Hamad Rashid kujitoa CUF leo?

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Mwaliko Kwa Wahariri Katika Mkutano Na Hamad Rashid- Maelezo- 21.09.2012
TANGAZO ATT. WAHARIRI WOTE: MBUNGE WA JIMBO LA WAWI HAMAD RASHID MOHAMED ANATARAJIA KUKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI HAPA NCHINI KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA IDARA YA HABARI(MAELEZO) KUANZIA SAA 4 ASUBUHI. MH. HAMAD ATAZUNGUMZIA MAMBO MBALIMBALI. WAPI-=MAELEZO-DAR ES SALAAM MUDA- SAA 4.00 LINI -IJUMAA- 21.09.12 WAHUSIKA - WAHARIRI KUTOKA VYOMBO VYA HABARI

ADC nao watahudhuria?????
 
Hamad Rashid: CUF ijitoe serikali ya mseto

na Asha Bani


MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amelaani matumizi ya nguvu za Jeshi la Polisi wakati wa chaguzi mbalimbali huku akikishauri chama chake kujiondoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina yao na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kutowasaidia wananchi.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Hamad alisema kuwa ameshangazwa na nguvu kubwa ya Jeshi la Polisi iliyotumika katika uchaguzi mdogo wa Bububu uliomalizika hivi karibuni na hivyo kusababisha kujeruhi wananchi bila sababu.
Alisema CUF iliingia katika serikali ya mseto kwa lengo la kuweka uhuru na haki lakini wameshindwa kufikia azima hiyo na kwamba ikiwa muafaka huo ni kwa maslahi ya watu wachache basi wajitoe.
"Mimi nashangaa sana hayo mazungumzo sijui yalikuwa ya nini na ‘ndoa' ilikuwa ya nini kama ilikuwa ni kwa masilahi ya watu wachache huku wananchi hawanufaiki nayo, wanapigwa risasi, basi CUF wajiondoe kama si kwa masilahi ya wananchi wote," alisema Hamad.
Hata hivyo, Hamad alisema Serikali ya Zanzibar inaundwa na vyama viwili, hivyo ni dhahiri kwamba CCM na CUF ndio wametumia nguvu katika kuvikandamiza na kuhujumu vyama vidogo vya siasa ambavyo havikuwa na serikali.
Katika uchaguzi huo wa Jumapili ambao CCM iliibuka kidedea ikifuatiwa na CUF na Chama kipya cha ADC, vurugu kubwa zilizuka huku matokeo hayo yakipingwa vikali.
 
Kwa nini neno "MWISLAMU" limechomekwa hapa!!!? Sema Hamad hilo neno uliloongeza halina mashiko. Ushamba hauna dini

kwanini waislamu wanakuwa delicate kuliko yai, hawana subra kama za Mwenyezi Mungu, wanajazba kama Ibilisi Shetani, wao ni wa uzao upi Mungu au shetani!!!
 
kwanini waislamu wanakuwa delicate kuliko yai, hawana subra kama za Mwenyezi Mungu, wanajazba kama Ibilisi Shetani, wao ni wa uzao upi Mungu au shetani!!!

wanakuja wenyewe mi sisemi chochote
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom