Harakati za Julius Mtatiro na hujuma alizofanyiwa ndani ya UKAWA

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
JULIUS MTATIRO:- KARAI KUBWA KULIKO YOTE UPINZANI

KUPATA CHEO NDANI YA CUF/KUBADILI DINI.

Binafsi naheshimu haki ya mtu ya kuabudu na kuwa dini yoyote kama inavyosema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni haki ya kikatiba kwa mtu kuwa na dini, kubadili dini, kutokuwa na dini na kuabudu chochote atakacho. Ila ni jambo la kustaajabisha kwa mtu kubadili dini ili aweze kupata cheo. Julius Mtatiro ana haki ya kubadili dini, kama alifanya kwa hiyari kwa nini hadi leo anafanya kificho? Mtu huyu akipewa dhamana kubwa katika nchi hawezi kuiuza kwa ahadi ya maslahi? Kama alibadili dini kwa kupenda si atuambie jina lake na tumtambue kwa jina hilo kuliko kubaki kimya huku akiswali kwa kificho? Kwangu mimi hili lilitosha kumuona huyu kijana ni hatari, anafanana na viongozi waliopewa dhamana na wakaziuza kwa rushwa, kama ameuza imani yake huyu yuko tayari kuuza chochote.

VITA YA MAALIM NA HAMAD RASHID

Sote tunakumbuka vita iliyotokea kati ya maswahiba wawili ambao waliwahi kufungwa pamoja na kufanya harakati zao pamoja kwa muda mrefu, Mzee Maalim Seif na Mh. Hamad Rashid. Hitimisho la vita hiyo ilikuwa kufukuzwa uanachama wa Hamad Rashid na kuasisiwa kwa chama kipya cha siasa cha ADC.

Katika vita hii Maalim Seif alimtumia Julius Mtatiro kupigana vita yake ambayo kimsingi haimhusu hata kidogo, ila kwa kuwa ni mtu bei nafuu (cheap) aliweza kununua ugomvi na kuuendesha huku Maalim Seif akiwa kimya. Hitimisho lake Hamad Rashid alifukuzwa uanachama na kwa kuwa tayari Maalim alishamaliza kulitumia karai lake hilo uchaguzi uliofuata alipokwa cheo chake cha Naibu Katibu Mkuu CUF Bara maana Maalim alijua kama kamtumia kwenye vita dhidi ya adui yake na akatumika kuna siku anaweza kutumika kwenye vita dhidi yake pia, hivyo akawekwa kando na cheo chake akapewa Magdalena Sakaya.

UASISI WA UKAWA

Julius alikuwa mmoja wa makatibu wa UKAWA, hivyo alikuwa ni sehemu na kiungo cha muhimu UKAWA kutoka Chama Cha Wananchi – CUF. Na ikumbukwe alikuwa mmoja wa wajumbe wa bunge Maalum la Katiba. Mchango wake katika UKAWA ni mkubwa sana, asiyeutambua basi atakuwa na chuki binafsi, tena za kutosha. Baada ya kutumika ipasavyo kuijenga UKAWA, wakati watu wananufaika kupitia UKAWA, wenzake walimhujumu na kumuweka kando maana walijua kazi yake kama KARAI imekwisha na sasa ni muda wa kumuweka stoo. Hivyo akawekwa stoo hadi wakati mwingine wa kutumika.

MTA2.jpg
MTA1.jpg
mtatiro.jpg
MTA2.jpg
MTA1.jpg
mtatiro.jpg
MTA2.jpg
MTA1.jpg
mtatiro.jpg

UBUNGE SEGEREA

Ilipofika wakati wa kugawana majimbo miongoni mwa vyama shiriki vya UKAWA, jimbo la segerea waliachiwa Chama Cha Wananchi – CUF, ambapo mgombea wake alikuwa Ndugu Julius Mtatiro. Lakini nyuma ya pazia huenda CHADEMA hawakutaka Julius awe mbunge, huenda wanajua uwezo wake na angesaidia CUF kuwa na muwakilishi mwenye nguvu bungeni, na kwa kuwa mkakati wa chadema siku nyingi ni kuua vyama vyenye nguvu bara kibaki chenyewe na CCM basi ilibidi wamhujumu Mtatiro.

Hawakuzingatia hata kidogo kazi aliyoifanya Mtatiro kama mmoja wa Makatibu wa UKAWA toka Bunge Maalum la Katiba hadi walipohamishia mapambano nje ya Bunge maalum la katiba.

Kwa makusudi kabisa chadema walimuwekea mgombea na kuhakikisha anakuwepo na wanagawana kura jambo liliopelekea Mtatiro kushindwa uchaguzi ule na ilikuwa huenda ndio fursa adhimu ya Mtatiro kuwa Mbunge, huenda nafasi kama ile isitokee tena katika maisha yake, kwenye mpira wanasema ile ilikuwa Golden chance. Kwa kuwa alishatumika kujenga UKAWA na kazi yake ikasiha basi karai likahujumiwa na kuwekwa kando.

VITA YA MAALIM SEIF NA PROF. LIPUMBA

Baada ya kuhujumiwa na kuwekwa kando 2015 akabaki kuandika makala gazetini ili aweze kupata mkate wa familia yake, mara paap 2016 Profesa Lipumba akaandika barua kwa katibu mkuu wa CUF kuwa ameondoa dhamira ya kujiudhuru hivyo anarudi ofisini kwake. Sote tunajua mtifuano uliotokea, kwa kuwa Maalim Seif anajua Julius ni karai lake zuri kwa kubeba zege la kila aina basi akaenda stoo na kulitoa huko na kumpa Uenyekiti wa kamati ya Uongozi na kumpa jukumu la kupambana na Prof. Lipumba waziwazi huku Maalim Seif kakaa kando anaangalia mpambano. Yaani huyu ndugu yangu anasikitisha, anakumbukwa wakati wa kutumika tu, wakati wenzake wanakula yeye huwa kawekwa kando, Mungu amsaidie kijana huyu kujitambua.

KUSUSIA UCHAGUZI MDOGO WA MAJIMBO

Baada ya CHADEMA kupitia Kamati Kuu yao kuamua kususia uchaguzi wa mdogo wa majimbo matatu ilibidi watafute uhalali wa kususia kupitia vyama vingine. Mara paap msemo wa vijana wakakumbuka karai lao lenye uzoefu lipo, wakaenda stooni kwa Maalim Seif wakalichukua wakafanya nalo press kuwa UKAWA tumesusia uchaguzi, huku hakumbuki huo UKAWA ulimsababishia yeye kukosa ubunge kwa chadema kumhujumu waziwazi kabisa kwa kumuwekea mgombea. Ila kwa kuwa walijua udhaifu wake basi wakamuita na kumtumia na sasa karejeshwa stooni anasubiri assignment nyingine.

HITIMISHO

Julius Mtatiro ni mfano wa vijana wanaotumika kama makarai ndani ya UKAWA, nimeamua kumtolea mfano maana yeye anaonekana na yote anayotumika na kufanyiwa yanajulikana, kuna sasa vikarai vidogovidogo vingi, vinatumika sana na baada ya hawa jamaa kupata ruzuku nyingi wanaishia kujenga familia zao huku haya makarai yakisahaulika na kusubiri wakati mwingine wa kutumika. Nawashauri vijana wenzangu mgutuke na kujitambua.
 
Dini ya mtu sisi inatuhusu nini? Abadili asibadili hakuna hasara wala faida kwa nchi.

Kuna Mambo makubwa makubwa yanayotetelesha nchi yetu hayo ndiyo yanafaa kutupotezea muda, sio jambo la mtu kubadilisha dini.

Mfano tuambie namna rais anavyokandamiza mihimili mingine na kuathiri utendaji wa mihimili hiyo, tuambie namna vyombo vya dora vinavyotumika kinyume na nia iliyokusudiwa, tuambie matumizi mabaya ya Kodi zetu, tuambie namna rais anavyoamua Mambo makubwa ya nchi kwa kufikiri kichwani kwake peke yake.

Tuambie namna wabunge wa chadema (wanaohama) wanavyotutia hasara nchi kwa kurudia uchaguzi, hizo gharama tunabeba sisi wavuja jasho.

Mambo ya Mtatiro kubadili dini muachie yeye na mkewe.
 
kusoma uzi wote mpa mwisho sijaona jina lililo mbadilisha imani.zaidi ya nukta za karai
 
Kweli hii dunia ni kuwa uyaone.

Hakika nayaona na bado nitona ya ajabu.

Aiseeeeh....
 
JULIUS MTATIRO:- KARAI KUBWA KULIKO YOTE UPINZANI

KUPATA CHEO NDANI YA CUF/KUBADILI DINI.

Binafsi naheshimu haki ya mtu ya kuabudu na kuwa dini yoyote kama inavyosema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni haki ya kikatiba kwa mtu kuwa na dini, kubadili dini, kutokuwa na dini na kuabudu chochote atakacho. Ila ni jambo la kustaajabisha kwa mtu kubadili dini ili aweze kupata cheo. Julius Mtatiro ana haki ya kubadili dini, kama alifanya kwa hiyari kwa nini hadi leo anafanya kificho? Mtu huyu akipewa dhamana kubwa katika nchi hawezi kuiuza kwa ahadi ya maslahi? Kama alibadili dini kwa kupenda si atuambie jina lake na tumtambue kwa jina hilo kuliko kubaki kimya huku akiswali kwa kificho? Kwangu mimi hili lilitosha kumuona huyu kijana ni hatari, anafanana na viongozi waliopewa dhamana na wakaziuza kwa rushwa, kama ameuza imani yake huyu yuko tayari kuuza chochote.

VITA YA MAALIM NA HAMAD RASHID

Sote tunakumbuka vita iliyotokea kati ya maswahiba wawili ambao waliwahi kufungwa pamoja na kufanya harakati zao pamoja kwa muda mrefu, Mzee Maalim Seif na Mh. Hamad Rashid. Hitimisho la vita hiyo ilikuwa kufukuzwa uanachama wa Hamad Rashid na kuasisiwa kwa chama kipya cha siasa cha ADC.

Katika vita hii Maalim Seif alimtumia Julius Mtatiro kupigana vita yake ambayo kimsingi haimhusu hata kidogo, ila kwa kuwa ni mtu bei nafuu (cheap) aliweza kununua ugomvi na kuuendesha huku Maalim Seif akiwa kimya. Hitimisho lake Hamad Rashid alifukuzwa uanachama na kwa kuwa tayari Maalim alishamaliza kulitumia karai lake hilo uchaguzi uliofuata alipokwa cheo chake cha Naibu Katibu Mkuu CUF Bara maana Maalim alijua kama kamtumia kwenye vita dhidi ya adui yake na akatumika kuna siku anaweza kutumika kwenye vita dhidi yake pia, hivyo akawekwa kando na cheo chake akapewa Magdalena Sakaya.

UASISI WA UKAWA

Julius alikuwa mmoja wa makatibu wa UKAWA, hivyo alikuwa ni sehemu na kiungo cha muhimu UKAWA kutoka Chama Cha Wananchi – CUF. Na ikumbukwe alikuwa mmoja wa wajumbe wa bunge Maalum la Katiba. Mchango wake katika UKAWA ni mkubwa sana, asiyeutambua basi atakuwa na chuki binafsi, tena za kutosha. Baada ya kutumika ipasavyo kuijenga UKAWA, wakati watu wananufaika kupitia UKAWA, wenzake walimhujumu na kumuweka kando maana walijua kazi yake kama KARAI imekwisha na sasa ni muda wa kumuweka stoo. Hivyo akawekwa stoo hadi wakati mwingine wa kutumika.

View attachment 657609 View attachment 657610 View attachment 657611 View attachment 657609 View attachment 657610 View attachment 657611 View attachment 657609 View attachment 657610 View attachment 657611

UBUNGE SEGEREA

Ilipofika wakati wa kugawana majimbo miongoni mwa vyama shiriki vya UKAWA, jimbo la segerea waliachiwa Chama Cha Wananchi – CUF, ambapo mgombea wake alikuwa Ndugu Julius Mtatiro. Lakini nyuma ya pazia huenda CHADEMA hawakutaka Julius awe mbunge, huenda wanajua uwezo wake na angesaidia CUF kuwa na muwakilishi mwenye nguvu bungeni, na kwa kuwa mkakati wa chadema siku nyingi ni kuua vyama vyenye nguvu bara kibaki chenyewe na CCM basi ilibidi wamhujumu Mtatiro.

Hawakuzingatia hata kidogo kazi aliyoifanya Mtatiro kama mmoja wa Makatibu wa UKAWA toka Bunge Maalum la Katiba hadi walipohamishia mapambano nje ya Bunge maalum la katiba.

Kwa makusudi kabisa chadema walimuwekea mgombea na kuhakikisha anakuwepo na wanagawana kura jambo liliopelekea Mtatiro kushindwa uchaguzi ule na ilikuwa huenda ndio fursa adhimu ya Mtatiro kuwa Mbunge, huenda nafasi kama ile isitokee tena katika maisha yake, kwenye mpira wanasema ile ilikuwa Golden chance. Kwa kuwa alishatumika kujenga UKAWA na kazi yake ikasiha basi karai likahujumiwa na kuwekwa kando.

VITA YA MAALIM SEIF NA PROF. LIPUMBA

Baada ya kuhujumiwa na kuwekwa kando 2015 akabaki kuandika makala gazetini ili aweze kupata mkate wa familia yake, mara paap 2016 Profesa Lipumba akaandika barua kwa katibu mkuu wa CUF kuwa ameondoa dhamira ya kujiudhuru hivyo anarudi ofisini kwake. Sote tunajua mtifuano uliotokea, kwa kuwa Maalim Seif anajua Julius ni karai lake zuri kwa kubeba zege la kila aina basi akaenda stoo na kulitoa huko na kumpa Uenyekiti wa kamati ya Uongozi na kumpa jukumu la kupambana na Prof. Lipumba waziwazi huku Maalim Seif kakaa kando anaangalia mpambano. Yaani huyu ndugu yangu anasikitisha, anakumbukwa wakati wa kutumika tu, wakati wenzake wanakula yeye huwa kawekwa kando, Mungu amsaidie kijana huyu kujitambua.

KUSUSIA UCHAGUZI MDOGO WA MAJIMBO

Baada ya CHADEMA kupitia Kamati Kuu yao kuamua kususia uchaguzi wa mdogo wa majimbo matatu ilibidi watafute uhalali wa kususia kupitia vyama vingine. Mara paap msemo wa vijana wakakumbuka karai lao lenye uzoefu lipo, wakaenda stooni kwa Maalim Seif wakalichukua wakafanya nalo press kuwa UKAWA tumesusia uchaguzi, huku hakumbuki huo UKAWA ulimsababishia yeye kukosa ubunge kwa chadema kumhujumu waziwazi kabisa kwa kumuwekea mgombea. Ila kwa kuwa walijua udhaifu wake basi wakamuita na kumtumia na sasa karejeshwa stooni anasubiri assignment nyingine.

HITIMISHO

Julius Mtatiro ni mfano wa vijana wanaotumika kama makarai ndani ya UKAWA, nimeamua kumtolea mfano maana yeye anaonekana na yote anayotumika na kufanyiwa yanajulikana, kuna sasa vikarai vidogovidogo vingi, vinatumika sana na baada ya hawa jamaa kupata ruzuku nyingi wanaishia kujenga familia zao huku haya makarai yakisahaulika na kusubiri wakati mwingine wa kutumika. Nawashauri vijana wenzangu mgutuke na kujitambua.
Kwa hyo hlo kovu katika paji la uso ndo limekwambia kuwa alibadili din au??????
 
Mleta uzi bogus kabisa; unasema Julius alibadili dini, kisha unachagiza akutajie jina lake la dini mpya. Sasa kama hujui jina lake la dini mpya locus stand ya tuhuma zako iko wapi? bogus!
 
Kwa kuzaliwa kwako 3 sept, nyota yako ni Virgo ie mwanamke, na jina lako limeanza na M
M; Inawakilisha Mabadiliko baada ya kurejea au baada ya Talaka.
Wenye jina linaloanza na herufi “M” ni Watu Wenye kujiamini sana, wachapa kazi na hupata mafanikio, Ni watu WAROPOKAJI, wenye haraka na wepesi sana kukasirika.
 
Hiyo alama katika paji la uso ipo kuanzia namuona akiwa waziri wa mikopo udsm na sidhani kama ina chochote cha kufanya na dini, alama nyingine ni ngeu za ngumi wala hakuna uhusiano na kupiga vichwa sakafuni.
 
Mtoa mada unaonekana unaumia sana kwa mtatiro kubadili dini kama unavosema, picha ni mbili tu lakini umezirudia ili watu wazione
 
Back
Top Bottom