Hali ni mbaya Tarime: Polisi watembeza Mabomu usiku huu; Kina Lissu wakamatwa

....Kwa kawaida dalili ya serikali isiyojali wananchi wake ina sifa zifuatazo...

  1. kuwadharau wananchi...kumbukeni kauli hizi "Ni bora watanzania wale nyasi ndege ya raisi inunuliwa" by Mramba na hii "waliopoteza maisha walikuwa ni majambazi waliovamia mgodi wa madini" by Kagasheki
  2. Kuwaua.
  3. Kutojali maisha yao..angalia gharama ya maisha yanavyopanda kila siku
 
Unajua kuchoka sasa mimi polisi wa tz ndio nimewachoka bora tuishi kama wanyama yani kama simba akiwahiwa na mbwa mwitu analiwa kuliko kuwa na sheria zinazowalinda watu flan hii sheria kisu sio msumeno na siku tukifanikiwa kuigeuza ikate upande wao wataishi kama idi amin dada pumbavu
 
Kama freedom ndo inatafutwa hivi!! Basi Tanzania inayokuja itakuwa na walemavu wengi kuliko.
 
Mmmmhh! Sasa! Hebu ngoja naondoka then nitarudi na wazo la leo maana nimekosa cha kusema. Chama Cha mapapa imenichosha. Uuuuwiiiiiiiii! Jamani jamani hii serikali tawala wata2weka wapi? Ngoja nirudi!
 
Safi sana Polisi, Lissu hana kinga ya uheshimiwa pale anapo vunja sheria. Na hili ni somo kuwa utawala wa sheria lazima ufuatwe hata km awe nani
Huu utawala wa sheria ungeanza kwenye ile list of shame inayoongozwa na Mh Jakaya KIkwte kwa kweli tungejua utawala wa sheria umeshika hatamu Tanzania vinginevyo usituletee upupu wako hapo
 
Waziri Kivuli yupi? Washeria na Katiba....yuko ndani kaka. Wao wamevikwa vilemba vya ukoka wanadhani hata wakivunja sheria wataachiwa?. Ngoja waziri kivuli wa mambo ya ndani GL naye atie pua aone kama ataachiwa. By the way waziri wa kazi (kivuli) vipi?.

Maana huyu mama nae anavyopenda ukubwa!! shurti aweke '' Waziri kivuli wa kazi na ajira''..basi mpaka kwenye JF!!!

ndugu kuwa na akili,acha uendawazimu ndugu.
 
sikuatakapo kosa kupigiwa makofi anaweza atakumuwekea bangi mtu mfukoni ili apate umaarufu,jiulizeni hyo bangi atakuwa kaipata wapi?
 
Ukichunguza sana uko Tunisia kulianza hivi hivi kwa Mtu mmoja kutotendewa aki na Polisi, Sasa nadhani CCM wamekamata pabaya wanakwenda kulekule, Tumevumilia sana sasa Tunakaribia kuchoka Move ikianza Polisi wote watakimbia.RIP wote walio poteza Maisha kwa kutetea Aki yao ya Msingi.
 
Ni wajibu wa polisi kuwalinda raia na mali zao. Suala la haraik ya watu kukusanyika na kwenda kuzika tena kwa itikadi ya chama na tena wakiwa na hasira ni suala HATARISHI. Na katika mkusanyiko huo kuna watu hawashabikii itikadi hizo za chama hicho, ukitokea msuguano kidogo tu mlipuko wake ni mkubwa utawaathiri hata raia wapenda Amani,, kumbuka Arusha mliruhisia kwa sababu kuu 2. Moja waliofariki inasadikika walikuwa wanachama wa CDM kwasababu walikuwa kwenye maandamano. Pili viongozi wakuu wa kichama walisign makubaliano maalumu ya kuhakikisha hakutatokea sintofahamu ambayo itasababisha police kuingilia ili kuwalinda raia na mali zao pia wawe tayari kushtakiwa... Je haya ndo yaliyojiri tarime?? Sasa usilolijua si vema kulizungumzia kwa kulipa hoja VIRAKA na kulibarikia HAKI ISIYO YAKE.

Raia wapenda amani kwa maana yako ni wale wasiowapigia kelele watawala wapuuzi. Nashindwa kukutenganisha na watawala wapuuzi wasiojali hata maiti. "Pili viongozi wakuu wa kichama walisign makubaliano maalumu ya kuhakikisha hakutatokea sintofahamu ambayo itasababisha police kuingilia ili kuwalinda raia na mali zao pia wawe tayari kushtakiwa... Je haya ndo yaliyojiri tarime?? " Yaliyojiri Tarime ni polisi kuiba maiti na kutupa barabarani kwa maagizo toka JUU. Kama wewe uko huko juu hamkini unajua zaidi yangu mpango mzima
 
Back
Top Bottom