameambiwa naye afike kituoni hyo siku.
 
Knatuna shida na mambo ya tigo pesa, m-pesa, airtel money, z-pesa nk maana ni ufisadi mwingine pia maana unaweka pesa bila kupata riba ila ukitaka kuzitumia unatozwa riba kwa pesa zako hii ni balaa ni haikubaliki. Lakini jamaa wa mitandao siku hizi wako kama zamani ilivyokuwa Posta nadhani pesa wanaziwekeza katika kitu fulani kwa hiyo wana-regulate kwa kuweka mtandoa uwe na mwendokasi kidogo ili kama unataka kupokea pesa wakuambie mtandao si mzuri na hivyo kukukosesha kukidhi hitaji la pesa uliyotumiwa.
 
Labda National Mkabwela Bank
Kweli wewe bandabichi na akili yako mbichi kabisa haiwez kuwaza lolote sasa hapo NMB imeingiaje acha dharau za bila sababu,kwa taarifa yako katika mdaua ambae hayo makampuni ya cm yanamtegemea kumkusanyia hela kutoka kwa mawakala wao ni hyo NMB unayo idharau hv wakal yupo Nkasi Rukwa bila kuwepo Nmb float yake ikiisha angemwekea dealer hela kupitia bank gan.Here are the fact y Nmb co bank ya makambwela na ujue y iliitwa bank ya makwabwela naic wewe wakati wa spil ya Nbc ulikuwa mdogo sana,Nmb iliundwa kutoka Nbc na mtaji wote Nbc ilichukua na ikaanza na sifur na operation chache sana co zote za kibenk hapa wakifanya kaz kubwa ya kupokea na kutoa hela tu,kutokana na kutokuwa na mtaji mkubwa na service chache kulinganisha bank zingine nadhan B W Mkapa ndio akasema bank ya makabwela na akijua it won't last long itakufa na wkt huo serikali ilikuwa na share 100%.Kwa kujituma kwa wazalendo ikaanza kukukua na kupata faida na kutoa huduma zote za kibank na kwa miaka minne mfululizo ndio bank inayoongoza kwa faida na gawio kwa wanahisa wake na pia ndio bank ambayo share zake ktk DSE ziko juu kitu ambacho kinaonesha good perfomance.Sasa nashangaa kukusikia wasema bank ya makabwela beside siamini kama kuna watanzania still wanadeserve kuitwa makabwela
Nmb ndio bank yenye matawi mengi kuliko bank yoyote so bank ya mtanzania yoyote
Nmb ina mtandao mkubwa sana wa atm nchi daima popote nawe 24/7
Mwanzilishi wa huduma ya mobile banking kwa mabank wengine wakafuata
Nmb ndio bank ambayo ina gharama ndogo sana kwa riba za mikopo yote,gharama ya kuendesha akaunti
Sasa y useme ya makabwela kabla ya kuandika uwe na data
 
Back
Top Bottom