Halmashauri ya Jiji la Dar yawakaanga Ridhwani, Mama Salma

Na kampuni ikishakuwa na hisa halafu ziwe sokoni,unaweza leo ukawa majority shareholder,kesho ukawa hauna control ya kampuni kama share zako zinapungua,
sijui hizi share za UDa Zimeuzwaje,lakini SIMON GROUP sio wajinga wainvest mabilioni yao katika UDA ili baadae Uda ichukuliwe,lazima wameangalia kama sheria iko upande wao ama vipi,sasa huyu mhitimu wa darasa la saba pamoja na elimu za hapa na pale ngoja tuone hii gemu atafika nayo wapi...
Hii Game haitaki hasira
 
Sasa nimemwelewa Mh JPM alivyosema lazima atafungua mahakama ya MAFISADI wakati wa kampeni zake, mimi nilijua mahakama hii itakuwa ni kuwanyoosha wapinzani ili wakafike jela - alaa kumbe kuna MAFISADI PAPA within... ambayo yanatakiwa yawe na mahakama yao -- aisee!!

Kweli tulifikia pabaya, yaani kujipatia hela kwa kona kona ilikuwa jambo la kawaida tu - kila sehemu ukigusa ni usaa mtupu!!!! - pole JMP kazi uliyoomba na ukapewa ni ngumu mno.

Ila tunaomba uongeze kidogo sheria kuwabana waficha habari ili press iwe huru zaidi ili wakusaidie kuyaanika hadharani haya MAJIPU, pia tusaidie (ingawa ulisema wewe ni mtumishi wetu) kuwashauri Bunge warushe Bunge Live ili sisi wananchi tukubali falsafa yako ya UTUMBUAJI - Maana tunasikia hata Bungeni MAJIPU mengi mno!!

Kitu chochote kinachofichwa fichwa ama kitu chochote cha siri siri, cha gizani gizani huwa hakina BARAKA za mwenyezi Mungu, sasa bunge linaficha ficha nini??

Tunaomba Bunge liwe Live, ili tuone wawakilishi wetu wanafanya nini mjengoni.

Watanzania tunakuombea !!
 
Sasa Kubenea anashtuka leo wakati Mh. Rais JPM alishalisema hilo kuwa kuna watu walitaka kujimilikisha UDA wamezuwiwa na ndo maana ya mradi huo kukwama? Rais alishayatolea hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa fly over pale Tazara.
 
Sasa nimepata picha ya alichokisema Rais Dr. JPM wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Flyover pale TAZARA.

Katika hili naunga mkono jitihada za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kulinda mali zake kwa maslahi mapana ya wana DSM, na Taifa kwa ujumla.
 
tatizo huyu kubenea yuko very unproffesional,yaani ana bifu za binafsi,personal beef kwenye mambo ya msingi hayasaidii.
Makampuni duniani kote yana underperform nakuwa takenover na makampuni mengine regardless lilikua kampuni la umma ama la binafsi,
kule russia tumeshuhudia makampuni makubwa ya serikali yaliunderperfom na kuuzwa kwa makampuni binafsi na yakafanya vizuri.
Badala ya kung'ang'ania kulaumu watu binafsi kwa malengo ya kisiasa,angestick kwenye figure na taratibu zipi zimekiukwa na kwa ushahidi upi,ama kama vipi si mahakama zipo,afungue kesi ya kudai UDA irudi,



Hana beef anaongea ukweli

Zoezi la kupata mzabuni halikuwa sawa
Shirika la uma halipaswi kuendeshwa na watu wenye tabia za kiswahili
 
•Sh285 milioni: Fedha pekee zilizolipwa na Simon Group kununua hisa za Uda
•Sh320milioni: Kiasi alicholipwa Idd Simba kwa ushauri wa kuiuza Uda.
•76 : Idadi ya mabasi yaliyostahili kununuliwa na Uda-RT kwa mkataba uliopo badala ya 140 yaliyopo.

By Waandishi Wetu, Mwananchi ; mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kuchunguza mikataba kati ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kuhusu Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametia pilipili kidonda kwa kuibua udanganyifu unaolizunguka shirika hilo.

Kwenye ripoti yake ya mwaka wa fedha 2014/2015 aliyoitoa bungeni Jumatatu, CAG Profesa Mussa Assad amebainisha kwamba Dart ilifanya makubaliano na msimamizi wa uendeshaji, Uda-RT kutoa huduma ya mpito ya usafiri kwa kutumia mabasi 76 yenye vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.

Tofauti na makubaliano hayo, Uda ilinunua mabasi 140 ambayo yalikuwa na nembo ya Uda-RT badala ya Dart kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.

Meneja wa Miundombinu wa Dart, Mhandisi Mohamed Kuganda alisema wenye taarifa sahihi ni Uda-RT.

Hata hivyo, alikiri kufahamu ununuzi wa mabasi hayo na kusema waliwauliza Uda-RT na wakajibiwa kuwa, “barabara za kutumika mabasi hayo zipo nyingi.”

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group na Uda-RT, Robert Kisena alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa limeelekezwa serikalini: “Hoja za CAG zinaihusu Serikali hivyo siwezi kujibu.”

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru alisema Serikali hairidhishwi na uendeshwaji wa Uda, lakini haina la kufanya.

Alifafanua kuwa Serikali haijawahi kujitoa katika umiliki wa shirika hilo na kwamba bado inazo asilimia 49 ya hisa zote na Simon Group ina asilimia 51 zilizobaki.

Alieleza kuwa uendeshaji wa shirika hilo: “Hauna utawala bora.” Hata hivyo, alisema ni vigumu kwa sasa kumiliki shirika hilo kwa asilimia 100 kwa sababu wenye hisa nyingi ndiyo wenye uamuzi.

“Tulichukuaje hilo shirika? Labda kama wenzetu watakubali kutuuzia hisa, vinginevyo hatuwezi kuwanyang’anya,” alisema.

Uchunguzi wa CAG

Akikumbusha juu ya ufuatiliaji baada ya ubinafsishaji, CAG ameiambia Serikali kuwa hisa za Uda ambazo hazikugawiwa, ziliuzwa kwa kampuni ya Simon Group kwa Sh1,142,643,935.

Alisema kampuni hiyo ililipa asilimia 24.9 tu ya makubaliano ya bei ya mwanzo, Sh285 milioni kwenye akaunti ya Uda yenye namba 01J1021393700 iliyopo Benki ya CRDB. Ripoti inasema hakuna ushahidi wa malipo ya asilimia 75.1 ambazo ni sawa na Sh858 milioni zilizobakia.

CAG amebainisha pia kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa Uda, Idd Simba alipokea Sh320 milioni alizowekewa katika akaunti yake binafsi kwa ajili ya huduma ya ushauri wa kitaalamu kutoka Simon Group Limited.

Utata uliopo ni kwamba Simon Group inadai kuwa kiasi hicho: “Ni sehemu ya malipo ya mauzo ya hisa za Uda.”

Akizungumzia suala hilo hivi karibuni, CAG mstaafu Ludovick Utouh alisema anashangaa kuona Uda ikiuzwa na fedha zake kuwekwa kwenye akaunti ya mtu binafsi kitendo ambacho ni kosa la jinai lakini kesi hiyo ilifunguliwa na kisha kufutwa.

Ingawa mwaka 2013 aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea kuwashtaki Idd Simba na wenzake, CAG ameendelea kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Hazina kufuatilia kwa karibu juu ya ubia wake ndani ya Uda ili kuhakikisha: “Maslahi ya umma hayapotei.”

Hata hivyo, Mafuru alisema kwa kuwa kesi iliyokuwa mahakamani imekwisha na uamuzi umeshatolewa, itakuwa vigumu kulirejesha serikalini shirika hilo. “Kesi zilizokuwa mahakamani zimekwisha ndiyo maana ninaweza kuzungumzia… Uda inaendelea kufanya kazi.”

Simba, aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika awamu ya tatu, alishtakiwa pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa shirika hilo, Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu, Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Simon Group Limited, Simon Kisena, kwa kosa la uhujumu uchumi.

Kupuuzwa mapendekezo

CAG alisema alitoa mapendekezo ya kukiukwa kwa kanuni za uuzaji wa hisa hizo tangu mwaka 2011/2012 lakini yalipuuzwa. Alisema Uda iliuzwa bila kibali cha Serikali na hisa zilithaminishwa kwa Sh744.79 kwa kila moja Oktoba 2009, lakini Novemba 2010, zikashushwa mpaka Sh656.15.

Hata hivyo, katika uuzaji, Bodi ya Wakurugenzi ya Uda ilitoa punguzo la asilimia 60 kwa kila hisa kwa mwekezaji huyo. Bodi ilizingatia tathmini ya Oktoba 2009 bila kuwapo na sababu za kufanya hivyo.

CAG alisema: “Kwa mujibu wa majibu ya Mlipaji Mkuu wa Serikali, Serikali haitambui uuzwaji wa hisa hizo.”

Uda ni moja ya mashirika 158 yaliyokaguliwa na CAG kwa mwaka wa fedha uliopita kati ya 185 yanayostahili.

UDA

Licha ya tahadhari iliyotolewa mwaka jana na wabunge wa upinzani juu ya uharamu wa kuuzwa kwa hisa za Uda, ripoti ya CAG imeweka wazi kilichokuwa kinaelezwa.

Kwa nyakati tofauti, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wa Kibamba, John Mnyika walisema shirika hilo liliuzwa kwa: “Bei ya kutupwa.”

Imeandikwa na Julius Mathias, Kelvin Matandiko na Elias Msuya
 
....napomsoma Pendo Omary wa Mwanahalisi( si BAK...maana naona watu wanamshambulia bure humu)....napata picha ya kwanini issue ya umeya wa dar ilikuwa mwiba kwa baadhi ya watu hawa...Nashukuru Kubenea kapenya na kuingia halmashauri ya jiji la dar....maana kwa investigative Journalism hii watanzania tutajua mengi dhidi ya ubadhirifu wa mali za dar.....

........issue ya uda imeelezwa hata kwenye report za CAG....hili si jambo dogo hata kidogo....na jambo hili kwa vile limelalamikiwa na CAG....hapa hata JPM hawezi kumtetea mtu...kama alivyoshindwa kuwatetea kwenye issue ya umeya wa dar...
 
Watu wanaoshambulia gazeti badala ya kuchambua na kujua ukweli sijui wana tatizo gani...! Ni aibu watanzania jamani...mnajulishwa watu wanavyojinufaisha kwa kutumia Mali ya Umma bado mnakejeli! Hatari!

UDA kama iliuzwa bila ya kufuata utaratibu, haijalishi ni Nani alijimilikisha, cha msingi kila kitu ni batili na kampuni irejeshwe kwa wamiliki wake ili haki itendeke, na hili lifanyike bila kuangalia sura ...
 
Sitaki kutetea Simon Group kwa sababu ni majizi na wanatakiwa wawe mahakamani.

Kinachoshangaza ni baadhi ya watu hapa Jamiiforums wanataka kutuaminisha ni wazalendo lakini hawana lolote. Hao ni wanafiki wanaojificha katika kichaka cha ujinga na usahaulifu wa Watanzania.

Kwa sasa ukimgusa Lowassa wanakuambia peleka ushahidi lakini wakati wao wanamgusa huyo huyo Lowassa mpaka kumuweka kwenye list of shame walikuwa hawataki kusikia neno peleka ushahidi.

Wamiliki wa gazeti la Mwanahalisi wametajirika kwa sababu ya kuandika habari/makala za ufisadi wa Lowassa na genge lake.

Leo hii wanataka tena kutajirika kwa kuandika makala za kumsafisha Lowassa na genge lake.

Tunaambiwa na Mwanahalisi kuwa, Lowassa na genge lake ndiyo wanafaa kusimamia maslahi ya nchi huku wakimsafisha bila ushahidi!

Kundi la wanafiki lipo nyuma ya Mwanahalisi likipiga vigelegele na nderemo!


mwanahalisi ni kitu gan wewe? we jenga hoja mwanahalisi ni watu tu kama wewe hofu yako nn? hapa hatujadili mwanahalis tunajadili uwiz wa uda we unawatoa watu ktk wizi unakimbilia mwanahalis, upo sawa kwel wewe?
 
Nachotaka kuongezeka ni kuwa wao wenyewe wanachofanya ni kuendeleza tuhuma tu kwa watu wengine! Basi na ukawa na hili gazeti lao kama wanaushahidi ni zamu yao kutangulia mahakamani!
Kwanini kubenea na halmashauri ya jiji wanaloliongoza hawaendi mahakamani kuwashtaki riz1 na Mama yake? Au wamekosa ushahidi wa hizi tuhuma zao?
Vipi kuhusu pendekezo la CAG unaliongeleaje hilo?
Kweli nimeamini mtanzania ukitaka kunyonya vizuri mkaririshe kwamba Mtu wa champ chetu hata akiiba mtete even till the last drop of your blood.
Hapo utamuibia kiulainii..yeye atakazana kutetea tu.
 
Ugumu wa UDA pamoja na mambo mengine ni zile milioni alizowekewa Idi Lion kwenye account binafsi na jinsi kesi yake ilivyofutwa mysteriously!
Najaribu kuchora picha kama Membe au Dr. Migiro wengelikuwa marais nchi ingekuwaje.
 
YAANIKWE NA YATUMBULIWE TUU. MIJIZI KILA SEHEM INAIBA HAINA HATA KIASI. LOOTERS

Majipu ya ukweli yananyea ndoo saa hizi, hujaona picha za Kitilya na mkwewe Lowassa?

Hayo mengine ni majipu ya kwenye mioyo yenu tu. Kumbuka kuwa hayo ya kwenye mioyo yenu yatawauma daima hakuna wa kuyatumbuwa.

Vipi, ya Dau mmegonga ukuta?
 
This is entangled wanamtandao affairs!

Wanapomkaanga Ridhiwani, Salma na Kapuya, ni sawa na kumkaanga Lowassa kwa sababu Kapuya ni mtu ambaye waingereza wanasema, He is Lowassa's right-hand man.
DSC_0771.JPG

MASHEKHE wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi Lowassa kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania Urais 2015. Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia kwenye picha juu) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.
Wewe ulitakaje? Waache kwa sababu wana uhusiano Na Lowassa?
 
Back
Top Bottom