Habari Njema - Je Mnayajua haya?

Sasa hapa unazungumzia kumuuzia Osama. Sisi kama nchi hatuwezi ku-base projections zetu kwenye bei ya kumuuzia Osama kwenye black market! Badala ya kudai mgao, tukigundua kuwa kuna watu wanafanya hivyo inabidi tuwapeleke mbele ya sheria. Kama vile ambavyo tukimkuta mtu anauza viungo vya Albino. Vyote ni criminal activities.

Kwa kugida kidogo kidogo kwenye hizo sample zinazochukuliwa kila siku huwezi kujua anakwenda kuuziwa nani ,hicho ambacho nisafi. Ndio kusema mambo haya yataisha lini ? Project zipo matunda tayari yameshaonekana na watu weshapanga mahesabu ,yaani ukichunguza mambo ya migodi ya dhahabu utaona ni jinsi gani pasi zinavyokwenda na local businessman ambao ni wakubwa huwa wanaweka saini kiulaini,sasa kila miaka inapokwenda hakuna kinachofikia mwisho na kujulikana palipofikiwa na mwisho wa kuchukua sampuli utakuwa lini kwani kila anepasiwa hutaka kuondoka na sampuli ili akakaguwe zaidi au kwa nini baada ya uchunguzi wa mwanzo Serikali haiweki kumbukumbu na badala yake anaekuja aambiwe uchunguzi ni huu hapa ,hakuna haja ya kufanya uchunguzi mwengine au hizi chunguzi zinazofanywa baada ya kukamilika serikali huwa haipewi na hubakia mikononi mwa waliochungua na kuwa ni mali yao ,na kama ndio hivyo kwa nini haiwekwi sheria kwa kila anaechunguza uchunguzi utakuwa ni mali ya nchi na riporti yake kuwepo katika wizara husika ? Uranium ilianza kuchunguzwa na wajerumani katika miaka ya 70 na sehemu ni hizo hizo zinazochunguzwa leo.
Au hizi leseni zikishatolewa ndio serikali haitakiwi tena kuingilia au kuhoji kinachoendelea na wenye leseni huwa huru kuuza au kuikodisha sehemu wenye leseni nayo kwa mwengine bila ya shaka yeyote atalipwa dau kubwa kuliko gharama za leseni na serikali huwa inakodoa macho tu. wateja wanauziana rasilimali za nchi kama yao na hakuna wa kuwahoji sijui kama hawana viwanja vya ndege ndani ya maeneo yao ambayo wataruka kuelekea nchi jirani bila ya kupingwa.
 
Explaration inachukua muda mrefu sana. Ni wajibu wa serikali kupitia Wizara ya Madini na Nishati kutoa elimu kwa umma kuhusu hili.

Ni mambo ya kitalaamu ambayo yanahitaji ufafanuzi wa kina. Watu wakiona mwekezaji anasafirisha sample za mchanga kupeleka Australia au Canada kwenye maabara wanasema kwamba anaiba madini!

Wacha hizo hata lebo za chuo kikuu zinaweza kabisa kutowa analysis ya mchanga ,na wataalamu wa kweli hawahitaji kusafirisha mchanga wanakuwa well equiped na wanamalizia kusoma data ndani ya nchi ,haya ya kusafirisha ni mambo yaliopitwa na wakati na matapeli ndio wanaotumia mbinu hizi naona ipo haja ya kulazimisha makampuni kufanya uchunguzi wa data zao ndani ya nchi badala ya kutumia kisingizio cha kusafirisha mchanga,tupo kwenye ulimwengu wa teknolojia na chombo kidogo sana kinaweza kukupa data ambazo zitaweza kuwekwa kwenye mtandao na kufanyiwa uchunguzi , jamani hebu tuchokeni kudanganywa.
 
Mkuu hata nchi zilizoendelea sample huwa zinasafirishwa nje ya nchi especially za exploration au crime kubwa kubwa. Kwa exploration sababu kubwa ni kutengeneza credibility ya data hasa ukizingatia exploration companies mara nyingi hawachimbi madini. Hivyo hizo concession zao huwa wanaziuza na hapo kwenye kuuza ndipo unatakiwa unadi vzuri utafiti wako kwa kusema Lab X, Lab Y, Lab Z na hata Lab M zote zinaelezea matokeo yanayofanana.
 
Kwa kugida kidogo kidogo kwenye hizo sample zinazochukuliwa kila siku huwezi kujua anakwenda kuuziwa nani ,hicho ambacho nisafi. Ndio kusema mambo haya yataisha lini ? Project zipo matunda tayari yameshaonekana na watu weshapanga mahesabu ,yaani ukichunguza mambo ya migodi ya dhahabu utaona ni jinsi gani pasi zinavyokwenda na local businessman ambao ni wakubwa huwa wanaweka saini kiulaini,sasa kila miaka inapokwenda hakuna kinachofikia mwisho na kujulikana palipofikiwa na mwisho wa kuchukua sampuli utakuwa lini kwani kila anepasiwa hutaka kuondoka na sampuli ili akakaguwe zaidi au kwa nini baada ya uchunguzi wa mwanzo Serikali haiweki kumbukumbu na badala yake anaekuja aambiwe uchunguzi ni huu hapa ,hakuna haja ya kufanya uchunguzi mwengine au hizi chunguzi zinazofanywa baada ya kukamilika serikali huwa haipewi na hubakia mikononi mwa waliochungua na kuwa ni mali yao ,na kama ndio hivyo kwa nini haiwekwi sheria kwa kila anaechunguza uchunguzi utakuwa ni mali ya nchi na riporti yake kuwepo katika wizara husika ? Uranium ilianza kuchunguzwa na wajerumani katika miaka ya 70 na sehemu ni hizo hizo zinazochunguzwa leo.
Au hizi leseni zikishatolewa ndio serikali haitakiwi tena kuingilia au kuhoji kinachoendelea na wenye leseni huwa huru kuuza au kuikodisha sehemu wenye leseni nayo kwa mwengine bila ya shaka yeyote atalipwa dau kubwa kuliko gharama za leseni na serikali huwa inakodoa macho tu. wateja wanauziana rasilimali za nchi kama yao na hakuna wa kuwahoji sijui kama hawana viwanja vya ndege ndani ya maeneo yao ambayo wataruka kuelekea nchi jirani bila ya kupingwa.

Tatizo lingine tulilo nalo ni hilo la kuchanganya mali ya nchi na mali ya mwananchi. Mwananchi akishapewa sehemu, ana haki ya kuifanyia chochote bila kuingiliwa ili mradi havunji sheria. Akiweza kuiuza, kuikodisha kwa mtu mwingine kwa dau kubwa sehemu ya serikali ni kukodoa macho na kuhakikisha kuwa mwananchi wake analipia kodi hayo mapato yake. Kwa mtazamo wako basi serikali itabidi imfidie mwananchi wake kama akiuza, kukodisha sehemu yake kwa hasara! Tusiendekeze wivu, hautatufikisha mbali. Hauwezi kulinganisha mgodi wa dhahabu na mradi wa uranium. Hautapata jawabu.

Wanaojua zaidi yangu wameishakufahamisha kuwa kazi ya uchunguzi si lele mama. Kama tumeukubali ubepari basi hizi ndizo gharama zake. La sivyo, turudi kule kule ambako serikali ihodhi kila kitu hadi hapo itakapokuwa yenyewe ina uwezo wa kukiendeleza!
 
Wacha hizo hata lebo za chuo kikuu zinaweza kabisa kutowa analysis ya mchanga ,na wataalamu wa kweli hawahitaji kusafirisha mchanga wanakuwa well equiped na wanamalizia kusoma data ndani ya nchi ,haya ya kusafirisha ni mambo yaliopitwa na wakati na matapeli ndio wanaotumia mbinu hizi naona ipo haja ya kulazimisha makampuni kufanya uchunguzi wa data zao ndani ya nchi badala ya kutumia kisingizio cha kusafirisha mchanga,tupo kwenye ulimwengu wa teknolojia na chombo kidogo sana kinaweza kukupa data ambazo zitaweza kuwekwa kwenye mtandao na kufanyiwa uchunguzi , jamani hebu tuchokeni kudanganywa.

Masaki has a point. Sometimes let us be sober in discussing these issues. Lab za Chuo haziwezi kueleza kiwango cha madini kilichopo na kama kitadumu kwa muda gani iwapo uchimbazi ukianza na uchimbaji utakuwa kiwango gani kwa mwaka. Tanzani hatujawa bado na labs hizo. Sio nchi zote duniani zina labs hizo na sio teknolojia rahisi.
Tatizo lililopo kwetu ni kuwa watafutaji hawa hawasimamiwi vya kutosha na hivyo baadhi ya maeneo ya nchi madini kama dhahabu yapo juu sana na hivyo 'sample' zinazochukuliwa huwa zina dhahabu. Ukosefu wa usimamizi hupelekea watafutaji wa madini, baadhi yao, kujichukulia madini mengi sana kabla ya kuanza uchimbaji rasmi.

Moja ya suluhisho la suala hili ni kuhamasisha watanzania wengi wengi uwezo kifedha kuwekeza katika makampuni ya utafutaji ili kuweza kuju kiasi cha udongo unaochukuliwa na kiasi gani kina madini fulani - kama ni chuma, dhahabu, shaba, fedha, nikeli, platinum etc. Hivi sasa kampuni za kitanzania zilizopo katika utafutaji (contractors) ni chache mno na hivyo kukuta kazi hizi kufanywa na kampuni za kigeni. Hivyo hatupati fursa ya kujua data hizi.

Kamati ya Rais ya Madini (Kamati ya Bomani) imependekeza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Madini ambayo itakuwa pamoja na mambo mengine na jukumu la kusimamia shughuli hizi ili kudhibiti wizi wa mchanga wenye madini.

Kazi ya utafutaji (explorations) ni kazi yenye kuchukua muda mrefu sana. Watafutaji hutakiwa kutoa ripoti za utafiti wao kila mwaka. Ndio maana nikasema miradi ambayo Mwiba ameilist hapo juu tutaifuatilia kwa swali bungeni ili kujua imefikia wapi. Hii ni public info na ni rahisi kupatikana.

Naelewa wasiwasi tulionao watanzania kutokana na kuibiwa au kudanganywa katika sekta ya madini. Lakini ili tuweze kutatua matatizo ya sekta hii ni lazima tuwe na habari sahihi. Vinginevyo wataendelea kutuibia tu nasi kubaki twalalamika. Mwiba asante kwa taarifa yako.
 
Wacha hizo hata lebo za chuo kikuu zinaweza kabisa kutowa analysis ya mchanga ,na wataalamu wa kweli hawahitaji kusafirisha mchanga wanakuwa well equiped na wanamalizia kusoma data ndani ya nchi ,haya ya kusafirisha ni mambo yaliopitwa na wakati na matapeli ndio wanaotumia mbinu hizi naona ipo haja ya kulazimisha makampuni kufanya uchunguzi wa data zao ndani ya nchi badala ya kutumia kisingizio cha kusafirisha mchanga,tupo kwenye ulimwengu wa teknolojia na chombo kidogo sana kinaweza kukupa data ambazo zitaweza kuwekwa kwenye mtandao na kufanyiwa uchunguzi , jamani hebu tuchokeni kudanganywa.

Lebo ya Chuo Kikuu kipi? Vyuo vingapi vina lebo ambazo zinatambulika kimataifa? Usichanganye initial analysis inayoweza kufanyika site na detailed analysis ambayo mwekezaji anahitaji kabla ya kufanya uamuzi wa ku-invest!
 
... Hivi sasa kampuni za kitanzania zilizopo katika utafutaji (contractors) ni chache mno na hivyo kukuta kazi hizi kufanywa na kampuni za kigeni. Hivyo hatupati fursa ya kujua data hizi.

Taratibu Mheshimiwa, ngoja kwanza.

Kuna tofauti gani kati ya kampuni ya kigeni na kampuni binafsi ya Kitanzania inapokuja kwenye urahisi au utayari wao wa ku-share information na serikali?

Hakuna taratibu vitabuni zinazoshurutisha kampuni hizi kufungua madaftari yao, ya kigeni au ya kienyeji ?

Kamati ya Rais ya Madini (Kamati ya Bomani) imependekeza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Madini ambayo itakuwa pamoja na mambo mengine na jukumu la kusimamia shughuli hizi ili kudhibiti wizi wa mchanga wenye madini.

Mlipendekeza iundwe Mamlaka ya Madini ?

STAMICO ni nini, na inafanya nini, na kwa nini haiwezi kufanya hiyo kazi, na mkianzisha Mamlaka nyingine STAMICO itakuwa inafanya nini ?

And then hapo utamlaumu mwananchi kama Masatu alipoku lambast kwamba mlikuwa kwenye Tume ya ulaji tu ? Mamlaka ya Madini ?

...miradi ambayo Mwiba ameilist hapo juu tutaifuatilia kwa swali bungeni ili kujua imefikia wapi. Hii ni public info na ni rahisi kupatikana.

Public informat..? Say whaaat ? Samahani Zitto, you're supposed to be the last one to say such thing.

"Mradi wa Jeshi" wa meremeta ulipata details zake ? Si mwenzio Dr. Slaa alitishiwa kufungwa kwa kuongelea hizi "siri" in public ? Umesahau ?

Mradi wa Buhemba ulipata kujua nani anamiliki ? Mzee Mkono kakuomba data juzi hapa, kasema hadi Tume yako haikuweza kujua hizi info, umesahau ?

Mradi wa Kiwira si nyinyi mlisema kwenye ripoti yako kwamba mnahitaji Tume nyingine kutafuta ukweli? Umesahau ?

Most importantly, most significant of all, ukasema Tume yako haikuwa na subpoena power za parliamentary privileges and immunities kufukua hizo nyeti. Sasa toka lini public information ikahitaji subpoena power kuijua?

Public information kwenye sekta ya madini Tanzania ?
 
Tutafuatilia kujua maendeleo ya miradi hii. Kitu kimoja tu muhimu ni kwamba Leseni hotelewwa kabla ya mikataba. Leseni za kutafuta madini na baada ya madini kugundulika na vigezo kutumia ndipo mkataba hufuata. Kwa miradi yote hiyo bado ni utafutaji. Sasa kujua utafuutaji umefikia wapi ngoja tufuatilie, may be a parliamentary question!

Zitto hii sio mara yako kwanza kuahidi kufuatilia.

Wewe na kiongozi mwenzio Kikwete hamna tofauti katika kutoa ahadi then mnanyamaza kimya bila kutoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi zenu. Nakuweka katika kundi la viongozi wa serikali m-badala wa sisiemu kwa sababu unaonyesha juhudi kuliko wenzio.

In general, i think there will be no significant difference between the present government and the expected alternative government (itakayoongozwa vyama m-badala) in term of kutekeleza ahadi zinazotolewa na viongozi kwa wananchi (check link hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/13190-madini-yetu-kulikoni-jamani.html)
 
Naomba niwasaidie kwa hapa kuhusu hizi projects kama zipo na lini zimeanza na tutarajie nini!
Kwa upande wa Mining Labda kidogo watu ni wageni na namna uchimbaji unavyofanyika. Ukweli ni kuwa hizi project si za kuanza leo wala kesho kwa jinsi ninavyojua! Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kabla hujaanza kuchimba!
Ninavyojua mimi inaweza kuchukua mpaka miaka kumi kabla hujaanza kuchimba wakati wote huo unafanya utafiti (exploration) Hata hivyo hatutegemei baada ya hapo hizo project zoteziwe viable! Nyingi ya hizo tumeanza kusikia siku nyingi lakini hakuna mtu aliyewahi tupahela kufanya utafiti akajua kama kuna (coal, uranium au Gold nk) ipo ipo na kwa kiasi gani na kama inaweza kuchimbika! Kujiu kuwa kuna Uranium ni hatua moja lakini kuchimba ni hatua nyingine! Kwa wale ambao hawana taarifa project zote zinazoendelea sasa na uchimbaji zinazaidi ya miaka 60 ya ufaham wa uwepo wa madini! Maeneo yote ambayo kwa sasa wanachimba taarifa zilikuwepo hata kabla ya uhuru! Baada ya kuruhusiwa kuchimba iliwachukua zaidi ya miaka kumi huku wakiwa na hii ilisaidiwa na taarifa nyingi za utafiti ambazo serikali wakati huo chini ya STAMICO ilishakuwa imefanya!
Kwa jinsi ninavyojua Uranium mining siyo deal at all kama kuna mtu mmoja aliandika kwenye gazeti la Raia Mwema! Tatizo linakuja pale hayo madini yatakapoanza kuwa processed (kuchambua) kwani pale ndo unaipata uranuim radioactive element yenyewe. Hata hivyo je watatengeneza plant hapa! Kwa nchi kama kanada ambako kuna migodi mingi ya uraniuma wana underground plant plant na system nzuri za namna ya kuandaa! Labda sasa ni suala la kujua hawa jamaa wanataka ya nini hii uraium!. Kama wanataka itumike tanzania basi ni heri kwani uwezo wa uranium kutoa energy kwa tani (tani moja ya uranium inatoa sawa na tani 16 za coal)
Kitu kingine ambacho nadhani watu hawajui! Kwenye Mining kuna kitu kinaitwa cartels and monopolies kwa baadhi ya madini! Ni kuwa huwezi kuchimba hayo madini unless umempata mnunuzi wa hayo madini na huyo ndo atakayekupangia bei! Unless tukazanie industrial minerals ambazo tukichimba tutakuwa na uwezo wa kuzitumie wenyewe kama wanavyofanya cement campanies. Nchi kama vile china zimeendelea kwa kusaidiana na coal kama source of Energy lakini industrial mineral zimesaidia na ndo maana kila siku tunauziwa vyombo kutoka china! Tunazo nyingi industrial minerals ambazo hao wawekezaji hawawezi na hawataweza kuja kuwekeza ukiacha cement companies ambazo wanajua lazima watu watanunua cement!
Kwa upande metals na precious mineral nadhani kuna tatizo kubwa ambalo si tanzania tu inalo hata nchi nyingine! Kumbukeni Ghana iliitwa Gold Coast kwani pwani yote ilikuwa n ukanda wa dhahabu na wamechimba kwa zaidi ya miaka 100 lakini haijawasaidia sana Waghana na sasa hakuna tena dhahabu! Sauth Afrika wamechimba kwa zaidi ya miaka 300 mpaka hivi sasa lakini ni wazungu tu wamefaidika! Zimbabwe nao hivyo hivyo! Zambia serikali iliamua kuwa inachimba Copper na ilisaidia sana kuinua maendeleo ya nchiile na kwa kiasi kikubwa uchumi wake ulitegemea copper kwa zaidi ya miono mitatu lakini wakakumba na kigingi cha monopoly! Ikadrop ghafla na wakafunga migodi yote mpaka walipowaruhu ndo sasa wanachimba! Tanzaia tulijifanya hatutaki wawekezaji tukawa tunachimba almas ya mwadui tukakutana na kigingi hicho cha monopoly tukasurrender na kwa hakika hakuna serikali iliyofanikiwa kuendesha migodi! Zipo chache sana duniani nadhani chile!
Labda niseme hivi hatupende rasilimali zetu ziibiwe! Lakini je ni kwa kiasi gani tumejandaa kukabiliana na hawa watu ambao wamekuwa kwenye biashara ya madini zaidi ya miaka 200! Je tunao wataalam wa kutosha kuangalia namna hii bishara ambavyo imkuwa ikifanyika na ni kwa jinsi gani nchi ambazo zilifaidi na zinafaidi zinaweza kufaidi! Je hawa watu wana ufahamu wa kutosha kuhusu hii busness! Je wanaweza kuanticipate kwa kusoma report ya feasibility study! Je sheria zetu na regulation zetu zimecover risk zote ambazo ni mining related risks! Kwa mfano Autralia na Cana wana special act na regulation kwa ajili ya mining tu! Ok tuna mining act ambayo hata mimi ninayo! Kwa kuiangalia tu hamna kitu hapa inaoesha walioianda walikuwa na haraka sana kuianda hii act!
Kwa mfano sasa hivi watu wanalalamika na Royality (Mrahaba) kwamba serikali inapata asilimia tatu tu! Hii ni international kwa dhahabu ni asilimia tatu, coal asilimia 1.5, almasi inategemeana kama ni final unapata asilimia 3 kama siyo final ni 5 %. Tunategemea kodi iwe asilimia si zaidi ya 40 kama serikali haiana shear. Sisi wanasema ni 30% ya NPV (net present value) Na hiyo wanasema baada ya payback period yaani watakaporudisha gharama za mtaji! Lakini je wataalamu wetu wanauwezo wa kuinterptrate financial statement of mining industry ambao serikali inawatumia! Au ni hawa akina karamagi kusain mikataba uingereza!
Tatizo kwa mimi ninavyojua ni makampuni ya madini ila ni umbumbu wa viongozi wetu! For sure codi ni sehem ndogo sana ambayo kama taifa inaweza kupata kutokana na wao kuchimba hayo madini! Kama wangeambiwa kwa mfano kila wanapotengeneza mgodi wahakikishe lami imefika mji wa jirani au hata hapo! Maji yamefika! Kuna shule kama kulikuwa hakuna, Hosipitali, na umeme nadhani hii ingekuwa ni hazina ambyo tungebaki nayo hata baada ya wao kuondoka! Pili kama tukisema supplie kwenye mining lazima wawe wabongo tungepata faida sana! Lakini je tuna uwezo wa kusauply mining service! Vitu vyote ni vigeni kwetu!
Anyway tutafika kidogo kidogo kwa kuelimishana! Kwanza watu wajue halafu pili ndo twende mbele! Kumbuka siyo sekta ya madinii tu kwenye wanyama pori nako kumeoza na wasiwasi kuna wataalam wa kutosha tu wa wanyamapori lakini nashindwa kuelewa wanafanya nini! Kuna tatizo na hili tunahitaji kulimaliza!
 
Lebo ya Chuo Kikuu kipi? Vyuo vingapi vina lebo ambazo zinatambulika kimataifa? Usichanganye initial analysis inayoweza kufanyika site na detailed analysis ambayo mwekezaji anahitaji kabla ya kufanya uamuzi wa ku-invest!

Maabara za Tanzania ziko mbele ukilinganisha na hizo zinazotambulika au umesahau kama walichunguza vumbi kama ni la kichawi katika mtafaruku wa uchawi pale bungeni ni maabara gani iliyofikia hatua hiyo waTz wamefikia kutumia viungo vya albino kuyaona madini (Jokes)
 
Ndugu Mnyisunura hayo uliyoyaeleza ni ya maana sana na yameniweka katika ufahamu mzuri ,lakini zaidi ya yote hayo wananchi wanakuwa na kuona kila siku miradi ikifanya kazi na mali kuchimbuliwa ,sasa ukiwachukulia wananchi wanaoishi kandokando ya migodi hiyo utawakuta ni masikini ombaomba ,hawana maji safi wala watoto wao hawana shule za kisasa ,haya ndio mambo yaliopelekea mapigano kule Nigeria na mpaka leo hufumka vita katika machimbo ya mafuta ,sababu ni hizi za serikali kujifanya ndie pekee anaefaidi malipo na kutowajali wakazi waeneo,katika sehemu yako ya mwisho ni muelekezo mzuri kabisa kuwa hawa wanaopewa leseni na kuruhusiwa kubukua hazina ya eneo fulani walazimishwe kuweka shule zaidi ya moja ,kuwapatia wakazi maji safi kuwajengea barabara japo oneway na guzo la taa kila baada ya mita mia tano badala ya ahadi hizi kuchukuliwa na chama tawala ambao wakipata feza wanaitafuna,nafikiri WaTanzania wakihahakikishiwa kuwa mwekezaji kabla hajaekeza au pale akipata leseni tu kwanza afanye mambu hayo ili kuwafurahiusha wakazi pia nafasi za kazi kama za udereva ulinzi na kazi zingine za kushughulikia machimbo ,usafi na kazi ndogo ndogo ambazo hazihitaji elimu ya vyuo vikuu wapewe wakazi kwanza yaani wakazi wawe nambarione ,hapo tungelipiga hatua na mayowe yangepungua ,lakini leo Tanzania ni ya Tatu,SouthAfrica ya pili na Ghana ni ya kwanza(Japo umesema Ghana hakuna kitu) lakini chati inaonyesha ni ya mwanzo katika uchimbaji bado unaikuta mikoa ya Mwanza ,Musoma,Mara na Shinyanga hali zake ni duni kabisa kabisa kuanzia makazi,vipando,barabara na mashule kwa kweli wananchi hawataacha kupiga makelele na kusema wanaibiwa na wazungu wachache wakishirikiana na mafisadi Tanzania haihitaji uchunguzi tena kumeshafanywa uchunguzi na mali ipo ya kutosha hata Mheshimiwa Kikwete alisikika akisema hakuna madini unayoijua ambayo haipo Tz ,akijitapa sana kwenye hotuba yake kuwaita wawekezaji ,hivyo asingekuwa na nguvu za kuwaita wawekezaji kama uhakika wa uchunguzi bado haujatimia au haujulikani au utahitaji miaka kibao ,tayari muheshimiwa alikwishaona data tokea akifanya kazi ya Uwaziri.
 
Zitto hii sio mara yako kwanza kuahidi kufuatilia.

Wewe na kiongozi mwenzio Kikwete hamna tofauti katika kutoa ahadi then mnanyamaza kimya bila kutoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi zenu. Nakuweka katika kundi la viongozi wa serikali m-badala wa sisiemu kwa sababu unaonyesha juhudi kuliko wenzio.

In general, i think there will be no significant difference between the present government and the expected alternative government (itakayoongozwa vyama m-badala) in term of kutekeleza ahadi zinazotolewa na viongozi kwa wananchi (check link hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/13190-madini-yetu-kulikoni-jamani.html)

Mama, this is very rare to see you being critical of Mheshimiwa Zitto and opposition in general.

You, as many others here, are always super protective of Zitto and Dr. Slaa.

Every time we call out the CHADEMA's of the country for some blatant blunders you think we are doing CCM's bidding, and undermine the opposition.

I'm glad you understand that they also can, and do, screw up. Tremendously fresh and open-minded outlook from you.
 
Mama, this is very rare to see you being critical of Mheshimiwa Zitto and opposition in general.

You, as many others here, are always super protective of Zitto and Dr. Slaa.

Every time we call out the CHADEMA for some blatant blunders you think we are doing CCM's bidding, and undermine the opposition.

I'm glad you understand that they also can, and do, screw up. Tremendously fresh and open-minded outlook from you.

You are right, I always second Zitto lakini naona kidogo anajisahau sasa.

Tunahitaji mgombea binafsi haya mambo ya vyama haya sio ya kuleta mabadiliko kwa Tanzania ambayo iko darasa la kwanza shule ya msingi demokrasia (Gottee????) na maendeleo
 
Tutafuatilia kujua maendeleo ya miradi hii. Kitu kimoja tu muhimu ni kwamba Leseni hotelewwa kabla ya mikataba. Leseni za kutafuta madini na baada ya madini kugundulika na vigezo kutumia ndipo mkataba hufuata. Kwa miradi yote hiyo bado ni utafutaji. Sasa kujua utafuutaji umefikia wapi ngoja tufuatilie, may be a parliamentary question!

Strictly on the subject of parliamentary questions. I understand everything needs to be closely followed, however we must be cognizant of our limited resources and how to be most effective, especially with the population we have.

I am afraid too many "parliamentary" questions get "parliamentary" answers, which could most likely be rooted in the skillful art of some ombudsman's obfuscation.

To be effective, an extensive investigation is in call.If indeed the government can be indicted by way of an expose in the form of a parliamentary question, then throw them the hook, line and sinker by all means.

Sasa hivi tunataka milipuko ya supernovae tu, kila watu wakisikiliza wasikie kuna mu-EPA, mara kuna Mwananchi Gold Mine, mara BOT Towers, kama kuna vitu ambavyo viko katika prospective stages na kuna question marks inawezekana visiwe effective katika kufanya expose iliyo na maana.

Tukumbuke watu wetu wengi hawana means za kufuatilia nuances za intricately detailed shenanigans, si tunataka milipuko mikubwa mikubwa tu ambayo hata kiziwi ataisikia na kipofu ataiona. Na kwa sababu iko mingi tu, tusipoteze muda sana katika vitu ambavyo vinahitaji wataalam kuvifahamu.
 
Last edited:
Labda niulize pengine nitapata jibu inakuwaje miradi kumina moja ya Uranium inakuwa na leseni zisizopungua mia moja na miradi 13 ya dhahabu kuna leseni kama 50 ,inaonyesha leseni ni nyingi kuliko miradi , Kivipi ? Na hizi leseni zinadhibitiwa na chombo gani ,ukiangalia tu miradi 13 keseni zaidi ya mia basi hutawacha kuweka shinikizo la kuwa kuna ulaji hapo wakubwa mambo haya vipi ?tunahitaji kujulishwa wakazi na wananchi kwa ujumla.
Na nani mtoaji au anaepewa leseni mwanzo na nae anaweza kutoa leseni kwa wengine ?
 
Taifa letu linasikitisha na tunahitaji mapinduzi na wala si eti mageuzi.

Nimesikitishwa sana na habari kuwa hakuna anaye monitor hiyo exploration ya makampuni hayo licha ya kwamba inasemekana kuwa info hizo ni public.

Ni public at the same time hatuwezi kuzipata kwasababu ni makampuni ya nje yenye kufanya utafiti huo...Na serikali naona kuna viongozi wamemuwa kuwa majambazi kiwazi wazi kabisa...Ni sawa na kuziweka rasilimali za nchi kwenye position kama vile ama hazina mwenyewe ama hazi exist kabisa at least mawazoni mwa watanzania kama walivyokuwa wakitaka na kama wanavyoendelea kutaka..Kuwa tusahau na hiyo pasenti inawatosha hao mafisadi.

Ni ujambazi unaokuwa justified na vigezo kama muda wa uchunguzi, gharama, monopoly nk

Kwasababu kampuni kama De Beers inamiliki zaidi ya asilimia 80 ya almasi duniani...Na hivyo wao kama monopoly wanapanga bei za madini hayo...Kwa hiyo hapo unaweza kuona kuwa kuna watu wanaoweza kusema wao ni kama wanaimiliki migodi yetu...Ni kama yao tu na sisi ni kama wanyama ambao tuko kwenye mapori hayo wanayomiliki...Hivyo ndivyo mafisadi na mkoloni wametufanya tujisike kwenye ardhi yetu wenyewe....Kwamba mwekezaji akiondoka kwenye pori hilo basi wanyama hao hawatakuwa na kazi ya kuyafanyia madini hayo kwani hawajui hata umuhimu wake.

Nimeshtushwa sana tu pia kugunduwa kuwa hata mapendekezo ya Bomani yametolewa hivi majuzi tu...Nashangazwa sana kuona kuwa viongozi wetu waliopita kwanini hawakuliona jambo kama hilo ambalo ni kama common sense tu....Kwasababu hata kwenye biashara si kuna inventory? Mali bila daftari hupotea bila habari...Ni utamaduni gani huu tumejijengea? Nina wasiwasi sana kama viongozi wetu ni watanzania ama kama wana akili timamu...Yani hakuna rekodi ya mambo ya rasilimali zetu?

Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na wale wanaotaka kuona tunajijengea mazingira ya kufanya processing muhimu ndani ya nchi badala ya kusafirisha rasilimali zetu kwa vigezo vya kutokuwa na maabara...Hapa ni sawa tu na kutegemea choo cha jirani kwa visingizio kuwa choo chako si bora...Tatizo ni kwamba kwenda msalani will remain there so ni muhimu kufix choo chako kwasababu utakihitaji na huwezi kuepuka utumiaji wake...
Kuendelea kununuwa maziwa na wakati tuna posibility ya kuwa na ng'ombe wa maziwa hakuna maana...Hizo maabara zina uspecial...Wakati wa ukoloni na kabla ya hapo walizisafirisha raw materials..Nani mwenye kufikiri wamebadili mawazo?

Na sisi ni kweli hatujabadili mawazo? Ukweli tunaujuwa na historia tunaujuwa.....Historia tumeisoma, Lakini sisi ni wabongo tu no wonder hata karata tatu wanapiga watu bao..Yani ni upande wa pili wa shilingi umegeuzwa na sisi tunadhani ni a brand new deal....Upuuzi ni ule ule tu technically from the slavery era.

Utaratibu wa mkoloni kuwatumia vibaraka kwa manufaa yao bado upo.

Kama tunaona kuna potential kwenye sekta hizo za madini basi ni muhimu kuwekeza na kuhakikisha tunajipanga kwa kusoma ramani na kuachana na mawazo ya kitumwa. This is extremely neccessary kwasababu ndugu zangu ni lazima tufanye mapinduzi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Sisi kutonufaishwa na rasilimali zetu tutakuja kulaumiwa na vizazi vijavo na mtu asitegemee eti ni wazungu tu ndio watakaolaumiwa kwasababu wao si watasema hata wakiyaacha madini hayo bado tutayakalia tu na kutokuyafanyia kazi? Si watatumia mifano ile ile kama ya zamani kuhusiana na mababu zetu kutojuwa thamani ya madini na kubadilishana na shanga?

Vizazi vijavyo si lazima vitajuwa kuwa 25% ama 10% zilienda wapi?

Ni lazima tujipange upya na tuwe na mkakati wa kuhakikisha tunabadilisha utaratibu huu mbovu...Hata kama itatu cost wakati huu ni sawa tu kwasababu there is always gonna be costs...Hata kama manufaa ni ya kizazi kijacho...Tufanye tu.

Uranium sasa hivi ndiyo inageuka kuwa hot kutokana na ukweli kuwa ina kazi nyingi sana haswa ya nishati ili kuweza kupunguza utegemezi wa mafuta .

Inashangaza sana kuona kuwa kumbe hata hizo wanazoita sample...Huo mchanga hakuna anaye monitor na serikali imelala tu na huku viongozi wakiendekeza uomba omba na huku utajiri tunao.

Msimamo ni jambo la maana sana na kwahivyo hao viongozi waache kwenda kuomba pesa za kuwanufaisha wao na familia zao,badala yake waje na mipango madhubuti ya kutukwamua na hata kama hawatapata pesa za kutosha kununua majumba ya kifahari popote pale na maisha ya anasa na magari ya kifahari,wafunge mkanda kwaniaba ya watoto na wajukuu na vitukuu wetu.Hakuna haja ya kuomba omba na hili limeshakuwa kama norm kwetu sisi waafrika kwa ujumla na matatizo kama hayo yanapelekea sisi kuedelea kuwa bara la kitumwa tu.

Kwanini tujuwe kuwa wakoloni walifuata rasilimali zetu, tukawaondoa kwa nguvu na sasa tunaamini eti ni uchunguzi tu?
Nani kasema wakoloni hawajui utajiri na mahali madini hayo yapo?
Kama hakuna chombo cha serikali kilichokuwa ama kinachosimamia data hizo basi ni wazi wazungu wanaijuwa Afrika kuliko waafrika wenyewe.

Walipogawana Afrika walikuwa hawajui kuna madini na rasilimali nyingine?
Wakati wakiedelea kutowa misaada ya chakula, mitumba, madawa na kondom...Bado wanaendelea pia kuchuguza kama tuna madini? Ama wanaenda kupima kama mchanga huo ni madini?
Hii kali.
 
Labda niulize pengine nitapata jibu inakuwaje miradi kumina moja ya Uranium inakuwa na leseni zisizopungua mia moja na miradi 13 ya dhahabu kuna leseni kama 50 ,inaonyesha leseni ni nyingi kuliko miradi , Kivipi ? Na hizi leseni zinadhibitiwa na chombo gani ,ukiangalia tu miradi 13 keseni zaidi ya mia basi hutawacha kuweka shinikizo la kuwa kuna ulaji hapo wakubwa mambo haya vipi ?tunahitaji kujulishwa wakazi na wananchi kwa ujumla.
Na nani mtoaji au anaepewa leseni mwanzo na nae anaweza kutoa leseni kwa wengine ?

Wanasoma alama za nyakati na hawachezi mbali...Kwenye dunia ya sasa na huko tunakoelekea uranium ni hot cake kama alternative kubwa sana ya oil kama energy power resource...Na sisi tunaweza kuitumia nafasi hiyo.
Hata hivyo kama walivyosema wengine waliotangulia kuna uwezekano wengine wanazishikilia ili waziuze tena baadaye.
Cha muhimu ni sisi tumejipanga vipi ili tuweze kunufaika na pia tuweze kui utilize techology hii ili na sisi tuwawekee umeme hata simba na tembo wetu huko porini lol!

Serikali ni lazima iwahakikishie wananchi kuwa their stakes will be protected...Ufuatiliaji ni lazima uwepo na wananchi wapewe ripoti hakuna tena mambo ya siri ya jeshi ama usalama wa Taifa wa kuuza nchi.
 
Uranium ni madini ambayo yanaathari mbaya sana kwa afya ya binadamu kwahiyo hata kama imegundulika kuwa tunayo kama ilivyodhihilika huko mkoa wa Ruvuma, serikali inabidi iwaelimishe wananchi juu ya madini haya na jinsi yanavyoewza kuathiri afya zao iwapo hawatachukua tahadhali. Umuhimu wa kufanya a thorough environmental impact assessment kabla ya kuanza uchimbaji wa madini haya lazima uzingatiwe.
 
...Nimesikitishwa sana na habari kuwa hakuna anaye monitor hiyo exploration ya makampuni hayo licha ya kwamba inasemekana kuwa info hizo ni public.

...Ni public at the same time hatuwezi kuzipata kwasababu ni makampuni ya nje yenye kufanya utafiti huo

...Yani hakuna rekodi ya mambo ya rasilimali zetu?

...Huo mchanga hakuna anaye monitor na serikali imelala tu na huku viongozi wakiendekeza uomba omba na huku utajiri tunao.

hizo basi ni wazi wazungu wanaijuwa Afrika kuliko waafrika wenyewe.

J Mushi, umeshtukia ? Yani sijui Zitto kaeleza nini pale.

Eti kampuni binafsi ya Kibongo ndio tunaweza kupata data zake halafu ya Kigeni ambayo imeandikishwa Bongo na inafungwa na taratibu na sheria za Bongo hatuwezi kupata data zake !

Halafu hizo data eti ni public!

Mradi wa Serikali "wa Kijeshi" hatuna data zake itakuwa hizi za kina Jim bandit Sinclair ?
 
Wakuu
Kwenye Mining kuna kitu kinaitwa Due Deligency in Feasibility Study! Kwa nchi za wenzetu walioendelea kama vile Autralia na Canada (Natoa mfano nchi hizi kwa sababu ni ndo nchi wanaochimba sana kwa sasa) wanaitumia sana hii! Kama nilivyoeleza kwenye post yangu ya mwanzo, due deligency inawahusu hasa wahusika wa pale ambapo mgodi utakuwa! Kwa ujumla mambo ambayo yanafanyika wakati wa due deligency ni kuangalia sustainability ya project and the well fare of native! Kwa maana nyingine basi mambo ambayo huangaliwa ni pamoja na mazingira, operations, employements, social issues, intfrastructure, economics, na vikorokoro vyote ambavyo project hiyo itaathiri! Bahati mbaya huko kwetu due deligency inafanyikia hotelini na wananchi wanaarifiwa tu!
Otherwise kwa jinsi ninavyojua mining as a whole ni kitu kizuri kama serikali imeamua na inatumia wataalamu specifically ambao wanajua what is mining. Ninasikitika sana kwa kuwa hatufaidiki na uchimbaji wa madini lakini vilevile hatuwezi kukataa wasichimbe! Nasema hivyo kwa sababu ya hali ilivyo kuwa hatuwezi rudi alikofikia nyerere miaka ya 67 alipofunga migodi yote akasema mpaka tutakapojua kuyatumia madini yetu! Lakini tunaweza kuwabana kwa kutumia sheria zetu ambazo zinaendana na mazingira yetu! Na tunaweza kutengeneza sheria bora kama tunatumia wataalam na si kama ilivyo sasa! Kwa mfanyo mtu aliyesoma sheria nadhani inaweza kuwa ngumu kwake akienda kwenye Mining Law! Hii nayo ni specialized field na kuna vyuo vinavyoitoa hiyo! Sasa wataalam wetu ni wale wa sheria za chuo kikuu akiambia marginal cut off grade of the project amepotea ndo hapo sasa mwekezaji anapata upenyo wa kumburuza!
Mimi kwa ujumla naamini tunaweza na au tukishindwa basi serikali ianze mpango wa shear! Nadhani hii itasaidia! Wanasiasa ndo wanaotuangusha kwa ujumla kwa jinsi ninvyojua otherwise hatuwezi kuepuka!
Nitatoa mfano, Canada ambako Barrick ndo original lakini ipo Campuni kubwa huku ambayo ilikuwa inamilikiwa na wakanada lakini wameshindwa na wamewauzia wabrazili. Lakini all managements is by canadian! Hii ni kuonesha tu kuwa hatuwezi kuepuka wawekezaji ila sheria ndo zitatuokoa!
Nilitoa mfano wa kutegemea service kama moja ya source of tax generated from the mining ukiacha wafanyakazi
Mahali popote pale kwenye mining consumption kubwa ni
baruti (explosive)
Fuels
Food
Stationaries
Pipe for civil works na vitu vingine vingi ambavyo sihitaji kuvimension!
Sasa je ni watanzania wangapi wanaweza kusuply hivi vitu ili serikali itoze kodi na watu kupata ajira! Ukweli ni kuwa hatukujiandaa na ndo maana kila kitu ni kigeni kwetu! Matokeo yake wawekezaji wanaingiza na ni tax free!
Kitu kingine ambacho tunatakiwa kujua( kuanzisha mgodi kama Buly inahitaji uwe na Capital si chini ya $1000 M, keep in mind that hawa watu wanarisk! Wakiona upenyo wanautumia kisawasawa! Ni sheria tu ndo zitatuokoa!
 
Back
Top Bottom