Anna Mwaigomole
Member
- Aug 23, 2023
- 15
- 54
Naamini hunijui. Na mimi nakiri kuwa sikujui. Hatujuani! Lakini zamani wakati sijajiunga JF ulikuwa unaandika sana hasa kuhusu ushauri wa kimahusiano, malezi ya watoto, familia, mambo ya kiroho; na maisha kwa ujumla.
Mwaka 2018 au 2017 (sikumbuki vizuri), nilisoma comment yako moja hivi. Ilikuwa ni comment ndefu ukimshauri mtu kuhusu ndoa yake. Ni Mungu Alikutumia katika comment ile maana ilinigusa sana. Nakumbuka nilii-print nikawa naisoma na kuanza kutendea kazi kipengele kimoja kimoja.
Napenda tu kusema kuwa everything changed in my marriage. A miracle happened, and my dying marriage was revived. Una upako we dada hata kama hujui. Comments zako nyingi tulikuwa tunazishea huko kwenye magroup yetu ya wanandoa FB na WhatsApp. Umesaidia watu wengi sana!
Siku hizi nasikitika huandiki tena kama zamani. Pengine majukumu ya ndoa na ulezi yamekutinga. Na yote ni mema maana ni kila wakati na majira yake!
Basi niruhusu leo angalau tu nikutakie Happy Birthday dada; just as a token of goodwill and appreciation 🙏🏿
Unaposherehekea Birthday yako leo basi kumbuka kuwa kuna watu baki huku duniani uligusa na kubadilisha maisha yao. Umepanda mbegu njema sana. Naamini hizo mbegu za wema zitakurudia wewe na kizazi chako!
Nakuombea ndoa njema yenye furaha na amani. Familia iliyobarikiwa. Watoto wanaomtambua Mungu na kila lililo jema katika maisha yako wewe pamoja na mumeo na watoto wenu wote. Hebu na ukaishi maisha marefu ukaone si vijukuu vyako tu bali hata vitukuu na vilembwe.
You are a true shining light!
Heaven Sent ❤️❤️❤️
Happy Birthday 🙏🏿