Halmashauri ya Jiji la Dar yawakaanga Ridhwani, Mama Salma

Kikwete kweli ni jipu linalostahili kutumbuliwa tena haraka kabla halija athiri wananchi zaidi.
 
Sitaki kutetea Simon Group kwa sababu ni majizi na wanatakiwa wawe mahakamani.

Kinachoshangaza ni baadhi ya watu hapa Jamiiforums wanataka kutuaminisha ni wazalendo lakini hawana lolote. Hao ni wanafiki wanaojificha katika kichaka cha ujinga na usahaulifu wa Watanzania.

Kwa sasa ukimgusa Lowassa wanakuambia peleka ushahidi lakini wakati wao wanamgusa huyo huyo Lowassa mpaka kumuweka kwenye list of shame walikuwa hawataki kusikia neno peleka ushahidi.

Wamiliki wa gazeti la Mwanahalisi wametajirika kwa sababu ya kuandika habari/makala za ufisadi wa Lowassa na genge lake.

Leo hii wanataka tena kutajirika kwa kuandika makala za kumsafisha Lowassa na genge lake.

Tunaambiwa na Mwanahalisi kuwa, Lowassa na genge lake ndiyo wanafaa kusimamia maslahi ya nchi huku wakimsafisha bila ushahidi!

Kundi la wanafiki lipo nyuma ya Mwanahalisi likipiga vigelegele na nderemo!
Nachotaka kuongezeka ni kuwa wao wenyewe wanachofanya ni kuendeleza tuhuma tu kwa watu wengine! Basi na ukawa na hili gazeti lao kama wanaushahidi ni zamu yao kutangulia mahakamani!
Kwanini kubenea na halmashauri ya jiji wanaloliongoza hawaendi mahakamani kuwashtaki riz1 na Mama yake? Au wamekosa ushahidi wa hizi tuhuma zao?
 
hili gazeti si ndio lile lile lilikuwa likitaka Lowass ma kina Sumaye na wengine ni mafisadi papa.baadae wakabadili gia angani kwa maslahi yao binafsi wakaamua kuwasafisha. gazeti hilihili likaanza propaganda za kuwasafisha utafikiri wao ni vyombo vya dola vya uchunguzi. wakalamba walizolamba biashara ikaishia hapo. leo wanatakaje tuwaamini tena. labda ipite miaka 50 mingine ya uhuru. kama wana ushahidi wakimbilie mahakamani wasituhusishe na maujinga yao. watu wanajitambua sasa hatutaki uhuni wao. watu sssa hivi wako busy na kazi tu.
 
Kampuni ya Kapuya (swahiba wa Lowassa) ndo inayoosha magari yote ya UDA kwa Sh 140,000/- kila wiki kwa kila gari.
 
Wewe utaona vipi tofauti wakati akili na fikra zako hazitofautiani na zake.

Birds of a feather flock together!
Ndio maana nika address neno pathetic peke yake. Hayo mengine ni ya kwenu! Labda sio neno zuri sana kulitumia lakini kwa jinsi alivyolitumia ni sawa sawa. Watu tuache kuwa sensitive kwenye masuala ya lugha.
 
Yani hawa wanaopiga kelele ni sawa na watu wanamuona dema wa kijijin kachoka wanampotezea. Unapomuweka ndani ukamrembesha, nao hao, wanaanza kumtokea. Sasa UDA lilikuwa ni shirika lililochoka zaidi ya Air Tanzania. Likiwa na mabasi ya Isuzu yasioyozidi matano ambayo yalikuwa yamechokaa. Zaidi ya majengo yaliyoko kule bandarini, UDA lilikuwa ni shirika 'hewa' sawa na mfupa usio na nyama...
 
unajua ukiwa na elimu ya kuungaunga ya media inasumbua sana ni bora ipelekwe sheria ya habari bungeni ili chekecheke lipitie wenye elimu ya habari(makanjania) waumbuke
Nyie ni majizi wakubwa na mtawakoma ukawa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Humu JF kuna watu hawasomi kichwa cha habari ila wanaanza kuchangia mawazo kama wametoka usingizini.Jamani kuweni makini na kichwa cha habari.
 
Hivi wakati wanauza hii UDA si walikuwa wamebaki na mikweche tu ya gari isiyofika hata 20?

Unajua hapa mwanahalisi wangetuweka wazi Uda ilikua na asset zipi kwanza na iliuzwa kwa bei ipi ili tujue tumeibiwa au vipi,
maana maneno yanakuwa mengi mara kapuya,sijui riziwani,
hapa si tuinadeal na entity,ambayo ni SIMON AGENCY ,i mean simon group,step by step mwanahalisi wangeandika ilikuwaje waweke figure na pengine taratibu zipi zimekiukwa kwa kunukuu vifungu at least tutaanza kuelewa hasa wanaongelea nini
 
Yaani kubenea na toilet paper yake asipoiandika vby familia ya Jk hajiskii kabisa! Akiambiwa athibitishe kama wanahisa hawezi! Habar za umbeaumbea tu!poyoyo sana
tatizo huyu kubenea yuko very unproffesional,yaani ana bifu za binafsi,personal beef kwenye mambo ya msingi hayasaidii.
Makampuni duniani kote yana underperform nakuwa takenover na makampuni mengine regardless lilikua kampuni la umma ama la binafsi,
kule russia tumeshuhudia makampuni makubwa ya serikali yaliunderperfom na kuuzwa kwa makampuni binafsi na yakafanya vizuri.
Badala ya kung'ang'ania kulaumu watu binafsi kwa malengo ya kisiasa,angestick kwenye figure na taratibu zipi zimekiukwa na kwa ushahidi upi,ama kama vipi si mahakama zipo,afungue kesi ya kudai UDA irudi,
 
Waandishi wa habari wa Tanzania kwa kweli ni janga jingine kubwa tu, huwezi andika habari kumhusu mtu tena unamtaja kwenye kichwa cha habari halafu ndani yake huna uhakika hata kua huyo mtu anahusika moja kwa moja na hicho ulichokitaja, nadhani kuna haya ya hawa watu kukumbuishwa maadili yao ya kazi badala ya kufanya mambo kwa lengo la kuuza magazeti tu, hapo bila shaka watu watanunua magazeti kwa sababu ya majina ya wahusika lakini kumbe habari yenyewe ndani yake ni udaku tu.
 
Back
Top Bottom