Halaiki na Elimu

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,458
3,209
Nimesikitika kwa kusikia kutoka kwa watoto waliocheza halaiki katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru huko Shinyanga ya kwamba walianza maandalizi tangu mwezi Julai. Tangu mwezi Julai mpaka mwezi Oktoba watoto zaidi ya 600 walitolewa madarasani kwa ajili ya mazoezi. Kwa kipindi hicho watoto walikuwa wakinywa uji mkavu, chakula kibichi au chakula kisicho na chumvi, na kufan ya mazoezi juani. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, halaiki zinalenga kujenga uzalendo, wanapewa chakula, na wanapewa mavazi. Jana watoto hao wameandamana kudai malipo ambao hawakuahidiwa. Najua watoto wamegadhabishwa kwa kuwa wanahisi wanahujumiwa. Je kwa hali kama hii malengo ya elimu yatafikiwa?. Tukumbuke kuna halaiki za Muungano, Uhuru na kuzima Mwenge; halaiki zote hizo zinahitaji takribani mwezi mmoja mpaka mitatu kwa maandalizi, je ni saa ngapi za elimu zinapotea?
 
Back
Top Bottom