Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

Probox inabeba watu wangapi kwani???? Duu yani hao wote 8 walikiwa kwenye probox
Nane mbona wachache jomba? ... Siku moja nimeshuhudia watu wanapangwa, wanne mbele akiwemo dereva. Katikati wanne na nyuma kwenye boot wanne pamoja na mizigo. Na bado dereva alitaka kuongeza ... Nikashuka na kuchukua boda boda Kakonko - Kibondo kwa 20,000/=
 
Wee chonza kumbe alishafariki? Yule alikuwa anaishi block Q? Baba khalid?
Kama sijachanganya majina, ndiye ninayemzungumzia. Maana huyo jamaa alifariki mwaka 2005 au 2007, alipata ajali barabara ya Kaliua. Na alipofariki, pale mjini habari zilianza zushwa kuwa ni Rama Mangozi, ndiye ikajulikana muhusika sio rama mangozi. Siku anakufa, nilikuwa kituo cha polisi. Ndio taarifa zilinikutia pale.
 
Kibondo hadi Kakonko kwa dakika 25!!!!
sio kweli, na ile barabara ya vumbi....Hapana.
 
Kuna siku natokea Dodoma niko kwenye speed ya 120km/Hr ikatokea V8 ikani-ovetake. Si nikasema nile nayo ligi, kufika speed ya 160km/Hr nikasema hivi nikipata ajali kwa mwendo huu kweli nitapona?

I later slow down to 80km/Hr nikaiacha V8 ikipotea machoni kwangu

Kusema kweli Ajali nyingi huchangiwa na Mwendokasi

Mwendokasi unaua....

Poleni kwa misiba

ukishakuwa na familia lazima upuuze hizo ligi, sasa hivi hata mimi ni heri upite uende zako tutakutana Msolwa/Ubena kula nyama choma
 
ukishakuwa na familia lazima upuuze hizo ligi, sasa hivi hata mimi ni heri upite uende zako tutakutana Msolwa/Ubena kula nyama choma
Kwa kweli Mkuu, nimegundua ajali nyingi ni mwendokasi.

Niliponyeka ajali kwa uzembe huo huo wa Mwendokasi.

Bado familia zetu zinatuhitaji Mkuu

Heri ya Mapumziko ya mwisho wa Mwaka Mkuu kwako na familia yako

Peace 🥂
 
Back
Top Bottom