Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,535
- 8,620
Katika miaka ya karibuni ukianzia utawala wa Magufuli hadi sasa, tukianza kuorodhesha kuna Watanzania wengi sana wameteuliwa kuwa Mabalozi na wapo wengi tu ambao wameteuliwa na hawajawahi hata kupangiwa vituo vya kazi, hii ni kuwaumiza watanzania kwani hizo hadhi zinatolewa kama zawadi au adhabu au kuwaondoa watu nchini na sio sifa halisi za kusaidia nchi yetu.
Hata kwenye uteuzi wa juzi tu kuna ambao walikuwa wameapa kama mabalozi na hata kabla hawajapangiwa vituo wanapangiwa kazi zingine, kuna wengine wameteuliwa ubalozi wamekaa nje miaka hata miwili haijafika wanarudi nchini, hizo zote gharama za kuwasafirisha na familia zao na mambo mengine ni za watanzania na kuishia kurudishwa nchini hata kabla mikataba yao haijaisha hii sasa inaondoa HADHI ya cheo cha UBALOZI wamekua wengi sasa kama wa NYUMBA KUMI KUMI.
Kuna wengine kama Balozi Nchimbi yeye anakuwa victims wa siasa muda wote kuna wenzake hawataki arudi nchini, hata majuzi ilitangazwa kabisa kuwa amerudishwa nyumbani apangiwe kazi nyingine lakini huyo huyo jana kaonekana anawapeleka ujumbe wa TFF na waziri wa michezo makao makuu ya CAF
Kulikuwa na haja gani ya kutangaza kumrudisha kama muda bado , ikumbukwe kuwa aliporudi nchini baada ya kuwa “exciled” na Magufuli yeye na Afisa Mombo ilitegemea angebaki nchini hata kupumzika ikizingatiwa pia kuwa alikuwa kamaliza kumzika Baba yake lakini ghafla hata kabla ya mwezi akakimbiziwa Egypt Bila hata kutangazwa na bila hata kuambiwa Balozi Maj Gen Bahati amerudishwa.
NADHANI washauri kuwa makini mnajikuta mnaliingiza taifa kwenye gharama kubwa bila sababu. Mabalozi walio mtaani wanaosubiri kupangiwa vituo wamekuwa wengi sana ..wote hao pale tu wanapotangazwa wanalipwa mishahara na stahiki za ubalozi.