Habibu Mchange aikacha ACT-wazalendo na kuachana na siasa

Huyu ameamua kujisalimisha CCM. Wanaanzaga hivi hivi..!
Kama ambavyo huna haya kufuatana na FISADI LOWASSA, siku akienda ACT-WAZALENDO utakuwa naye huko. Wewe hakuwa CCM bali ulikuwa kwa LOWASSA na hata leo hauko CHADEMA bali kwa LOWASSA, hiyo ndiyo njaa kuu, ya kumlamba mtu viatu
 
Sa
Chadema watanyooka tu.

Nasikia kuna mwingine amejiteka
Sasa hapa CHADEMA inahusikaje?
Hawa ni vijana wa Zitto aliotoka nao CHADEMA kwa ahadi kedekede;alikuwepo Mchange,Juliana,Mwampamba na kina Gwakisa.They are No More.

Kina Mwampamba na Juliana waliamua kusalimu amri CCM na sasa wamekula ajira.Wengi waliombatana na Zitto kama Machali ndio huyo karudi CCM,Vijana walidhani watatoboa kupitia ACT,lkn uvumilivu umewashinda.

Kujenga Chama sio kazi ndogo,Na hasa chama cha Upinzani,hiyo CUF unayoiona pale Buguruni kuna watu wameitolea damu na jasho;ile CHADEMA ya Ufipa ipo pale kwa sbb ya sadaka na maisha ya watu.Hii CCM unayoiona ina wenyewe,walitoka jasho na damu kuiweka hapo ilipo.

Ndio maana unapoona kina Mbowe wanakomaa na chama chao,wanajua walipokitoa na wanajua mapito yake.Hawa kina Mchange walikuwa wanawatukana kina Mbowe,wakafikiri kujenga chama pinzani upinzani ni kama kula pizza margaleta kwa uma.Ni kazi nzito ya jasho na damu.

Sasa anakuja mtu mmoja,ametoka huko Mwisho wa Reli;anasema Mbowe si lolote si chchote,chama changu ndio kitakuwa mbadala,anasahau ujanja wote wa town na ulimwengu wa siasa walimuingiza hao hao kina Mbowe.Shule ni zaidi ya Utoto wa mjini,down town kitambo....Politics is more than being in the class,its a game of the hastlers!!

Sasa Zitto ndio ataelewa kwanini aliambiwa kaa pembeni muachie Mbowe uenyekiti
 
Ben Saa Nane yupo fungate,amechukuliwa na wale wazungu anaowafanyia ushushu,amekwenda ulaya kuto taarifa ya upepelezi aliopewa,
 
Habibu buana....nilikutabilia haya mambo tangu dalili za kufeli kwako elimu ya chuo na ku-disco zilipoanza. Najua tutakutana nitakukumbusha kauli yangu hii. Pole sana rafiki yangu. Nimeumia kuona umeambulia machozi yasiyo ya lazima cha ajabu ndo kwanza unataka uanze maisha....shule yenyewe ndo hiyo uliifanyia utakavyo ikakutenda.........kitumie vema hicho cheti chako cha fomu sita labda kitakusaidia.
 
Sa

Sasa hapa CHADEMA inahusikaje?
Hawa ni vijana wa Zitto aliotoka nao CHADEMA kwa ahadi kedekede;alikuwepo Mchange,Juliana,Mwampamba na kina Gwakisa.They are No More.

Kina Mwampamba na Juliana waliamua kusalimu amri CCM na sasa wamekula ajira.Wengi waliombatana na Zitto kama Machali ndio huyo karudi CCM,Vijana walidhani watatoboa kupitia ACT,lkn uvumilivu umewashinda.

Kujenga Chama sio kazi ndogo,Na hasa chama cha Upinzani,hiyo CUF unayoiona pale Buguruni kuna watu wameitolea damu na jasho;ile CHADEMA ya Ufipa ipo pale kwa sbb ya sadaka na maisha ya watu.Hii CCM unayoiona ina wenyewe,walitoka jasho na damu kuiweka hapo ilipo.

Ndio maana unapoona kina Mbowe wanakomaa na chama chao,wanajua walipokitoa na wanajua mapito yake.Hawa kina Mchange walikuwa wanawatukana kina Mbowe,wakafikiri kujenga chama pinzani upinzani ni kama kula pizza margaleta kwa uma.Ni kazi nzito ya jasho na damu.

Sasa anakuja mtu mmoja,ametoka huko Mwisho wa Reli;anasema Mbowe si lolote si chchote,chama changu ndio kitakuwa mbadala,anasahau ujanja wote wa town na ulimwengu wa siasa walimuingiza hao hao kina Mbowe.Shule ni zaidi ya Utoto wa mjini,down town kitambo....Politics is more than being in the class,its a game of the hastlers!!

Sasa Zitto ndio ataelewa kwanini aliambiwa kaa pembeni muachie Mbowe uenyekiti
Kaka hzo nondo unazoshusha ndizo zinazoleta maana ya JF km home of GT co hoja za kitoto znazoshushwa daily hapa. BIG UP
 
Mara nimeachana na siasa mara mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanywa vinginevyo.
Huyu bado hajaachana na siasa,anapima upepo tu ukiwa sawa atarudi tena majukwaani kupitia chama kingine cha siasa.

Hakuna unafiki mkubwa kama kuomba msamaha kwa matendo uliyoyafanya ukiwa na akili zako timamu.
Hakika sitokusamehe Mchange kwa matusi uliyomtukana Mzee wangu Lowassa.
 
Kutoka kwa HABIBU MCHANGE.

TAARIFA KWA UMMA
--------------------------------------
YAH:- KUJIVUA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO NA KUTOSHIRIKI SIASA.
----------------------------------------
Mimi Mchange Habibu Mchange, Leo Jumaamosi tarehe 10.12.2016, ninaujuza umma wa Watanzania, Rafiki zangu, ndugu na jamaa.

Kwamba kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikijihusisha na harakati za kisiasa, awali nikiwa mwanachama wa Chadema na baadae ACT WAZALENDO.

Kwamba katika Chama cha ACT WAZALENDO nimepata heshima ya kuwa kiongozi mwandamizi kama katibu wa Mipango na Mikakati na baadae Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika secretarieti ya Chama hicho.

Na Kwamba tangu kujiunga kwangu na Chama hicho nimekuwa mjumbe wa kamati kuu, mjumbe wa Halimashauri kuu na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Chama.

Kwa moyo mkunjufu kabisa, na kwa mapenzi mema na taifa langu.

Ninathibitisha Kwamba nimejitoa rasmi katika ushiriki wa aina yote ya siasa ili nipate muda mwingi zaidi kufanya na kusimamia shughuli zangu za kijasiriamali zinazonitaka nitoe fursa na huduma Sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa.

Kwa mantiki hiyo basi, kuanzia Leo hii, nitaiomba jamii katika yote nitakayofanya inione nimefanya kama Mchange huru asiye mwanachama wa Chama chochote cha siasa.

Ninaomba uamuzi wangu huu uheshimiwe na kamwe nisihusishwe na aina yoyote ya siasa bali utanzania wangu.

Ningeweza kufanya uamuzi wangu huu kimya kimya, lakini kwa hatua niliyoifikia na ili kuweka kumbukumbu sawia ni budi niutoe kwa umma.

Ninafahamu kuwa kuwa mwanachama wa Chama cha siasa ni haki yangu ya kikatiba, lakini nimeamua kuihifadhi haki yangu hiyo kwa sasa Mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanywa vinginevyo.

Ninawatakia kila la heri waliokuwa wanachama wenzangu wa ACT WAZALENDO katika kuyafikia malengo ya msingi ya uanzishwaji wa Chama hicho.

Kujiondoa kwangu kushiriki katika siasa kusihesabiwe kama sehemu ya kukwamisha au kurudisha nyuma matarajio na au malengo ya Chama hicho.

Tafadhali ichukueni hii kama chachu ya kuwafanya mfikie malengo mahsusi kwa wakati muafaka bila kurudi nyuma.

Msivunjike moyo, msirumbane, pendaneni,heshimianeni na shikamaneni ili mfikie lengo

Sasa nitabaki na kuendelea kuwa ndugu yenu, rafiki na swahiba. zaidi mtanzania mwenzenu. Tutaendelea kushirikiana katika mambo yote ya kijamii na kimaisha yasiyohusiana na mlengo wa kiitikadi wa kisiasa.

Kwa wanachama wa vyama vinginevyo kama CHADEMA, CUF, CCM, ADA TADEA na kadharika, nitaendelea kuwa rafiki mwema kwenu, jirani na ndugu wa kweli kama au pengine zaidi ya ilivyokuwa hapo awali.

Ninawatakia heri wanasiasa wote wa vyama vyote hapa nchini.

Ninawaomba radhi wote niliowahi kuwakosea, kuwa kwaza ama kuwafanya wajisikie vibaya kutokana na matendo yangu, maandishi yangu Misimamo yangu, matamshi yangu ama na mwenendo wangu wa kisiasa kwa kipindi chote nilichokuwa mwanachama wa vyama vya siasa hapa nchini.

Ninaahidi kuendelea kuwa mtanzania Mtiifu mwenye mapenzi mema kwa taifa langu huku nikiwatakia heri wanachama wapenzi na viongozi wa vyama vyote vya siasa.

Itoshe tu kufahamika Kwamba Mimi Habibu Mchange, kwa sasa si mwanachama, mpenzi wala mshabiki wa Chama chochote cha siasa.

Zaidi, Ninawaomba radhi watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine nitakuwa nimewakwaza kutokana na uamuzi wangu huu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Wasalaam
Habibu Mchange,
0762178678.
Morogoro Tanzania
Kazi mliyotumwa mmeimaliza
 
Bora huyu jamaa ameachana na siasa, maana sijapata kuona kijana mwenye siasa za chuki na husda ya waziwazi kama huyu. Na sina hakika kama kweli amestaafu siasa ila nadhani alichotarajia kimekwama hivyo anatafuta njia za kijanja kukwepa aibu. Sasa nimeamini ule msemowa jeolous never win
 
Tatizo ule mfereji wao pale NSSF umekatwa njaa imechukua nafasi yake,kiongozi mkuu anatafuna fedha zake za ubunge taratibu Mama Anna mialiko ya semina na makongamano yanamwingizia vijisenti kiduchu.Wenzangu na mimi hawana kitu kila dakika wanapiga miayo na matumbo yananguruma ungedhani honi za meli hakuna namna lazima kujisalimisha tu.
 
Sa

Sasa hapa CHADEMA inahusikaje?
Hawa ni vijana wa Zitto aliotoka nao CHADEMA kwa ahadi kedekede;alikuwepo Mchange,Juliana,Mwampamba na kina Gwakisa.They are No More.

Kina Mwampamba na Juliana waliamua kusalimu amri CCM na sasa wamekula ajira.Wengi waliombatana na Zitto kama Machali ndio huyo karudi CCM,Vijana walidhani watatoboa kupitia ACT,lkn uvumilivu umewashinda.

Kujenga Chama sio kazi ndogo,Na hasa chama cha Upinzani,hiyo CUF unayoiona pale Buguruni kuna watu wameitolea damu na jasho;ile CHADEMA ya Ufipa ipo pale kwa sbb ya sadaka na maisha ya watu.Hii CCM unayoiona ina wenyewe,walitoka jasho na damu kuiweka hapo ilipo.

Ndio maana unapoona kina Mbowe wanakomaa na chama chao,wanajua walipokitoa na wanajua mapito yake.Hawa kina Mchange walikuwa wanawatukana kina Mbowe,wakafikiri kujenga chama pinzani upinzani ni kama kula pizza margaleta kwa uma.Ni kazi nzito ya jasho na damu.

Sasa anakuja mtu mmoja,ametoka huko Mwisho wa Reli;anasema Mbowe si lolote si chchote,chama changu ndio kitakuwa mbadala,anasahau ujanja wote wa town na ulimwengu wa siasa walimuingiza hao hao kina Mbowe.Shule ni zaidi ya Utoto wa mjini,down town kitambo....Politics is more than being in the class,its a game of the hastlers!!

Sasa Zitto ndio ataelewa kwanini aliambiwa kaa pembeni muachie Mbowe uenyekiti
Huyu jamaa na gazeti lao la Jamvi la Habari walizidi ilikuwa too much kila post ni kumtukana Mbowe na Lowassa bila heshima kabisa.
 
Huyu Machange siku ACT wazalendo wanafungua kampeni zao mbagala kama sijakosea aliongea ujinga sana juu ya Lowassa hasa juu ya afya yake kama mtu anayeumwa ugonjwa usioeleweka na anayekaribia kufa .Zitto alipoanza kuongea akamkosoa mbele za watu na kumwambia hatuko hapa kukejeli watu na lazima tuheshimu wengine. Nilianza kumdharau toka siku hiyo zaidi namtakia maisha mema ajue tu SIASA YATAKA MOYO.
 
Back
Top Bottom