HATARI: Tigo Pesa, MPesa, Zpesa, Airtel Money Zinaweza kukupeleka Jela dakika yeyote!

Nimerudia kusoma post yako..hii ishu ni ndogo sana..km alikuwa anarudiarudia maana yake pesa imeenda kwenye namba ile ile ambayo alikuwa anaiwekea pesa..ni kiasi tu cha kuingiza kwenye system na kurudisha pesa iliyozidi.. Km hiyo pesa mteja ameshaitoa itabidi mteja atafutwe na Polisi(kwa watu wenye system hii ishu ndogo sana).

Rogi, Hii issue si kubwa (lakini as we are writing kuna mtu yuko rumande, tena inawezekana akaa huko hadi jumatatu) ndio maana nikasema hizo tigo Pesa ni hatari, kwa issue ndogo kama hii mtu anaenda mahabusu?

tatizo hapa ni huyo mwenye kibanda.

  1. Hataki kushirikiana, hajasema chochote, amemsomba tu dogo kampeleka Polisi.
  2. According to dogo, Tigo waligoma kumpa transaction report/statement kwa sababu wanasema mtu sahihi kwenda kuchukua hiyo ni richard (huyo bwana mwenye kibanda), ingekua rahisi kama huyu bwana mmiliki wa kibanda angekua tayari kutoa ushirikiano, sasa yeye anasisitiza tu dogo amlipe pesa, hataki kwenda Tigo
 
Duh! Pole sana mkuu haya yote yanatokea kwa sababu ya mfumo mbovu wa ajira . Dogo anateseka kwa kuwa maskini ana thamani tena katika mfumo huu wa kibepari ..Tajiri ndio anasikilizwa,HAKI hakuna sioni sababu ya kunyimwa dhamana kama hakuna harufu ya rushwa hapo kituoni ebu wataalamu wa sheria watusaaidie hapo....pia hizi kampuni sijui kwanini zinawtumia watanzania kuwaingizia pesa lakini panapotokea matatizo wanakaa pembeni? Naomba dogo akitoka jaribu kuchukua hatua yeye kama alimwajiri kwa mkataba rasmi Je, anamlipa inavyostahili? anamlipia NSSF au ? Matajiri tuwe wastaarabu sio tunajali PESA TU.
POLE sana MKUU yataisha tu
 
Inaelekea huyo dogo keshafanya uzembe sana hapo kwenye hicho kibanda na pengine kina anapoulizwa loss yeye hutoa macho tu bila hata kujali kuwa hiyo loss inawaathiri wote wawili, yeye anajua iimradi sijachukua mimi ahh potelea mbali. Sasa mwenye kubanda kaamua kumuweka ndani kwasababu ya uzembe, ili ikifika jtatu apate akili. Waha vijana tunao waajiru siku hizi hapawpo siriasi akipoteza au kuibiwa kitu yeye hilo halimuumi na ukimuuliza anakuambia uncle, uncle, sielewi yaani labda wameniwekea dawa. anakutolea macho tu. hawataki kuwa makini katika kazi.
unapopokea hela kwa mteja ili uzitume( au umwekee kwenye simu ) ukajaribu na lets say hujapata ujumbe wowote, usimrudishie mteja hela wala kurudia kutuma. subiri sana au piga simu kastama kea. wao watakuambia hiyo hela iko wapi.
huu ni uzembe wa dogo. mimi kuna siku nilikuwa natoa hela za mgonjwa sh 300,000/ lakini kwa uzembe wangu nikakosea nikanunua mda wa maongezi. ila kwa ujanja wangu nikampigia yule aliyeziweka kwangu awapigie vodacom kulalamika kwamba ametuma hela kwenye namba ambayo siyo aliyokusudia. basi kilichofanyika ni voda kuzichunguza na kumwambia aahh huyo uliye mtumia kimakosa ameshanunua mda wa maongezi so walichofanya ni kuzirudisha kuwa mpesa na kisha wakazirudisha kwa jamaa.
chakushangaza hawa voda ukiwaambia umenunua mda wa maongezi kimakosa wao wanakuambia haiwezi kuwa reversed. lakini ukitumia trick kama hiyo eti mda wa maongezi unaweza kuwa reversed. this is bullshit!!!!!!!!!!
 
Duh! Pole sana mkuu haya yote yanatokea kwa sababu ya mfumo mbovu wa ajira . Dogo anateseka kwa kuwa maskini ana thamani tena katika mfumo huu wa kibepari ..Tajiri ndio anasikilizwa,HAKI hakuna sioni sababu ya kunyimwa dhamana kama hakuna harufu ya rushwa hapo kituoni ebu wataalamu wa sheria watusaaidie hapo....pia hizi kampuni sijui kwanini zinawtumia watanzania kuwaingizia pesa lakini panapotokea matatizo wanakaa pembeni? Naomba dogo akitoka jaribu kuchukua hatua yeye kama alimwajiri kwa mkataba rasmi Je, anamlipa inavyostahili? anamlipia NSSF au ? Matajiri tuwe wastaarabu sio tunajali PESA TU.
POLE sana MKUU yataisha tu

Asante Blaque,

Haikua ajira rasmi hivyo, i mean sio kitu kinachoweza kumuwezesha kusimama, i thought ilikua kumsaidia dogo kujua pesa inatafutwa, pia asikae tu home wakati huu anasubiri kitu kingine cha kufanya

 
Tatizo neno afande watanzania tunalitumia vibaya. Neno Afande hutumiwa na wapiganaji/askari wa vyeo vya chini ku-address wakubwa/mkubwa wake, vilevile neno Askari hutumiwa na askari wenye vyeo vya juu ku-address wale wa vyeo vya chini.

Ssa kosa la wa TZ wengi wanapoenda popote pale wakiona askari hata akiwa private, utasikia habari afande, hapo naye anajua amekutana na poyoyo kwa nini asikubutue!

Mpe mtu cheo anachostahili bana............
 
Pole..huyo mwenye kibanda nae anaonekana sio mstaarabu huwez mpeleka mtu Polisi wkt suala linatakiwa uwasiliane na Kampuni ya Simu kwa msaada. Tatizo pia Polisi wetu,wangeweza kumuuliza mwenye kibanda km ameshafanya mawasiliano na kampuni ya simu na wamefikia hatua gani.
Vumilia mpk jumatatu kwa maana kwa vyovyote vile lazima atakuwa ameambiwa naye afike kituoni hyo siku.

Kama polisi wanataka kufanya upelelezi,hatua ya awali si wangewasiliana na kampuni ya simu? Hili ni suala dogo lakn kulipeleka polisi linakuzwa bila sababu.
 
mi nafikiri kuna laziada alilofanya likamfikisha pale kwani si kosa lake ni kosa la kimtandao wangefatilia wangepata printout kama mteja alotumiwa kazitoa ndo anae takiwa atafutwe mteja uwezimweka mtu polisi kwa kisa icho tulaazma kuna la ziada kesho fuatilia uje na report hasa kilichotokea mana hata hujawezaongea nae mtuhumiwa ukajua hasa uhalisia
 
Dogo alikua amelala Polisi Jumamosi, Jumapili tumeweza kumuwekea dhamana lakini ilikua shughuli pevu, Kuna dalili zote za rushwa! Mazingira yanaonesha kuna mtu kapewa pesa ili amfundishe adabu dogo.

Toka asubuhi tuko polisi, waliokuwepo wanasema hiyo issue anaishughulikia afande Nuru (ni mwanamke) afande nuru kapigiwa simu asubuhi saa mbili kasema yuko njiani anakuja, hadi saa nne hajafika, saa nne akapigiwa akasema nyie endeleeni na shughuli njooni saa saba, ilipofika saa saba akapigiwa simu akasema yupo njiani anakuja, hadi saa tisa alikua hajafika!


Alipofika kitu cha kwanza anasema tumsubiri Richard (huyo bwana aliyeshtaki), baada ya kueleweshana na kujiridhisha kwamba dhamana kwa mtu anayetuhumiwa sio lazima anayetuhumu awepo (sio requirement ya kisheria) Afande Nuru akasema anataka huyo Richard aje ili kuepusha majungu!

Tuliendelea kumsubiri huyo Richard hadi karibu saa kumi na moja jioni! Afande anasita kutoa dhamana kwa sababu anaogopa majungu.

Kitu kingine cha ajabu, dogo alipokamatwa jumamosi, hakuchukuliwa hata maelezo ya awali, Kwa maelezo niliyoyapata polisi ni kwamba Richard alimpigia simu afande kwamba kuna mtu kamdhulu, afande bila ushahidi wowote wa awali, bila hata kuchukua maelezo kutoka upande wa pili akafanya maamuzi ya kumkata dogo na kumtupa rumande, Jana (baada ya kuwa dogo kuwa amelala rumande tayari) Afande Nuru ndio kachukua kamwandikisha maelezo (hiyo ilikua saa tisa mchana)

Nitaendelea kuwajuza mambo yanayoendelea katika hili sakata la bwana mdogo.
 
Back
Top Bottom