Hali ni mbaya Tarime: Polisi watembeza Mabomu usiku huu; Kina Lissu wakamatwa

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Habari zilizonifikia hivi punde ni kuwa huko Tarime hali ni mbaya sana baada ya Polisi kupiga Mabomu na kuwakamata Lissu ,Waitara na Makamanda wengine wa CHADEMA.Polisi wamepiga mabomu hayo ili wapate nafsai ya kuvamia Mochwari walikohifadhiwa marehemu.Hali si shwari kabisa.

Naomba tuwaombee wenzetu wote wa Tarime ili MUNGU awalinde na kuwaepusha na mabaya zaidi.
 
Daa mungu atasaidia tu kwenye vita hii ya hawa Magamba hawawezi kushindana na nguvu ya Umma.Endelea kutujuza
 
jamani amani inatafutwaje bila haki? Mbona serikali inakosa busara? Wanachotaka wananchi mbona si jambo zito kiasi hicho?
 
Jamani nchi hii imegeuka somalia, kwa nini viongozi wetu wanatufanyia hivi lakini?????????? Yani ninatamani hata nife kuliko kuona haya maovu yote yanayotendwa na serikali ya kikwete
 
Hawa magamba wanataka kuleta uchafuzi mwingine hawajaridhika na maouvu wanayoyafanya wanataka kuongeza mengine
 
Sasa wanataka kuchukua miili wakazike wao au wanata kufanya kitu gani ? Huu ndiyo utawala wa sheria au ndiyo mabavu kwamba wana jeshi ? CCM wanategmea kweli kuchukua jimbo la Tarime kwa mwendo huu ? Mungu ni mwema
 
upo umuhimu wa kupitia upya mitaala ya majeshi na hasa polisi,amri za watawala hazitoshi kuwafanya watii kila jambo!
 
CCM muflisi. Kama kawaida yao, wakishindwa kwenye hoja, basi hutumia ubabe. Sumaye aliwaambia wasitumie vyombo vya dola kujibu hoja za wapinzani, wajibu kwa hoja.

Isitoshe hao hao polisi ndiyo waliouwa wananchi na kusingizia eti watu 1000 walivamia mgodi -- idadi iliyokuzwa ili kuelezea kuhalalisha uuwaji kwa kisingizio eti polisi walizidiwa.

Hoja ya kijinga kabisa. Lakini inafurahisha kuona jinsi polisi wanavyoharakisha kuondoka kwa CCM.
 
Ndio Wasira kawatuma nini?
Hadi kieleweke Mungu yupo pamoja na Umma,atawalinda na kuwasimamia Makamanda wote.
 
Jamani wapendwa mwenye taarifa zaidi aendelee kutujuza, wengine tuko mashimoni hata taarifa kupata ni ishu
 
askari wetu wananidhamu ya ajabu sana na inapandikizwa depo.labda kugusa wake na watoto wao ndo wanaogopa!
 
Duh! Jamani hawa polisi mbona wamekuwa hivi? Kwanini wanafanya mambo ambayo yanaweza kusababisha mauaji makubwa sana? Sasa Wananchi wakienda kuchukua silaha walizonazo kama vile marungu, mapanga, magobore na kusema liwalo na liwe si kutakuwa na maafa ya kutisha!?
 
Serikali hii inamambo ya ovyo na kijinga kabisa!
Sasa wanadhani hii ndiyo itafanya serikali iaminike?
 
mimi nasema ccm ni wapuuzi na serikali yao wote wanaoiongoza awana busara na hekima hata kidogo ni kihereher gani kinawafanya kuwavamia na kuwapiga mabomu? Sasa kama wananchi wamewakata kwa nini wajilazimishe kwenda kwenye chumba cha maiti? Au ndo wanazidi kupandikiza chuki kwa wana tarime kwa huyo mbunge wao mchapa vitabu? Au wao wanacho kitaka sana sana ni kitu gani juu ya wana nyamongo walipigiwa ndugu zao na kupoteza maisha yao sasa hapo ndipo wanawasha moto sasa ngoja waje waungane kwenda kudai viongozi wao sijui itakuaje mziki wake huo mto autazimika
 
Na huwezi ukashangaa ukakuta order ya kwa polisi kufanya hivyo ilitoka kwa yule Nape wa CCM. JK hana habari kabisa ya kinachoendelea.
 
Wamechukua maiti kwa nguvu wameondoka nazo wakati wazazi wa marehemu nao wamekamatwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Waliokuwa wanatupa taarifa hivi sasa na wao hawapatikani.Tunajitahidi kupata taarifa kadiri tutakavyoweza.

MUNGU walinde wananchi wote wa Tarime asipotee hata mmoja katika tukio hili.
 
Back
Top Bottom