Habari na Picha Nape, Mwigulu ziarani Sumbawanga

Nape jana kaiua sana Chadema! Kuna ulazima wa Chadema kurudi kusini tena! Kaipiga sana na kuwambia Chadema ni genge la wahuni ndio maana hawajari hata Nchi isipo tawalika! Amesema huyo alie kataa mshahara mkubwa Bungeni leo amelazimisha au pate kwenye chama masikini! Anasema dr slaa ni padre na ana fuata kanuni ya msifuate matendo yangu ila fuateni maneno yangu!

Mnajulikana mnachokijua ni Dr. Slaa tu, maendeleo ya nchi si hoja yenu.
 
Nawashauri viongozi wa Chadema Sumbawanga wafuatilie na kuona ni kwa nini, na kwa jinsi gani kadi hizo za uanachama wa Chadema zilirudishwa!

Mkuu,

Nina swali moja rahisi. Hivi watu wakiwa mitaani au wanapokwenda kwenye mikutano ya vyama vya siasa uwa wanabeba kadi za vyama vyao mifukoni au kwenye matiti? Nashindwa kuhamini kwamba hao kina mama walioamua kurudisha kadi za Chadema wanatembea na kadi hizo kila waendapo. Nafikiri kadi hizo zilitolewa na CCM kwa wanachama wao ili kudanganya umma kwamba CCM inakubalika kuliko Chadema!!!!!

Tiba
 
Inashangaza sana kuwa fanya watanzania wote ni wajinga kwa kweli naomba niwaambie watanzania wenzangu si kila siku jumapili au siku zina fanana, la. Nape na wenzako Tanzania ya leo sio ile ya miaka 45 iliyopita jamani Hapa nikiangalia najiuliza maswali mia kidogo
**hivi hawa watoto ndio maelfu ya watanzania waliorudisha kadi maana naona watoto tu labda macho yangu.
**wanaorudi CCM ni kutoka CHADEMA tu au mnataka kutuaminisha kuwa mnavuna kutoka chadema tu ndio wasio jua
**tafuteni mada nyingine nyie sio kihivyo jamani hatuwaamini hasilani MAGAMBA NYIEEEEEEEEEEEE
Khaa! we si ndiye uliyepost upupu wa matusi ya nguoni hapa jamvini jana? kwa maana hiyo mods hamkuiona post ya huyu shegaboy iliyosema Uzinduzi wa bendi mpya? chonde chonde mods itafuteni hiyo topic na muisome! huyu hafai kabisa kuwepo hapa jamvini
 
Wanachadema wala msitishwe na kurejeshwa kwa kadi hizo.Kadi zilininunuliwa jana asubuhi na iliofika saa 6 uongozi wa CHADEMA mkoa ukashituka namna kadi zilivyonunuliwa kwa wingi kuliko siku zote na kugundua juu ya kupelekwa katika mkutano husika.Hivyo kadi zote hizo zilinunuliwa jana na watu waliotumiwa na CCM-magamba.Idadi hiyo ya watu mbona ndogo sana ni sawa na 1/8 ya mkutano wa CHADEMA uliopita.Mimi nikiwa katika mji huu,mkutano ulikuwa umepooza hauna lolote na waliojaza ni watoto wadogo na wacheza ngoma wazee.Watu wote maarufu na wazarendo wenye mapenzi mema na nchi hii walihudhuria mazishi ya dereva wa NMB Sumbawanga ambao walikuwa wengi zaidi ya mara kumi ya mkutano wa CCM. Nape bado ana kazi kubwa sana!!!!!!!!. aliyeleta picha na maandishi hayo ni mwandishi uchwara :mod:

Tumeona ITV umati ni mkubwa na watu wako maikini kumsikiliza Ndugu Nape Nnauye kwa umakini sana wengi wao wakiwa akina mama! Chadema nashauri mrudi tena Rukwa jamaa kawapiga sana! Msidharau hili jambo CDM!
 
Mh Jamani mi na maswali kadhaa kuhusu hii tour ya kina Nape Rukwa
Je ni kweli CCM inapata wanachama toka CDM tu? vipi je hakuna wa vyama vingine? au wale waliokuwa hawana vyama hawajiungi na CCM?
Je? wanalinganisha umaarufu wao na CDM? na ka wanasomba watu wanamdanganya nani? je kuna uwiano wa hao waliorudisha kadi za CDM na wale waliojiunga wakati wa operation ya CDM huko kusini?
Badala ya CCM kuonyesha walichofanya, au kuelekeza ilani yao wanashambulia CDM au hiyo ndio Ilani yao ya uchaguzi?
Je CCM wamejisahau ka wao ni Chama tawala? Sidhani ka kwa mtaji huu tutafika
Hivi siasa za malumbano zina tija? kwetu CDM ni wapinzani wao wanachofanya ni kuonyesha weakness kwa chama tawala CCM kazi yao ni kuonyesha walichofanya na wanachofanya kwa vitendo, si kinadharia wala malumbano tunataka majibu kuhusu ugumu wetu wa maisha sio habari eti DR Slaa alikuwa padre hiyo tunajua njooni na mpya
 
Wamekosea sana,Tanzania inaserikali moja tu,serikali iliyoundwa na CCM.Wapiga kura wameipa CCm majukumu ya kuongoza nchi katika matawi yote ya serikali,CCM imeshinda uraisi,ubunge kwa hiyo inahiari ya kuwashirikisha wapinzani au kufanya kila kitu bila ya kushirikiana.Lakini ilichagua kushirikiana,ndio maana ikawapa wapinzani kuongozi baazi ya kamati zabunge,Mrema ,Zitto n.k.Wapinzani kama wanataka hoja zao zipite wachague kushirikiana na CCM kuendeleza nchi yetu .Haya mambo ya kwenda mitaani ni uhuni na uvunaji wa sheria kama mtawashawishi watu kuichukia serikali.
 

Attachments

  • 2.jpe
    2.jpe
    38.8 KB · Views: 55
  • 4.jpe
    4.jpe
    33.6 KB · Views: 51
  • 128229.jpe
    128229.jpe
    46.7 KB · Views: 43
  • 528129.jpe
    528129.jpe
    43.2 KB · Views: 39
  • A5B15D.jpe
    A5B15D.jpe
    227.1 KB · Views: 44
  • C5B15D.jpe
    C5B15D.jpe
    190.5 KB · Views: 43
  • D5B15D.jpe
    D5B15D.jpe
    286.7 KB · Views: 42
  • E5B15D.jpe
    E5B15D.jpe
    136.4 KB · Views: 42
  • F5B15D.jpe
    F5B15D.jpe
    217.9 KB · Views: 51
Wapinzani wengine wameheshimu demokrasia na CCM inaheshimu pia,CDM imeamua kufanya fujo tutapambana mpaka mjifunze na kujua maana ya demokrasia ni nini.
 
mimi nilikuwa kwenye mkutano wa leo na wajana kwa kweli hawa vijana wameiteka Sumbawanga kwa kiwango cha hali ya juu sana! Awali nilidhani kuwa hawatapata watu hasa kutokana na watu walivyojitokeza kwenye mkutano wa CHADEMA. Lakini kuwa wakweli umati wa jana na leo umezidi ule wa chadema kama nne ulikuwa mtiti kweli kweli na watu walikuwa makini wakisikiliza na kushangilia.
 
Nawashauri viongozi wa Chadema Sumbawanga wafuatilie na kuona ni kwa nini, na kwa jinsi gani kadi hizo za uanachama wa Chadema zilirudishwa!

Hivi tunajuaje hizo kadi sio zakutengeneza? Sio kwa CCM tu lakini labda vyama vingine pia wanaweza kufanya huu usanii; lakini CCM ndio wenye hela zakutapanya so kwao ni rahisi sana kutengeneza kadi zinazofanana naupinzani na ku-waandaa watu kuzirudisha. Labda kama hizo kadi zina-security mark somewhere ambayo mtu hawezi ku-copy. Otherwise hii mambo yakuchukua na kurudisha kadi naona kama usanii fulani. I might be wrong though.
 
Nape aliwakuna wanasumbawanga pale alipotoa mfano wa busara za mfalme Suleiman pale alipoletewa wa mama wawili waliogombea mtoto. Mfalme akasema basi tumpasue mtoto katikati mgawane. Yule ambaye mtoto si wa kwake akasema mara moja sawa kwa sababu alikuwa hana uchungu naye, lakini yule mwenye mtoto akasema mwache tusimpasue ila mtoto huyu apewe mwenzangu. Alimfananisha huyo mama asiye na huruma na CHADEMA wanaotaka nchi isitawalike kwa sababu hawana uchungu
 
Kwani mnadhani WANACHADEMA hawawezi kurudisha kadi kwa CCM? Tatitoza hamtaki kukubali ukweli kuwa maamuzi ya CCM ya Dodoma yamerudisha imani kwa watanzania wengi sana hasa wale waliokuwa wanaiona CCM kama chama kisichobadilika.
 
Mkuu,

Nina swali moja rahisi. Hivi watu wakiwa mitaani au wanapokwenda kwenye mikutano ya vyama vya siasa uwa wanabeba kadi za vyama vyao mifukoni au kwenye matiti? Nashindwa kuhamini kwamba hao kina mama walioamua kurudisha kadi za Chadema wanatembea na kadi hizo kila waendapo. Nafikiri kadi hizo zilitolewa na CCM kwa wanachama wao ili kudanganya umma kwamba CCM inakubalika kuliko Chadema!!!!!

Tiba

Umeona ee! I thought the same way too. It looks so much staged kwa-kweli but I hope am wrong. Ni rahisi kugundua though, unatafuta sura ya mtu/watu unayemfahamu au uanyemuona hapo unamuuliza kishkaji her/his views kuhusu vyama hivi viwili na nini kilimvuta kurudisha kadi etc etc. Hii inaweza ikawa kama survey, unarekodi kisiri siri if possible with no cameras. Then ukweli utakaopatikana unatawasidia vyama vyote viwili kuelewa ukweli/mawazo waliyonayo wananchi wa kawaida. Otherwise picha tu ni kama propaganda sio kipimo chochote.
 
Nape jana kaiua sana Chadema! Kuna ulazima wa Chadema kurudi kusini tena! Kaipiga sana na kuwambia Chadema ni genge la wahuni ndio maana hawajari hata Nchi isipo tawalika! Amesema huyo alie kataa mshahara mkubwa Bungeni leo amelazimisha au pate kwenye chama masikini! Anasema dr slaa ni padre na ana fuata kanuni ya msifuate matendo yangu ila fuateni maneno yangu!
magamba hawana lolote la maana, wao kwenye mkutano wanavuna wanachama hamsini sisi tunavuna maelfu, sasa nani zaidi hapo
 

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM, Theresia Mwanakatwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi, jana katika mji mdogo wa Laela, wilayani mkoani Rukwa. Jumla ya wanachama wapya 82, waliojiunga na CCM walikabidhiwa kadi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu.
** HUYU NI MWANACHAMA MPYA KWANINI AMEVAA KANGA YA CCM? ALIHONGWA???
 
CCM inapata wancahama wa kutoka CHADEMA tu? yaani hakuna wanachama wa vyama vingine wanaohamia CCM bali wale wa CHADEMA tu. Nina wasiwasi na credibility ya matukio hao ya Sumbawanga kuwa yanaweza yakawa staged.
 
nashangaa, kwanza sioni maelfu ya watu kama posti inavyosema, pia naona idadi ndogo ya watoto wa shule, tatu uwanja unaosemwa ni uwanja wa mandela lakini mandhari ni ya viwanja vya msakila high school,nne kadi ninazoziona ni mpya ni kama zimetolewa jana zikarudishwa leo. aliyepost thread alikuwa na malengo mazuri kwa wakubwa wake waliompa kazi lakini hana akili za kuweza kufikisha ujumbe,inaonyesha hata sumbawanga hakujui. pole ccm kwa kutumia vilaza.
 
Back
Top Bottom