kuna waislamu wajanja
Hapo kwenye red tu kapigilia msumari,sasa wanaposimama wakina mtatiro na vibaraka wenzake pale jangwani kukanusha inakuwaje hapa?Asante amadi kwa kuanza kudai talaka...Hamad Rashid: CUF ijitoe serikali ya mseto
na Asha Bani
MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amelaani matumizi ya nguvu za Jeshi la Polisi wakati wa chaguzi mbalimbali huku akikishauri chama chake kujiondoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina yao na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kutowasaidia wananchi.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Hamad alisema kuwa ameshangazwa na nguvu kubwa ya Jeshi la Polisi iliyotumika katika uchaguzi mdogo wa Bububu uliomalizika hivi karibuni na hivyo kusababisha kujeruhi wananchi bila sababu.
Alisema CUF iliingia katika serikali ya mseto kwa lengo la kuweka uhuru na haki lakini wameshindwa kufikia azima hiyo na kwamba ikiwa muafaka huo ni kwa maslahi ya watu wachache basi wajitoe.
Mimi nashangaa sana hayo mazungumzo sijui yalikuwa ya nini na ndoa ilikuwa ya nini kama ilikuwa ni kwa masilahi ya watu wachache huku wananchi hawanufaiki nayo, wanapigwa risasi, basi CUF wajiondoe kama si kwa masilahi ya wananchi wote, alisema Hamad.
Hata hivyo, Hamad alisema Serikali ya Zanzibar inaundwa na vyama viwili, hivyo ni dhahiri kwamba CCM na CUF ndio wametumia nguvu katika kuvikandamiza na kuhujumu vyama vidogo vya siasa ambavyo havikuwa na serikali.
Katika uchaguzi huo wa Jumapili ambao CCM iliibuka kidedea ikifuatiwa na CUF na Chama kipya cha ADC, vurugu kubwa zilizuka huku matokeo hayo yakipingwa vikali.
CDM ilikataa ushirika na CUF bungeni kwa kuwa CUF ilikuwa na ushirika na CCM serikalini Zanzibar. Unakumbuka mashambulizi ya huyu Rashid kwa Mbowe na kambi nzima ya upinzani bungeni? Do not trust this crook. Hata yeye yupo kwa maslahi ya tumbo lake tu.Hapo kwenye red tu kapigilia msumari,sasa wanaposimama wakina mtatiro na vibaraka wenzake pale jangwani kukanusha inakuwaje hapa?Asante amadi kwa kuanza kudai talaka...
Kweli mkuu huyu jamaa ni mnafiki wa kutupwa,alipovuliwa kiongozi wa upinzani bungeni aliongea sana na kutaka kuleta kanuni zake za kiajabu ajabu huku akijua atasaidiwa na mumewe gamba....CDM ilikataa ushirika na CUF bungeni kwa kuwa CUF ilikuwa na ushirika na CCM serikalini Zanzibar. Unakumbuka mashambulizi ya huyu Rashid kwa Mbowe na kambi nzima ya upinzani bungeni? Do not trust this crook. Hata yeye yupo kwa maslahi ya tumbo lake tu.
Kuna waislamu wajanja