Napongeza Maoni Gazeti la Mtanzania kuhusu Habari ya Tukivitaka vyama vingi tuheshimu utamaduni wake

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,775
3,100
Katika gazeti la Mtanzania toleo la jana jumatano October 26 2016, Sehemu ya maoni ya mhariri ilikuwa na kichwa kikisomeka "TUKIVITAKA VYAMA VINGI TUHESHIMU UTAMADUNI WAKE". nimeguswa na maoni ya mhariri kwa sababu nyingi sana, mhariri mambo mengi aliyotaja anglau kwa ufupi ni kuwanyima vyama shindani sehemu za kufanyia mikutano mwaka jana wakati wa uchaguzi e.g uwanja wa taifa na Jangwani, ukiukaji wa makusudi wa CCM kama kupitisha muda wa kufanya mikutano, kuwawekea restrictions ya kutembea mahali fulani wagombea wa vyama shindani wakati wa uchaguzi, figisu za uchaguzi wa mameya wa kinondoni na Ubungo, n.k. mhariri anamaliza kwa kushauri kwamba kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi si kuwapo kwa vyama tu bali pia kuheshimu misingi yake, haki na utamaduni wake wa kushindanisha hoja bila kupigana.

Mimi binafsi nilitamani mhariri aendelee kudadavua zaidi lakini kwa kuwa safu yake ni fupi aliishia hapo. Mimi nitaongezea alipoishia, Ni takribani miaka ishirini toka tuingie katika mfumo wa vyama vingi lakini watu na taasisi bado zinaonyesha "ushamba" wa kisiasa wa hali ya juu, ushamba huu unaweza kuwa wa kujitakia "willful ignorance" au wa mifumo mibovu tiliyojiwekea. nikitoa mifano ya yanayotokea sasa hivi taratibu na sheria tulizojiwekea zimekuwa hazifuatwi, madiwani kila siku wanawekwa ndani na wakuu wa wilaya na mikoa kumpendezesha "mkulu" maana ndo imekuwa ngazi ya kupanda vyeo, polisi wamekuwa wakitumika ndivyo sivyo. Miradi mbalimbali ya maendeleo haipelekwi katika sehemu amabazo UKAWA walishinda ili kuwakomoa. Kwa mfano mkoa wa Arusha mkuu wa mkoa amesimamisha shughuli zote za maendeleo na ndiye anafanya kazi kama mkurugenzi. Mkurugenzi aliyepo amebaki kujipendekeza na kuonekana kama bulldog, ukiukaji huu wa taratibu si tu unaonyesha ignorance ya mfumo wa vyama vingi bali pia unakiuka haki stahiki za watu ambao wanalipa kodi bila kujali itikadi. Kwa maana nyingine tunaendesha nchi kwa ubaguzi wa maeneo kisa hawaamini kile ambacho wewe unaamini, utamaduni huu ni utamaduni wa kigaidi, magaidi ndo wanataka lazima uamini wanachoamini wao ndo utaweza kuishi. Kma hivyo ndivyo watu wataupinga kwa nguvu zote ugaidi huu.

Ningeweza kuendelea zaidi lakini sitaki kuwachosha wasomaji labda na mimi nitoe maoni yangu kwamba tunahitaji kuanza upya mfumo wa vyama vingi, watu na taasisi nyingi zinahitaji kufanyaiwa capacity building. Kwa bahati mbaya wakati tunaanzisha vyama vingi taasisi nyingi hazikufanyiwa capacity building as a result hawajui namna ya kufanya kazi under multi party democracy. Kwa mfano jeshi la polisi linahitaji kufundishwa upya kwamba chini ya mfumo wa vyama vingi wanatakiwa kufanya kazi namna gani, wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa wa-behave nanma gani n.k

Nawasilisha wakuu
 
Nami naweka mada ndani ya mada, kuna vitu vinanisumbua kichwani.
Hivi kati ya mchaguliwa na mteuliwa nani ni mheshimiwa kwa mujibu wa azimio la bunge sijui mwaka gani sikumbuki.

Pili kwenye harakati za kampeini zinazoendelea Marekani, mbona Clinton anayetoka chama tawala kwa sasa sijamuona akitumia polisi au jeshi kumdhibiti Trump hata pale wanapotukanana adharani?!
 
Ndugu yangu ndo maana nasema tuliingia katika mfumo wa vyama vingi bila kufanyiwa capacity building matokeo yake watu wenye mtazamo tofauti wanaonekana waahini, huu ndo maana nikauita ushamba wa kisiasa, cha kushangaza zaidi hata vijana wa juzi kama Gambo na wenyewe wameingia katika mtego wa ujinga wakanasa.
 
Au ni kwa vile wanasemaga waliokubali mfumo wa vyama vingi ni 20%?!
Kwamba wengi wana negativity nao hasira yake wanaielekeza kunyanyasa wapinzani sio?
 
Kiukweli hata mimi nakuunga mkono kwa mada safi na murua,si vyema na haki kuwashambulia wapinzani,utaratibu huu wa kudharau wapinzani unaanzia juu kushuka chini tena kwa sasa hivi ndiyo umezidi,yaani watu tunaogopa hata kusema ukweli kisa Chama tawala,chonde chonde ndugu zangu punguzeni munkari maana ni kweli hata huyo mpinzani unayemnyanyasa ndiye anakulipa kodi na kukuweka hapo ulipo.Sasa basi niwaombe wawakirishi wetu ambao tutashiriki kutunga katiba tusisahau kuingiza haya mambo uliyoyasema yawemo kwenye katiba ili kuondoa huu mkanganyiko kwa wapinzani.
 
Wapinzani wangekuwa na Tabia ya kuheshimu na kutodharau watawala nao wasingalidharauliwa. Wasilalame kwa tabia waliyoijenga wenyewe kuwaaminisha wapenzi na wanachama wao wanaweza kudharau na kutukana watawala wa wasifanywe chochote sababu ni demokrasia. Tuliwahi kusema ujenzi wa tabia za ukorofi wanazojengewa wafuasi wa Chadema ikitokea wakachukuwa nchi watapata shida sana sababu ni mbegu iliyopandwa na ikikomaa wao pia hawataweza kuikabiri, kwa sababu mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
 
Wapumbavu sana hawa watu, wanawanyanyasa na kuwanyima uhuru wapinzani lakini kodi zao hawakatai kuzipokea na kuzila.
 
Wapinzani wawe na tabia ya kusema ukweli kwani kwa sasa wengi wao wanadanganya. Kwa mfano wapinzani walituaminisha kuwa Lowasa ni fisadi papa, hadi tovuti yao waliliweka hilo. Haohao wakampa bendera ya kugombea urais na kusema ufisadi si mtu ila mfumo. Hapo jee ukweli uko wapi? Vilevile Mbowe alidai kuwa yeye li mlipa kodi mzuri na kuwa NHC wanamuonea, kumbe Mahakama kuu imethibitisha kuwa NHC iko sawa. Sasa hapo upinzani utaheshimikaje? Hapohapo wapinzani wanamnanga sana rais wa nchi eti ni dictator, hivi mi najiuliza, kwa chokochoko hizi rais akija kuwa dictator kweli, tutamlaumu nani? Kwa mawazo yangu wapinzani na hasa Chagadema wanatupeleka kubaya.
 
Ukiangalia chaguzi zetu; bunge letu; utungaji katiba mpya ulivyokuwa;na uhusiano wa serikali na vyama vya siasa ; kweli hii ecosystem haijakaa vizuri....tunajilazimisha tu kuwa na multiparty system lakini mioyo inatamani mfumo huu husingekuwepo kabisa.....ni kama kuwa na uhuru wa bendera!
 
Chaguzi zetu ni kama maigiuzo. watu wanachukulia siasa kama ajira badala ya utumishi wa umma.
 
Wapinzani wangekuwa na Tabia ya kuheshimu na kutodharau watawala nao wasingalidharauliwa. Wasilalame kwa tabia waliyoijenga wenyewe kuwaaminisha wapenzi na wanachama wao wanaweza kudharau na kutukana watawala wa wasifanywe chochote sababu ni demokrasia. Tuliwahi kusema ujenzi wa tabia za ukorofi wanazojengewa wafuasi wa Chadema ikitokea wakachukuwa nchi watapata shida sana sababu ni mbegu iliyopandwa na ikikomaa wao pia hawataweza kuikabiri, kwa sababu mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Kama umesoma vizuri maoni ya mhariri hapo juu utaona anaongelea neno utamaduni, utamaduni wa vyama vingi unatoa uhuru wa kuongea yanayokukwaza, kwa kuwa utamaduni huo hamjauzoea unaona kama unatukanwa kumbe siyo! huo ndo utamaduni wa vyama vingi amabao manashindwa kiuendana nao matokeo yake mnatumia nguvu pasipo sababu. Hivi watu wakitaka kuandamana ukawapa ulinzi wakafanya maadamano yao wakaondoka unakosa nini? huo ndo utamaduni wa vyama vingi.
 
Huo utamaduni unaotoa Uhuru wa kuongea yanayokukwaza una mipaka na wajibu. Ndiyo maana umetungiwa Sheria za kuongoza Uhuru na wajibu huo. maana yake utamaduni wa vyama vingi unatakiwa uendane na utamaduni wa kufuata sheria na miongozo katika kutekeleza Uhuru wa kuongea yanayokukwaza.
 
Umesema vizuri ndugu hapo kwenye red, sheria na miongozo, sheria zetu na miongozo inaruhusu kufanya maandamano na mikutano, je haki hii inatekelezeka kwa sasa? jibu ni hapana kwa kuwa tunaendesha nchi kwa decree ya mtu mmoja! kwa hiyo utamaduni wa vyama bado hamjauelewa. Katika mfumo wa vyama vingi unatakiwa uwe na kifua kikubwa kuweza kusikiliza hata yale usiyoyataka - huo ndo utamaduni wa vyama vingi.
 
Hiyo sheria inayotoa ruhusa ya maandamano, kumbuka imewekewa kanuni za kufuata ili ufanye hayo maandamano usipoyafuata ni maandamano haramu. Na inamaanisha umeenda kinyume na sheria!!!!!!!
 
Pili kwenye harakati za kampeini zinazoendelea Marekani, mbona Clinton anayetoka chama tawala kwa sasa sijamuona akitumia polisi au jeshi kumdhibiti Trump hata pale wanapotukanana adharani?!

Kiongozi usilinganishe yanayotokea US na yale ya Tanzania...
Kumbuka kuwa hatuna hata robo ya uzoefu walio nao..
Tungependa yanayotendeka kwao yatokee na kwetu lakini sisi bado sana...

Cha ajabu hata huku kwenye taasisi za elimu wengi wanatoka kapa bila uwezo wa kutetea haki zao za msingi..
 
Back
Top Bottom