Habari za kutisha gazeti la mtanzania kuhusu chadema

Tatizo ni kwamba 61% ya watanzania hawakupiga kura kwa chaguo la maaskofu, dr.slaa sasa maaskofu hawakubali hilo na wanalazimisha wanachotaka ndio sababu ya tatizo la vurugu arusha
 
Walipoandamana katika mazishi ya wale marehemu kulitokea mauaji?????????!!!!!!!!

Nilijua uko smart kama picha yako. kwani walienda polisi? w=mazishi hayakua na mawe ila siku ile ya mauaji vijana walikua na mawe na walienda polisi makusudi. Nyie mlitaka polisi wawape maandazi mlipoenda na mawe polisi au hukuona kwenye mkanda wenu ambao haukuchakachuliwa najua TBC haukuangalia.

Shida ya chadema ni mbili
1. KIBRI
2. KUJUA SANA hawawezi kukosolewa wakiambiwa jambo mmefanya wanasema mmechakuchua au waongo. nyie malaika?
 
Forget about Mtanzania, kwanza mmiliki wake ni kadi wa CCM, pili, it is not a serious paper so na credibility yake ni ndogo, na mwisho halina mauzo makubwa sokoni, so very few people watasoma upuuzi (propaganda) za kitoto kama hizo,Watanzania wengi wanafuatilia kuhusu jambo hilo na they know the truth.Chadema is on the side of the people.
 
Mtanzania kwani ni gazeti la nani?
Je mnategemea aandike kipi chema kilicho fanywa na chadema?
 
Hakuna "Fake Report" au Utumiaji wa Vyombo vya Habari Hasa Mengi Production Kutawadanganya Wananchi Tanzania. Poleni CCM...Kama Amani Inachafuliwa kwa Hii Njia "Tutaona Nani Atashinda" Wananchi au Mafisadi. Mengi Sio Fisadi? Chadema Wakiingia Madarakani, Mengi Atakwenda Jela Nae...Hizi Resources Zote za Mengi Amepata Wapi Huu Utajiri? Wananchi Tangu Siku Nyingi Tunajua There is No Way Mengi is That Honest...
Niweze, kweli hili la kipindi maalum, naomba nimtetee Mengi na ITV yake, kile kipindi kimetayarishwa na Idara ya Habari Maelezo na sio ITV wala Mengi had nothing to do with it zaidi ya kulipwa kurushwa.

I wish kama Chadema, nao waandae cha kwao, warushe their version of the story. Polisi wanadai walitumia risasi za moto walipoona wanazidiwa kituo cha polisi kikitaka kuvamiwa. Waliokuwepo wamethibitisha risasi zilirindima mitaani na sio polisi. Wenye ithibitisho kuwa waliouwawa hawakutaka kuvamia kituo cha polisi, Kamanda Mwema na Andagenya wanafikishika kwa Acompo!.
 
Kipindi nilikiona kilitayarishwa na Idara ya Habari Maelezo. Mimi ndiyo mara yangu ya kwanza kuona Maelezo wameandaa kipindi wakati never on earth wamewahi kudeploy camera zaidi ya still!.

hivyo sishangazwi na hoyo habari ya Mtanzania pale newsroom yao wanavichwa moto chini ambao kwenye tasnia ya habari niwapiganaji wenye vyeo vya makamanda, kama makamanda wamtumikia fisadi mkuu unategemea nini?!.

Viongozi wa Chadema kama wana akili ya ukweli, wasireact wala wasijibishane kabisa na Mtanzania. Wao waendelee na agenda zao wanaowaelewa. wanawaelewa?

Hivi jamaa yangu unategemea nini kutoka gazeti la Boss fisadi(TUMIKIA KAFIRI UPATE MRADI). Hayo si mawazo ya hao waandishi maarufu, lakini wapo jela ya ajira hawapo huru tusiwalaumu.Jamaa wanatapatapa wamenasa. Ushauri wangu CHADEMA wasijibu hizo cheap allegations, watu wenye busara wanaelewa kinacho endelea. Jamaa wamebanwa kwanye kona wanajaribu kujinasua, wangojee hukumu ya jamii( uma wa watanzania). Aluta Continua CHADEMA.
 
wametumwa na hawataweza kutimiza malengo waliyotumwa kutimiza kwani ni makubwa na wameshachelewa sana

Chombo kinachomilikiwa na RA unategemea kiandike nini juu ya CDM. Huhitaji hata kufikiria na ninakushauri usiangalie hat hrading tu maana kwa ustahimilivu nmdogo ulionao unaweza kufa na pressure.
 
Wadau nimekufa ganzi asubuhi hii baada ya kuona gazeti la mtanzania la leo,limeandika habari za matusi makubwa dhidi ya Chadema.Limeandika kwamba Chadema wamevurugana kwa sababu ya udini waliouanzisha,pili wamesema vurugu za Arusha wamewahadaa wananchi kwa sababu ya udini wao na tatu wanasema mauaji ya Arusha yamesababishwa na Chadema.Ni habari mbaya kwa mtu yeyote akisoma.Habari hii kwa jinsi ilivyoandikwa nikihusisha na kipindi maalum kilichorushwa na ITV juzi inaonekana kuna mkakati maalum umesukwa wa kuichafua na kuiangamiza Chadema.Yeyote anayeweza kulipata hilo gazeti alisome aone hayo matusi.....kwa uandishi huu sijui kama tutafika.

aiseeee hata mimi nilichokuwa nakisikiliza TBC jana usiku kilikuwa kinatisha sana..JK na MM wameamua huiua hii nchi sasa jamani.. these guys has to be stopped
 
Hivi hawa watu ndo kusema wana mwogopa kikwete?
Ni nani anae imba udini kila siku na sasa umeanza kuonekana?
eti chadema na udini wanao eneza,toka lini?

Hapa hakuna mjadala tena. Kama wameanzisha Udini CCM basi na uwe. Tumechoka. Mtanzania wanaleta na kuendeleza ujinga. Nadhani na wele wanao NUNUA magazeti yao ama ni wapuuzi au ni wale wanaojipa matumaini ya kuendeleza shamba la wanyama.
 
Mbona wadau wa hii blog wanaitetea chadema hata palipo uhalisia wao wanaugeuza kuwa ukweli kwa namna yao? kila kitu wanataka wote tufikirie kama wao kwa mtazamo wao, tuache hizo jamani. Kuna mwingine alisema waliokufa arusha damu yao imeandika katiba mpya sasa huyo unataka Mtanzania wareport nini? Nafikiri ni muhimu kufanya hii blog iwe ya kijamii kiukwelii na siyo ya chadema. Na kama ikiendelea hivyo nalazimika kurudia aliyosema Jenerali Ulimwengu kuwa tutaiondoa ccm madarakani wataingie wengine lakini hatutafika tunapoelekea.

We huna jipya. Ni walewale mafisadi au mafisadi mategemeo au wale wanaojikomba. Damu ilishamwagika na ulitaka Marando asemeje? Kama una akili ya kufikiria basi jiunge na wale misukule wasiojua lolote linaloendelea nchini ufe nao. Punguza jamani, jamani... ktk hoja zako. Hapa hakuna wa kudanganyika
 
Kilichoandikwa hakunajipya kwani bado ukweli unabaki palepale polisi wasingeingilia maandamano kusingekuwa na vurugu yoyote ingetokea, ndiyo maana hakukuwa na vurugu siku ya kuwaaga waliyokufa hasa ukisingizingatia kwamba siku hiyo watu ndiyo walikuwa na hasira baada ya kupigwa na kujeruhiwa hata wengine kuuwawa na hakukuwa na polisi yeyote, kwanini wasitumie fursa hiyo kufanya vurugu taarifa zinaonyesha baada ya kuagwa marehemu pale viwanja vya NMC watu walijirudia nyumbani wengine kwa makundi makundi kwanini wasifanye vurugu? So lazima utafakari hili, inaonekana polisi walipewa maagizo ya kuhakisha wanazua maandamano ya chadema kama walivyofanikiwa ndiyo maana wawakuwa na haja ya kutoa ulinzi wakati wa kuaga waliyokufa, mapambano daima msiogope TAFAKARI.
 
Mauaji ya Raia tena wasio hatia,wasiokua na silaha, Bado Chagonja (Mkuu wa operesheni wa Polisi) anasimama kwenye chombo cha propaganda TBC1... anawaita wachochezi, wakosefu wa amani,na mafedhuli wa kutokutii Mamlaka! Kweli tunakoelekea sijui!
 
Tatizo ni kwamba 61% ya watanzania hawakupiga kura kwa chaguo la maaskofu, dr.slaa sasa maaskofu hawakubali hilo na wanalazimisha wanachotaka ndio sababu ya tatizo la vurugu arusha

Umeandika pumba. nadhani una mambo matatu unayotaka nasi tuwe waumini wako. 1. labda wewe si mkristo 2. Una mapungufu ya akili 3. Umetumwa pasipo sahihi kubadilisha watu .....
 
Gazeti hili huwa tunaliamini kwa ukweli lakni leo nashangaa habari zilizoandikwa ndani. Mtu mzima hatishiwi nyau. Tunaomba Watanzania kuwa wavumilivu kisiasa kwa sababu haya ni maneno ya kisiasa ila ukweli utabaki pale pale na bado tutaendelea kutetea ukweli na ukombozi wa Nchi yetu.

check kwny red hapo juu!!unaliamini mtanzania au??kama unaliamini mtz basi unamwamini RA,anyway una utashi wa kuamini chochote unachotaka kuamini..nakushauri usiliamini gazeti la mtz...
 
Back
Top Bottom