Habari na Picha Nape, Mwigulu ziarani Sumbawanga

Lets be honest,ni watanzania wangapi hawana kadi za chama?
na wangapi hawajishughulishi na mchakato wa iasa(vyama)?
tukishajua hayo mawili ndio tupime kwa CCM kupata kadi Za CDM inawasaidia nini?
kwani isije ukawa ikawa unavua samaki kwenye beseni badala ya bahari...fikirini,fuatilia kwa makini alafu tusaidiane mawazo!
 
Ushauri wangu kwa CCM ni kwamba waache kujidanganya, bali washughulikie kero za wananchi. Kama wanadhani ujanja ujanja utamaliza tatizo la CCM kwa wananchi hii itakuwa ni ndoto kabisa. CCM wanatakiwa wajue kuwa matatizo ya wananchi ni halisi na yanahitaji ufumbuzi harisi na si kuzunguka kupiga siasa kama Mr. Nape anavyo fanya. Ni kweli kuzunguka atazunguka hata kama ataimaliza Tanzania nzima. Ukweli utabaki kuwa wananchi wanahitaji mabadiliko na si masimulizi ya kisiasa. Faida pekee ya uzungukaji wa Mh. Nape ni wingi wa posho atakazo jipatia na si kuondoa tatizo la CCM machoni pa Watanzania. Kama kweli ninyi viongozi wa CCM mnamasikio sikeni, na kama kweli mna macho tazameni, nakama kweli mna akili basi eleweni. Vinginevyo 2015 itawahukumuni, maana ninyi mkizani ni ujuzi wa kusimama majukwaani na kupiga kelele kana kwamba CHADEMA ndio tatizo. Watanzania wanataka maisha bora kwa kila Mtanzania, hicho ndicho kilio chetu.
 
ma elfu ya watoto kumbe hawa nao cdm, nadhani hapo walikuwa wanamwambia maliza basi bendi itupigie kiduku tucheze
 
Back
Top Bottom