Hataki kuolewa na mimi msaada tafadhari

Habari wakuu ni hivi nina demu wangu wa kitambo kidogo na mimi ndio nilimtoaga usichana sasa alihama mitaa yetu kuna mahali anaishi,sasa kipindi hiki nimempa ofa ya ndoa amegoma kuishi na mimi na nazani hata tabia zake ni za ajabu kwan avai nguo za stara mimi nilitaka nimbadilishe but anaonesha kureact msaada wakuu nifanyaje na mimi naitaji kuoa.

Tafadhari = tafadhali
 
Hakuna mademu wengine ambao unaweza kuwaoa?
Kwa nini unamtaka zaidi huyo?
 
We jamaa jitambue ndoa haipewi offer kama bia utaka uoe limbukeni ambaye bado dunia inamchanganya kiufupi hyo demu ana washikaji kibao ndo maana hakupi uzito ww
Nahisi hilo jambo mkuu.sawa wacha nijaribu mpotezea tu kwan yeye sio mzazi wangu
 
Huyu mleta mada seems kuna mengi hajawahi ona au ku experience.

Mwanangu haya mambo hatukurupuki....u got a great life ahead of u. Majuto mjukuu. Wanawake ni wengi wengi sanaa....Be Patient.

Ifike wakat ujue the difference between True Love and what u think is True Love.
 
M
Mkuu wala usilazimishe ndoa sbb huyo sio wako mpaka hapa. Tayari ana mwingine anayempenda sana na anatamani aolewe naye ila sio ww. Mtu anayekupenda kwanza ukimwambia suala ndoa anafurahi sana na hawez kukataa hata kusita kwa sekunde. Zaid ya kusema YES
Huyo muache tu, wala usisumbuke naye. Mapenz hayalazimishi. Wanawake wapo wengi tu mkuu japo unaumia lkn jikaze kiume utayashinda mapenz ndiyo yalivyo.
Tafuta binti mzuri kuliko yy uoe kbsa
mkuu nashukuru sana nimekuelewa
 
Nadhan hufaham ndoa ni nin otherwise usingemlazimisha.
mkuu umeniweka njia panda please nipe ushauri usinikatishe tamaa kumbuka we live at oncee na tunajifunza thru life thats why nataka jf members wenzangu mnipe mawazo yenu
 
Sasa mkuu kama kashakataa, mwache! Hapo wala ulikuwa huna haja ya kukimbilia kulia huku, zaidi huku hakuna kipya utakachokipata cha kumfanya atake kuwa na wewe kama ndo maumuzi yake!
ni kweli mkuu but huku nimefata ushauri mzuri kama wako how to avoid them
 
Habari wakuu ni hivi nina demu wangu wa kitambo kidogo na mimi ndio nilimtoaga usichana sasa alihama mitaa yetu kuna mahali anaishi,sasa kipindi hiki nimempa ofa ya ndoa amegoma kuishi na mimi na nazani hata tabia zake ni za ajabu kwan avai nguo za stara mimi nilitaka nimbadilishe but anaonesha kureact msaada wakuu nifanyaje na mimi naitaji kuoa.

Wanaojielewa wengi wana allerg na neno demu!
 
Aisee mshukuru sana kwa kuwa muwazi na kukukatalia wazi, moyo wa mtu ni fumbo. Huyo hakupendi na tafadhali muache kabisa kabisa wala usipuuze ushauri wa wajumbe hapo juu.

Pia kaza kutafuta pesa ili uwe huru katika maisha mengine nje na ndani ya ndoa na familia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom