Habari za kutisha gazeti la mtanzania kuhusu chadema

Kuwa mvumilivu, ndio siasa. unataka kila mtu afikiri sawa na wewe?
hata mimi nadhani kuna ukweli kiasi ktk hayo, chadema wasingelazimisha kuandamana kungetokea mauaji?
Kama wewe ni mweupe kichwani si lazima uchangie hapa,chadema hawakulazimisha kuandamana,walitumia haki yao yakidemokrasia kufanya yale maandamano wakiwa na kibali cha kufanya hiyo demo kutoka kwa rpc wa
arusha na baadaye bila maandishi igp anaongea uhuni kwa xcuse ya inteligensia kusifanyike maandamano.fuatlia kwa makini sana utagundua cdm hawakurupuki wanapoamua kufanya jambo lolote.
 
Hivi hawa watu ndo kusema wana mwogopa kikwete?
Ni nani anae imba udini kila siku na sasa umeanza kuonekana?
eti chadema na udini wanao eneza,toka lini?
 
msiwalaumu waandishi, mlaumu Rostam anayewaambia nini waandike maana yeye ndo mmiliki wa gazeti. Mimi niko Arusha ukweli wote tunaujua hatuna haja ya kudanganywa na video wala magazeti ya ROSTAM AZIZ
 
Hilo gazeti si la huyo RA sasa mtategemea waandike kuwasifu CHADEMA thubutu.
 
CHADEMA wawe na mkakati maalumu wa kuwa na chombo cha habari (Radio na TV) itakayowawezesha kuwa fairly covered...
 
Mbona wadau wa hii blog wanaitetea chadema hata palipo uhalisia wao wanaugeuza kuwa ukweli kwa namna yao? kila kitu wanataka wote tufikirie kama wao kwa mtazamo wao, tuache hizo jamani. Kuna mwingine alisema waliokufa arusha damu yao imeandika katiba mpya sasa huyo unataka Mtanzania wareport nini? Nafikiri ni muhimu kufanya hii blog iwe ya kijamii kiukwelii na siyo ya chadema. Na kama ikiendelea hivyo nalazimika kurudia aliyosema Jenerali Ulimwengu kuwa tutaiondoa ccm madarakani wataingie wengine lakini hatutafika tunapoelekea.
 
ah sijui wana maana gani unajua nchi hii mtu yeyote yule anayesema ukweli huwa anaonekana mbaya watu wanatakiwa waupende ukweli wauache uongo.Hakuna mtu anayekipendelea chama fulani watu hatutaki kuona nchi inaliwa na watu wachache wengi wakinyanyasika.Hiyo ndio mbaya.Hapo hatukubali kabisa.Hata siku moja Mtanzania haliwezi kuandika vizuri Chadema kwani hilo si gazeti la .....nazani wadau mnalijua hilo.Tuache siasa za ushabiki ukweli ufanyiwe kazi nchi isonge mbele.
 
Hata hivyo tutasikia mengi mwaka huu kuhusu CHADEMA, senior officials wa chadema wanatakiwa wajue kwamba pale CCM kuna watu walioenda shule kusomea propaganda za kisiasa, mkakati walionao kwa sasa ni kutumia media ili chadema iwe discredited na watu kufikia mwaka 2015. Wakifanikiwa kwa hilo wataendelea kutawala.

Ni hivi juzi niliona gazeti linaitwa jambo leo likiwa na kichwa cha CHADEMA YATANGAZA VITA !. Leo hii ukienda ukawauliza ni vita gani waliyotangaza CHADEMA hawana majibu, huu ni upuuzi, wanadhani watanzania wanaweza kutishwa kwa vichwa vya magazeti. Kwa hiyo viongozi wa CHADEMA wanatakiwa kufanya smart move, wanatakiwa wajue ni wapi pa ku strike na ni wapi pa kufanya pre-emptive move.

Kwa kadri dunia inavyobadilika kama ni propaganda nawashauri CCM wabadili mbinu, hizi wanazotumia they will backfire, they did not work during election and they will not work after election .CCM can no longer resist the wind of change.
 
rostam1_thumb_thumb.jpg




Fisadi Rostam Azizi


Hili gazeti la Mtanzania pamoja na Rai,The African,Dimba,Bingwa linamilikiwa na RA.

RA anahasira na CHADEMA. Kwa hiyo lazima aandike habari za uongo na uzushi kujaribu kuwashawishi Watanzania kuwa CHADEMA ni chama chenye vurugu. RA na CCM wanajidanganya. Watanzania wa sasa si watu wa KUDANGANYIKA KWA PROPAGANDA ZA KINA Rostam.

Picha za Video zilizorushwa na ITV/TBC kuhusu mauaji ya Arusha ni USANII MTUPU.



Ni kipofu tu anaweza kuamini uongo ulioonyehwa pale. Kama kweli walitaka kuonyesha uhalisia matukio,MBONA HAWAJATUONYESHA PICHA ZIFUATAZO:
  1. Polisi wakiwapiga risasi hao MAREHEMU 3 wakti wakivamia hicho kituo cha Polisi chenye silaha kama walivodai?
  2. Wafuasi wa CHADEMA wakivunja vioo vya magari kazi ambayo ilifanywa na Polisi wenyewe.
  3. Polisi wakimpiga mke wa Dr. Slaa.
  4. Polisi wakiwakamata Viongozi wa CHADEMA walipokuwa wakitaka kuongea na waandishi wa habari hotelini.
Polisi,TBC,ITV,Mtanzania wanataka kutumia propaganda za kiintelinjisia kuwahadaa Watanzania.

TAMKO LA SERIKALI KUTOKA KWA WM PINDA LIKO WAPI?

Last week Membe alipoongea na vyombo vya Habari baada ya kubanwa na Mabalozi kuhusu mauaji ya Polisi kule Arusha alijikanyaga na kuahidi kuwa wiki hii(Last week) serikali kupitia Waziri Mkuu ingelitoa tamko rasmi kuhusu mauji hayo ya Arusha. MPAKA SASA BADO KIMYA. Tunachoshuhudia ni UCHAKACHUAJI WA PICHA ZENYE UKWELI KUHUSU HAYO MAUJI.
NI DHAHIRI KUWA CCM NA SERIKALI YAKE WANATAPATAPA MAANA CHADEMA IMEWASHIKA PABAYA.
 
CHADEMA ni chama cha siasa. Bado wapo wanaoamini kwamba ni lazima mtu ashawishiwe ili kujiunga kuwa mwanachama. Hiyo ni historia. Hakuna mtu anayeshawishiwa kuwa mkatoliki, mlutheri au muislamu. Makanisa mapya ndio yanatafuta wafuasi! Chadema inajijenga kuwa kama imani. Ni mtu kukiamini na kukipenda chama chake! Imani ikijengeka propaganda hazisaidii kubadili mtu!
 
MH,NADHANI UYO MUANDISHI ATAPATA FEDHA ZA DOWANS ILA AJUE KAMA WAMEMUAIDI BAC KAFULIIA WATANZANIA CYO WAJINGA KIASI HICHO KWANZA CZANI KAMA KOZI YA UANDISHI KAMALIZA ,HIVI KAMA UNA HABARI PIGA KIMYA KWANI LAZIMA UTUBOE WABONGO KILA CKU PUMBAVUUUUUUUUUUUUUUU WE NA :behindsofa:UNA BAHATI CKUFAHAMUUUU NG'OMBE WEEEEEEEEEEEEEE
 
usitishike na hilo gazeti.ccm inatafuta kila mbinu kuiharibu chadema lakini hawawezi.Muda wao umefika mwisho.Wamisha firisika kisiasa.
 
Kipindi nilikiona kilitayarishwa na Idara ya Habari Maelezo. Mimi ndiyo mara yangu ya kwanza kuona Maelezo wameandaa kipindi wakati never on earth wamewahi kudeploy camera zaidi ya still!.

hivyo sishangazwi na hoyo habari ya Mtanzania pale newsroom yao wanavichwa moto chini ambao kwenye tasnia ya habari niwapiganaji wenye vyeo vya makamanda, kama makamanda wamtumikia fisadi mkuu unategemea nini?!.

Viongozi wa Chadema kama wana akili ya ukweli, wasireact wala wasijibishane kabisa na Mtanzania. Wao waendelee na agenda zao wanaowaelewa. wanawaelewa?

Halafu uchakachuaji hauwezi kuwa sahihi. Wameandikia imetayarishwa na Wizara ya Habari. Sidhani kama tuna hiyo Wizara bali tuna Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
 
Ili dhahabu iwe safi lazima ipi tie kwenye moto kwanza
Ili CDM kiwe imara lazima wakubali changamoto tena hizi cha mtoto, na ukisikia utamu wa siasa ndo hapa na na safari ya kuelekea kwenye nchi ya asali na mazima ndo kwanza imeanza na katika safari hii tutashudia mengi usishangae kuona wale dhaifu wakakihama chama.. tafakari.
 
Ni gazeti la Mtanzania. Taratibu limegeuka gazeti la udaku. Walioshiriki maandamano ya Arusha wanaujua ukweli hawahitaji kuonyeshwa picha. Walio na uelewa na ambao hawakushiriki wanaujua ukweli hawatabadilishwa kwa propaganda! Suala la Arusha kwa CDM ni msiba na hakuna haja ya kulumbana na magazeti. La msingi ni kuendelea kuwatetea watanzania! CCM wanajizika wenyewe!

Ahsante kwa kuendelea kuwapa Watanzania moyo wa kuamini chama chetu.
 
Habari nilizopata kutoka kwa rafiki yangu mwandishi aliyeko huko New Habari ni kwamba waandishi wengi, wahariri na wafanyakazi wa kampuni hiyo leo hii wamesikitishwa na stoiri hiyo ambayo anasema ilishinikizwa kutoka juu kwa mmiliki.

Wanasema kwamba hivi karibuni gazeti la Mtanzania lilianza kukubalika sokoni, lakini hiki kitu cha sasa kinaonyesha litarudi kule kule kwenye mauzo duni na wafanyakazi kukosa mishahara kwa miezi kadha.

Baadhi yao hata wamediriki kusema kqwamba moto wa Chadema hauwezi kuzimwa tu na gazeti moja lililopoteza muelekeo.
 
Gazeti hili huwa tunaliamini kwa ukweli lakni leo nashangaa habari zilizoandikwa ndani. Mtu mzima hatishiwi nyau. Tunaomba Watanzania kuwa wavumilivu kisiasa kwa sababu haya ni maneno ya kisiasa ila ukweli utabaki pale pale na bado tutaendelea kutetea ukweli na ukombozi wa Nchi yetu.
 
Mkuu bado unanunua na kusoma magazeti ya kifisadi!

Gazeti lenyewe la Rostam Aziz wa CCM ,fisadi no. 1 Tz. Unategemea liandike nini? Wala halinunuliwi f.y.i . Hakuna njia yo yote ya kuspin .Mapambano ni mbele kwa mbele
 
Back
Top Bottom