Gazeti lagawiwa buree ili usome

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Leo nimepita maeneo ya Tegeta nikakutana na kijana mmoja ameshika magazeti lundo ya Tazama Tanzania’ anayagawa na akaniambia anatoa ofa,

nikamuuliza ni kitu gani kimekufanya ugawe magazeti tena ya aina moja tuu badala ya pesa au zawadi nyingine? Akasema tena huku akicheka “ Ndugu yangu usichague zawadi mimi nagawa hili gazeti kwasababu leo ni sikukuu watu wanapumzika nyumbani nataka wajisomee na kuhusu magazeti mengine bajeti yangu ilikuwa haitoshi mimi nilikuwa natafuta gazeti moja makini kwa bei ya mianne mianne hii ndiyo bajeti yangu” ni kashindwa kuendelea kumhoji kwasababu ni gazeti la leo nikalichukua baada ya kulipitia nikaona kuna habari moja kati ya zilizowekwa ukurasa wa mbele kabisa ikisema….

NGUVU YA CHADEMA YAANZA KUPOROMOKA.
*Tabora, Singida wamzomea Dk. Slaa.

Nikalazimika kuisoma kwa undani japo ni ndefu sana baadhi ya vitu vilivyoandika ni kama ifuatavyo.

1. Baada ya CCM kujivua gamba…….mamia ya wanafunzi wa secondary wamejiunga na CCM, na...............wamempongeza mwenyekiti wa chama hicho jk kwa kuchukua maamuzi mazito ktk kipindi hiki kigumu kisiasa kuliko vyote vilivyopita......................wanakiri kwamba chama hicho ndiyo tegemeo la watanzania na kutaka misingi yake iliyowekwa na baba wa Taifa isivunjwe.

2. Gazeti linadai limem-quote Sijale Siwale ambaye ni mwanachama mpya wa CCM mkoani iringa akisema yafuatayo kuhusiana na ni kwanini alisita kujiunga na chadema wakati wa kampeni japo alishakuwa kajiuzuru uanachama wa UVCCM.

“Nilikwenda kumsikiliza (Dr slaa) pale Mwembetogwa na muda wote aliohutubia nilizingatia sana dakika alizotumia. Alizungumza kwa dakika 50 ambazo hata hivyo alitumia zaidi dakika 40 kuwashambulia watu akiwemo Rais kikwete, mkewe mama salma, mtoto wao Ridhiwani Kikwete, Mnadhimu mkuu wa jeshi la wananchi, polisi pamoja na idara ya usalama wa Taifa. Dakika nyingine kama tatu au nne alizitumia kumtambulisha mchumba wake, Josephine na kisha aliongelea sera kwa takribani dakika tatu akaanza kuwatambulisha wagombea wa viti vya udiwani wa chama chake na mgombea ubunge”

3. Pia gazeti linadai idadi kubwa ya wananchi waliowahoji wanadai agenda ya ufisadi imepitwa na wakati hivyo Chadema waachane nayo kwani haina ushahidi na ni maneno tu na wakiendelea nayo wananchi wengi wataachana na Chadema wataelekea CCM.

4. Gazeti lina ongeza baada ya Slaa kumtaja Rostam na Ridhiwani kwamba ni mafisadi wananchi walianza kumzomea huku wakihoji………

“Sisi hatujui kama Ridhiwani kweli ni tajiri kiasi hicho na hilo haliwezi kutusaidia. Kwanza kama ametajirika kwa kinyume cha sheria na ushahidi unao inakuwaje uje uzungumze jambo hilo hapa badala ya kwenda kumfungulia kesi?”

Swali ninalo jiuliza huyu kijana amefikiria nini mpaka akaamua kutumia pesa nyingi sana kununua magazeti tena ya aina moja na kugawa bure kwa watu mitaani? Au kuna kitu kimejificha ambacho mimi sikijui? kwasababu katika watu tuliogawiwa hii zawadi wote tulikuwa na mitazamo tofauti wengine walidai ni promotion, wengine wakadai ni surprise na hata wengine wakadiriki kudai huenda ametumwa na watu wanaopenda habari za leo ziwafikie watu wengi zaidi.
 
Mimi nadhani hiyo inagawiwa kama zawadi zingine zozote ndugu yangu usifikirie sana kwamba kuna cha ziada hapo, hayo ni maoni yangu tuu
 
"Nilikwenda kumsikiliza (Dr slaa) pale Mwembetogwa na muda wote aliohutubia nilizingatia sana dakika alizotumia. Alizungumza kwa dakika 50 ambazo hata hivyo alitumia zaidi dakika 40 kuwashambulia watu akiwemo Rais kikwete, mkewe mama salma, mtoto wao Ridhiwani Kikwete, Mnadhimu mkuu wa jeshi la wananchi, polisi pamoja na idara ya usalama wa Taifa. Dakika nyingine kama tatu au nne alizitumia kumtambulisha mchumba wake, Josephine na kisha aliongelea sera kwa takribani dakika tatu akaanza kuwatambulisha wagombea wa viti vya udiwani wa chama chake na mgombea ubunge".

Duh....
 
Haya sasa!
Watayagawa sana kwa mtindo huu, lakini haitasaidia, zaidi sana nadio wanaitangaza cdm bila kujielewa!
 
Ahahahahaha
Tutaona na kusikia mengi. Watakuja na mbinu nyingi tu.
Dr Slaa kaza buti tuikomboe nchi na kuwafumbua watu juu ya yale wasiyoyajua juu ya watawala wao.
Mafisadi wameanza kutapatapa.
Mbona haweendi kuwasaidia wale wanaokosa chakula na chai ya asubuhi wanawasaidia watu magazeti.
Je watu wanahitaji magazeti zaidi? Je magazeti ndio suluhisho na mbadala wa matatizo ya watanzania yaliyosababishwa na uongozi mbaya?
Pole kwa kijana aliyekubali kutumiwa.
 
Ukiona gazeti linalomshambulia Slaa linagawiwa bure (zawadi) na lile linalomshambulia KJ linauzwa kwa bei ya ulanguzi, basi ujue hiyo ni ishara tosha ya nani anakubalika na jamii
 
sasa walikuwa na haja gani ya kuyagawa bure?manake wenye interest watanunua tu na kusoma.in the end of the day magazeti yao yataishia kufungia maandazi na vitumbua kwa kujiingiza kinyemela mitaani.aluta continua..
 
hahahaaa chi chi m banaaa,taften mbinu nyingine za kujisafisha achaneni na doctor wa ukweli WILLIE SLA
 
Back
Top Bottom