Goba hatuna maji wiki ya tatu sasa

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
998
Habari zenu wanaJF,

Mtendaji mkuu wa DAWASA habari za jioni. Tuna muda wa wiki tatu sasa hatuna maji kabisa hapa Goba, mimi nakaa Goba mitaa ya kwa Morgan na week ya tatu hii hatuna maji! Kikawaida hua tunapataga kwa wiki mara moja lakini kwa kipindi cha hivi karibuni tunakaa hadi wiki 3 ndo tunapata maji na kupelekea kuingia gharama za kununua maji ya kwenye malori.

Wito wangu;
Tuma timu ije ifanye uchunguzi kama kuna tatizo la miundo mbinu ya maji basi lishughulikiwe na maji yaweze kutoka. Tumsaidie Rais kwenye mambo madogodogo kama haya.

Mwananchi wa Goba.
 
Tanga kata Tangasisis na kwinginepo wiki ya tatu saa, bladifaken TangaUwasa
 
UKOSEFU WA MAJI NA UMEME KWENYE HII NCHI USHAKUWA UGONJWA USIOKUWA NA TIBA
 
Mbona siku chache hivyo mkuu! Usagara, Misungwi Mwanza. Ziwa lipo kilometer kama 13 tu hapo chini ambalo limepeleka maji mpaka Shinyanga, lakini Usagara haina maji toka Dunia imeumbwa
 
The same Kinyerezi 1month juzi Jumapili ndo yakatoka usiku asubuhi tukaagana nayo
 
Back
Top Bottom