Mnyisunura
Member
- Aug 3, 2008
- 69
- 7
Ndugu Mnyisunura hayo uliyoyaeleza ni ya maana sana na yameniweka katika ufahamu mzuri ,lakini zaidi ya yote hayo wananchi wanakuwa na kuona kila siku miradi ikifanya kazi na mali kuchimbuliwa ,sasa ukiwachukulia wananchi wanaoishi kandokando ya migodi hiyo utawakuta ni masikini ombaomba ,hawana maji safi wala watoto wao hawana shule za kisasa ,haya ndio mambo yaliopelekea mapigano kule Nigeria na mpaka leo hufumka vita katika machimbo ya mafuta ,sababu ni hizi za serikali kujifanya ndie pekee anaefaidi malipo na kutowajali wakazi waeneo,katika sehemu yako ya mwisho ni muelekezo mzuri kabisa kuwa hawa wanaopewa leseni na kuruhusiwa kubukua hazina ya eneo fulani walazimishwe kuweka shule zaidi ya moja ,kuwapatia wakazi maji safi kuwajengea barabara japo oneway na guzo la taa kila baada ya mita mia tano badala ya ahadi hizi kuchukuliwa na chama tawala ambao wakipata feza wanaitafuna,nafikiri WaTanzania wakihahakikishiwa kuwa mwekezaji kabla hajaekeza au pale akipata leseni tu kwanza afanye mambu hayo ili kuwafurahiusha wakazi pia nafasi za kazi kama za udereva ulinzi na kazi zingine za kushughulikia machimbo ,usafi na kazi ndogo ndogo ambazo hazihitaji elimu ya vyuo vikuu wapewe wakazi kwanza yaani wakazi wawe nambarione ,hapo tungelipiga hatua na mayowe yangepungua ,lakini leo Tanzania ni ya Tatu,SouthAfrica ya pili na Ghana ni ya kwanza(Japo umesema Ghana hakuna kitu) lakini chati inaonyesha ni ya mwanzo katika uchimbaji bado unaikuta mikoa ya Mwanza ,Musoma,Mara na Shinyanga hali zake ni duni kabisa kabisa kuanzia makazi,vipando,barabara na mashule kwa kweli wananchi hawataacha kupiga makelele na kusema wanaibiwa na wazungu wachache wakishirikiana na mafisadi Tanzania haihitaji uchunguzi tena kumeshafanywa uchunguzi na mali ipo ya kutosha hata Mheshimiwa Kikwete alisikika akisema hakuna madini unayoijua ambayo haipo Tz ,akijitapa sana kwenye hotuba yake kuwaita wawekezaji ,hivyo asingekuwa na nguvu za kuwaita wawekezaji kama uhakika wa uchunguzi bado haujatimia au haujulikani au utahitaji miaka kibao ,tayari muheshimiwa alikwishaona data tokea akifanya kazi ya Uwaziri.
Mkuu nimekuelewa unayoyasema! Lakini kwa ujumla labda niseme siyo kuwafurahisha wananchi! Iwe sheria kama sehem ya mgodi kufanya hivyo! Kuna kitu kinaitwa community involvement during mine design! Ni kwamba tunazungumza sheria iwabane kuwashirikisha wananchi na hao ndo wawe waamuzi wa rasilimali zao! Waseme tunataka tufanyiwe nini! Pili wapelekwe wataalam kuwaelimisha wananchi na kuwepo utekelezaji wa wakubaliano! Ni mambo ya ndani sana nashindwa hata namna ya kuyaeleza lakini kiufupi ni kuwa issue ya community involvement in mine design ndo inayoleta tija kwa wakazi! Siyo mwanasiasa awaamulie wananchi! Kwa kuangalia mambo yanayotokea Buzwagi kwa mfano inaonesha kabisa kuwa kuna mtu alifanya maamuzi kwa niaba ya wale watu!
Issue ya madini kuwepo mengi sometimes ni ya kisiasa! Unaweza ukawa na madini lakini hayachimbiki! Issue ni kuwa je haya ambayo tayari tunajua yapo na yanachimbwa yanatusaidia vipi? Wanasiasa wakienda migodini gari lake likitengenezwa na kupata kidogokidogo amechanganyikiwa! Nasikitika sana kwani tunaongozwa na mbumbu mno!