Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi hii Makala ya Nipashe ya leo 11/06/2023
Screen Shot 2023-06-11 at 11.26.12 AM.png
Screen Shot 2023-06-11 at 11.26.36 AM.png

Makala ya leo ni wito kwa Watanzania wenzangu, tujifunze kujikubali kuwa hatuwezi kila kitu!, hakuna nchi yoyote duniani ambayo wanaweza kila kitu wao wenyewe!. Hivyo hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote, taasisi yoyote, ana nchi yoyote kusaidiwa pale inaposhindwa.

Kuna vitu sisi Watanzania wenyewe hatuwezi!, na inapotokea kuna vitu hatuwezi, tunapojaribu kuvifanya na tukashindwa, lazima tujikubali hili tumeshindwa, hatuwezi!.

Swali ni unaposhindwa kuna ubaya wowote kukubali kusaidiwa au tuendelee tuu kujitutumua tukomae tuu mpaka tuweze?

Kiukweli kabisa uamuzi wa kulipa kampuni ya Dubai kutuendeshea Bandari yetu ya Dar es Salaam, Dar Port, ni uamuzi sahihi, kwasababu sisi tumeshindwa, tena kwa maoni yangu, sio Bandari pekee, hata kuiendesha ATCL kwa faida sisi wenyewe peke yetu hatuwezi, lazima tongie ubia!. Hata tukija kwenye SGR ndio kabisa!, lazima tushirikiane na wajuvi wenye uzoefu, wakati tukijenga uwezo wetu wa ndani.

Kuna vitu Watanzania hatuwezi na tunashindwa sio kwasababu ni vilaza, au hatuna uwezo, tunashindwa kwasababu tuu hatujui kutazama mbali!.

Mfano saa hizi tuko busy kujenga SGR, lakini hatuna mkakati wowote wa kujiandaa kwa mzigo wa kuiendesha hiyo SGR kwa faida ndio tukaja na Bandari ya Bagamoyo.

Kuendesha Reli ya SGR kwa faida sio mchezo!. Wenzetu Kenya yameshawakuta, wanaiendesha SGR yao law hasara. Jee sisi tusubirie SGR yetu ikamilike, tujaribu kuioparate tushindwe ndipo tutafute usaidizi?, au wakati ujenzi unaendelea, tutazame mbali kwa kujenga uwezo wa uendeshaji na maandalizi ya kutafuta mzigo wa kushiba wa kubebwa na SGR?.

Hivi tuu tuna reli ya TAZARA tumeshindwa kuiendesha!, Tunduma ndio the busiest border kwa mizigo ya Zambia inabebwa na malori, huku mabehewa ya Tazara yamelala bure!.

Reli ya kati tumeshindwa kuiendesha to it's full capacity!, nenda Bandari kavu ya Isaka!, ukiwa mzalendo mwenye machozi ya karibu, unaweza kutoa machozi!. Reli ya Tanga, Moshi, Arusha, zimetelekezwa!. Mtu aliyeshindwa kuendesha kidogo hiki uje umpe kukuendeshea li SGR!, unategemea nini?!. Kuna ubaya kuwaita watu wenye uwezo wakuendeshee kwa kipindi fulani huku unajenga uwezo wa ndani kuendesha, ukiwa tayari ndipo uendeshe?.

ATCL, tushukuru Magufuli kwa kuwa bold kukimbilia kununua midege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi, bila kuwa na business plan!.

Tumenunua midege ya masafa marefu, long hauls, tunaizungusha Dar-Mwanza-Kia!, tunaichosha bure, wear and tear ni kubwa!, matokeo yake by now, tume ground midege 4 kwa uchovu wa engine, tutatengeneza kwa millions of dollars halafu tuje kuharibu tena!. Ukiangalia abiria wa Tanzania wanaokwenda Ulaya na America kwa ndege za mashirika mengine ni abiria wa kujaza a 7 day flights, lakini sisi wenyewe hatuwezi!, lazima tusaidiwe!.

Pale unaposhindwa kitu fulani, hakuna ubaya wowote kuomba msaada kwa wenye uwezo usaidiwe!.

Tuliwahi kujaribu kwa ATC, TTCL, Tanesco, Dawasco, tukaja kuvunja mikataba hiyo.

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "Ukitaka kula ni lazima uliwe!", hivyo hata huu mkataba wa Bandari, kwavile tunataka kula, ni lazima tuliwe!. Wazungu wanasema "You can't eat your cake and have it!".

Kuna vitu vingi tuu tunashindwa na tunaomba msaada tunasaidiwa. Jengo la BOT lilipoungua, polisi wetu walishindwa kufanya uchunguzi, tuliomba msaada wa polisi wa Uingereza, The Scotland Yard, wakatusaidia.

Juzi kati Tundu Lissu kashambuliwa kwa kupigwa risasi mchana kweupe, Ben Saanane wa JF, kakosoa kitu, kayeyuka!. Azory Gwanda wa gazeti la Mwanamke kaandika kitu, kafuatwa na Toyota Land cruiser ya mkonga, kapotezwa!.

Serikali yetu imeshindwa kufanya uchunguzi wa matukio hayo kwasababu hatuna uwezo huo, lakini tumeona aibu kuomba msaada ili tusaidiwe!. Matokeo yake watu wasiojulikana bado wapo wanajivinjari tuu.

Kuna watu wanadhani Scotland Yard, wanazaliwa na uwezo huo!, no!, Scotland Yard wanafanya scouting kuwapata watu wenye uwezo huo!, hapa Tanzania watu hao tunao lakini hatuwatumii!.

Niliwahi kuuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?.

Ushauri:
Rais Nyerere japo alitupatia uhuru, lakini kulikuwa na watu wengine wenye uwezo kuliko Rais Nyerere, wangeweza kutututawala vizuri zaidi na kutufikisha mbali zaidi, ila ni Nyerere ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwa rais wetu!. Vivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia, haina maana kuwa ndio they are the best, but the chosen ones!, lakini the best wapo wanajijua wanaangalia tuu huku wamejinyamazia kwasababu hawajaombwa au kushirikishwa!.

Wito kwa serikali yetu Tukufu, tukishindwa jambo lolote, kabla hatujakimbilia huko nje kuomba msaada, lets exhaust the local remedies!, yaani tuwaulize kwanza Watanzania wenye uwezo kusaidia.

Serikali ijitokeze kwa uwazi kabisa very transparently iseme wazi kabisa kuwa hili limetushinda, kama kuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania inaweza kusaidia, na ina uwezo huo, ijitokeze isaidie.

Ikitokea hakuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania ina uwezo huo, ndipo tutafute wabia kwa kutangaza kwa uwazi kabisa, mabingwa wa uendeshaji wa Bandari duniani washindane kwa ushindani wa wazi tumpe mshindi.

Hivyo Watanzania tuache nongwa, tunaposhindwa jambo fulani, tusione aibu kusema tumeshindwa!, tuanze kuomba msaada kwa Watanzania kwanza, tukikosa ndio twende kwa wageni kutafuta msaada kwa uwazi na ushirikishwaji.

Huu mpango wa kumpa Mwarabu wa Dubai kutuendeshea Bandari yetu, ni mpango wenye maslahi makubwa kwa taifa la Tanzania, tuunge mkono ila tuwe makini na huyu Mwarabu wa Dubai maana...!.

Paskali
 
Kama kupigwa tulisha pigwa kabla hapajakucha P.Shida ni tabia za kitanzania zilizowazi kwa wote wenye kuona na wenye macho,hapa ni kusubiri tu matokeo ambayo yako dhahiri na yalishadhihirika mara kadha,pale TRC, TANESCO kwa uchache sana🤔
 
If it looks like a duck, swims like a duck, and quacks like a duck, then it probably is a duck.

Huko nyuma tulivyopigwa mazingira yalikuwaje? Mimi naona the same pattern.
 
Mkuu Pascal, nadhan this is sarcasm.

Kubinafsisha ni sawa, lakini kwanini serikal yetu haitaki kuwekeza kwa matajiri weusi? Zaidi ya kuwapiga vita na karibu wote wamefariki.

Kuna mentality kwamba mwekezaji lazima awe mzungu au mwarabu au muhindi.

Waakati huo huo, hao watu wanapewq special economic right. Sio za kikodi sio za kuingiliwa katika utendaji kazi wao...

Kwanini hatusaidii biashara za waafrica asili kunyanyuka tunawekeza kwenye kusubiri na kusifia wageni??
Alikuwemo Reginald na Mfuriki hapa, walipigwa vita hadi wakajifia wenyewe, tumebaki kusubir wajomba wa arabuni na ulaya.

Kwa sasa tumebaki na wahindi na wayemeni, nao hawathubutu kuwekeza kwenye miradi hii ya kimkakat kwa sababu ya historia mbaya ya nchi yetu kwa wafanyabiashara.

Bado Karnes ya 21 tunasubir kusaidiwa... nchi yetu haina kitu gani?

Nimejaribu kuchek ukubwa wa DP World ni kampuni imeanza juzi, haina miaka 30, na mitaj sio mikubwa Kivile.

Ni kampuni binafsi lakini angalia support kwa serikal yao... sisi tunacheka cheka tu hapa....
Ukiangalia namna Spika Tulia alivokuwa anaweka mkazo kudhibiti hoja yeyote ya kupinga, utadhani she was really into national interests, inahuzunisha sana.
 
Kuna mmoja alisema " kuweka watu kama wasimamizi huku wazawa makini wakijifunza kupitia wajuvi hao watakao kuwa wanalipwa ikiwa ni sehemu ya maendeleo na kama maendeleo ni kitu endelevu basi kugawa moja kwa moja mana yake hata mkiachiwa hamna la maana mtafanya".
 
Hiki ni Kipigo kikubwa sana, tena Kipigo hiki cha dpw ni cha hadaa za sungura mjanja,wadubai wamepiga ramli ya miaka Mia ijayo Dubai iwe vipi.
katika kitu muhimu sana ambavyo dubai hawana ni ardhi yenye rutba na mashamba ambao ya kuweza kuilisha dubai kwa uhakika kwa miaka 100 na zaidi.
Bandari ya tanzania ni lango kubwa sana kwa afrika ya mashariki na kati, makusanyo yote ya vyakula na raw material sasa yamepata uhakika wa kupita bila shida.watamiliki bandari ndani ya ardhi ya afrika hii strategically ni turufu kubwa sana na inatokana na akili inayoona mbali sana
 
Wananodi hii Makala ya Nipashe ya leo 11/06/2023
View attachment 2653617View attachment 2653619
Makala ya leo ni wito kwa Watanzania wenzangu, tujifunze kujikubali kuwa hatuwezi kila kitu!, hakuna nchi yoyote duniani ambayo wanaweza kila kitu wao wenyewe!. Hivyo hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote, taasisi yoyote, ana nchi yoyote kusaidiwa pale inaposhindwa.

Kuna vitu sisi Watanzania wenyewe hatuwezi!, na inapotokea kuna vitu hatuwezi, tunapojaribu kuvifanya na tukashindwa, lazima tujikubali hili tumeshindwa, hatuwezi!.

Swali ni unaposhindwa kuna ubaya wowote kukubali kusaidiwa au tuendelee tuu kujitutumua tukomae tuu mpaka tuweze?

Kiukweli kabisa uamuzi wa kulipa kampuni ya Dubai kutuendeshea Bandari yetu ya Dar es Salaam, Dar Port, ni uamuzi sahihi, kwasababu sisi tumeshindwa, tena kwa maoni yangu, sio Bandari pekee, hata kuiendesha ATCL kwa faida sisi wenyewe peke yetu hatuwezi, lazima tongie ubia!. Hata tukija kwenye SGR ndio kabisa!, lazima tushirikiane na wajuvi wenye uzoefu, wakati tukijenga uwezo wetu wa ndani.

Kuna vitu Watanzania hatuwezi na tunashindwa sio kwasababu ni vilaza, au hatuna uwezo, tunashindwa kwasababu tuu hatujui kutazama mbali!.

Mfano saa hizi tuko busy kujenga SGR, lakini hatuna mkakati wowote wa kujiandaa kwa mzigo wa kuiendesha hiyo SGR kwa faida ndio tukaja na Bandari ya Bagamoyo.

Kuendesha Reli ya SGR kwa faida sio mchezo!. Wenzetu Kenya yameshawakuta, wanaiendesha SGR yao law hasara. Jee sisi tusubirie SGR yetu ikamilike, tujaribu kuioparate tushindwe ndipo tutafute usaidizi?, au wakati ujenzi unaendelea, tutazame mbali kwa kujenga uwezo wa uendeshaji na maandalizi ya kutafuta mzigo wa kushiba wa kubebwa na SGR?.

Hivi tuu tuna reli ya TAZARA tumeshindwa kuiendesha!, Tunduma ndio the busiest border kwa mizigo ya Zambia inabebwa na malori, huku mabehewa ya Tazara yamelala bure!.

Reli ya kati tumeshindwa kuiendesha to it's full capacity!, nenda Bandari kavu ya Isaka!, ukiwa mzalendo mwenye machozi ya karibu, unaweza kutoa machozi!. Reli ya Tanga, Moshi, Arusha, zimetelekezwa!. Mtu aliyeshindwa kuendesha kidogo hiki uje umpe kukuendeshea li SGR!, unategemea nini?!. Kuna ubaya kuwaita watu wenye uwezo wakuendeshee kwa kipindi fulani huku unajenga uwezo wa ndani kuendesha, ukiwa tayari ndipo uendeshe?.

ATCL, tushukuru Magufuli kwa kuwa bold kukimbilia kununua midege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi, bila kuwa na business plan!.

Tumenunua midege ya masafa marefu, long hauls, tunaizungusha Dar-Mwanza-Kia!, tunaichosha bure, wear and tear ni kubwa!, matokeo yake by now, tume ground midege 4 kwa uchovu wa engine, tutatengeneza kwa millions of dollars halafu tuje kuharibu tena!. Ukiangalia abiria wa Tanzania wanaokwenda Ulaya na America kwa ndege za mashirika mengine ni abiria wa kujaza a 7 day flights, lakini sisi wenyewe hatuwezi!, lazima tusaidiwe!.

Pale unaposhindwa kitu fulani, hakuna ubaya wowote kuomba msaada kwa wenye uwezo usaidiwe!.

Tuliwahi kujaribu kwa ATC, TTCL, Tanesco, Dawasco, tukaja kuvunja mikataba hiyo.

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "Ukitaka kula ni lazima uliwe!", hivyo hata huu mkataba wa Bandari, kwavile tunataka kula, ni lazima tuliwe!. Wazungu wanasema "You can't eat your cake and have it!".

Kuna vitu vingi tuu tunashindwa na tunaomba msaada tunasaidiwa. Jengo la BOT lilipoungua, polisi wetu walishindwa kufanya uchunguzi, tuliomba msaada wa polisi wa Uingereza, The Scotland Yard, wakatusaidia.

Juzi kati Tundu Lissu kashambuliwa kwa kupigwa risasi mchana kweupe, Ben Saanane wa JF, kakosoa kitu, kayeyuka!. Azory Gwanda wa gazeti la Mwanamke kaandika kitu, kafuatwa na Toyota Land cruiser ya mkonga, kapotezwa!.

Serikali yetu imeshindwa kufanya uchunguzi wa matukio hayo kwasababu hatuna uwezo huo, lakini tumeona aibu kuomba msaada ili tusaidiwe!. Matokeo yake watu wasiojulikana bado wapo wanajivinjari tuu.

Kuna watu wanadhani Scotland Yard, wanazaliwa na uwezo huo!, no!, Scotland Yard wanafanya scouting kuwapata watu wenye uwezo huo!, hapa Tanzania watu hao tunao lakini hatuwatumii!.

Niliwahi kuuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?.

Ushauri:
Rais Nyerere japo alitupatia uhuru, lakini kulikuwa na watu wengine wenye uwezo kuliko Rais Nyerere, wangeweza kutututawala vizuri zaidi na kutufikisha mbali zaidi, ila ni Nyerere ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwa rais wetu!. Vivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia, haina maana kuwa ndio they are the best, but the chosen ones!, lakini the best wapo wanajijua wanaangalia tuu huku wamejinyamazia kwasababu hawajaombwa au kushirikishwa!.

Wito kwa serikali yetu Tukufu, tukishindwa jambo lolote, kabla hatujakimbilia huko nje kuomba msaada, lets exhaust the local remedies!, yaani tuwaulize kwanza Watanzania wenye uwezo kusaidia.

Serikali ijitokeze kwa uwazi kabisa very transparently iseme wazi kabisa kuwa hili limetushinda, kama kuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania inaweza kusaidia, na ina uwezo huo, ijitokeze isaidie.

Ikitokea hakuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania ina uwezo huo, ndipo tutafute wabia kwa kutangaza kwa uwazi kabisa, mabingwa wa uendeshaji wa Bandari duniani washindane kwa ushindani wa wazi tumpe mshindi.

Hivyo Watanzania tuache nongwa, tunaposhindwa jambo fulani, tusione aibu kusema tumeshindwa!, tuanze kuomba msaada kwa Watanzania kwanza, tukikosa ndio twende kwa wageni kutafuta msaada kwa uwazi na ushirikishwaji.

Huu mpango wa kumpa Mwarabu wa Dubai kutuendeshea Bandari yetu, ni mpango wenye maslahi makubwa kwa taifa la Tanzania, tuunge mkono ila tuwe makini na huyu Mwarabu wa Dubai maana...!.

Paskali
Nchi haijashindwa, walioshindwa ni wasimamizi wake. Na wameshindwa karibu kila mahali.
Kwanini wanang’ang’ania wakati wameshindwa?
 
Kama taasisi na mashirika ya serikali yanashindwa kujiendesha basi hapa shida ni serikali, je haiwezekani tukaibinafsisha serikali? Mfano kwanini wizara wa nishati tusiwape Gazprom au Total, Ujenzi na uchukuzi tukawapa wachina, wizara ya fedha na mipango tukawapa AfDB nk.
 
Kama CCM imeshindwa haiwezi ,usiseme Tanzania hatuwezi,

Kama Serikali under Sa100 imeshindwa usiseme Tanzania tumeshindwa.

CCM Si alpha na Omega kwamba ikishindwa, wote tumeshindwa.

USHAURI: Serikali chini ya CCM na sa100 Mmekiri kushindwa kusimamia raslimali zetu, mmepoteza uhalali kuongoza Nchi.

MTUPISHE.
 
Mkuu, Pascal Mayalla hivi sisi tunaweza kitu gani? Please, tafadhali.
Tusidanganyane, hakuna tunachoweza. Hata hizi ngono na ulevi bado tukishindanishwa kidunia hata kwenye mia na kumi (110) bora hatuingii.

Kuna mradi mwingine waarabu wanakuja nao, nasikia huo Mkataba wake ukishasainiwa tu, basi mtanzania kufanya kazi uwe umetaka mwenyewe. Kila mtu atakua anaingiziwa kama milioni tano kwa mwezi na ukienda kununu kitu chochote na popote hautatakiwa kulipi, muuzaji atakupa huduma halafu bill anapelekewa Mwarabu.
Tanzania yenye neema inakuja, hakuna haja tena ya kufanya kazi
 
Back
Top Bottom