Habibu Mchange aikacha ACT-wazalendo na kuachana na siasa

Mara nimeachana na siasa mara mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanywa vinginevyo.
Huyu bado hajaachana na siasa,anapima upepo tu ukiwa sawa atarudi tena majukwaani kupitia chama kingine cha siasa.

Hakuna unafiki mkubwa kama kuomba msamaha kwa matendo uliyoyafanya ukiwa na akili zako timamu.
Hakika sitokusamehe Mchange kwa matusi uliyomtukana Mzee wangu Lowassa.
Haaaaa! Nimependa kauli yako ya mtu hatakiwi kuomba msamaha kwa matendo aliyotenda akiwa timamu.

Nimekumbuka wakati wa kampeni nilikuwa Kigoma Mchange alipopanda jukwaani akasema chadema wametuletea mtu hawezi hata kushika maiki.

Zitto kwa busara zake akasimama akamnyanganya maiki akasema afya in majaliwa ya mwenyezi Mungu.

Nadhani Mchange ndio alikuwa kampeni meneja wa Anna
 
Sa

Sasa hapa CHADEMA inahusikaje?
Hawa ni vijana wa Zitto aliotoka nao CHADEMA kwa ahadi kedekede;alikuwepo Mchange,Juliana,Mwampamba na kina Gwakisa.They are No More.

Kina Mwampamba na Juliana waliamua kusalimu amri CCM na sasa wamekula ajira.Wengi waliombatana na Zitto kama Machali ndio huyo karudi CCM,Vijana walidhani watatoboa kupitia ACT,lkn uvumilivu umewashinda.

Kujenga Chama sio kazi ndogo,Na hasa chama cha Upinzani,hiyo CUF unayoiona pale Buguruni kuna watu wameitolea damu na jasho;ile CHADEMA ya Ufipa ipo pale kwa sbb ya sadaka na maisha ya watu.Hii CCM unayoiona ina wenyewe,walitoka jasho na damu kuiweka hapo ilipo.

Ndio maana unapoona kina Mbowe wanakomaa na chama chao,wanajua walipokitoa na wanajua mapito yake.Hawa kina Mchange walikuwa wanawatukana kina Mbowe,wakafikiri kujenga chama pinzani upinzani ni kama kula pizza margaleta kwa uma.Ni kazi nzito ya jasho na damu.

Sasa anakuja mtu mmoja,ametoka huko Mwisho wa Reli;anasema Mbowe si lolote si chchote,chama changu ndio kitakuwa mbadala,anasahau ujanja wote wa town na ulimwengu wa siasa walimuingiza hao hao kina Mbowe.Shule ni zaidi ya Utoto wa mjini,down town kitambo....Politics is more than being in the class,its a game of the hastlers!!

Sasa Zitto ndio ataelewa kwanini aliambiwa kaa pembeni muachie Mbowe uenyekiti

Duh nilifikiri uwanja wako ni masuala ya anga kumbe hata siasa upo,hongera sana mkuu wangu.
 
Imeandikwa kwenye Facebook page ya Chama cha ACT Wazalendo muda mfupi uliopita kuwa bwana Mshange amejiuzulu nyadhifa zake zote za ndani ya chama na pia amejitoa kwenye kushiriki mambo yote yahusiyo Siasa kwa kile alichodai kuwa ni kujipa muda mwingi kwenye shughuli zake za kijasiliamali.
Kila la heri ndugu Mshange na maisha yako mapya nje ya siasa.

Kila la Kheri Komredi Habibu Mchange, ACT Wazalendo tunakushukuru Sana kwa Mchango wako kwenye Chama.
 
Attachments

  • habib.jpg
    habib.jpg
    14.3 KB · Views: 59
Habibu Mchange nenda baba nenda, wewe si ni teacher secondary, nadhani uneenda kufundisha tu kwani ni kazi itakayokufaa, Siasa kwako wewe msaliti ni ngumu sana
 
Haaaaa! Nimependa kauli yako ya mtu hatakiwi kuomba msamaha kwa matendo aliyotenda akiwa timamu.

Nimekumbuka wakati wa kampeni nilikuwa Kigoma Mchange alipopanda jukwaani akasema chadema wametuletea mtu hawezi hata kushika maiki.

Zitto kwa busara zake akasimama akamnyanganya maiki akasema afya in majaliwa ya mwenyezi Mungu.

Nadhani Mchange ndio alikuwa kampeni meneja wa Anna
Mkuu usinikumbushe tukio lile,nilikuwa naangalia live na machozi ya uchungu yalinitoka.
Eti leo hii anaomba msamaha, WTF?

Asingeomba msamaha wa jumla...angemuomba mzee kivyake kidogo ingeleta maana.

Mungu Mkubwa,wote waliomtukana na kumdhihaki kila mmoja anayapata malipo yake kwa namna yake.
 
nampongeza huyu kijana kwa kumalizia kwa kutubu kwa wote Alio wa kwanza katika Harakati zake za kisiasa.

Nikweli aliwa kwaza wengi sana hasa propaganda zake kwa UKAWA kipindi cha Uchaguzi.

Akubalie kutubu basi mtu huyo ni Muungwana, mwisho hata mimi namtakia kila na Kheri kwenye maisha mapya nje ya siasa.

Ila Ajue siasa siyo vita na kuchukiana kurushiana tuhuma zisizo na ushahidi, kutengenezeana visasi na uadui.

Mwisho wa siku wote wanaotumia siasa vibaya wanakuja kuwa kama wakina Mchange kuomba radhi watu walio wakwaza.

Yatupasa tutambue nje ya siasa sisi ni watanzania na watanzania sote ni ndugu moja na tunaongea lugha moja kama watanzania.

Hivyo ni wito wangu watu walio jawa na pepo la siasa za Majungu fitina na visasi wajue mwisho wa siku sisi ni ndugu na siasa haituondolei utanzania wetu.
 
Mara nimeachana na siasa mara mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanywa vinginevyo.
Huyu bado hajaachana na siasa,anapima upepo tu ukiwa sawa atarudi tena majukwaani kupitia chama kingine cha siasa.

Hakuna unafiki mkubwa kama kuomba msamaha kwa matendo uliyoyafanya ukiwa na akili zako timamu.
Hakika sitokusamehe Mchange kwa matusi uliyomtukana Mzee wangu Lowassa.

teh teh....
 
Mkuu usinikumbushe tukio lile,nilikuwa naangalia live na machozi ya uchungu yalinitoka.
Eti leo hii anaomba msamaha, WTF?

Asingeomba msamaha wa jumla...angemuomba mzee kivyake kidogo ingeleta maana.

Mungu Mkubwa,wote waliomtukana na kumdhihaki kila mmoja anayapata malipo yake kwa namna yake.
Nashindwa kuchangia hoja hii kwa uzuri, lakini acha nitoe mchango wa kiujumla kuhusu kizazi hiki hasa wanasiasa wake wengi hawana adabu utadhani watoto wa mtaani.
Sorry to say that lakini ndiyo ukweli.
Tafakari chukua hatua
 
Back
Top Bottom