sun wu
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 2,020
- 1,419
Samahani Mkuu sikuona mwanzo comment yako ningekujibu before hii ni teknolojia nzuri tu (ingawa sio mpya wala ngeni) tatizo ni lugha ilivyotumika na anachosema huenda kika-misled watu wakazani wananunua magic box ambayo unaweza uchafu wako wa jana na kutumia milele na kusahau kwamba Input lazima iwe kubwa kuliko output.., kwahio mabaki ukiweka mengi utatumia sana kama ambavyo fungu moja la mkaa linapika chakula kidogo kuliko guniaMkuu, inaonekana wewe una-ufahamu mzuri juu ya hii kitu
Hebu tuelezee basi ili na sisi wengine tujue
Hapo mwanzo alisema kwamba hii gesi ukishanunua haiishi ambavyo sio kweli ni kwamba inakwisha ila ukiweka mabaki ya chakula ni kwamba unatengeneza gesi nyingine hivyo basi inabidi uendelee kuweka mabaki ya chakula ili uendelee kutumia., kwa sasa nimeona anasema gesi unalipa mara moja unatumia milele it depends what is kulipa.., sababu hata tukisema nguvu ni kulipa basi ni kwamba ulipaji wako itakuwa ni kuendelea kuweka mabaki ya chakula...,Ni kitu gani ambacho anatupotosha?
ni kwamba vitu vikioza vinatoa gas (methane) ambayo inawaka ndio maana hapo chini nikasema hata wewe kwako leo ukichukua debe au pipa ukaweka pipe kwa juu mpaka kwenye stove na kuweka kwenye pipa mabaki ya chakula au kinyesi utakuwa unapikia bila shida na mabaki yanayobaki ni mbolea tosha kabisa na nzuri ambayo haina harufu.Au infanyaje kazi?
Gasi hii ni nzuri kwa kupika na inafaa kabisa (the cheapest way to cook and save our environment) ila labda kwenye maabara (Bunsen burner) huenda isifae sana sababu inakuwa sio strong ila for home use its perfectUkali/nguvu ya gesi yenyewe?
Ni matumizi yako kwa pipa moja hata ukitengeneza mwenyewe kama una samadi ya ngome wawili unaweza kupikia familia yako kwa siku bila shida yoyote..., ila kama mpo wengi na unategemea tu nyanya unatokata na mabaki ya cabbage sidhani kama unaweza ukapika kuanzia asubuhi mpaka jioni (in short hakuna magic hapa what you put is what you will get, weka mabaki mengi utapata gesi nyingiInadumu muda gani?
Hapana haina madhara yoyote tena inasaidia mazingira sababu unatumia waste kupikia alafu mabaki yanakuwa mboleaIna madhara kwa mtumiaji?
Biogas (yaani gesi inayotoka kwenye hayo mabaki) digester ni kitu kinacho-digest hayo mabaki ili gesi ipatikane kwahio hata hii issue ya huyu bwana ni biogas digester, au hata wewe ukitengeneza ya kwako kutumia mtungi au pipa bado ni biogas digesterNa hii unayoiita Biogas digester .. ni nini tofauti yake na hicho anachotuambia?
Je inafaa kwa matumizi ya nyumbani au tuachane nayo?
Tuelezee mkuu
Hapana mkuu inafaa sana wala usiachane nayo ila sio jambo geni wala hakuna mtu aliye-reinvent the wheel hapa wachina wamekuwa wakitumia Biogas for years na wewe kama kwako kuna mabaki mengi, samadi au chochote kile sio vibaya kutumia hii sababu utapata na faida ya mbolea..., na ukikosa kabisa pesa maybe unaweza kununua stove na pipe kutoka kwa hao jamaa ukachukua pipa lako la kawaida na kutengeneza biogas digester mwenyewe