Hamad Rashid: Nitaunda chama kipya!

CUF sasa kumhoji Hamad Rashid

headline_bullet.jpg
Blue Guard waagizwa kufuatilia nyendo zake
headline_bullet.jpg
NCCR- Mageuzi nao wazidi kuvuana madaraka
headline_bullet.jpg
Safari hii ni bosi wa Kitengo cha Wanawake



Hamad%20Rashid%201%281%29.jpg

Mbunge wa Wawi visiwani Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed


Hali ya kisiasa ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi inazidi kugubikwa na migogoro kiasi cha kuvifanya kuwa mahali pasipokalika.

Wakati NCCR-Mageuzi inaendeleza `fukuza fukuza’ ya viongozi wanaodaiwa kutofautiana na Mwenyekiti wake, James Mbatia, CUF imemtangaza Mbunge wa Wawi visiwani Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed na wafuasi wake kuwa ni waasi wanaotaka kukipasua chama hicho.

Hata hivyo, Hamad Rashid amepuuzia madai hayo na kusema anayempachika sifa ya uasi ni ‘bwana wadogo’ asiyeijua historia ya CUF.

Tuhuma za uasi zilitangazwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam jana.

Mtatiro alisema kwa sababu hiyo wataitwa na kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Chama kuhusiana na tuhuma za kuasi na kutaka kukipasua chama hicho.

Alisema hatua hiyo itachukuliwa kwa madai kwamba vitendo vinavyofanywa na Hamad Rashid na wafuasi wake ni vya utovu wa nidhamu na pia ni kinyume cha taratibu halali za chama.

Mbali na kuitwa na kuhojiwa na kamati hiyo, CUF pia imewaagiza Blue Guard kumfuatilia Hamad Rashid na wafuasi wake popote watakapofanya mkutano ili kumhoji kama amefuata utaratibu wa kufanya mkutano husika wa chama au la.

Alitoa kauli hiyo ikiwa ni hatua mpya ya msuguano uliopo kati ya pande mbili za mgogoro ndani ya CUF unaomhusisha Hamad Rashid na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusu uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

“Tayari hawa watu wameshaasi chama. Wataitwa kwenye kamati ya nidhamu na maadili ya chama, watahojiwa kisha taratibu nyingine zitafuata,” alisema Mtatiro.
Hata hivyo, Mtatiro alisema hadi jana alikuwa hajui hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Hamad Rashid na wafuasi

wake, lakini akasema kwa mujibu wa Katiba ya chama, wanaweza ama kuonywa, kupewa karipio kali au kufukuzwa katika chama.

“Hakuna katika chama aliye juu ya katiba. Tusije kujidanganya kuwa huko mitaani kila mtu ana chama chake. Hata Maalim Seif hayuko juu ya katiba ya chama. Sasa aka kagenge ka watu wachache sisi akatutishi,” alisema Mtatiro.

Alisema Hamad Rashid na kundi lake ni waasi kwa vile wamekuwa wakifanya mambo, kama vile kuitisha mikutano kwenye matawi ya chama, kinyume cha taratibu halali za chama.

Mtatiro alisema katika kufanya mambo hayo, Hamad Rashid na kundi lake wamekuwa wakitumia fedha kukodi vikundi vya wahuni, vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadhi ya waandishi wa habari ili kutekeleza nia yake mbaya ya kukipasua chama.

Alisema baada ya kupewa fedha hizo, wahuni na vijana hao wa CCM wamekuwa wakitumia silaha, yakiwamo mapanga kuwashambulia walinzi wa chama hicho, maarufu kama “Blue Guard” kama walivyofanya katika tawi la CUF la Chechnya, Mabibo juzi walipojaribu kuwahoji wafuasi wa Hamad Rashid sababu za kufanya mkutano bila kufuata taratibu halali za chama.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF alisema kwa upande wa waandishi wa habari wamekuwa wakitumika, kueneza propaganda zinazoendeshwa na Hamad Rashid na wafuasi wake, bila kutoa fursa kwa upande wa chama, kinyume cha maadili ya uandishi wa habari.

Alisema propaganda hizo zinatumiwa na Hamad Rashid kuwachafua viongozi wakuu wa chama kwa lengo la kuwakatisha tamaa wanachama kwa kisingizio cha kutafuta Ukatibu Mkuu, wakati si kweli.

“Yanayoendelea yanayohusishwa na Hamad Rashid siyo sahihi kwa sababu chama kina utaratibu wake. Kwa hiyo kinachofanywa na Hamad Rashid siyo kutafuta Ukatibu Mkuu, ni zaidi ya hivyo. Ni kutaka kukipasua chama. Huwezi kutafuta Ukatibu Mkuu kwa kutumia umafia,” alisema Mtatiro.

Aliongeza: “Huwezi kutafuta Ukatibu Mkuu mwaka 2011 wakati uchaguzi ndani ya chama ni mwaka 2014. kuna matatizo katika kundi lake (Hamad Rashid).”

Matatiro alisema wafuasi wa Hamad Rashid katika harakati zake hizo, baadhi ni waliopunguzwa katika utumishi wa chama, wakiwamo walinzi.

Alisema wengine ni waliokuwa wabunge ambao waliangushwa kwenye kura za maoni walipojaribu kuwania tena kuteuliwa kuwa wagombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na wengine ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa Chama hicho.

“Wote hao hawana historia nzuri katika chama. Wanatumia propaganda kwa kutumia mikutano isiyo halali,” alisema Mtatiro na kuwataka waandishi wa habari kumhoji Hamad Rashid aeleze anakotoa fedha anazowagawia makundi hayo.

Aliongeza: “Kwenye Ukatibu Mkuu kuna biashara gani? Kuna nini hadi mtu anataka kujitoa mhanga kwa mamilioni ya fedha? Wakati akiwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, naibu ndiye aliyekuwa akisikika. Mbona hatukuona akipambana bungeni? Kama ilikuwa kujenga chama si ndio angejenga? Why (kwanini kazi yake kubwa ni kucheka na (Waziri Mkuu, Mizengo) Pinda? Hatutaki kumchokonoa kujua Hamad Rashid ni mtu gani.”

Alisema ibara ya 20 ya Katiba ya CUF imetaja haki za mwanachama, mojawapo ikiwa ni kuonana na viongozi wa chama anapotaka kufanya shughuli za chama, kama mikutano na kusema: “Huwezi kutukana viongozi wa chama na kuwakatisha tamaa wanachama. Tutachukua hatua.”

Mtatiro alisema Hamad Rashid mbali ya kuwa ni mbunge, pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa Chama Taifa, hivyo akahoji sababu zilizomzuia kupeleka maoni yake kwenye vikao vya chama.

Kutokana na hali hiyo, alisema Blue Guard wataendelea kukilinda chama.
“(Hamad Rashid na kundi lake) wasidhani kwamba kukodi vibaka na wahuni kwamba, watarudi nyuma. Hapana! Kwani tuna maelfu ya walinzi. Tukitaka kuwapeleka Ilala, Temeke watakwenda. Wakienda kufanya kikao popote bila taarifa, walinzi watakwenda kukuhoji, wakikataa wataondoka, wataleta ripoti,” alisema Mtatiro.

Alisema pamoja na harakati hizo za Hamad Rashid, CUF bado ni imara, haijatetereka na kwamba, hawatajibishana na Hamad Rashid kupitia magazeti.
Baada ya mkutano huo na waandishi wa habari, NIPASHE iliwasiliana na Hamad Rashid, ambaye kwanza

alisema amesikitishwa na mapigano yaliyotokea juzi katika tawi hilo, ambayo alisema katika historia ya CUF haijawahi kutokea kitu kama hicho.

Kutokana na hilo, alimtaka Mtatiro kuomba radhi kwa maelezo kwamba, ndiye aliyewapeleka Blue Guard na kuzua mapigano hayo yaliyosababisha wafuasi zaidi ya wanne wa CUF kujeruhiwa kwa kukatwa na mapanga juzi.

Alisema Mtatiro hana mamlaka ya kuwatumia Blue Guard na kuhoji taratibu alizofuata kuwatuma wakavamie mkutano uliofanyika katika tawi la Kosovo, Manzese, ambao alisema haukuandaliwa naye (Hamad Rashid), bali alikwenda hapo baada ya kuombwa na wanachama awapelekee viti na meza kwa matumizi ya ofisi.

Hamad Rashid alisema hawajawahi kuandikiwa barua yoyote na chama kuelezwa kama wanavunja katiba, hivyo akamtaka Mtatiro kuthibitisha madai kwamba, yeye Hamad Rashid amepewa fedha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuivuruga CUF.

“Atoe ushahidi wa kimahakama. Kwa sababu iweje urafiki wangu na Pinda uwe dhambi, lakini urafiki wa Jussa na Rostam Azizi usiwe dhambi?” alihoji Hamad Rashid.
Aliongeza: “Sina ugomvi na Katibu Mkuu, nina ugomvi na hali ya chama ilivyo hivi sasa. Aeleze Sh milioni 800 zimetumikaje katika uchaguzi wa Igunga. Pia naomba umweleze Mtatiro kuwa chama kimeshachoka namna anavyokiendesha atakavyo.”

Chimbuko la hali hii linadaiwa ni vuguvugu za ndani kwa ndani za uchaguzi wa viongozi wa chama hicho akidaiwa kutamani kiti cha Katibu Mkuu kitakaachoachwa wazi na Maalim Seif kama ataamua kustaafu.
Hamad Rashid analalamika kuwa Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya

Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, ana mwanachama anayemuandaa kwa ajili ya kiti hicho.
Harakati hizo pia zimesababisha viongozi hao wawili kulaumiana juu ya utendaji na ujenzi wa chama Tanzania Bara, huku Hamad Rashid akimlaumu Maalim Seif kwa kutokufanya kazi kubwa ya kisiasa Tanzania Bara.

Miongoni mwa lawama anazobebeshwa Maalim Seif ni kufanya vibaya kwa CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambao chama hicho kilishika nafasi ya tatu huku kikipata idadi ndogo ya wabunge Bara kiasi cha

kupoteza nafasi ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni nafasi ambayo wameishikilia tangu mwaka 1995.
Ndani ya NCCR-Mageuzi imebainika kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Samwel Ruhuza, amemtimua katika uongozi Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake (Taifa), Amina Suleiman.

Ruhuza alithibitisha kufikia hatua hiyo wakati akihojiwa na NIPASHE kwa njia ya simu jana, na kuongeza, “nasikitika kusema kwamba hizo habari mtazidi kuzipata kila siku…”
Awali, vyanzo vya habari vilieleza NIPASHE kuwa Amina ambaye ni miongoni mwa wanachama wa

NCCR-Mageuzi wanaodaiwa kumuunga mkono Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, aliandikiwa barua ya kufukuzwa ambayo hata hivyo bado hajaipokea.
Alipotafutwa kwa njia ya simu jana, Amina alithibitisha kupokea taarifa za kuandikiwa barua, lakini hakuipokea
kwa vile alikuwa nyumbani kwake mkoani Rukwa.

Alisema baada ya kupata taarifa za kuandikiwa barua hiyo, alimuagiza Afisa Tawala wa chama hicho aliyemtaja kwa majina ya Florian Rutayuga, amkabidhi mmoja wa wana-NCCR aliyekuwa jijini Dar es Salaam kwa shughuli za kikazi.

“Nilimuomba pia aifungue ili kunijulisha kilichoandikwa, ndipo akaniambia nimetimuliwa kutoka nafasi ya Uenyekiti,” Amina alisema.

Alisema hakuna sababu ya msingi anayoamini inayoweza kutumika kama kigezo cha kumvua wadhifa huo, isipokuwa ni harakati za kudai mabadiliko ya Katiba na kuondolewa madarakani kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Hata hivyo, Amina alisema ingawa hatua hiyo itaonekana kama moja ya njama za kumpunguza nguvu za kisiasa ndani ya NCCR-Mageuzi, lakini ataendeleza kile alichokiita kuwa ni ‘harakati za kuleta mageuzi’ ndani ya chama hicho.

Kwa mujibu wa Amina ambaye hana mpango wa kukata rufaa uamuzi huo, miongoni mwa mkakati wake ni kujiimarisha ili agombee nafasi ya Uenyekiti pindi uchaguzi utakapofanyika ndani ya chama hicho.
Amina alisema hata kabla ya kutimuliwa, alifikiria kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na kubanwa na viongozi wa

juu wa chama hicho, kiasi cha kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Alisema miongoni mwa majukumu yaliyokwamishwa na viongozi hao aliowaita kuwa ‘mabwana wakubwa’ ni kutoruhusu utekelezaji wa mikakati mbalimbali ukiwemo wa kuongeza idadi ya wanawake ndani ya NCCR-Mageuzi.

Lakini akitetea uamuzi wa kumtimua Amina, Katibu Mkuu Ruhuza alisema Katiba ya chama hicho inampa mamlaka ya kuwafukuza katika uongozi wajumbe wa Sekretarieti pasipo kushauriana ama kuingiliwa na mtu yeyote.

Alisema kwa hali hiyo, aliamua kumtimua Amina kutoka nafasi ya uenyekiti wa kitengo cha wanawake, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuboresha vitengo vya chama hicho kwa kadri anavyoona inafaa.

Kutimuliwa kwa Amina kumejulikana siku moja baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu Katibu Mkuu huyo kumfukuza Kafulila, kutoka nafasi ya Mkuu wa Idara ya Uenezi na Uhamasishaji aliyokuwa akiishikilia.



CHANZO: NIPASHE
 
Watanganyika mbona munaumizana vichwa kwa huyu kilaza Hamad Rashid au hamna kazi za kufanya huko? Mbona sisi huku hatumjadili hata kwa bahati mbaya huyu mtu, hata Maalim mwenyewe leo alipozungumza na waandishi wa habari kampuuzia anajua kama huyu mtu ameshapotoka, kuna kitu kinamdhuru huyu na si chengine bali ni DUA za Wazanzibar juu ya Wanafiki wa Zanzibar.
Sio yale mambo ya kule hpemba kule! Wamuona mtu aongea,kumbe si yeye! Msalieni mtume
 
Nalikumbuka jina kama hili kwenye kashfa ya kuuza maeneo ya uwindaji huko Loliondo kwa mtoto wa mfalme Dubai miaka ya 1990s akiwa waziri wa utalii wakati wa Alhaji Mwinyi. Kama ni mwenyewe naomba tumpuzie kumjadili, kama siye naomba munisahihishe
 
Jamaa anaweza kuanzisha chama; Ubunge umekuwa ni private enterprise kama unauhakika wa kuchaguliwa na wananchi wa jimboni mwako ni rahisi sana kuanzisha chama, mbona tunao wabunge wa aina hiyo mfano mzuri John Cheyo, Augustino Lyatonga Mrema; kwa Hamadi anaendeleza utamaduni uliopo.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
cuf kinahitaji mabadiliko, mi nakubaliana na hamad rashid hata kama yeye asipate hayo madaraka lakini change in leadership ni muhimu sana.seif amekaa madarakani tangu cuf imezaliwa,atafia hapo?aache damu nyingine nayo ilete changamoto.kama si bias fuatilieni madai ya hamad rashid,ni ya msingi sana.
 
Back
Top Bottom